Iwapo bajeti ya kununua simu aina za iphone au matoleo ya samsung s23 ni ndogo basi kuna Tecno Spark 10 Pro
Tecno Spark 10 Pro ni tecno mpya ya mwaka 2023 inayokuja na kamera tatu
Ni simu ya daraja la kati hivyo bei ya tecno spark 10 pro haiwezi kuzidi laki nne na nusu
Simu ina sifa nzuri kwenye baadhi lakini pia ina kasoro kadhaa kama ilivyofafanuliwa kwenye hii post
Fuatilia mwanzo mwisho
Bei ya Tecno Spark 10 Pro ya GB 128
Kwa Tanzania, tecno spark 10 pro ya GB 128 inauzwa shilingi 415,000/=
Bei inaonekana ni kubwa kwa anayetarajia simu za laki mbili, ila kumbuka hii ni simu ya daraja la kati’
Ina sifa nyingi zinazojitofautisha na simu za bei ndogo sana
Kuanzia kamera na display(kioo) cha hii simu ni vya kuridhisha
Kuna vitu vya msingi unapaswa kuvielewa ili ujue iwapo tecno spark 10 pro inastahili kuuzwa bei iliyotajwa ama la
Na utaweza kuelewa kwa kuangalia sifa zote spark 10 pro
Sifa za Tecno Spark 10 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 256GB,128GB na RAM 8GB, |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.8inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 415,000/= |
Upi ubora wa Tecno Spark 10 Pro
Simu inakuja na kioo chenye refresh rate kubwa ambavyo huwa ni vizuri kwa ajili ya magemu
Betri yake ina ukubwa unaoweza kukaa na chaji masaa mengi
Ni simu ndefu hivyo vitu vinaonekana kwa ukubwa
Inakuja na sehemu kuweka earphone tofauti na matoleo ya sasa ambayo huondoa kipengele hiko
Pamoja na simu kuwa na memori kubwa ila ina sehemu ya kuongeza memori kadi
Ina utendaji wa kuridhisha kutokana na aina ya processor iliyotumika kuwa na nguvu
Kuna nyanja pia simu imepungukiwa ubora ila haishangazi kutokana na aina ya wateja inayowalenga
Uwezo wa Network
Spark 10 Pro inakuja na network ya 4G bila kuwa na 5G
Kwa Tanzania 4G imesambaa maeneo mengi kuliko teknolojia ya 5G
Ni hivi karibuni Tigo na Vodacom wameleta kizazi hiki kipya cha network
Aina ya 4G iliyopo kwenye simu ni LTE Cat 7
Kasi ya kupakua faili ya LTE Cat 7 inafika 300Mbps
Yaani kama unadownload app ya TikTok yenye MB 86 basi app itamalizika kuwekwa kwenye simu ndani ya sekunde tatu tu.
