Hii ni orodha ya simu kumi za nokia na bei zake nchini Tanzania.
Ni nokia za mwaka 2020, 2021 na mpya kabisa za 2022
Utaziona nokia za ubora wa juu, wa kati na wa chini kwenye utendaji wa processor, kamera, betri na network bila kusahau aina ya kioo na memori
Ukipitia sifa za simu zote kumi za nokia utaweza kujua nokia sahihi inayokizi mahitaji yako.
Simu za nokia zilizopo
Simu ya Nokia G21
Simu ya nokia g21 imetoka mnamo februari 2022.
Kioo cha nokia g21 kina refresh kubwa ya 90Hz inayoifanya simu kuwa nyepesi.
Simu inatumia processor aina ya Unisoc T606 yenye utendaji mkubwa wa kuweza kucheza magemu kama dream soccer kiurahisi
Memori zake hazina kasi kubwa kwani ni aina ya eMMC 5.1
Simu inakubali mtandao wa 4G na bands zake zinakubali mitando yote ya simu Tanzania
Zipo nokia g21 za GB 64 na ram ya GB 3 au GB 4,pia GB 128 na ram ya GB 4 au GB 6
Ni simu ya macho matatu yenye kamera za ubora wa kawauda
Bei ya Nokia G21
Bei ya nokia g21 ya ukubwa wa gb 128 na ram gb 4 ni shilingi 486,688.27/=
Hii ni bei ya soko la india.
Kwa maduka mengi ya simu ya kariakoo bei inaweza kuzidi laki tano
Simu ya Nokia C21 Plus
Nokia C21 plus ni simu ya daraja la mwisho ambayo imetoka mnamo februari 2022.
Simu ina utendaji mdogo kiasi cha kutumia umeme mdogo.
Betri yake ina ukubwa wa 5050mAh ambalo linachukua muda mrefu kuisha chaji
Na aina ya memori yake inasafirisha data kwa spidi ndogo kwani inatumia eMMC 5.1
Kioo chake kina resolution yenye pixels chache (720 x 1600)
Nokia c21 plus ina kamera mbili ambazo zinatumia autofocus ya kizamani
Simu ya nokia c21 plus zipo za aina nne, ambazo ni 32GB na RAM ya 2GB au 3GB, na nyingine ni 64GB na RAM ya 3GB au 4GB
Bei ya Nokia c21 plus
Bei ya nokia c21 plus kwa masoko ya nje inafika shilingi 306,936/=
Bei itaongezeka zaidi kama utanunua c21 plus ya GB 64
Simu ya Nokia 6.1 Plus
Nokia 6.1 Plus ni simu ya mwaka 2018
Imetokea kwenye orodha kwa sababu nokia 6.1 plus inaweza kupokea tolea la android la mwaka 2020
Hivyo ni simu nzuri kwa nyakati za sasa pia
Ina memori zenye ukubwa wa GB 32 na GB 64, ukubwa wa ram ni 4GB na 6GB
Ni simu ngumu na inatumia kioo cha ips lcd.
Utendaji wake ni wa wastani kwa sababu ya kutumika kwa kwa chip ya snapdragon 636
Kamera zake zinaweza kurekodi mpaka video za 4k, na betri lake sio kubwa
Saizi yake ni 3060mAh
Bei ya Nokia 6.1 Plus
Bei ya nokia 6.1 plus ya gb 64 inafika shilingi 372,000/=
Ni bei halisi kwa nchi zingine duniani.
Kwa Tanzania bei inaweza kuzidi kwani Nokia 6.1 ya gb 64 inauzwa shilingi 300,000/=
Simu ya Nokia XR20
Simu ya nokia xr20 ni nokia ya 5G yenye kamera mbili upande wa nyuma
Simu ina network bands za 4g nyingi
Ni simu ambayo haipitishi maji kutokana na kuwa na IP68
Kioo chake ni angavu na kina resolution kubwa ya 1080×2400 pixels
Ni nokia inayokubali toleo jipya la android 12 japokuwa ni simu ya 2021
Japo ni simu ya 5G ila utendaji wake ni wa wastani
Hii inasababishwa na kuwa na processor ya daraja la chini ya Snapdragon 480 5G
Nokia xr20 inalindwa na kioo kigumu kuvunjika aina ya gorilla victus
Bei ya Nokia XR20
Bei ya nokia xr20 ya gb 64 ni shilingi 1,476,792.00/=
Na yenye gb 128 inauzwa shilingi 1,625,400.00/=
Ukubwa wa bei unasababishwa na uimara wa simu katika vipengele vingi
Simu ya Nokia G11
Simu ya nokia g11 ni simu mpya ambayo imetoka machi 2022
Ni simu ambayo ina utendaji wa wastani kutokana na kuwa na processor ya daraja la kati
Processor yake ni Unisoc T606
Betri lake ni kubwa kwani ujazo wake ni 5050mAh, na chaji yake inapeleka umeme wa wastani
Kioo cha nokia g11 ni cha ips lcd chenye resolution ndogo ya pixels 720×1600
Nokia g11 ina matoleo mawili kwenye upande wa memori
Ipo ya gb 32 na gb 64 na ram za 3GB na 4GB
Bei ya Nokia G11
Bei ya nokia g11 ya GB 32 inafika shilingi 600,000/=
Bei inaweza zidi 650,000/= kwa nokia g11 ya gb 64
Simu ya Nokia X100
Nokia x100 ni simu ya macho manne ambayo imetoka mwaka 2021
Kamera zake zina ubora wa wastani
Kioo chake cha ips lcd kina resolution kubwa inayofikia 1080×2400
Ni simu ya 5g na 4g yake inakubali karibu mitandao yote ya simu Tanzania
Inatumia processor yenye nguvu ya wastani ya Snapdragon 480 5G
Kuna toleo la aina moja tu la nokia x100 upande wa memori.
