Katika simu nyingi zilizozinduliwa na Tecno mwaka 2022 mojawapo ni Tecno Spark 8C
Hii ni simujanja inayoingia moja kwa moja kwenye kundi la daraja la chini
Kitu kinachofanya bei ya Tecno Spark 8C kuwa chini ya laki tatu
Bei ndogo inasababishwa na simu kuwa na sifa za chini NYINGI ukilinganisha na simu zingine kama Redmi 10C
Bei ya Tecno Spark 8C ya GB 64
Kwa maduka mengi ya simu dar es salaam wanaiuza simu kwa bei ya 240,000/=
Sifa zake zinazidiwa kwa kiasi kikubwa na iPhone 6 Plus ya mwaka 2014
Itazame: ubora na bei ya iPhone 6 Plus 2022
Hivyo spark ilifaa iuzwe chini ya bei ya sasa kwa kulinganisha na sifa za iphone 6
Fuatailia sifa za tecno hii kwenye jedwari
Sifa za Simu za Tecno Spark 8C
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 64GB, na RAM 2GB,3GB,4GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 245,000/= |
Ni upi ubora wa Tecno Spark 8C
Hii ni simu ya daraja la chini hivyo kuna ubora kwenye sehemu chache
Ubora mkubwa ni simu kuja na memori inayoweza kuchukua vitu vingi
Pia ni simu ambayo inakaa na chaji masaa mengi
Ikizingatiwa inatumia memori na processor inayotumia umeme mdogo
Kwenye nyanja zingine hakuna ubora mkubwa kama utakavyoona.
Uwezo wa Network
Hii ni tecno ya bei nafuu inayosapoti mtandao wa 4G
Tovuti rasmi ya Tecno haijainisha processor iliyotumika kwenye simu
Hivyo inakuwa ngumu kujua spidi ya juu na aina ya 4G iliyotumika
Ndio, 4G imegawanyika katika makundi mengi kulingana na kasi
Ufafanuzi wa 4G upo hapa: Aina za 4G na maana yake
Lakini pia kuna Spark 8C zinatengenezwa kwa ajili ya soko la India
Hivyo kuwa makini na aina ya masafa ya 4G kama yapo ya Tanzania
Ubora wa kioo cha Tecno Spark 8C
Karibu simu zote zinazouzwa chini ya laki tatu hutumia vioo vya IPS LCD
Hiki kioo kinaoonyesha picha vizuri zaidi kama resolution yake itakuwa kubwa
Ila Spark 8C ina resolution ndogo ya 720 x 1612 pixels
Kiufupi, ubora wa kioo wa ips lcd huwa unaachwa nyuma na vioo vya AMOLED katika uonyeshaji wa vitu kwa rangi halisi
Na kioo cha amoled kinakuwa bora zaidi kama kinawekewa teknolojia ya HDR10+ au Dolby Vision
Nguvu ya processor
Hakuna taarifa zinazoonyesha processor inayotumiwa na simu ya tecno spark 8C
Ila kwa kutazama aina ya memori simu inayotumia na bei ya simu inatosha kusema kuwa processor yake ina nguvu ndogo
Hata mfumo endeshi wa Android Go Edition unawekwa kwenye simu zenye nguvu ndogo ya kiutendaji
Mara nyingi memori za eMMC hutumiwa na chip ambazo hutumia nguvu ndogo katika kufanya kazi zake
Na hata memori upande wa RAM zinafafanua pia utendaji wa chini wa chip
Uwezo wa betri na chaji
Kutokana na simu kuwa na betri kubwa na chip inayotumia umeme mdogo inafanya simu kukaa na chaji muda mrefu.
