SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Infinix Note 30 Pro na Ubora Wake

Simu Mpya

Sihaba Mikole

June 10, 2023

Infinix Note 30 Pro ni simu mpya ya infinix ambayo imetoka mwezi wa tano 2023

Imetoka pamoja ni toleo la infinix note 30

Tofauti ya infinix mbili hizi upo kwenye kioo, kamera na teknolojia ya kwenye chaji

infinix note 30 pro showcase

Kwa maana infinix note 30 pro ina vitu vya ziada ila kiutendaji simu zinaendana

Ndio maana bei ya infinix note 30 pro kwa Tanzania inazidi shilingi laki sita na nusu kutegemeana na ukubwa wa memori

Bei ya Infinix Note 30 Pro ya GB 256

Infinix note 30 pro yenye ukubwa wa GB 256 inauzwa shilingi laki saba (700,000)

Kuna gepu kama la laki moja ukilinganisha na infinix note 30

Utofauti huu unachangiwa na teknojia zilizopo kwenye simu

infinix note 30 pro summary

Kwa mara ya kwanza kwenye infinix utaweza kuchaji bila kutumia waya

Na chaji ya waya pia inatumia pia inawahi kujaza betri kwa muda mchache

Kwa sababu chaji yake ni mara mbili ya chaji inayotumiwa na Redmi Note 12

Utaelewa zaidi baada ya kupitia sifa zake kwenye vipengele vyote

Sifa za Infinix Note 30 Pro

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – MediaTek Helio G99
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.2 GHz Cortex-A76
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G57 MC2
Display(Kioo) AMOLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 13
  • XOS 13
Memori UFS 2.2, 128GB, 256GB na RAM 8GB
Kamera Kamera tatu

  1. 108MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(depth)
  3. QVGA
Muundo Urefu-6.78inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-68W
Bei ya simu(TSH) 700,000/=

Upi ubora wa Infinix Note 30 Pro

Simu ina utendaji wa kuridhisha unaoweza kufungua vitu vingi bila tatizo

Ina kamera yenye megapixel kubwa hivyo ukusanyaji wa data ni mzuri

Chaji inapeleka umeme mwingi unaojaza betri kwa haraka

Mfumo wake wa chaji unaweza kuchaji vifaa vingine

Kioo chake ni kizuri chenye uonyeshaji wa rangi ulio sahihi kwa kiwango kikubwa

Simu inakuja na viwango vya IP53 vyenye kuonyesha uwezo wa kuzuia vumbi na maji yanayochirizika kidogo

Hata 4G yake ni ile yenye kasi kubwa ya kupakua vitu

Uwezo wa Network

Infinix Note 30 Pro inasapoti mpaka mtandao wa 4G kama kiwango cha juu kabiasa

Yenyewe haina 5G kama ilivyo kwa infinix Note 30 5G

Hata hivyo 4G yake ina kasi ya juu inayofika 650Mbps kwa maana ni 4G aina ya LTE Cat 13

Ila weka akilini kwa sasa hapa Tanzania si rahisi kupata kasi kutoka kwenye mitandao ya simu

Utaweza kutumia 4G kwa kutumia mtandao wowote

Kwani ina masafa yapatayo 15 yakiwemo yale yanayotumiwa na mitandao ya simu nchini

Ubora wa kioo cha Infinix Note 30 Pro

Infinix hii inatumia kioo cha AMOLED ambacho kina resolution ya 1080 x 2460 pixels

Ubora wa kuonyesha rangi halisi za vitu ni wa kiwango cha juu ukilinganisha na simu zinazotumia vioo vya IPS LCD

Ndio maana simu zenye vioo vya amoled vikiaribika bei zake huwa ni kubwa

infinix note 30 pro display

Moja ya kitu kinachofurahisha ni kuwa uangavu wake ni mkubwa unafika nits 900

Kwa maana hutohitaji kwenda kivulini kuangalia skrini ya simu yako unapokuwa juani

Na kitu kingine kizuri ni uwepo wa refresh rate inayofika 120Hz

Yaani ukiwa unagusa kioo simu inakuwa fasta na muonekano unaobadirika wa kuvutia

Nguvu ya processor Mediatek Helio G99

Infinix Note 30 pro inatumia processor ya mediatek helio g99

Imegawanyika katika sehemu mbili ambapo sehemu yenye nguvukubwa sana ina idadi ya core zipatazo mbili

Na zinatumia muundo wa Cortex A76 ambayo utendaji ni wa wastani na wa kuridhisha

infinix note 30 pro processor

Magemu mengi yanaweza kucheza vizuri

Ila itakulazimu uweke settings za picha ziwe saizi ya kati kwa ajili ya kucheza bila kukwama kwama

Ulaji wa betri sio mkubwa kutokana na chip kuwa  na utendaji wa wastani

Hivyo maisha ya betri ni ya muda mrefu

Uwezo wa betri na chaji

Kwenye eneo la kuuzia simu ya toleo la infinix note 30 pro ni eneo la chaji

Inakuja na chaji yenye wati 68 inayojaza betri lake la 5000mAh  kwa 80% kwa muda wa dakika 30

