Kwenye wiki ya nne ya mwezi wa tano 2023 infinix waliingiza sokoni toleo jipya la simu
Toelo hilo ni Infinix Note 30
Ni toleo la daraja la kati hivyo kuna ubora kwenye maeneo ya kamera, chaji, kioo na hata muonekano wa simu
Kitu kinachofanya bei ya infinix note 30 kuzidi laki tano
Sifa zake nyingi ni za wastani kiasi cha kwamba haiwezi kuwa kwenye kundi moja na Tecno Camon 20 Premier
Fuatilia kila kuifahamu note 30 kiundani
Bei ya Infinix Note 30 ya GB 256
Infinix yenye ukubwa wa GB 256 utaipata kwa kiasi cha shilingi 600,000/=
Memori ya simu ni kubwa sio rahisi kupata simu yenye ukubwa huu kwa kiwango hiko
Kwa maana hayo kuna baadhi ya vitu ni lazima viwe na ubora wa kawaida kama utakavyoona
Kwa maana hata simu shindani zenye bei chini ya laki sita huwa na memori za GB 128 na 64
Hata kama bei yake ni kubwa infinix wanakupa pia chaguo la GB 128
Sifa za Infinix Note 30
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 256GB,128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.78inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 600,000/= |
Upi ubora wa Infinix Note 30
Simu inakuja na skrini yenye resolution kubwa tofauti na simu za bei nafuu zinazotumia vioo vya ips lcd
Utendaji wa simu ni wa kiwango cha kuridhisha kutokana na aina ya chip iliyotumika
Inatumia mfumo mpya kabisa wa android kitu kinachokupa uhakika wa matumizi ya miaka mingi
Betri yake ni kubwa na chaji yake ina kasi kubwa ya kujaza simu kwa muda mfupi
Kioo chake kina refresh rate kubwa inachangia uwepesi na ulaini wakati wa kutachi
Inakuja na memori kubwa na yenye kasi
Kamera inatoa picha nzuri kama utakavyoona baadae
Uwezo wa network
Infinix Note 30 inasapoti mpaka mtandao wa 4G kama kiwango cha juu
Aina ya 4G inayotumika na simu ni LTE Cat 13
Kama hufahamu kasi ya juu ya kupakua mafaili kwenye LTE Cat 13 ni 650Mbps ambayo ni sawa 81MBps
Hii inamaanisha kama unapakuwa gemu la Dream Soccer 2023 ambalo lina ukubwa wa MB 560 basi simu italidownload kwa sekunde 70 sawa na dakika 1 na sekunde 10
Kwa Tanzania mitandao mingi kasi ya 4G huwa ipo kati ya 20Mbps mpaka 75Mbps
Kwa maana sio rahisi kuipata kasi ya 650Mbps hapa nchini
Kuhusu masafa, simu ina masafa yote yatumikayo ni mitandao ya simu nchini
Kuna baadhi ya simu huwa yanakosa masafa yote ya 4G mfano mzuri ni baadhi ya vishikwambi walivyopewa walimu vinakosa masafa ya 4G ya halotel
Ubora wa kioo cha Infinix Note 30
Kioo cha infinix note 30 ni aina ya ips lcd chenye refresh rate inayofika120Hz
Mbali na kutumika kwa aina hii ya kioo ila ina resolution kubwa ya 1080 x 2460 pixels
Refresh rate ya 120Hz huleta uwepo na ulaini kwenye simu unapokuwa unaperuzi au kucheza gemu
Kwa mfano ukiwa una-scroll kuangalia picha mbalimbali kwenye simu yako utaona simu ni nyepesi na inabadirika kwa uzuri