Memori yake ina ukubwa wa GB 128 na RAM GB 6
Bei ya Nokia x100
Unaweza ipata nokia x100 ebay kwa bei shilingi 417,960.00/=
Hii ni bei ya nokia x100 ya gb 128
Bei inayoifanya kuwa moja simu ya 5g ya bei nafuu
Simu ya Nokia G20
Nokia G20 ni simu ya mwaka 2021 yenye android toleo la 11
Kwenye memori, G20 ina matoleo mawili pekee
Kuna ya ukubwa wa GB 64 na 128GB na RAM ya 4GB
Utendaji wa simu si mkubwa kutokana na kutumia chip ya daraja la chini ya MediaTek Helio G35
Ni simu ya macho manne yenye kamera za ubora wa wastani
Kioo chake cha IPS LCD kina resolution ndogo ya pixels 720×1600
Betri yake ni kubwa inayoweza kukaa na chaji muda mwingi
Ukubwa wa betri ni 5050mAh
Bei ya nokia g20
Bei ya nokia g20 inafika shilingi 365,039.02/=
Hii ni kwa g20 ya GB 64.
Hivyo bei ya simu ya nokia g20 ya 128GB inaweza kuvuka shilingi laki nne
Simu ya Nokia G50
Simu ya nokia g50 ilizinduliwa mwishoni mwa 2021.
Hii ni simu ya 5G inayotumia processor yenye nguvu ya wastani kiutendaji ya Snapdragon 480 5G
Simu ina bands nyingi za 4G zinazokubali mitandao ya simu yote hapa Tanzania
Ina memori za ukubwa wa GB 64 na GB 128, na Ram za 4G na 5gb
Chaji yake inapeleka umeme kwa spidi ndogo itakayojaza betri lake kubwa la 5000mAh masaa zaidi ya matatu.
Ila ni nokia inayokaa na chaji muda mrefu
Bei ya Nokia G50
Bei ya nokia g50 ya ukubwa wa GB 128 inauzwa shilingi 673,380.00/=
Kwa toleo la GB 64 linaweza kuuzwa chini ya 620,000/=
Bei yake ina unafuu ukilinganisha na nokia xr20
Simu ya Nokia X20
Simu ya nokia x20 ni simu ya 5G yenye ram kubwa zinazofikia gb 6 na gb 8
Kiutendaji inafanana na nokia g20
Ni simu ya mwaka 2021 inayoweza kupokea toleo jipya la android 12
Memori yake ina ukubwa wa 128GB unaoweza kuhifadhi vitu vingi
Kioo chake kina uangavu wa wastani na resolution kubwa ya 1080×2400 pixels
Betri yake si kubwa sana kwani lina 4470mAh na chaji yake inapeleka umeme wa wati 18.
Hii ni simu ya macho manne yenye kamera inayoweza kupiga picha eneo pana sana
Bei ya nokia x20
Bei ya nokia x20 inashangaza kwani inafika shilingi 808,056.00/=
Nadhani bei kubwa inasababishwa na simu kutumia network ya 5G yenye bands nyingi
Na simu kupokea matoleo mapya ya android mara kwa mara
Simu ya Nokia C21
Nokia C21 ni simu mpya inayotarajiwa kuzinduliwa mwezi wa nne 2022
Hakuna tetesi zinazozungumzia bei ya nokia c21.
Hivyo hatutaingalia kiundani mpaka uzinduzi rasmi utakapokuja
Maoni 3 kuhusu “Simu za Nokia na Bei Zake 2022”
Nahitaji kujua office zenu
NOKIA 8000 4G Ni ya kampuni yenu?
Sijakuelewa. Ila Sisi sio na wala hatuhusiki Kwa vyovyote na kampuni ya nokia