Hii ni orodha inayohusisha simu ambazo zinauzwa na kampuni ya vodacom na bei zake
Kwenye orodha kuna simu zipatazo nane (8) za bei nafuu, kati na bei kubwa
Ni simu zenye ubora wa kawaida na nyingine ubora mkubwa ila zinaweza saidia kwa shughuri za kawaida za kila siku
Simu zenye ubora wa chini zinauzwa chini ya laki tatu
Kwa mtu mwenye kiasi kidogo cha pesa ni vizuri ukafuatilia kila simu ya vodacom na bei yake kujua kama zinakustahili ama la.
Na pia ukinunua baadhi ya simu vodacom wanatoa GB za intaneti
Simu za Vodacom na bei yake
Oppo A16K
Oppo A16K ni simu ya mwaka 2021 ambayo ni ya daraja la chini
Vodacom wanaiuza oppo a16k kwa kiwango cha shilingi 280,000 (laki mbili na themanini)
Ina jumla ya kamera moja tu ambayo uwezo sio mkubwa
Kiutendaji pia uwezo wake ni mdogo kwa sababu inatumia processor yenye nguvu ndogo aina ya MediaTek Helio G35
Inatumia kioo cha ips lcd ambacho resolution yake ni 720 x 1600 pixels (ni ndogo pia)
Betri yake ina ukubwa wa 4230mAh ambayo ni mkubwa
Na ukaaji wa chaji ni wa kuridhisha, ni simu ya 4G
Samsung Galaxy A04E
Simu ya Samsung Galaxy A04E ni simu ya android iliyotoka mwaka 2022
Kiuwezo inaendana na oppo a16K kwa maana zote zinatumia processor zenye muundo mmoja japo zina majina tofauti
Samsung galaxy A04E ina kamera mbili ila moja ndio inayopiga picha na ina megapixel 13
Kioo chake na chenyewe ni cha IPS LCD na resolution ya 720 x 1600 pixels
Ukubwa wa betri ya hii simu ni 5000mAh kwa maana ukaaji wa chaji ni wa masaa mengi
Simu inakuja na android toleo la 12 yaani Android 12
Bei ya Samsung Galaxy A04E kwenye maduka ya Vodacom ni 270,000 (laki mbili na sabini)
Tecno Pop 7
Simu ya Tecno Pop 7 ni simu ya mwaka 2023 unaweza iita tecno mpya 2023
Inakuja na RAM ya GB 2 ambayo sio kubwa kwa viwango vya sasa
Na ukubwa wa memori ni GB 64
Kwenye upande wa mfumo endeshi inatumia Android 12 Go edition
Go Edition ni mfumo wa android kwa ajili ya simu zenye RAM ndogo bila hivyo simu inakuwa nzito
Na yenyewe inatumia kioo cha IPS LCD chenye resolution ya 720 x 1612 pixels
Voda wanaiuza hii simu kwa kima cha shilingi 240,000 (laki mbili na arobaini)
Vivo Y02
Vivo Y02 ni simu ambayo imetoka mwishoni mwa mwaka 2022
Ni simu ya daraja la chini hivyo ina bei ndogo
Kwani Vodacom wanaiuza kwa kiwango cha shilingi 265,000 (laki mbili na sitini na tano)
Bei ndogo ya vivo y02 inatokana na simu kutumia processor ya MediaTek Helio P22 ambayo ina nguvu ndogo
Na pia kuwa na skrini aina ya IPS LCD yenye resolution ya 720×1600 pixels
Na bodi yake upande wa nyuma na pembeni plastiki
Memori ya hii simu ina GB 32 tu na RAM ya GB 3 au 2 ambazo bado ni ndogo pia
Ina kamera moja tu yenye megapixel 8
Infinix Smart 7 Plus
Infinix Smart 7 Plus ni moja ya simu mpya ya Infinix ya mwaka 2023
Sifa zote za Tecno Pop 7 ndio sifa za smart 7 plus
Isipokuwa memori ya infinix smart 7 ina gb 64 ILA RAM yake ni ya GB 4
RAM ya GB ni kubwa kiasi ambayo inatosheleza kufungua vitu vingi
Kwa sababu hiyo bei ya infinix smart 7 plus inaongezeka kidogo
Maduka ya Vodacom wanaiuza kwa kiasi cha shilingi 260,000 (laki mbili na sitini)
Itel p17 Pro
Kwenye hii orodha itel P17 Pro ndio simu ya bei ndogo zaidi kuliko zingine zinazouzwa na vodacom
Bei yake ni shilingi 165,000 (laki moja na sitini na tano)
Hii inatokana na kutumia processor ambayo ina utendaji wa chini
Processor hiyo ni Spreadtrum SC7731 ambayo ina core nne
Processor za siku hizi huwa na idadi ya core zipatazo nane
Pia memori yake ni GB 32 na RAM ya GB 2 pekee
Inatumia kioo cha IPS LCD chenye resolution ndogo kama ilivyo kwa simu zingine zilizotangulia
Tecno Camon 20
Tecno Camon 20 ni simu mpya kabisa ambayo imetoka mwaka 2023
Ukinunua hii simu kwenye maduka ya vodacom unapata ofa GB 96
Hii ni kwa mujibu wa ukurasa rasmi wa Vodacom Tanzania
Bei yake haijainishwa hivyo ni vizuri ukawatembelea kupata taarifa zake kiundani
Lakini kiujumla inaendana kama ilivyoelezwa hapa, bei ya camon 20
Kwenye kundi hili hii ni simu ya daraja la kati na nzuri kwenye maeneo mengi tofauti na simu kuanzia namba moja hadi sita
Samsung Galaxy S23 Ultra
Hii ndio simu bora kwa hapa na moja ya simu kali duniani
Kama unataka ubora kwenye kamera, utendaji, ukaaji na chaji, network na kila kitu unachokijua wewe basi samsung galaxy s23 ultra ndio chaguo lenyewe.
Kumbuka hii sio simu ya laki mbili wala laki moja na nusu ni simu ya milioni mbili kwenda mbele
Hivyo bei yake kwenye maduka ya vodacom ni kuanzia mbili kwenda mbele
Fahamu: Ubora na Upekee wa Samsung Galaxy S23 Ultra
Maoni 18 kuhusu “Simu Mbalimbali za Vodacom Tanzania na Bei Yake”
Naitaji simu common 20 ila nalipa kidogo kidogo nko mwanza
Naitaji simu niko musoma
Naitaji simu common 20 nalipa kindogo kindogo niko musoma
Tembelea maduka ya mitandao ya simu utazikuta
Nahitaji vivo y02 nipo sengerema mwanza
Nahitaj vivo y02 nipo sengerema mwanza
naita samsung galaxy s23 ultra nipo mbeya
Nataka simu ya masomo
Nahitaji namba ya kulipa malipo ya simu naomba niipate kwa Leo,kwani Leo ndo mwisho.nipo ilala dar.
Tarehe ya malipo ya simu yangu ya mkopo ni Leo,nimesahau namba ya kulipa naomba mnitumie kwa haraka niweze kukamilisha malipo.
Wasiliana na Vodacom kiongozi Sisi sio voda
Nahitaji cm ya mkopo nipo Tanga Nina advance 20000
Hatuna hii huduma Kwa sasa, tembelea maduka ya voda
Nahitaji finix nipo tunduma naipataje kwa mkopo
Nahitaji simu ya mkopo finixi nipo tunduma
Nahitaji simu ya Tecno camon20
Nimevutiwa na Infinix Pop 7, inatolewa kwa mkopo?
Naiitaji Tecno camon20 Niko mwanza napataje