Ni infinix kwa mara nyingine inajaribu kutengeneza hisia chanya juu ya ubora wa simu zao
Unaweza kuliona hili kwa toleo jipya la Infinix Zero 30 5G
Hii ni simu kali kwenye idara nyingi
Kwa jicho haraka unaweza ukahisi haina tofauti na iPhone 15 Pro (natania)
Vitu vingi vya maana inafanya bei ya infinix zero 30 5g kuwa zaidi ya milioni moja kwa Tanzania
Baadhi ya watu wataanza kujiuliza kwa nini ununue infinix kwa zaidi ya milioni
Ukitazama sifa zake utaacha kujiuliza swali la aina hii.
Bei ya Infinix Zero 30 5G ya GB 256
Bei ya infinix zero 30 inatarajiwa kuwa ni shilingi 1,060,000/=(milioni moja na themanini)
Hii ni bei ya pre order kwa hapa Tanzania
Kwa nchi za nje hasa india bei ya hii simu inaenda shilingi 800,000 kwenye mtandao wa amazon india
Ukijumlisha na gharama zingine bei yake inaweza isifike milioni ukiagiza kutoka India
Ila kuna changamoto zake kuagiza simu kutoka nje
Hii bei kwa kiasi kikubwa inashabiana na ubora na sifa zake kiujumla
Sifa za Infinix Zero 30 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:144Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 256GB na RAM 8GB,12GB |
Kamera | Kamera Tatu
|
Muundo | Urefu-6.78inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,060,000/= |
Upi ubora wa Infinix Zero 30 5G
Kuna maeneo mengi ambayo yenye ubora mkubwa katika hii infinix
Ila upande wa utendaji, kamera, chaji, na kioo yana uimara mkubwa wa kushindana na matoleo ya simu toka kwenye kampuni nyingine
Kioo cha infinix zero 30 kimeundwa kuwa na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi
Uwezo wa kuonyesha rangi nyingi inasaidia kioo kuonyesha kitu kwa ranfi zake halisi kwa kiwango kikubwa
Infinix hii ina nguvu ya utendaji kubwa sababu ya kutumia processor yenye nguvu
Chaji yake inawahi kujaza betri kwa dakika chache
Na ukaaji wake wa chaji ni wa kiwango cha kuridhisha
Utafahamu mengine kadri utakavyofuatilia taarifa zote zilizopo kwenye hii post
Uwezo wa Network
Infinix Zero 30 5G inaweza kutumia aina zote za network pamoja na 5G
Inaonekana ni simu inayolenga kutumika maeneo mengi duniani
Hii inatokana na aina ya 5G inayosapoti
Inasapoti karibu aina zote za 5G ikiwemo SA(yaani Standalone)
SA ni aina ya 5G inayotumia miundo mbinu mipya iliyouniwa kwa ajili ya 5G bila kutegemea miundombinu ya zamani
5G ya NSA(Non Stand Alone) inasafirisha mawimbi yake kutumia mifumo ya 4G
NSA imesambaa na inatumika kwenye nchi nyingi ikiwemo hapa Tanzania kwenye mitandao ya Vodacom, Tigo na Airtel
Hata hivyo 5G bado inapatikana maeneo machache hapa nchini hasa jijini Dar Es Salaam
Ubora wa kioo cha Infinix Zero 30 5G
Simu inatumia kioo cha AMOLED kinachosapoti refresh rate 144Hz
Hii refresh rate kwa mpenda magemu inafanya gemu kuonekana vizuri na kwa ustadi hasa gemu kama za magari
Pia kiwango hiki hufanya simu kuwa nyororo unapoperuzi kitu kama kusoma vitabu, kutafuta meseji, kuangalia majina nk
Changamoto ni kuwa sio kila kwenye simu inahitaji refresh rate kubwa
Kama muda wote utakuwa unatumia refresh rate kubwa basi betri itawahi kuisha kwa haraka
Kwenye infinix kuna chaguo la kubadirisha na kuiweka ndogo mpaka 60Hz
Pamoja na uzuri wa kioo kitu kimoja kinachokesekana ni teknoljia ya HDR10
HDR10 huboresha muonekano wa kitu kwa kuongeza kina cha rangi kwenye skrini
HDR10 hujaribu kuonyesha kitu kwa rangi halisi kama kinavyoonekana kwenye uharisia wake
Hata hivyo hii simu kioo chake bado ni kizuri ukizingatia resolution yake ni kubwa ambayo ni 1080 x 2400 pixels
Nguvu ya processor Mediatek Dimensity 8020
Meditek dimensity 8020 ni processor ya simu ambayo imeingia sokoni mwaka 2023
Kila kitu unachofanya kwenye infinix zero 30 5g kinawezeshwa na processor ya dimensity 8020
