Simu ya Google Pixel 5 ni simu ya Android toleo la 11 iliyotoka mwaka 2020
Pamoja na kuingia sokoni miaka miwili iliyopita bado ni simu inayozizidi simu NYINGI za daraja za kati za mwaka 2022
Kitendo kinachofanya bei ya Google Pixel 5 kuzidi shilingi milioni moja kwa Tanzania
Sifa zake zinafikirisha kiasi kama bei yake inastahili kuzidi milioni moja
Ikizingatiwa kuna matoleo mapya yanayoizidi Pixel 5 kwenye nyanja nyingi na ukubwa wa memori
Bei ya Google Pixel 5 ya GB 128 Tanzania
Bei inatofautiana kutokana na hali ya simu
Pixel 5 ya GB 128 ambayo ni used inauzwa kwa shilingi 1,100,000/=
Kwa baadhi ya wauzaji simu unaweza kuipata hata kwa 950,000/=
Kama ilivyoelezwa kwenye utangulizi, simu inapatikana kwa pesa kubwa
Sifa zake zinaweza kukushawishi kuinunua
Ila unaweza ukahairisha kuimiliki kama utazipitia sifa za simu ya xiaomi 12 pro ambayo inaendana bei
Sifa za Google Pixel 5
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | OLED, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.1,128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.0inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,100,000/= |
Ni upi ubora wa simu ya Google Pixel 5
Google Pixel 5 inaweza kuzuia maji kuingia ndani ya simu
Na inatumia kioo chenye kuonyesha vitu kwa ustadi wa juu.
Ni moja ya simu inayoweza kupoekea matoleo mapya ya Android
Ina kimo cha wastani inayofanya simu kuwa nyepesi kubebeka
Ubora mkubwa wa kipekee wa pixel 5 ni kwenye kamera
Ina software inayosaidia simu kutoa picha safi
Utendaji wake ni wa kuridhisha kutokana na aina ya chip inayotumia
Kiuhalisia , ukitazama ubora wa network mpaka software utaona simu ina mapungufu machache.
Fuatilia zaidi
Uwezo wa Network
Pixel 5 ina aina karibu zote za network ikiwemo 5G
Kwa kuwa Tanzania bado hajianza kutumia 5G basi hatutoiangalia bali tutazamia zaidi 4G
Ila sio mbaya ukafahamu: maana ya 5G ni nini
Aina ya 4G iliyonayo ni ya LTE Cat 18 inayopatikana kwenye modem ya X52 ya Qualcomm
Spidi ya juu ya kudownload ya Cat 18 ni 1200Mbps (Ni kubwa)
Ila tia akilini hakuna mtandao wa simu Tanzania unaotoa kasi hii
Japokuwa Google huwa wanalenga nchi zilizoendelea ila simu ina masafa yote ya 4G yaliyopo Tanzania
Ubora wa kioo cha Google Pixel 5
Hii simu inatumia kioo cha OLED
Vioo vya OLED huwa vinasifika kuwa na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi
Ubora wake unachagizwa na kuwa na refresh rate inayofika 90Hz
Refresh rate kubwa huwa inaifanya simu kuwa nyepesi unapokuwa unacheza gemu ama kuperuzi majina au sms
Kioo kinakuwa kinabadirika kwa haraka
Kitu kizuri kingine ni kuwa simu inatumia HDR10+ kitu kinachosaidia kioo kuonyesha vitu vinavyoendana na jinsi vinavoonekana kwenye mazingira.
