Simu ya Tecno Spark 8 Pro ni tecno mpya ya mwaka 2022 iliyotoka mwezi wa kwanza
Ni moja ya tecno ya macho matatu yenye utendaji wa wastani
Bei ya tecno spark 8 pro kwa maeneo mengi Tanzania inaanzia shilingi laki tatu
Hii imu inatofautina na kiuwezo na sifa na simu ya tecno spark 8 ya mwaka 2021
Ukizisoma sifa zote za spark 8 pro utagundua kuna maboresho na spark ya mwaka 2021 pamoja na tecno spark 5
Bei ya Tecno Spark 8 Pro Tanzania
Bei ya Tecno Spark 8 Pro inatofautiana kulingana na ukubwa wa memori
Spark 8 Pro ya 64GB inauzwa shilingi 310,000/=
Bei yake inaakisi ubora wa simu na zinashabihiana hasa ukiziangalia sifa zake upande wa processor
Tecno spark 8 pro ina bei sawa na infinix hot 10 play ila tecno ina uwezo mkubwa zaidi
Sifa za Tecno Spark 8 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 128GB, 64GB na RAM 6GB, 4GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.8inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 310,000/= |
Upi ubora wa Tecno Spark 8 Pro
Simu ina betri inayokaa na chaji masaa mengi
Chaji yake inapeleka umeme mwingi unaojaza betri masaa machache
Spark 8 Pro ni simu yenye uwezo wa kuridhisha kwa sababu ya aina ya chip inayotumia
Moja ya kamera yake ina sensa kubwa
Pia inakuja na nafasi kubwa ya kujaza vitu vingi
Uwezo wa Network
Tecno Spark 8 Pro ni simu ya 4G aina ya LTE Cat 7
Spidi ya kudownload ya juu zaidi ni 300Mbps
Hivyo mafaili makubwa yanaweza kudownloadiwa kwa haraka kama mtandao wa simu unatoa kasi kubwa
Network ya 4G ina network bands zote ambazo laini za halotel, vodacom, tigo, ttcl na airtel inatumia
Hivyo mtumiaji ana uwanja mpana wa kuchagua mtandao anaoutaka
Ubora wa kioo cha Tecno Spark 8 Pro
Kioo cha tecno spark 8 pro ni aina ya IPS LCD.
Japokuwa huwa ni kioo chenye rangi chache ukilinganisha na amoled ila ubora upo juu kiasi
Kwa sababu kioo kina resolution kubwa ya 1080 x 2460 pixels tofauti na spark 8 yenye resolution ndogo
Uangavu wake si mkubwa
Hivyo kwenye jua kali screen inaweza isionyeshe vizuri
Nguvu ya processor MediaTek Helio G85
Processor ya simu ya Tecno spark 8 ni mediatek helio g85
Ni chip ya toleo la kati hivyo utendaji wake ni wastani
Ni chip ya core nane inayoipa spark ya 2022 nguvu ya kuweza kucheza gemu za aina nyingi
Kwenye geekbench 5, processor ina alama 358
Uwezo huu unachangiwa na muundo wa core kubwa mbili
Core kubwa zina kasi inayofika 2.0 GHz na ni za Cortex A75
Cortex A75 ni muundo unaweza kufanya kazi nyingi kubwa kwa wakati mmoja.
Kuielewa processr ya Helio G85, pitia uwezo wa kiutendaji wa simu ya tecno camon 17
Uwezo wa betri na chaji
Simu ya spark 8 pro ina betri kubwa inayoweza kukaa na chaji masaa mengi
Ukubwa wa betri yake ni 5000mAh
Simu nyingi zinazotumia betri la ujazo huu hukaa na chaji kwa zaidi ya masaa 14 simu ikiwa inatumia intaneti muda wote
Hivyo hata hii simu itakuwa na uwezo huo
Betri yake inaweza kuwahi kujaa chini masaa mawili wakati wa kuchaji
Kwa sababu ina chaji yenye kasi ya kupeleka umeme wa wati 33
Simu yenye chaji ya aina ni kama Redmi Note 10
Redmi Note 10 hujaa ndani ya dakika 80, hivyo hata tecno inaweza kujaa kwa muda huo
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo mawili ya tecno spark 8 pro upande wa memori
Kuna ya 128GB n a 64GB
Ukubwa wa memori unatosheleza simu kuwa na app nyingi.
Na pia kuhifadhi mafaili mengi
Ila memori zake hazina kasi kubwa ya kusafirisha data kwa kasi
Hilo linatokana na memori ya simu kuwa ni aina ya eMMC 5.1 badala ya UFS
Hvyo simu inaweza kuwaka kwa taratibu na baadhi ya app kufunguka kwa taratibu
Uimara wa bodi ya Tecno Spark 8 Pro
Simu imetengenezwa kwa plastiki upande wa nyuma na upande wa pembeni (fremu)
Kikawaida bodi za plastiki zinahitaji kava kuepusha kuchunika kwa rangi
Uimara wake huwa sio mkubwa kama simu zilizo na glasi za gorilla upande wa nyuma
Simu ni ndefu na ni nzito kiasi fulani.
Urefu na upana wake ni inchi 6.8
Ubora wa kamera
Tecno spark 8 pro ni simu yenye jumla ya kamera tatu
Ila ni kamera moja tu ndio yenye ubora stahiki japo si sana
Kamera hiyo ina ukubwa wa resolution ya 48MP na inatumia teknolojia ya ulengaji ya PDAF
Kamera nyingine ya qvga resolution yake inatoa picha mbaya.
Ni kamera za kizamani ambazo simu nyingi haizutumii kwa miaka hii
Kamera ina uwezo mdogo wa kurekodi video za aina nyingi
Kwani inaweza kurekodi video za full hd kwa kasi ya 30fps pekee
Ubora wa Software
Spark 8 Pro ni simu inayokuja na toleo la android 11 japokuwa ni simu ya mwaka 2022
Na inatumia software ya tecno ya HIOS 7.6
HIOS 7.6 inaruhusu kufanya vitu vingi bila kuroot
Yapi Madhaifu ya Tecno Spark 8 Pro
Udhaifu mkubwa wa simu upo kwenye kamera
Mfumo wake wa kamera haujawekewa mfumo wa kutuliza video wakati wa kurekodi
Ulengaji wake si wa kiwango kikubwa kwa sababu haina dual pixel pdaf
Na pia simu haina viwango vya IP angalau IP53
Hivyo inaonyesha spark ya 2022 haina uwezo wa kuzuia maji kama ilivyo kwa spark ya 2021
Kuzifahamu simu zisizopitisha maji, zitazame hapa simu mbalimbali za sony
Neno la Mwisho
Bei ya tecno spark 8 pro inaifanya simu kuwa simu nzuri ya daraja la chini.
Kwa maana hata simu za redmi za bei rahisi huuzwa kwa bei sawa na hii spark
Na unafuu huo unakuja kutokana na simu kuwa na chip yenye uwezo wa kati
Hivyo kwa mtumiaji wa simu ambaye anapenda simu inayokaa na chaji masaa mengi basi Tecno Spark 8 Pro itamfaa sana
Maoni 3 kuhusu “Ubora na Bei ya Tecno Spark 8 Pro (na Sifa Zake)”
Je utajuaje kuwa simu uliyo uxiwa mtu kafogi gb feki ya tecno spark 8c
tazama specification za simu halafu pakua app ya cpu x utazame kama zinaendana
Je kuna tecno spark 8c ya gb 128 na bei ni shingapi