Oppo Reno7 ni simu ya mwaka 2022 yenye mambo mengi ambayo yanaipa ubora unaendana na simu mpya za 2023
Kwa mfano simu ya Tecno Spark 10 Pro ya 2023 inaachwa nyuma na hii simu kwenye baadhi ya vitu.
Hivyo basi bei ya oppo reno7 bado ni kubwa na inazidi laki saba kwa hapa Tanzania
Fuatilia sifa zake zote muhimu utambue ubora wake ambao unaweza kukuvutia kuimiliki hii oppo ya 2022
Bei ya Oppo Reno7 ya GB 128
Reno7 yenye RAM ya GB 8 na ukubwa wa memori wa GB 128 inauzwa shilingi 850,000/=
Bei yake inaizidi simu ya iPhone 7 plus ikiwa used japo kiutendaji iphone ina nguvu kiasi
Hata Oppo inakuja ne teknolojia nyingi ambazo huwezi kuzikuta kwenye matoleo ya simu za zamani
Kuanzia kioo mpaka kamera na hata uimara wa simu kudumu kipindi kirefu, reno7 iko mbele
Kiwango cha bei kinaipelekea hii oppo kuwa mshindani wa Tecno Camon 19
Sifa za Simu ya Oppo Reno7
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 256GB,128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 850,000/= |
Upi ubora wa Oppo Reno8
Kama unajua kuzitafsiri vitu vilivyopo kwenye jedwari, tayari utakuwa ushaelewa maeneo ambayo yana ubora mkubwa kwenye hii simu
Moja wapo ni uwezo wa kupeleka chaji kwa kasi kubwa kitu kinachokupunguzia muda wa kuisubiria simu kujaa
Ina mfumo wa memori wenye kasi kubwa ya kusafirisha data
Kamera zake zinatoa picha zenye ubora
Pia kamera zake zinaweza kukipiga kitu kidogo na kuonekana kikubwa
Inatumia kioo chenye mgawanyiko mpana wa rangi hivyo rangi za vitu vingi vitaonekana kwa uhalisia wake
Uwezo wa Network
Simu inasapoti mpaka mtandao wa 4G
Haina teknolojia 5G japokuwa ni simu ambayo imetoka mwaka 2022
Kwa simu ambazo zilikuwa zinauzwa bei hiyo nyingi huwa zinasapoti mtandao wa 5G
Mfano wa simu hiyo ni Redmi Note 11 5G Pro+
Aina ya 4G ya hii oppo ni LTE Cat 13 ambayo kasi yake ya juu kabisa kwenye kupakua ni 390Mbps sawa na 48MBps
Hii ina maana kama mtandao wa simu unatoa kasi hii ya 4G basi simu inaweza kudownload app ya whatsapp kwa sekunde mbili tu.
Kasi hii kwa hapa Tanzania unaweza kuipata kwenye mtandao wa faiba na kwa gharama
Ila kwa mitandao ya simu za mikononi ni ngumu
Ubora wa kioo cha Oppo Reno7
Reno7 ina kioo cha AMOLED ambavyo huwa na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi
Kioo chake kina resolution kubwa ya 1080 x 2400 pixels
Yaani kama unatazama picha na video kwenye mitandao ya kijamii muonekano wa vitu unakuwa na ustadi mzuri
Kioo pia kina refresh rate inayofika 90Hz hivyo unapotachi kioo simu inakuwa nyepesi
Reno7 inaruhusu kuzima refresh rate ya 90Hz maana ikiwa kubwa na matumizi ya chaji yanaongezeka pia
Kiwango cha juu cha unagavu wa hiki kioo ni 800 nits
Ina maana kuwa kioo kitaonyesha vitu kwa uwazi na vizuri ukiwa unaitumia simu kwenye jua
Unajua kuwa ukiwa juani skrini huwa hainekani vizuri kama uangavu wa kioo cha simu ni mdogo
Kitu utakachokikosa kwenye kioo cha reno7 ni HDR10 au Dolby Vision
Nguvu ya processor Snapdragon 680 4G
Chip ya Snapdragon 680 4G ni chip ya daraja la kati hivyo nguvu ya utendaji wa simu ni ya wastani
Simu haiwezi sumbua kuwa nzito hata kama mafaili yamejaa kwa sababu processor yake ina muundo wenye core kama Cortex A73(Kryo 265 Gold)
Uzuri wa hii chip ina ulaji mdogo wa chaji ambao unachangiwa kuwa na utendaji wa kiwango cha kati
Kwenye uchezaji wa magemu itakulazimu useti resolution ndogo ya graphics(picha za gemu) ili ucheze vizuri na kupunguza simu kupata moto mara kwa mara
Magemu makubwa mengi yanacheza vizuri kwenye hii simu kwa kiwango cha 58fps kwenye resolution ndogo
Tofauti na hapo ni ngumu kupata fremu nyingi
Hii processor ina sehemu(core) zingine zipatazo nne ambazo ni kwa ajili
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya oppo reno7 ina kasi ya wati 33
Ni kiwango kikubwa cha umeme na simu inajaa chini ya masaa mawili