Kutokana na resolution kuwa kubwa muonekano wa vitu pia ni mzuri kwenye hii infinix
Inapokuja kwenye uangavu simu inafika mpaka nits 600
Hii inamaanisha kioo kitaonyesha vizuri pale unapokuwa unaitumia juani
Kikawaida kwenye jua kali skrini huonekana kwa shida kama kiwango cha uangavu wa simu ni kidogo
Nguvu ya processor Mediatek Helio G99
MediaTek Helio G99 ndio chip inayotumika na infinix note 30 kufanya kazi zake
Ni processor ya daraja la kati hivyo utendaji wake ni wa wastani
Imegawanyika katika sehemu mbili huku sehemu yenye nguvu zaidi ikitumia muundo wa Cortex A76 katika core zote mbili
Utendaji wa Cortex A76 ni wa kuridhisha na matumizi madogo ya umeme japo si sawa kama ilivyo kwa Cortex A78
Kwenye app ya kupima nguvu za processor ya geekbench inaipa hii simu alama 555
Kwa maana kiuwezo inaendana na simu ya Redmi Note 10 ya 2021
Kwa kifupi ni kuwa ina uwezo wa kufungua vitu kwa wakati mmoja na pia kucheza gemu kubwa bila shida ya kukwama kwama
Japo kwa baadhi ya gemu utalazimika kupunguza ubora wa “graphics”(muonekano wa picha)
Kwa sababu kwenye kama PUBG Mobile kwenye resolution kubwa inachezeka kwa kiwango cha 30fps (ni ndogo)
Ila kwenye resolution ndogo inazidi 40fps
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya Infinix Note 30 ina kasi ya wati 45 kwa ajili ya kujaza betri yake ya 5000mAh
Chaji yake inajaza betri kwa dakika 57 kutoka 0% mpaka 100%
Ukaaji wa chaji kutoka kwenye betri unadumu takribani masaa 14 ukiwa unaperuzi intaneti muda wote
Ni masaa mengi ambayo yanakupa uhuru wa kutumia simu muda mrefu bila kuwa na mashaka ya chaji kuwahi kuisha
Kwa kasi ya kujaa kwa simu inaamanisha kwa siku unaweza kuichaji mara mbili tu na ukawa unatumia intaneti au kucheza gemu muda wote
Ikizingatia muda wa kucha ni dakika 57, hivyo utachaji masaa mawili kwa siku na kutumia kwa masaa 28
Ukubwa na aina ya memori
Kwenye memori kuna matoleo ya aina mbili
Kuna yenye ukubwa wa GB 128 na nyingine ya GB 256 zote zina memori ya GB 8 ambayo inaweza kuongezwa
Aina ya memori inayotumika ni UFS 2.2 ambayo huwa ina kazi kubwa ya kusafirisha data
Kasi ya UFS 2.2 inafika 1200MBps kwa njia moja wakati ufs huwa ina njia mbili
Hii inaongeza ufanisi kwenye utendaji wa simu na kufanya simu kufungua apps kwa haraka
Uimara wa bodi ya Infinix Note 30
Kimuonekano wa nyuma simu inafanana na iphone 14
Kiasi unachoweza kudhani ina glasi lakini si hivyo
Infinix note 30 ina bodi ya grassi mbele na nyuma na kwa pembeni ndio ina plastiki
Uzuri wa bodi za glasi inazuia michubuko ya rangi kwa kipindi cha muda mrefu
Hivyo ule muonekano wa simu haupotezi ubora kwa kipindi cha miaka mingi
Haijaainishwa kama simu inaweza kuzuia maji ya kuchuruzika kupenya ndani kwani haina viwango vya IP.
