Hii ni orodha ya simu kumi za Huawei ambazo zimetoka kati ya mwaka 2017 mpaka 2022
Simu nyingi za Huawei zilizopo kwenye orodha ni zile za daraja la kati na la juu
Hivyo bei zake ni kubwa ambazo zinazidi laki tatu
Utaziona simu bora za huawei ambazo zinatumia mfumo endeshi wa Android na HarmonyOS
Baadhi Simu Nzuri za Huawei
Tuchambue simu moja baada ya nyingine kuufahamu ubora wa simu za Huawei kiufasaha
Huawei P50 Pro
Simu ya Huawei P50 Pro ni simu ya mwaka 2021 inayotumia mfumo endeshi wa HarmonyOS 2.0
HarmonyOS 2.0 ni mfumo uliotengenezwa na Huawei kama mbadala wa Android
Kumbuka serikali ya USA iliiwekea vikwazo huawei vinavyoizuia kutumia teknolojia za kampuni za marekani ikiwemo Google
Kitu kinachoilazimisha huawei kutotumia huduma zinazomilikiwa na google kama youtube na Android yenyewe
Mbali na hiyo, P50 ni simu yenye utendaji mkubwa sababu inatumia processor ya Snapdragon 888 4G
Kwa bahati mbaya simu haina 5G
Hii inatokana na kampuni inayounda chip ya TSMC ya Taiwan kusitisha kuitengenezea Huawei chip mpya zenye 5G
Sababu kubwa ni vikwazo vya Marekani
Kiujumla simu ni nzuri kwani haipitishi maji, inatumia kioo cha oled, ni moja ya simu yenye kamera nzuri betri yake inawahi kujaa chaji haraka kwa sabau chaji yake ina kasi ya Wati 66
Iwapo Huawei isingekuwa na vikwazo basi Huawei P50 Pro ingewekwa kundi moja na matoleo ya Samsung S21
Bei ya Huawei P50 Pro Tanzania
Kwenye masoko ya duniani hasa china na ulaya bei ya Huawei P50 Pro ni shilingi 2,097,900.00/=
Hii simu janja ina ubora karibu kwenye kila nyanja
Hivyo kwa Tanzania bei yake inaweza kukaribia milioni tatu
Huawei Nova 9 SE
Simu ya Huawei Nova 9 SE ni simu mpya ya Huawei ambayo ipo kundi la kati
Imetoka mwezi machi mwaka 2022
Na inatumia mfumo endeshi wa Android 11 ambao hauna apps za google kama gmail, youtube na google search
Utendaji wa simu ni wa wastani kwa sababu simu inatumia processor yenye uwezo wa kawaida
Processor hiyo ni Snapdragon 680 4G hivyo simu haina 5G
Kioo chake ni aina ya IPS LCD chenye resolution ya 1080 x 2388 pixels na refresh rate ya 90Hz
Hivyo uonyeshaji wavitu ni mkubwa lakini ubora wa LCD si mkubwa sana kama amoled au oled
Betri ya Nova 9 SE ina ukubwa wa 4000mAh na chaji yenye kupeleka umeme wa kiwango cha Wati 66
Kiwango hiko cha umeme kinajaza betri kwa 75% ndani ya dakika 25
Pia upande wa kamera upo vizuri kiasi chake japo si sana
Kuna jumla ya kamera nne ambazo hazitumii teknolojia dual pixel pdaf kwenye ulengaji
Bei ya Huawei Nova 9 SE
Bei ya Huawei nova 9 se yenye ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 8 ni shilingi 1,247,085.00/=
Sifa za huawei nova 9 se zinaifanya simu kuwa na bei kuwa kubwa kuliko uhalisia
Simu zinazotumia processor ya Snapdragon 680 huuzwa chini ya laki tano
Kiuhalisia simu kama Infinix Note 12 VIP inaiacha mbali Nova 9 SE
Huawei P30 Lite
Huawei P30 Lite ni simu ya mwaka 2019 ambayo inakuja na Android 9
Lakini inaweza kupokea toleo la Android 10
Hizi ni simu ambayo haikukutana na vikwazo vya USA
Hivyo applikesheni za google zinaweza kutumika
Simu inatumia chip ya yenye utendaji wa wastani hivyo utendaji wake sio mkubwa
Kioo chake ni cha IPS LCD chenye resolution kubwa 1080 x 2312 pixels
Betri yake ina ukubwa wa 3340mAh kitu kinachofanya ukaaji wa chaji kuwa mdogo
Simu ina jumla ya kamera nne huku kamera kubwa ikiwa na resolution ya 48MP
Bei ya Huawei P30 Lite
Bei ya Huawei P30 Lite inafika shilingi 1,031,417.15/= za Tanzania
Hii ni bei kubwa ambayo inaweza kununua simu bora zaidi ya OPPO A96 5G na chenji ikabaki
Bei haina uhalisia na ubora wa simu
Kwani washindani wana simu nzuri za bei nafuu kuliko hii
Huawei Nova 9
Simu ya Huawei Nova 9 imetoka mwaka 2021
Inatumia mfumo endeshi wa HarmonyOS kwa simu za china
Ila kwa Nova 9 zinazopatikana ulaya hutumia android yenye EMUI 12
Lakini EMUI 12 haina youtube, gmail, google search, google play store na app zingine za google
Kioo cha nova 9 ni kizuri kutokana na kuwa na OLED ambacho kina rangi nyingi zinazofikia bilioni moja
Betri yake ina ukubwa wa 4300mAh
Ukubwa huu unaifanya simu kukaa na chaji masaa chini ya 100 kama ikiwa haitumiki mara kwa mara
Kamera zake nne zinaweza kurekodi video mpaka za 4K kwa spidi ya kawaida.