Chip hii imegawanyika katika sehemu mbili kama ilivyo kawaida ya processor nyingi za simu
Sehemu yenye nguvu kubwa kuna idadi ya core zipatazo 4, na kwenye nguvu ndogo kuna core zipatazo 4
Kwenye swala la nguvu kiutendaji, dimensity 8020 imashajaribiwa kwenye simu ya Motorola Edge 40
Katika app ya geekbench app ina alama 1124 kwenye core moja
Alama ni nyingi japo inazidia zaidi ya mara mbili na processor ya Apple A17 Pro iliyotumika kwenye matoleo ya iPhone 15 Pro
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya infinix zero 30 5g ina uwezo wa kupeleka umeme wa wati 68 kwenye betri
Ndani ya dakika 51 chaji inajaza betri kutoka 0% hadi 100%
Kwa nyakati hizi za umeme kukatika mara kwa mara chaji ya haraka inafaa zaidi
Betri yake inaweza kuchukua mpaka masaa 13 simu kuisha chaji ukiwa unatumia intaneti muda wote
Kwa mantiki hii kama unatumia sana intaneti utalazimika kuichaji simu mara mbili kwa siku
Waya wake wa chaji ni USB Type C 2 (waya wenye kichwa kipana)
Ndio chaji nyingi siku hizi zinatumia tundu la aina hii
Ukubwa na aina ya memori
Kuna infinix zero 30 5g za aina mbili zenye ukubwa sawa wa memori na RAM zikiwa tofauti
Kuna yenye RAM ya GB 8 na nyingine ina GB 12
Zote zina ukubwa wa GB 256
Mfumo wake wa memori ni UFS 3.1
UFS 3.1 inaweza kusairisha data kwa kasi inayofika 2400 kwenye njia moja
Hii inachochea vitu vingine kufanyika kwa haraka na kwa muda mchache mfano kukopi vitu kwenda kwenye simu
Uimara wa bodi ya Infinix Zero 30 5G
Hii ni moja ya simu chache za infinix zenye kioo cha Gorilla 5
Gorilla 5 ni kioo stahimilivu kwani kinaweza kuepuka kupasuka kama ikianguka urefu wa mita mbili
Hivi vioo hulinda skrini kiasi cha kwamba unaweza usione umuhimu wa skrini protekta
Pia hii simu ina uwezo wa kuzuia maji kwa kiwango kidogo kama ilivyo kwa Tecno Camon 20
Kwani ina viwango vya IP53, uwezo wa kuzuia maji haupo sawa na Samsung Galaxy S23 Ultra
Ubora wa kamera
Infinix Zero 30 5G ina jumla ya kamera tatu
Kamera yake kubwa inatumia teknolojia ya ulengaji ya PDAF
PDAF inazidiwa na dual pixel pdaf kwenye utambuzi wa kinachopigwa picha kwa haraka
Ubora wa picha nyakati za mchana ni wa kuvutia kwa kiwango kikubwa
Uhalisia wa rangi katika kamera kwa kiasi kikubwa unaakisi jinsi kitu kinavyoonekana kwenye mazingira yake
Ila kuna hali ya kuzidisha rangi hasa unapotumia HDR
Hii kamera inaweza kurekodi mpaka video za 4K
Ubora wa Software
Infinix Zero 30 5G inakuja na Android 13 na XOS 13
XOS 13 ina mpangilio mzuri wa battan na app kitu kinachomsaidia mtumiaji kutumia simu kwa uwepesi
XOS inakuja na app zingine ambazo unaweza usizihitaji na huwezi kuzitoa kiurahisi
Infinix wameiunganisha hii na mfumo wa akili bandia unaoitwa ChatGPT
ChatGPT ni akili bandia unayoweza kuuliza kitu chochote na ikakujibu
Uzuri ni kuwa inasapoti maswali ama mjadala kwa njia ya sauti
Washindani wa Infinix Zero 30 5G
Sokoni, infinix itabidi ionyeshe umwamba mbele ya Samsung Galaxy 34, iPhone 15 na hata matoleo ya Redmi na Oppo
Bei ya infinix zero 30 5g inaendana na hizo simu tajwa na kama kuna tofauti ni ndogo
Kwa bahati mbaya ama nzuri nyingi ya hizo zina vitu vingine vya ziada
Kwa maana ni rahisi kwa mtu anaefuatilia kununua simu toka kampuni nyingine
Hitimisho
Pamoja na uboreshaji wa matoleo ya Infinix kadri muda unavyoenda, bado kuna vitu vinapaswa kuboreshwa zaidi
Isingekuwa mbaya kama infinix hii ingeboreshwa uwezo wake wa kuzuia maji na kuwa na viwango vya IP68 badala ya IP53
Na hata kamera dual pixel na laser AF hizi ni teknolojia nzuri zaidi ya PDAF kwa sasa
Wazo moja kuhusu “Ubora na Bei ya Infinix Zero 30 5G (Infinix Kali)”
Daah Infinix wapo vizuri