Uwezo wa Kamera
Infinix Note 30 unaweza kuita infinix macho matatu
Kwa maana ina jumla ya kamera zinapatazo tatu
Ila kiuharisia kuna kamera moja kwa sababu kamera iliyoandikwa depth haipigi picha
Bali huwa inapima umbali wa kitu kinacholengwa kupigwa picha
Inatumika zaidi kupiga picha zinazotenganisha upande wa nyuma wa kitu kinachopigwa
Kiujumla ubora wa picha ni mzuri sana japo kuna kukolea kwa rangi kitu kinachopunguza muonekano halisi wa kitu
Ila kwa watu wa instagram na mitandao ya kijamii itawafaa maana hutohitaji filter
Ina uwezo wa kurekodi video za full hd pekee
Ubora wa Software
Simu inatumia toleo la Android 13 na mfumo wa XOS 13
Kwenye XOS 13 kuna vitu vingi vinavyoambatana na simu
Moja ya utakachokutana nacho ni app ya XARENA inayokupa uwezo wa kuzuia shughuli zingine wakati unacheza gemu
Mara nyingi unaweza ukakuta notification zinatokea au simu zinapigwa wakati akili yako ipo kwenye gemu
Basi xarena inakupa uwezo wa kuzuia hilo
Na pia simu inakuja na voice assistant inaitwa Forax Voice Assistance ambayo inaweza kusoma kwa sauti vitu kama sms nk
Washindani wa Infinix Note 30
Washindani wa Infinix Note 30 wapo wa aina mbili
Kuna ushindani kutokana na bei na pia ushindani kutoka kwenye simu zinazoendana sifa
Moja ya mshindani wake ni Samsung Galaxy A24 4G
Simu ya Galaxy A24 4G ina kamera ya kupiga eneo pana na inatumia kioo kizuri zaidi cha super amoled
Bei ya galaxy a24 4g ya gb 128 ni shilingi 480,000/=
Na mshindani mwingine ni Poco M5 na pia simu ya Vivo V27e, hizi zote bei zake ni pungufu ya infinix
Neno la Mwisho
Kwa muhitaji wa simu nzuri za infinix daraja la kati infinix note 30 ni chaguo sahihi
Bei yake inaendana kwa kiasi kikubwa na ubora wa simu ukizingatia inakuja na memori kubwa
Na sio tu ujazo wa memori ila inakupa memori yenye kasi kubwa kusafirisha data
Pia sio mbaya ukatizama simu zinazoendana kisifa ujue vitu vya ziada vilivyopo kwa washindani wengine
Maoni 24 kuhusu “Bei ya Infinix Note 30 na Sifa Zake Muhimu”
Sasa infinix note 30 charge yake Ina wireless?
Pro ndio inayo
Samahan inatumia type gan? ya chaji
Inatumia type c
Mm binafsi naitumia simuhii ulioelezeahapa infinix note 30
Ahsante kwa maelezo mazuri. Hii 600,000/= ni kiasi kikubwa hasa kwa watumiaji walio wengi, vipi hamna utaratibu wa kukopesha mteja akalipa kidogokidogo?
Uaminifu ni changamoto
infinix note 30 vip naipata kwa shiling ngapi
Infinix note 30 vip ni 790,000
Aiseee, umeeleza umeeleweka vizuri kabisa, shukrani
Kuna hiki ki taili chake kina sehemu ya kuchajia bado sijakuelewa kina maana gani
Nauza infinix note 30. Nipo Kilimanjaro
Nimeipata kwa 550,000 mpya
kungekuwa na uwezekano wa kupata sim kwa mkopo mwenz unaokuja ningechukua
Jamaa mimeingia YouTube nimeona sifa kubwa ya huu simu ni kudumbukiza kwa maji na isiharibike mbona hujaweka sifa hiyo ni nataka simu ambayo naweza kufua kama nguo
Naipenda sana hii sim jamani
Infinix note 30 ukiangalia kwenye mtandao inakuletea helio 99 na pixel ya 2460 Ila ukifungua sim yenyewe inakuletea helio 85 na pixel 2400. Hii inakuwaje mtaalam
Inawezekana ikawa ni reading error maana g85 na g99 zimefuatana na kimuundo hazitofautiani Sana. Ili kupata tumia app ya CPU X itakuonyesha Cpu iliyopo
Asante kwa ufafanuzi
Nahitaji kujua toleo la infinix note 30 imegawanywa makundi mangapi na bei zake mfano 1.infinix note 30 VIP, infinix note 30 pro, infinix note 30 play, infix note 30 5G. Nini utofauti wa hiz simu na bei zake zikoje?
Infinix no 12 shingapi
Jamani simu umepasuka screen bei shilingi ngapi note 30
Umejaribu kuulizia maduka ya infinix
Nmenunua infinix note 30 Wireless lakin ni W33 au n feki??