Ila video za HD kamera hurekodi kwa fremu nyingi zipatazo 960fps
Bei ya Huawei Nova 9
Bei ya Huawei nova 9 yenye ukubwa wa GB 128 ni shilingi 932,400.00/=
Bei ni kubwa kuliko ubora wa simu
Huawei Mate Xs 2
Huawei Mate Xs 2 ni simu ya kujikunja (Foldable) iliyotoka mwaka 2022
Unaweza ukiafanya simu kuwa pana kwa kuikunjua (inakuwa kama Tablet)
Ama unaweza kuifanya simu kuwa na upana mdogo kwa kuikunja(inakuwa simu ya kawaida)
Utendaji wa simu ni mkubwa kwa sababu simu inatumia chip ya Snapdragon 888 4G
Hivyo simu haina mtandao wa 5G
Ina kioo bora kinachoweza kuonyesha rangi nyingi
Kioo hiko ni OLED chenye resolution kubwa ya 2200 x 2480 pixels
Ukaaji wa chaji ni wa kuridhisha kwa sabau simu ina betri yenye ujazo wa 4600mAh
Na pia chaji yake inapeleka umeme mwingi wa wati 66 unaojaza betri chini ya dakika 60
Pia Mate Xs 2 inakuja na memori inayofika mpaka GB 512
Inatumia mfumo endeshi wa Harmony pekee
Bei ya Huawei Mate Xs 2
Bei ya Huawei Mate Xs 2 ni shilingi 4,911,510.24/=
Kama hujaona vizuri bei yake ni zaidi ya shilingi milioni nne na laki tisa
Kama ikija Tanzania bei yake lazima izidi shilingi milioni tano
Huawei Y9 Prime
Mwaka 2019 huawei walizindua toleo la simu ya daraja la kati ambayo ni Huawei y9 Prime
Hii simu inatumia mfumo endeshi wa Android 9 (Pie)
Lakini inaweza kupokea mfumo endeshi uliofuata yaani Android 10
Utendaji wa simu sio mkubwa kwa sababu chip ya huawei ya Kirin 710F ndio imetumika
Kioo cha Huawei Y9 Prime ni cha IPS LCD chenye resolution kubwa ya 1080 x 2340 pixels
Hivyo ubora wa kuonyesha vitu ni mzuri japo si kama kioo cha OLED
Chaji yake sio kubwa kama ya Huawei Mate, kwani ukubwa wake ni 4000mAh
Kwa hiyo simu haitokaa na chaji masaa mengi sana
Bei ya Huawei Y9 Prime
Bei ya Huawei Y9 Prime ni kubwa inayofika 540,266.13/=
Ni kubwa kwa sababu ni bei ambayo inaweza kununua simu ya Redmi Note 10
Ambapo Redmi Note 10 ina vitu vizuri vingi kuliko hii simu ya Huawei
Huawei P50 Pocket
Huawei wanatengeneza simu nzuri nyingi lakini changamoto ya vikwazo inawafanya kutumia chip zisizoendana na ubora wa simu
Mfano mzuri ni hii simu ya mwaka 2021 Huawei P50 Pocket
Ina kamera kali yenye kutumia teknolojia ya Laser Af kwenye ulengaji
Haitoshi inatumia kioo kinachoweza kujikunja cha OLED
Ambacho kina resolution kubwa ya 1188 x 2790 pixels
Hii simu unaweza ukaikunja na ikawa kama pocket (kipochi)
Japo betri si kubwa ila chaji yake ina kasi ya kuijaza betri kwa haraka
Kwani umeme unaoenda kwenye betri ni wati 40
Na inaweza kuchaji kifaa kingine kwa wati 5
Lakini pamoja na mazuri yote simu inatumia chip ambayo haina 5G japo utendaji ni mkubwa
Chip hiyo Snapdragon 888 4G
Pitia hapa uelewe, aina ya processor za simu na kazi zake
Bei ya Huawei P50 Pocket
Hii ni simu nyingine ya Huawei yenye gharama kubwa kwani bei yake shilingi 2,797,200.00/=
Simu za kujikunja(Folding Phone) zimekuwa zikiuzwa bei kubwa
Kwa bahati mbaya hii huawei ubora wake si mkubwa sana ukilinganisha na bei
Bei hii inanunua simu ya iPhone 13 Pro Max
Huawei P50
Huawei P50 inaweza ikawa simu ya daraja la juu ya bei nafuu kutoka kwa kampuni ya Huawei
Kwani za hii simu pia inapiga picha nzuri
Kioo chake kinaonyesha picha vizuri na kwa uangavu
Kwani ni cha oled ambacho kina resolution ya 1224 x 2700 pixels
Pia simu inatumia mfumo endeshi wa HarmonyOS 2.0
Huawei P50 ni simu ambayo haipitishi maji kama ikidumbukia kwenye kina cha mita moja kwa muda wa nusu saa
Kwani ina viwango vya IP68
Utendaji wake ni mkubwa lakini simu inatumia mtandao wa 4G kwani haina 5G
Betri yake ina ukubwa wa 4100mAh na chaji yake inapeleka umeme wa wati 66
Bei ya Huawei P50
Bei ya Huawei P50 ni shilingi 1,678,320.00/=
Bado bei ni kubwa kwa nyakati za sasa zenye ushindani mkubwa
Zitazame, simu za sony na bei zake halafu linganisha na hizi za huawei
Utaona kuwa simu za sony bei zake ni nafuu.
