SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Tecno Spark 5 na Sifa Zake Muhimu (2022)

Bei Nafuu

Sihaba Mikole

May 1, 2022

Simu ya tecno spark 5 iliingia sokoni mwaka 2020

Ina miaka karibu miwili tangu ilipozinduliwa

tecno spark 5

Ila ina changamoto ya kuweza kushindana na matoleo mapya ya android ya daraja la chini

Pamoja na ukweli kuwa bei ya tecno spark 5 inapatikana chini ya laki mbili na nusu ila ni simu yenye sifa chache nzuri

Ukiijua bei yake na sifa zake itakulazimu kuangalia mshindani wake ambae ni Redmi 9A

Bei ya Tecno Spark 5 Tanzania

Kwa Dar Es Salaam hasa maduka ya kisutu bei ya tecno spark 5 yenye GB 32 ni shilingi 170,000/=

Ubora wa simu aina tecno spark si mkubwa katika idara nyingi

Hivyo bei yake inaendana na uwezo wa simu kiutendaji

Uwezo mdogo wa simu unachangiwa na sifa zake upande wa processor na aina ya memori.

Hivyo pitia sifa zote na maelezo yake kuelewa ubora wa spark 5 ya 2020

Sifa za simu ya Tecno Spark 5

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
 • CPU – Mediatek Helio A22
 • Core Zenye nguvu(-) –
 • Core Za kawaida(8) – 8 x 2.0 GHz Cortex-A53
 • GPU-PowerVR GE8320
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
 • Android 10
 • HIOS 6.1
Memori  32GB na RAM 2GB
Kamera Kamera nne

 1. 13MP,PDAF(wide)
 2. QVGA
 3. 2MP(macro)
 4. 2MP(depth)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
 • 5000mAh-Li-Po
Bei ya simu(TSH) 180,000/=

Upi ubora wa tecno spark 5

Ubora wa Tecno spark 5 upo kwenye ukaaji wa chaji kwa kiasi kikubwa

Kwani simu inakuja na betri na utendaji unaoisaidia simu kukaa na chaji masaa mengi

Tecno spark 5 summary

Lakini pia ni moja ya simu ya 4G inayopatikana chini ya laki mbili kwa maeneo mengi nchini Tanzania

Ubora wa maeneo mengine ya simu unatofautiana kama utakavyoona

Uwezo wa Network

Spark 5 ni simu ya 4g aina ya LTE Cat 4

Spidi ya juu kabisa ya kudownload ya LTE Cat 4 ni 150Mbps

Tecno spark 5 network

Ni spidi ndogo ukilinganisha na simu ya Tecno Spark 8 Pro yenye LTE Cat 7

Mitandao yote ya simu nchini Tanzania inakubali mtandao wa 4G kwenye hii simu

Kwa sababu simu ina network bands za 4G zinazotumika nchini

Ubora wa kioo cha tecno spark 5

Simu ina ubora mdogo upande wa kioo.

Kwa sababu kioo cha tecno spark 5 ni cha aina ya IPS LCD na kina resolution ndogo 720 x 1600 pixels

Viwango vya mwaka 2022 simu nyingi huwa na resolution 2400 pixels

Kwa maana hiyo ubora wa screen kuonesha picha ni wa kawaida

Na simu haina uangavu mkubwa.

Hivyo simu inaweza ikawa haionyeshi vitu vizuri ukiwa unatumia juani

Nguvu ya processor Mediatek Helio A22

Mediatek helio a22 ni chip ya simu ya daraja la chini

Ndio processor ambayo spark 5 inatumia

Pamoja na chip kuwa na core nane ila uwezo wake kwenye utendaji ni mdogo

Uwezo mdogo unasababishwa na core zote kutumia muundo wa Cortex A53

Cortex A53 hutumika zaidi kwa ajili ya kazi ndogo.

