SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ujio wa Simu mpya za Tecno Camon 40

Simu Mpya

Sihaba Mikole

March 15, 2025

Huu mwezi wa tatu 2025 tecno imetangaza ujio wa matoleo mapya ya Tecno Camon 40

Simu hizo ni

  1. Tecno Camon 40
  2. Tecno Camon 40 Pro 5G
  3. Tecno Camon Pro
  4. Tecno Camon 40 Premier

Kwenye hii post utafahamu baadhi ya sifa za muhimu za kila tecno

Na tecno kali zaidi kati ya zilizotangazwa

Tuzame kiundani na kwa kifupi sana.

Tecno Camon 40

Tecno Camon 40 inakuja na mfumo endeshi wa Android 15

Utendaji wake ni wa wastani kwa sababu inatumia processor ya Mediatek Helio G100 Ultimate

camon 40

Inakuja na memori ya GB 128 na GB 256 na RAM ya GB 8 ama 12

Betri yake kubwa ina mAh 5200

Pia ina kamera mbili kubwa ikiwa na megapixel 50

Tecno Camon 40 Pro 5G

Kioo cha Tecno Camon 40 Pro 5G kina refresh rate ya 144hz ambazo huwa ni smooth

Hii ni tecno iliyowekwa waterproof aina ya IP68 ambayo inaashilia maji hayatoingia kwenye simu ikizama kwenye kina ch mita 2

camon 40 pro 5g

Upande wa kamera, zipo kamera mbili moja ya 8MP na nyingine ya 50MP

Ukubwa wa memori ni GB 256 ila RAM unaweza pata ya GB 8 na GB 12

Kasi yake ya kuchaji ni 45W na betri ukubwa wake ni 5200mAh

Utendaji wake ni wa wastani kwa sababu ya utumiaji wa chip ya Dimensity 7300

Tecno Camon 40 Pro

Tecno Camon 40 Pro ni simu ya daraja la kati

Utendaji wake ni wa wastani kwani processor yake ni Helio G100 Ultimate

Kioo chake ni cha amoled chenye refresh rate ya 120Hz

camon 40 pro

Kasi yake ya kuchaji ni 45W na betri yake ina 5200mAh

Ukubwa wa memori ni wa aina moja ambayo ni GB 256 NA RAM ya GB 8

Ina kamera mbili pekee ambapo kamera kubwa imewezeshwa OIS

OIS hufanya kamera kutulia wakati ukiwa unarekodi video huku unatembea

Tecno Camon 40 Premier

Tecno Camon 40 Premier ndio tecno bora zaidi kati ya zilizotangazwa

Ina kamera tatu na zote ukubwa wake ni 50MP

Kamera ya Periscope Telephoto inasapoti ya optical zoom inayoweza ku-zoom mara tatu

Chaji yake inapeleka umeme wa wati 70 na betri lake lina ukubwa wa 5100mAh

Kioo chake ni cha LTPO AMOLED chenye refresh rate ya 144Hz

Na yenyewe ina waterproof ya IP68

 

Maoni 4 kuhusu “Ujio wa Simu mpya za Tecno Camon 40

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

Bei ya Infinix Smart 20 na Sifa Zilizoongezwa

Kiuhalisia Infinix Smart 20 ni simu moja na Infinix Smart 10 Sifa karibu zote zinafanana ila utofauti upo maneneo matatu Hizi tofauti zinaweza kuonekana kuwa ndogo lakini zinaweza leta upekee […]

Hizi ndizo Simu 100 za Bei Ndogo Kabisa (ipi kali zaidi?)

Una bajeti ndogo na unataka simu ya kukidhi mahitaji yako? Basi hii ni orodha ya simu zipatazo mia moja ambazo za bei nafuu zaidi Hii orodha inaorodhesha simu kutoka kampuni […]

thumbnail samsung s26+

Bei ya Samsung Galaxy S26+ na Sifa Zake Muhimu

Japokuwa Samsung Galaxy S26+ ni simu mpya, haina ubunifu mkubwa unaoitofautisha na Samsung Galaxy S25+ Na hata Samsung Galaxy S24+ ina sifa zinazofanana na hii samsung mpya kwa karibu 90% […]

Bei ya Samsung Galaxy S26 Ultra na Sifa Zake Muhimu

Samsung wamezindua simu mpya ya Samsung Galaxy S26 Ultra Imekuja na upekee fulani lakini hauleti utofauti mkubwa sana na Samsung GalaxyS25 Ultra Kama ingekuwa ni mimi nisingeona haja ya kubadili […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company