Huawei P Smart
Hii ni simu ya kitambo kidogo kwani imetoka mwaka 2017
Ni simu ya daraja la chini kutokana na kutumika kwa chip ya Kirin 659
Utendaji wa Kirin 659 ni wa kiwango kidogo
Kutokana na simu kuwa kwenye kundi la mwisho tegemea vitu vingi kuwa kwenye ubora wa kawaida au wa chini
Kwa mfano, kioo chake ni cha IPS LCD chenye resolution ya 1080 x 2160 pixels
Na memori zake ni aina ya eMMC 5.1
eMMC 5.1 huwa na kasi ndogo ya kusafirisha data ukilingansha na memori za UFS
Kamera zake haziwezi kutoa picha nzuri hasa kutokana na kutmua ulengaji wa kawaida yaani AF
Simu ina betri dogo ambalo linafanya simu kukaa na chaji masaa machache
Bei ya Huawei P Smart
Wakati simu imetoka bei yake ilikuwa ni shilingi 417,478.37/=
Lakini kwa sasa bei yake inaweza ikawa ni chini ya shilingi laki mbili
Hii ni simu ambayo ipo kundi moja na simu za itel
Huawei Nova 9 Pro
Simu ya Huawei Nova 9 Pro ni simu ya mwaka 2021 inayotumia mfumo endeshi wa HarmonyOS 2.0
Ni Huawei yenye kamera nne ambapo kamera moja ina ulengaji wa PDAF
Utendaji wa simu ni wa kuridhisha kwa sababu inatumia chip yenye nguvu ya Snapdragon 778G 4G
Kwa bahati mbaya hii chip haina 5G
Tembelea ukarasa huu unaofafanua, maana ya 5G na aina zake na umuhimu wake
Kioo chake kina uangavu na uonyeshaji wa rangi zipatazo bilioni moja
Kwa sababu simu inatumia kioo cha OLED
Betri yake ya ukubwa wa 4000mAh inawahi kujaa kwa 100% ndani ya dakika 20
Hii inatokana na chaji ya Huawei Nova Pro kuweza kupeleka umeme wa wati 100
Bei ya Huawei Nova 9 Pro
Bei ya Huawei Nova 9 pro ni shilingi 1,129,647.36/= za Tanzania
Ukilinganisha na huawei nyingi ambazo zimeorodheshwa hapa hii ni nafuu
Lakini bei hii inakupa simu kali ya Samsung kama Samsung s21 FE 5G
Maoni 6 kuhusu “Simu 10 Nzuri za Huawei na Bei Zake (2022)”
Simu zipo Kali lakini Bei ghali mnaweza mkatuokoa level za chini ingekuwa fresh
Kiukwel sim zenu n nzur sn na hilo swala lenu la kutokuwa na google kwa baadhi ya sim munafikiriaje ili kuepukna na huwo mgogoro wenu kuhusiana na google ila jaribun kutengeneza na sim za bei rahisi zenye uwezo mnzur zaid ili muweze kupata wateja waaina zote wenye vipato vikubwa na wenye vipato vidogo
Itategemea na maelewaona kati ya China na Marekani maana huawei ni mhanga
Nina simu ya Huawei nova 7i nahitaji kujua kama kwa bahati mbaya ikiibiwa munaweza kunisaidia kuipata kwani naipenda sana????
inawezekana kikubwa hifadhi imei ya simu na pia location iwe on muda mwingi
Simu zenu nzuri sana ila mnauza bei sana jaribuni kutengeneza za bei ya chini ili kwamba na watu wahari ya kawaida waweze kununua