Simu ya infinix hot 10 play ni simu ya android 11 iliyotoka mwaka 2021
Bado bei ya infinix hot 10 play inazidi shilingi laki tatu mpaka sasa kwa maduka mengi ya simu kariakoo na kinondoni
Ukizifahamu sifa za hot 10 play na simu mbadala utaona kuwa ni simu yenye bei kubwa.
Kwenye posti hii kuna taarifa ya bei na ufafanuzi wa simu kiundani
Ni vizuri kufahamu bei yake na sifa ya simu kabla ya kutoa pesa kuipata simu
Bei ya Infinix Hot 10 Play Tanzania
Kwa maduka ya simu ya kariakoo bei ya infinix hot 10 play ya ukubwa wa GB 64 ni shilingi 340,000/=
Unaweza ukaipata simu hii chini ya bei hiyo
Bei yake ni kubwa hapa nchini kwani kwa masoko ya India simu inauzwa chini ya laki tatu
Sifa za simu ya Infinix Hot 10 Play
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 64GB, 32GB na RAM 2GB,4GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.82inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 340,000/= |
Upi ubora wa infinix hot 10 play
Ubora wa infinix hiot 10 play unapatikana kwa kiasi kikubwa kwenye upande wa betri
Betri yake ni inayoifanya simu kukaa na chaji muda mrefu
Ukiongeza na utendaji mdogo wa simu chaji yake itachelewa kuisha
Pia simu ni ndefu na inavutia kwa macho
Ila upande wa sifa zingine simu inakumbana na changamoto
Kiasi cha kwamba inakumbana na ugumu kupambana na simu kama ya samsung galaxy a03s
Zifuatatlie sifa na ufafanuzi wa kila sifa kisha uone utofauti na simu zingine za laki tatu
Uwezo wa Network
Infinix hot 10 play ni simu ya 4g aina ya LTE Cat 7 na LTE Cat 4
Spidi ya LTE Cat 7 inaweza kudownload faili la ukubwa wa 1.2GB kwa sekunde zipatazo 40
Ila inategemea na spidi ya mtandao simu inayotumia
Simu inakubali network bands za mitandao yote ya simu nchini Tanzanina
Hivyo hakuna laini ya 4G itakayoshindwa kufanya kazi kwa hapa nchini
Ubora wa kioo cha infinix hot 10 play
Kioo cha infinix hot 10 play kina ubora mdogo kwa sababu ni cha IPS LCD na resolution ndogo ya 720 x 1640 pixels
Ni ngumu sana kulinganisha ubora wake wa kioo na kioo cha iphone yoyote ya bei nafuu
Uangavu wa kioo ni wa kiwango cha chini.
Hivyo simu inaweza isioneshe vizuri ukiwa unaitumia kwenye jua kali
Kiujumla ubora vioo vya IPS LCD unazidiwa na kioo cha super amoled hasa kwenye kuonesha rangi nyingi
Mfano tu ni muonekano wa rangi nyeusi
Nguvu ya processor MediaTek Helio G25
Processor ya mediatek helio g25 ina core nane.
Ndio processor ambayo hot 10 play inaitumia katika kazi zake
Lakini utendaji wa chip ni wa chini.
Kwenye app ya geekbench inayopima nguvu ya processor ya simu, Helio G25 ina alama 135
Hivyo simu inapata shida kucheza gemu nyingi za simu kama Fortnite
Kwa nini Helio G25 ina nguvu ndogo?
Kwa sababu inatumia core aina ya Cortex A53 pekee
Kikawaida muundo wa cortex a53 unatumia nguvu ndogo na matumizi ya umeme huwa ni madogo pia
Chip nyingi za simu zenye nguvu huchanganya aina ya core
Kama hufahamu aina ya core zenye nguvu, pitia makala hii ya aina mbalimbali ya processor za simu
Uwezo wa betri na chaji
Infinix hot 10 play ni moja ya simu za android zinazokaa na chaji muda mrefu.
Ina betri lenye ukubwa wa 6000mAh
Kuzingatia nguvu ndogo ya chip, hii simu inaweza kukaa na moto mrefu kuliko simu nyingi za android
Pia zingatia betri ikiwa kubwa simu inachukua masaa mengi kujaa hasa kama hakuna fast chaji
Chaji ya infinix hot 10 play inapeleka umeme kidogo
Hivyo betri inaweza chukua zaidi ya masaa matatu kujaa
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo mawili tu ya hot 10 play kwenye upande wa memori
Unaweza kukutana na infinix ya 32 GB na infinix ya 64 GB.
Infinix ya memori kubwa inakuwezesha kuhifadhi vitu vingi
Ila memori zake hazina kasi kubwa ya kusafirisha data
Kitu ambacho kinaweza kufanya simu kufungua baadhi ya app taratibu
Uimara wa bodi ya infinix hot 10 play
Hii ni simu ya daraja la chini
Kama ilivyo simu nyingi za aina hii, hot 10 play ina plastiki upande wa nyuma na pembeni
Bodi za plastiki ni za bei nafuu na uimara wake huwa sio mkubwa
Hivyo mtumiaji wa simu analazimika kuweka kava na protector
Ili kuimarisha uimara wa simu hasa inapoanguka kwa kimo kirefu.
Kama unapenda simu ndefu infinix hot 10 play inakupa unachokipenda
Ubora wa kamera
Kamera za hot 10 play hazina ubora mzuri.
Kwa maana haitumii teknolojia ya ulengaji yenye usahihi mkubwa kutambua kinachopigwa kwa haraka
Kwani infinix hii ina autofocus aina ya AF ambayo ni ya kizamani
Kamera nyingine ni ya QVGA ambayo huwa na resolution ndogo hivyo utoaji wa picha ni mbaya
Kamera zake zinarekodi video za aina moja tu za full hd kwa spidi ya 30fps
Ubora wa Software
Hot 10 Play ni simu ya android 10 toleo la Go Edition
Go Edition ni aina ya android maalumu kwa simu zenye utendaji mdogo
Hivyo ni mfumo endeshi unaokuja na app za muhimu kwa matumizi ya kila siku
Go Edition inaongeza ufanisi wa simu kiasi fulani kama uwezo wake ni mdogo
Yapi Madhaifu ya infinix hot 10 play
Mfumo wake kamera hauwezi kutoa picha na video nzuri
Kwani Infinix hawajaweka autofocus nzuri angalau ya PDAF
Kioo chake kina resolution ndogo iliyokinyume na viwango vya sasa
Simu haina ulinzi madhubuti wa kuifanya kudumu muda mrefu bila kupoteza uzuri wa bodi ya simu
Inatumia aina ya memori zenye kusafirisha data kwa kasi ndogo
Kubwa zaidi ina processor yenye nguvu ndogo.
Hivyo si simu nzuri kwa mtumiaji mwenye matumizi mengi
Neno la Mwisho
Bei ya Infinix hot 10 play haiendani na sifa zake
Kuna simu nzuri za laki tatu za oppo na redmi ambazo uwezo wake ni wa kuridhisha
Zifuatilie hapa, simu za oppo za bei rahisi
Lakini kama ni shabiki wa simu za infinix basi simu inafaa kuwa nayo
Itakuwa jambo zuri kama utaipata simu kwa chini ya laki tatu