Japo kwa nchini si rahisi kupata kiwango hiki ila kama intanet ya starlink ingekuwepo hiyo spidi ingeweza kupatikana
Kwa 5G ya Tigo na Voda hiyo ni spidi ya kawaida kuipata
Ubora wa kioo cha Tecno Spark 10 Pro
Kioo cha Tecno spark 10 pro ni aina ya IPS LCD chenye resolution ya 1080 x 2460 pixels
Resolution yenye pixels kama hizo huitwa FHD+ (full hd plus)
Kwa sifa za kioo ni kizuri na picha zinaokana zikiwa safi japokuwa hakina HDR10 ama Dolb Vision
HDR10 na Dolb Vision huboresha muonekano wa vitu na kufanya rangi zake zionekane kama zilivyo kwenye mazingira halisi kwa kiasi kikubwa
Changamoto kubwa ya vioo vya LCDÂ na kutokuonyesha rangi nyeusi halisi
Na ukoleaji wake wa rangi unazidiwa sana na vioo vya AMOLED
Unaweza kuliona kama ukilinganisha muonekano kwenye kioo cha Samsung Galaxy A54 5g
Ila isikushangaze sana kwani Spark 10 pro ina bei ndogo hivyo baadhi vitu lazima viwe vya kawaida
Nguvu ya processor MediaTek Helio G88
MediaTek Helio G88 ni chip yenye uwezo wa kati katika utendaji
Ndiyo iliyopo kwenye tecno spark 10 pro
Imegawanyika katika sehemu mbili ambapo sehemu yenye nguvu sana ina core mbili inayoweza fanya mizunguko bilioni mbili kwa sekunde
Na inatumia core aina ya Cortex A75 na ile sehemu yenye nguvu ndogo zinatumia Cortex A55
Hii inacheza gemu nyingi bila shida ila kuna baadhi ya magemu simu inahitaji kupunguza resolution
Mfano wa gemu hizo ni Genish Impact yenye GB 20 kwa processor ya Helio G88 inacheza kwa settings za chini
Yote kwa yote ni kuwa Mediatek helio g88 inaifanya simu kuweza kufungua app yoyote bila shida
Uwezo wa betri na chaji
Kutokana na simu kutumia chip yenye nguvu ya wastani na betri kuwa kubwa ya 5000mAh ukaaji wake wa chaji ni wa kuridhisha pia
Kikawaida simu za 5000mAh zina uwezo wa kudumu na chaji kwa kipindi cha masaa yanazidi 13
Chaji ya Tecno Spark 10 Pro ina kasi ya wati 18
Ni kasi ya wastani hivyo betri yenye ukubwa wa 5000mAh inaweza chukua muda kidogo kujaa
Kuna simu zenye chaji ya wati 30 na huwa zinajaza betri ya kiwango hiko kwa lisaa
Kwa viwango vya chaji za siku hizi wati 18 ni kiwango cha wastani na si fast chaji
Ukubwa na aina ya memori
Tecno spark 10 pro ina matoleo mawili kwenye upande wa memori na zote zinakuja na GB 8 ya RAM
Aina ya memori simu inayotumia ni eMMC 5.1
Hizi ni memori za zamani na kasi ya usafirishaji wa data si mkubwa kama memori za UFS
Simu hii inakuja na sehemu ya kuongeza memori card kama simu ikiwa imejaa na haitoshi
Uimara wa bodi ya Tecno Spark 10 Pro
Bodi ya Tecno Spark 10 Pro ina glassi upande wa nyuma ila sio vioo vya gorilla
Na kwenye screen imewekwa protekta ya plastiki
Hii simu haina uwezo wa kuzuia maji kama ikidumbukia kwenye kina kikubwa
Ni tofauti na simu za samsung galaxy s23
Kikawaida simu zisizopitisha maji huwa zina bei kubwa inayozidi milioni
Hii simu inaweza pia kukaa muda mrefu bila kuharibika sababu ya kuwa na kioo upande wa nyuma
Hata hivyo ni muhimu kuweka kava kuepuka uharibifu unaweza tokea ghafla
Ubora wa kamera
Kamera za Tecno Spark 10 Pro zipo tatu ambapo mbili hazijaainishwa ni za aina gani
Kwa maana haijaelezwa kama ni kamera za kupiga eneo pana au ni vitu ambavyo vipo mbali sana