Kwenye majaribio ya GSMArena, betri ya reno7 ilichuukua dakika 70 tu kujaa kutoka 0% mpaka 100%
Kwa mtu mwenye haraka hatosubiri muda mrefu
Pamoja na kwamba kiwango cha betri sio kikubwa (4500mAh) ukilinganisha na simu ya redmi note 10;;;, reno7 inakaa na chaji masaa mengi zaidi
Ukiwa unatumia intaneti muda wote simu inachukua masaa 16 mpaka chaji kuisha
Na ukiwa unacheza magemu wakati wote, betri inachukua masaa 11 mpaka kuisha chaji
Ukubwa na aina ya memori
Upande wa memori kuna matoleo mawili ya Oppo Reno7 na yote yana GB 8
Kuna yenye ukubwa wa GB 128 na GB 256 ambazo zinatofautiana bei
Hata hivyo hiki ni kiwango kikubwa kwa watumiaji wengi ila kwa mtumiaji sana wa simu hiki ni kiwango kidogo
Kwa maana utalazimika kuongeza memori kadi kwani inayo sehemu ya memori kadi
Aina ya memori simu inayotumia ni UFS 2.2 ambayo ina njia mbili na kila njia inaweza kusafirisha data mpaka 1200MBps
Ni ngumu kukuta simu inakuwa nzito sababu ya kujaa mafaili
Uimara wa bodi ya Oppo Reno7
Uzuri wa simu nyingi za oppo ni kuwekea ulinzi wa kuzuia angalau vumbi na maji ya kiwango cha kunyunyiza
Kwani ina viwango vya IPX4, ila haifai kuizamisha kwenye maji haina uwezo wa kuzuia maji kupenya kama ikizama
Upande wa mbele simu imewekewa skrini protekta ya kioo cha Gorilla 5
Kioo cha gorilla 5 kinaweza kuzuia mpasuko kama simu ikianguka kwa kimo cha mita 1.5
Hata hivyo unapaswa kuwa makini japo gorilla inakuhakikishia ulinzi
Hii simu ina fingerprint kwenye kioo sio upande wa nyuma
Fingerprint yake iko fasta pamoja na kuwa kwenye skrini kuna kioo kigumu
Ubora wa kamera
Oppo Reno7 ina kamera tatu aina ya wide, microscope na depth sensor
Ila kiuhalisia ni kamera mbili tu ndio zinapiga picha kamera ya depth sio kwa ajili ya kupiga picha
Kamera ya microscope yenye 2MP imeundwa kwa ajili ya kupiga picha vitu ambavyo ni vidogo sana kama sisimizi
Hii kamera inakikuza hiko kitu na kuonekana kikubwa
Kamera kuu ina upigaji wa picha mzuri ila kuna kukolea kwa rangi usiondana na muonekano halisi
Kama mtu mwenye rangi nyeusi kama ilivyo kwa waafrika wengi kamera inamg’arisha
Kwa watu wa mitandao wanaopost picha instagram hii inaweza kuwafaa zaidi
Upande wa video simu inaweza kurekodi video za full hd pekee yake kwa fremu 30
Kamera ina gyro-EIS inayomaanisha utulivu wakati wa kurekodi huku ukiwa unatembea
Ubora wa Software
Oppo Reno7 inakuja na Android 12 pamoja na CorolOs 12.1
ColorOS 12.1 inakupa uwezo wa kubadirisha muonekano wa picha(icon) za app
Pia inakupa uwezo wa kubadirisha kiwango cha refresh rate kutoka 90Hz kwenda 60Hz na kinyume chake
Kingine ni kuwa simu inapokea updates za mfumo wa ColorOS mara kwa mara
Hii inakuhakikishia kuwa utaendelea kupata maboresho ya app mbalimbali kwa muda mrefu
Washindani wa Oppo Reno7
Bei ya Oppo Reno7 inaweza kuleta utata hasa unapokuja kufahamu matoleo mengine yanayouzwa kwa bei hiyo
Matoleo ambayo yanaweza kuipa hii simu changamoto ni Redmi Note 11 Pro+ 5G, Redmi Note 10, Realme 9 Pro+, Samsung Galaxy A53 5G
Ukianza na samsung kwanza ina 5G na ni simu yenye nguvu kubwa kiutendaji na haipitishi maji simu ikiiingia kwenye maji
Ukija kwa Redmi Note 11 Pro+ 5G ina kioo kikali cha amoled na HDR10 na refresh rate 120Hz pia kamera inayoweza kurekodi video mpaka za 4K
Mbaya zaidi redmi inapatikana kwa chini ya laki nane kwa mwaka 2023
Upande wa Realme 9 Pro+ inaendana kidogo na Reno7 ila Realme ni nzuri zaidi hasa upande wa kamera na utendaji na ina 5G vilevile
Realme 9 Pro+ na yenyewe inauzwa laki nane na nusu
Neno la Mwisho
Kama washindani wa hii simu hawakuvutii basi oppo reno7 bei yake itakuvuta kuimiliki
Ni simu inayokuhakikishia maisha marefu ya betri na ukaaji wa chaji wa muda kwa utendaji wa wastani
Kwa mtumiaji wa simu mwenye matumizi ya wastani oppo reno 7 ni chaguo zuri
Wazo moja kuhusu “Bei ya Oppo Reno7 na Sifa Muhimu 2023”
Naitaji kubadilisha kioo cha oppo reno 7