Hivyo simu ya tecno spark 5 inapata shida kucheza magemu yenye graphics kubwa kama Call of Duty Mobile

Uthibitisho wa uwezo mdogo unaweza ukauona kwenye alama za geekbench 5

Geekbench 5 inaipa Helio A22 alama 161

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya spark 5 ina ukubwa wa 5000 mAh

Bila shaka ni simu inayokaa na chaji masaa mengi ukiongezea na aina ya utendaji

Ikumbukwe kuwa processor zenye muundo wa Cortex a53 hutumia umeme mdogo na utendaji mdogo

Simu haina fast chaji

Hivyo tegemea betri kuchukua masaa zaidi ya matatu kujaa

Ukubwa na aina ya memori

Kuna toleo moja tu tecno spark 5 kwenye memori ambayo ipo ni 32GB na RAM 2G

Hiki ni kiasi kidogo kisichohifadhi app na mafaili mengi

Na uwezo mdogo wa simu kiutendaji unasababishwa pia na aina ya memori zilizotumika.

Spark 5 ina memori aina ya eMMC 5.1 ambayo kasi ya kusafirisha data sio kubwa

Uimara wa bodi ya tecno spark 5

Simu nyingi za daraja la chini huundwa na bodi za plastiki upande wa nyuma

Hio inatokana na gharama kubwa simu inapotumia glasi

tecno spark 5 bodi ya simu

Hata spark 5 pia ina bodi ya plastiki ambazo si imara sana pale simu inapoanguka kwa kimo kirefu

Kwa hiyo ni jambo la msingi kuweka screen protector na kava

Ubora wa kamera

Tecno Spark 5 ina jumla ya kamera nne.

Ina kamera aina ya macro inayoweza kupiga picha vitu vya karibu na vidogo

Ila kamera ya nne ni QVGA, ni kamera zenye ubora mdogo kuotakana na kuwa na resolution ndogo

tecno spark 5 camera

Ni kamera za kizamani kiujumla

Ubora wa kurekodi video ni mdogo

Simu inaweza kurekodi video za full hd kwa spidi ya 30 fps pekee.

Na kamera kubwa ina 13MP na inatumia PDAF kwa ajili ya ulengaji

Ubora wa Software

Hii simu ni ya android 10 ambayo haiwezi kupokea toleo jipya la android

Na hata software ya tecno inatumia HIOS 6.1

Yapi Madhaifu ya tecno spark 5

Simu ina kamera zenye ubora wa chini.

Kiubora haiwezi kuendana na infinix yenye kamera nzuri ya Note 11 Pro

Tecno hii inatumia bodi za plastiki ambazo kuchunika ni kawaida

Simu ina uwezo mdogo kiutendaji

Na kioo chake sio kizuri kwani resolution yake ni ndogo

Pia network yake ina spidi ya chini

Na haiwezi kuhifadhi vitu vingi kwa sababu memori yake ni ndogo

Neno la Mwisho

Kama unaweza kuongeza pesa ni vizuri ukaangalia simu zingine za oppo za bei rahisi

Kiujumla simu ya tecno spark 5 haiendani na nyakati za sasa.

Itumie iwapo bajeti ikiwa imekaba sana

Vinginevyo ni bora kutumia tecno spark 8 angalau

Maoni 3 kuhusu “Bei ya Tecno Spark 5 na Sifa Zake Muhimu (2022)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

tecno camon premier 30

Ubora wa simu za Tecno Camon 30 na bei zake(Pro, Premier)

Tangu mwezi wa nne kampuni ya walitoa matoleo ya Tecno Camon 30 Matoleo ya Camon 30 yapo matatu ambayo ni ya daraja la kati yaani mid range Ubora wa kiujumla […]

tecno camon 30 thumb

Bei ya Tecno Camon 30 Pro na Sifa Muhimu

Simu ya Tecno Camon 30 Pro ilitangazwa mwezi februari ila imetoka rasmi mwezi wa nne 2024 Ni simu ya daraja la kati(midrange) hivyo bei yake sio sawa na Tecno matoleo […]

tecno camon 30 premier thumbnail

Bei ya Tecno Camon 30 Premier 5G na Sifa zake muhimu

Kwenye matoleo bora ya simu kutoka Tecno, matoleo ya Tecno Camon huja na ubora katika vipengele vingi Hata bei za matoleo ya Camon huzizidi bei za Tecno Spark na Tecno […]

Bei ya Tecno Spark 20 Pro+ na Sifa zake

Simu ya Tecno Spark 20 Pro+ ilitoka rasmi desemba ya mwaka 2023 ila kwa Tanzania imeanza kupatikana miezi ya karibuni Kwa Tanzania bei ya juu kabisa ya Tecno Spark 20 […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company