Kwa baadhi ya video za youtube kuhusu hii simu ni kuwa haina kamera za ultrawide wala telephoto
Kamera yake kuu yenye 50MP inapiga picha zenye wa kawaida sana na ubora hafifu kwenye mwanga mdogo
Nyakati za usiku noises (chengachenga) zinaweza kuonekana kwa uwazi
Kamera inapiga video za full hd pekee kwani haipigi video za resolution kubwa zaidi za 4K
Hii inachangiwa na ufinyu wa utendaji wa processor yake kutokuwa na uwezo wa kuchakata video za aina hiyo
Wakati wa kurekodi video huku ukitembea itakulazimu kuwa makini
Kwani simu haina OIS ya kutuliza mitikisiko
Ubora wa Software ya HiOS 12.5
Tecno Spark 10 Pro inakuja na mfumo endeshi wa Android 13 na HiOS 12.5
HiOS 12.5 inakupa chagua la kuonheza ukubwa wa ram
Android ni mfumo endeshi unaotumia sana RAM na kuna app huwa zinatumia ram nyingi
Kulitambua simu za siku hizi zinatoa uwezakaono wa kutumia sehemu ya memori ya simu kama ram
HiOS 12.5 inaweza kupokea simu moja kwa moja pindi unapoweka sikioni
Sio lazima kubofya kitufe cha kupokelea simu
Yapi Madhaifu ya Tecno Spark 10 Pro
Chaji yake haina kasi kubwa
Mfumo wake wa kamera si wa kuvutia na haina aina zingine muhimu za kamera
Inatumia mfumo wa memori wenye kasi ndogo ya kusoma na kuandika data
Kioo chake hakina HDR
Neno la Mwisho
Tecno Spark 10 Pro ina bei shindani ila hii bei inaenda moja kwa moja kwenye ushindani na simu aina ya Redmi Note 10
Ukikaa na kuringanisha hizi simu utagundua kuwa Spark 10 pro inaachwa mbali sana
Ila redmi note 10 ni toleo la mwaka 2021, kwa mpenzi wa matoleo mapya anaweza kuchagua hii tecno mpya ya 2023
Maoni 32 kuhusu “Bei ya Tecno Spark 10 Pro na Ubora Wake”
Nataka kukopa hio simu
Jaribu kutembelea maduka ya mitandao ya simu
Tunaomba bei iwe lafiki kwa wateja wote
Tunaomba mpunguze bei iwe rafik kwa wateja
Wangejitaidi kuboresha upande wa camera maana siku uzi watu wengi tunaangalia camera bora
Na ufanyaji wa kazi kwa haraka atupendi cm iliyokua slow
Punguzeni bei
Cm ni nzr ila upande wa camer waongezee jitiada
Bei kidogo Iko juu cm ni nzuri kweli inavutia wekeni bei rafiki
Tecno haijawahi kuwa sim ni kifaa cha mawasiliano punguzen bei 415k iwe hata 100k
Kwani simu ni nini? Hata hivyo simu zote ni vifaa vya mawasiliamo, kumbuka hilo
Sm. IPO vizuri kidogo ila sema haina mvuto mzuri kama tecno camon 19.
Sim iko sawaa ila Bei iko juuu nimeipenda punguzen Bei bas
Sim kiukweli iko sawa nimeikubali ila Bei iko juuu punguzen Bei
Bei elekezi
HAPA BEI SI RAFIKI
Simu iko vizuri lakini upande wa kamera bado sana
Bei iko juu xna
ni nzuri lakini mbona zinachelewa kuenea nchi nzima
Ni nzuri
Cm ni nzuri San lkin as upande wa camera uboreshwe
Twambie na sifa za camon 20 pro 5g
Inakuja kiongozi
Hii simu nime ipendaa Sanaa na Nina hamu ya kuinunuaa hii mwezii uki ishaa majaliwa ya moola
Kenye nataka kujua ni huwa wakati ina chkua moto ina kuwa mooto saana hpo kwa kichwa ?
Ni kama sijaelewa swali?
Nahitaj kukop Hy cm
Upo mkoa gani
Simu ni nzuri sana ninayo mimi binafsi sijaona mapungufu yoyote Yale,Kamera ipo vizuri ,kudownload ni fasta
Nazitaka
Simu ni mzuri kwa muonekano wa nje ila ndani mapungufu yapo mengi, punguzeni bei
Kwakwel simu iko poah xana nimeikubali ila bei ipungunzwe.
Punguzeni bei jamani
Tecno iyo kaz waboleshe camera na bei ipungue