Kama umefuatilia sifa na bei ya Tecno Camon 20, utaona kuwa ina viwango vya IP53
IP53 ni nini hasa?
Kwanza neno IP kirefu chake ni Ingress Protection
Inaasharia kiwango cha uimara wa simu kuzuia maji na vumbi kuingia ndani ya kifaa cha umeme mfano simu
IP53 ni kiwango kinachoashiria uimara wa simu kuzuia maji ya kiwango kunyunyuruzika
Sio kiwango kinachomaanisha uwezo simu kuhimili kutopitisha maji kama ikizama kwenye ndoo ya lita ishirini
Hivyo Tecno Camon 20 inaweza kuzuia maji kwa kiwango fulani na kwa muda mchache kama inavyoonekana kwenye hii video
Je Camon 20 haipitishi maji ikizama kwenye swimming pool
Tegmemea simu kufa iwapo itadumbukia katika maji ya kiwango hiko
Achilia mbali kuzama kwenye swimming pool, simu inaweza kuathirika kwa haraka hata ikizama kwenye jagi
Jinsi tecno camon 20 ilivyoundwa imeleka kuwa imara kwenye maji yenye kasi ndogo
Kwa maana hata kama ukiwa unatumia kwenye mvua kubwa sana itakulazimu kuwa makini vile vile
IP53 inalenga kuzuia vumbi na maji yenye kasi ndogo kwa kingeleza wanasema splash resistant
Kiwango cha maji simu inaweza kuhimiri ni maji ya levo isiyozidi sentimita mbili ndani ya muda mfupi na kwenye eneo dogo
Ukizidisha hapo maisha ya simu yatakuwa mashakani
Hivyo unapokuwa unafanya kwenye mazingira yenye maji ni muhimu kuwa mwangarifu.
Kwani hii simu haina uwezo wa iPhone 15 Pro inayoweza kuzuia maji kwa muda wa nusu saa kwenye kina cha mita sita(6).
Muda wa kuhimiri kutopitisha maji
Kama ilivyotanguliwa kuelezwa hapo awali, camon 20 ikiingia kwenye maji haiwezi kustahamili kwa muda wa nusu saa
Unapaswa uwahi simu ndani ya dakika mbili
Hali ni tofauti na simu za madaraja ya juu mabazo zimetetengenezwa kuhimili kutopitisha maji kwa dakika nyingi tena kwenye eneo kubwa
Kwa mfano Samsung Galaxy S23+ ikizama kwenye maji mengi ya kina cha mita 1.5 maji hayatoingia na unaweza itumia simu hata ndani ya maji
Ndio maana bei ya samsung galaxy s23+ ni kubwa zaidi kuliko camon 20
Kitu ambacho hutokuwa na wasiwasi nacho kuhusu camon 20 ni nyakati za mvua za rasha rasha
Unaweza kutoa simu yako na kisha ukawa unaangalia mambo mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii au kutazama video youtube
Na bado simu inaweza isiathiriwe na maji
Ila mvua ikiwa kubwa hapo ndipo unapopaswa kuilinda simu kwa kutoitumia kwenye hiyo mvua
Cha kufanya pindi camon 20 ikiingia majini
Kitu cha kwanza ifute simu maji kutumia kitambaa kisafi
Zingatia muda ambao simu imekuwapo ndani ya maji
Kwa sababu kwa kiasi fulani tecno camon 20 ni himilivu kwenye kina kidogo
Jaribu kuona kama simu inafanya kazi
Anza kujaribu tachi, kuchaji, sehemu ya earphone, tazama sehemu ya laini kama haina maji
Ukiona kila kitu kipo sawa basi simu inaweza kutumika vizuri
Iwapo simu imezama kwenye kina kikubwa na ukagundua haifanyi kwenye vitu vingi
Basi simu inapaswa ifunguliwe na vizuri ukamuona mtaalamu ya simu kuharibika kila kitu
Je Camon 20 haipitishi maji kabisa?
Simu ya tecno camon 20 haiwezi kuwekwa kwenye kundi la simu zisizopitisha maji
Kiwango cha IP53 ni kiwango kidogo
Hivyo ni upotoshaji kuita simu kuwa inaweza kuzuia maji
Kikawaida simu zisizopitsha maji zinaweza kuhimili dakika nyingi na kwenye mazingira tofauti
Camon 20 inaweza kuingiza maji kama ikizama katika kina cha mita 1, tena hata dakika moja inaweza isichukue
Hii inamaanisha nini?
Kuna kiwango cha maji Camon 20 inaweza kuzuia na kingine inashindwa kabisa
Kwa mara nyingine, umakini ni muhimu.
Simu zingine zisizopitisha maji
Simujanja nyingi za daraja la juu hutengenezwa kuwa na uwezo wa waterproof
Mifano michache wa smartphone za aina hiyo ni matoleo mengi ya iphone na samsung matoleo ya S-series
Mfano wa simu hizo ni iphone 14, iphone 14 Pro, iPhone 14 Pro Max, Samsung Galaxy S23, Samsung Galaxy S23+, Samsung Galaxy S23 Ultra, Google 7 Pro, Google Pixel 6 Pro na nyinginezo nyingi
Utofauti ni kuwa hizi simu chache nilizotaja zenyewe zina viwango vya IP68
Hiki ni kiwango kikubwa kinachoashiria uwezo wa simu kutopitisha maji hata ikizamisha kwenye kina cha kuanzia mita 1.5 kwa muda wa nusu saa
Kwa mtu ambaye kazi zake ni za shambani kwenye umwagiliaji aina hii ya simu inamfaa zaidi
Changamoto kubwa ya simu zisizopitisha maji kabisa ni bei kubwa
Hapa ndipo matoleo ya Tecno Camon 20 yanapokuwa kimbilio kwa kuwa na uwezo wa kiasi kidogo cha kuzuia maji
Utajuaje uwezo wa simu kuzuia maji
Mara nyingi kampuni husika huanisha aina ya IP(Ingress Protection) iliyonayo
Na njia nyepesi kutambua ni kusoma sifa mbalimbali za simu husika
Kwani vitu huwekwa wazi
Na kwa kujihakikishia unaweza kutazama video mbalimbali za majaribio za simu husika
Kama simu haina kiwango chochote cha IP huwa haisemwi
Hitimisho
Kwa watu wenye bajeti ya wastani na wanahitaji simujanja isiyopitisha maji Camon 20 inaweza kuwa chagua zuri
Ila bahati mbaya simu haiwezi kustahimili kupitisha kwenye kina kikubwa, mvua kubwa na kwa muda mrefu
Hii simu inahimili maji ya kiwango kidogo sana tena kwa muda mfupi
Haipo sawa na matoleo ya simu za mbaya ambazo hutengenezwa kwa uimara mkubwa
Ila hizo simu ni kwa ajili ya watu wenye pesa ya kutosheleza ambazo watanzania hawawezi kumudu
Mbali na camon pia kuna matoleo ya OPPO na Redmi yenye IP53.
Wazo moja kuhusu “Uimara wa Tecno Camon 20 Kuzuia Maji (Waterproof)”
mko sahh maelezo yanaelewka