Betri yake ukubwa ni 5000mAh
Pia hakuna taarifa zinazoanisha spidi ya kuchaji
Lakini bila shaka chaji yake itakuwa inapeleka umeme mdogo
Hivyo tarajia masaa mengi ya kuchaji mpaka simu ijae
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo matatu ya Tecno Spark 8C yanayotofautiana ukubwa wa RAM pekee
Kwani matoleo yote yana memori ya ukubwa wa GB 64
Kasoro moja iliyopo kwenye upande wa memori ni kitendo cha Tecno kutumia memori za eMMC 5.1
eMMC 5.1 husafirisha data kwa kasi ndogo
Kitu kinachoweza kuifanya simu kuwa nzito ikizingatiwa na RAM zake ni ndogo 2GB na 3GB
Uimara wa bodi ya Tecno Spark 8C
Simu imetengenezwa kwa bodi za plastiki
Si kitu cha kushangaza ikizangitiwa ni simu ya bei nafuu
Kwani simu inapotengenezwa kwa glassi hasa za gorilla huongeza gharama inayopelekea simu kuuzwa bei ya juu
Kutokana na hilo itakulazimu utafute kava inayoendana na kimo cha spark 8C ambacho ni inchi 6.7
Na vizuri pia ukaweka screen protector kama utainunua hii simu
Ubora wa kamera
Tecno spark 8C ina kamera mbili tu ambazo ubora wake ni mdogo
Kamera kubwa ina ukubwa wa 13MP
Lakini haina teknolojia yoyote ya ulengaji ikiwemo PDAF
Hivyo ufanisi wa kupiga picha si mkubwa
Kamera ya pili ni aina ya QVGA (320 x 240 pixels)
QVGA ni kamera za kizamani ambazo huwa na resolution ndogo
Kitu kinachoifanya kamera kutoa picha mbaya
Kwenye kurekodi video, simu inarekodi video za full hd pekee kwa fremu 30 kwa sekunde
Ubora wa Software
Hii simu inakuja na Android 11 toleo la Go Editon
Go Editon ni aina ya mfumo endeshi ambao umetengenezwa kwa ajili ya simu zinazotumia processor zilizo na uwezo wa chini na RAM ndogo
Mfumo huo unasaidia kuongeza ufanisi wa simu kiutendaji
Bila hivyo tecno spark 8c ingekuwa ni nzito zaidi
Yapi Madhaifu ya Tecno Spark 8C
Simu Tecno Spark 8C ina madhaifu kwenye idara karibu zote
Hatutogusia kila kitu ila tutajikita kwenye udhaifu wa utendaji na kamera
Hii tecno haiwezi kurekodi video za 4K
Na inatumia memori ambazo kasi yake ya kusafirisha taarifa sio kubwa
Usafirishaji wa data taratibu unaifanya simu kufungua app taratibu
Neno la Mwisho
Hii simu inamfaa mtu ambaye hapendi mambo mengi
Kwa mtumiaji anayetembelea zaidi mitandao ya kijamii na kupiga simu au sms Spark 8C inaweza mfanikishia mahitaji hayo
Na ikizingatiwa bei ya Tecno Spark 8C inahimilika kwa Watanzania wengi
Ila zipo simu za bei nafuu nzuri zaidi ya hii kwa bei rahisi.
Pitia baadhi ya simujanja za pixel: simu nzuri za pixels zikiwezo zile za chini ya laki nneĀ
Maoni 14 kuhusu “Bei ya Simu ya Tecno Spark 8C na Sifa Zake Zote”
Ni kweli nimeifurahia Sana ihii sm kama mtumiajei
Nime ipenda Sana tu naifurahia Tena sana
Simu nzur sana naipenda
Simu nzuri Hana usumbufu
Simu ni nzuri ila na kuwa na changamoto kwenye system update kwangu inakataa sijajua tatizo ni nini?
Hii Simu mm nimeipenda sana Iko vizur lakn kipindi ilikua Bado mpya Kuna baadhi ya maeneo ilikua haishiki network lakn baada ya ku apdate ikawa good kabsa
Jamani me nina spark 8c og lakini inaaajabu Ina ram 2 rom 16 af simu yenyewe ni original kabisa itakuwa tatizo nini
Ulinunua Kwa MTU au dukan, ROM za spark 8c ni GB 64
Nipo nasoma comments
Nahitaji sim
Simu ipi
Simu inakidhi mahitaji yangu vyema
Nimependa unavyo elezea kwa ufanisi bila kudanganya, mm nataka simu ambayo haita zidi laki tatu na nusu, kipaumbele (mimi ni mpenzi wa magemu)
Simu ipo vzr sana nimeipenda