Unaweza kuitumia hii simu kama power bank

Ina teknolojia ya “Reverse Charging”, kwa maana inaweza kuchaji vifaa vingine japo kwa kasi ndogo

infinix note 30 pro chaji

Kubwa zaidi simu ina teknolojia ya “Wireless Charge”

Yaani uaweza kuichaji bila kutumia waya wa kuchaji na kasi yake ni 15W

Njia hii inahusisha kuigusisha simu na kifaa maalumu ambacho kinapitisha chaji

Ukilinganisha bei yake ni vitu vilivyopo vinafanya simu kuwa ya kiushindani sana

Ukubwa na aina ya memori

Simu inatumia memori aina ya UFS 2.2 ambayo kasi yake kusafirisha data inafika 1200MBps

Na kuna matoleo mawili tu upande wa memori

Unaweza ipata ya GB 128 au GB 256 na zote zikiwa na RAM ya GB 8

Unaweza kuongeza kiwango cha RAM kwa ukubwa wa GB 8

Ni vizuri kuwa na ram kubwa kwa kuwa android hutumia kiwango kikubwa ch ram hasa wakati wa kucheza gemu

Uimara wa bodi ya Infinix Note 30 Pro

Bodi ya infinix note 30 pro ni imara kwa kiasi fulani

Ina viwango vya IP53 vinavyoashiria uwezo wa kuzuia vumbi na maji ya kiwango cha kuchuruzika

Upande wa mbele na nyuma simu imewekewa glasi

Hivyo hutokuwa na wazi wa simu kupiteza ubora wa rangi

Kwa pembeni ndio kuna plastiki na pia ina fingerprint upande wa pembeni pia

Ubora wa kamera

Simu ina jumla ya kamera zipatazo tatu

Ila kiuhalisia ni kuwa simu ina kamera moja tu yenye ubora

infinix note 30 pro camera

Kamera aina ya QVGA ni kamera za zamani ambazo resolution zake ni ndogo sana kwa viwango vya sasa

Fahamu: maana ya qvga kiundani

Wakati kamera aina ya depth huwa haipigi picha bali ni kwa ajili ya kufanya vipimo

Ubora wa picha kwenye kamera kubwa ni mzuri kwa nyakati zote

infinix note 30 pro camera 1

Kwenye mwanga mdogo na mwingi vitu vinaonekana kwa ustadi

Simu inaweza kurekodi video za full hd pekee na sio 4K kama ilivyo kwa Tecno Camon 20 Premier

Ubora wa Software

Hii simujanja inakuja na Android 13 na XOS 13 kama ilivyo kwa note 30 kavu

Simu inakuja na vitu vingi na app nyingi

Zipo unazoweza kuzitoa na nyingine hutoweza bali utazizima kama huzihitaji

infinix note 30 pro software

Moja ya kitu utakachokutana nacho ni charge bypass

Charge bypassing inagawanya kiwango cha chaji wakati simu ikiwa inatumika huku ukiwa unachaji

Yaani inachukua 70% inaipeleka kwenye betri na 30% kwenye matumizi ya simu

Washindani wa Infinix Note 30 Pro

Kwenye simu hii washindani ndio watakuwa na shida

Pamoja na kuwa na utendaji wa wastani ila ni ngumu kupata simu yenye wireless charge kwa bei hii

Hata hivyo Tecno Camon 20 Pro, Redmi Note 12 Pro, Oppo A78 na Samsung Galaxy 54 ni matoleo yanayoweza mfanya mnunuaji kuacha infinix

Yana utendaji mkubwa na vitu vingine ambavyo unaviona kwenye hii infinix

Neno la Mwisho

Matoleo ya Note upande wa infinix yanaifanya infinix kuwa ni moja makampuni ya simu yanaunda simu nzuri za daraja la kati

Bei yake iko kiushindani ukizingatia maboresho yaliyopo kwenye chaji

Maoni 20 kuhusu “Bei ya Infinix Note 30 Pro na Ubora Wake

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

infinix note 30 vip thumbnail

Bei ya Infinix Note 30 VIP na Sifa Zake

Infinix kwa mwaka 2023 wameachia matoleo mengi yakiwemo ya note series Moja ya toleo hilo ni Infinix Note 30 VIP ambayo imetoka mwezi Juni Haina tofauti sana na infinix note […]

infinix zero 30 5g thumbnail

Ubora na Bei ya Infinix Zero 30 5G (Infinix Kali)

Ni infinix kwa mara nyingine inajaribu kutengeneza hisia chanya juu ya ubora wa simu zao Unaweza kuliona hili kwa toleo jipya la Infinix Zero 30 5G Hii ni simu kali […]

iphone 15 pro thumbnail

Bei ya iPhone 15 Pro na Sifa Zake Muhimu

Kama ilivyotarajiwa hapo awali kuhusu ujio wa simu mpya za iphone kwa mwaka huu 2023 Moja ya simu hiyo ni iPhone 15 Pro ambayo imeongezewa utendaji Kiumuonekano hauwezi kutofautisha sana […]

iphone feki 2

Simu Origino ni Zipi na Unazitambuaje? (Hatua za kufuata)

Matoleo ya simu yamekuwa yakitoka mara kwa mara yakiwemo yenye bei kubwa na zinazotamaniwa na watu wengi Aina hizi ya simu huvutia watu wasio waaminifu kutengeneza simu feki zenye ufanano […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company