Resolution yake ya 1080 x 2340 pixels inaongeza ubora mwingine wa kioo
Nguvu ya processor Snapdragon 765G 5G
Katika kitu unachopaswa kukitazama kwa makini unapohitaji kununua simu basi ni processor
Kila kitu unachokifanya kwenye simu kinafanyiwa kazi na processor
Processor ikiwa dhaifu basi jua kuwa una simu mbaya
Pitia : Jinsi ya kujua ubora wa processor ya simu
Google Pixel 5 inatumia processor yenye nguvu ya Snapdragon 765G 5G
App ya geekbench inaipa alama 585 kwenye core moja
Ijapokuwa uwezo wake unazidiwa mbali sana Snapdragon 8 gen 1
Ila inaweza kucheza gemu za kila aina zingine kwa resolution kubwa
Nguvu kubwa inatokana na muundo wa chip ambao una core mbili zenye kubwa zinazoitwa Kryo 475 prime na Gold
Uwezo wa betri na chaji
Uwezo wa simu kukaa na chaji ni wa kuridhisha kiasi fulani
Kwa sababu ikiwa inatumia intaneti mfululizo ukaaji wa moto unadumu kwa masaa 12
Ukaaji wa chaji unachangiwa na ukubwa wa betri kuwa ni 4080mAh
Chaji yake inapeleka umeme wa wastani
Kwani kiasi cha umeme kinachopelekwa na chaji ni wati 18
Google Pixel 5 inaweza kutumika kuchaji kifaa kingine
Ina mfumo unaoitwa Reverse Charging
Hivyo unaweza ukachaji simu nyingine kwa kuunganisha waya kuelekea kwenye simu ya google
Ukubwa na aina ya memori
Pixel 5 ina toleo la aina moja pekee
Toleo hilo lina ukubwa wa GB 128 na RAM GB 8
Pamoja na ukubwa huo wa memori, simu hii ya google imewekewa memori aina ya UFS 2.1
UFS 2.1 husafirisha data kwa kasi kubwa inayofikia 1200MBps
Memori za aina ya eMMC 5.1 husafirisha data kwa kasi ndogo
Aina ya memori za UFS huongeza uwezo wa simu kiutendaji
Uimara wa bodi ya Google Pixel 5
Simu ya Google Pixel 5 imetengenezwa kwa glasi za gorilla 6 upande wa nyuma
Na kwenye screen ina Gorilla 6
Gorilla 6 ni vioo stahimilivu kuvunjika
Simu inaweza isipasuke kama ikianguka kwa kimo cha mita 1.2
Japokuwa hilo linategemeana na vitu vingi
Pixel 5 ni moja ya simu isiyopitisha maji kama ukiizamisha kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa nusu saa
Uthibitisho ni kuwa simu ina viwango vya IP68
Lakini pia ni simu inayotumia laini moja pekee na haina sehemu ya kuweka memori card
Lieke akilini hilo
Ubora wa kamera
Pixel 5 ina kamera mbili aina ya wide(kamera kuu) na ultrawide
Ultrawide hutumika kupig picha eneo pana mfano uwanja wa mpira na kutokea eneo lote kwa nyuzi 117
Baadhi ya picha ambazo hii simu imezipiga kwenye mwanga haifiu zimetokea vizuri
Ukiitazama hii picha utaona kuwa,
Kamera inajitahidi sana kuonyesha rangi sahihi za vitu ambavyo vimetokea
Contrast imejitahidi kuweka mlinganyo sahihi wa rangi
Hata nyakati mchana ustadi wa picha unaonekana kwa usahihi ambao hauthiriwi na mwanga mwingi wa jua
Uzuri wa picha unachangiwa na software ya google camera na ulengaji wa dual pixel pdaf
Simu ina kamera zinazoweza kurekodi video za 4K
Ubora wa Software
Simu inakuja na Android 11
Lakini inapokea toleo jipya la android 12
Ukiwa na simu za google pixel utakuwa unapata android yenyewe halisia
Na pia utaweza kuwa unapokea matoleo mapya mara kwa mara
Kumbuka Google wako vizuri sana kwenye swala la software kuliko hardware
Yapi Madhaifu ya Google Pixel 5
Udhaifu mkubwa ni simu kutokuwa na sehemu ya memori kadi
Kwa nyakati za sasa GB 128 inaweza ikawa ndogo
Maana watu wanahifadhi video na magemu makubwa kiasi cha kwamba simu inaweza ikajaa haraka
Lakini ukiwa unarekodi sana video za 4K memori ya simu inaweza kuwahi kujaa
Simu haina sehemu ya kuweka earphone
Hivyo itakulazimu uwe unatumia earphone za bluetooth
Google Pixel 5 inatumia laini moja
Watanzania wengi hupendelea simu inayokubali laini mbili
Neno la Mwisho
Bei ya Google Pixel 5 inaendana na ubora wa simu kwa kiasi kikubwa
Ila kutokuwepo kwa earphone jack, sehemu ya memori card na kutumia laini moja inaweza ikawa sononesha baadhi ya watumiaji
Mbadala mzuri wa simu hii inaweza ikawa Redmi Note 11 Pro+ 5G
Ila hata Infinix Note 12 VIP inaweza ikafaa japo nayo bei si rafki ukilinganisha na ubora
Maoni 13 kuhusu “Bei ya Simu ya Google Pixel 5 na Sifa Muhimu (2022)”
Iwekeni sehemuya eirpon
Google wamekusikia
Kwa sasa ipi bora kuwa nayo kati ya pixel 5 na samsung s20
samsung s20
Maduka yenu yanapatikana wapi
Hapa TZ
Simu ipi ukikuwa unaulizia
Kioo complete bei gani simu yangu imezingua kiook
Hatuna vioo kiongozi
Nahitahi hii simu google pixle 5 ina bei gan kwa sasa
nataka simu google pixel 5
Nimeipenda ni nzuri camera nyepesi sana umbo lake zuri nk
Sababu la kuto unganisha Wi-fi na Xender ni nini?
Kioo kikiharibika marekebisho ni sh ngapi?