OnePlus inaweza ikawa ni jina geni kwa watumiaji wengi smartphone Tanzania
Ila OnePlus ni moja ya kampuni kutoka china inayotengeneza simujanja za madaraja ya kati na ya juu
Simu nyingi za OnePlus ni nzuri ni matoleo ya daraja la juu hushindana na simu za samsung na iphone
Hapa kuna orodha ya simu 20 za OnePlus na bei zake kwa mwaka 2024
1. OnePlus Nord N30 SE
Bei ya OnePlus Nord N30 SE: 450,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Simu ya OnePlus Nord N30 SE iliingia sokoni mwezi januari 2024
Inatumia chip yenye nguvu ya wastan, processor hiyo ni Mediatek Dimensity 6020
Ni simu ya kamera mbili ambapo kamera kubwa ina megapixel 50 na picha zake ni nzuri kwa kiasi fulani
Hii simu inasapoti chaji inayopeleka umeme wa wati 33
Hivyo betri yake ya 5000mAh inawahi kujaa kwa dakika chache
2. OnePlus 12R
Bei ya OnePlus 12R: 1,500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 8GB
OnePlus 12R ina kioo cha Amoled ambavyo huwa vina utajiri wa rangi
Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh na chaji yake inapeleka umeme mwingi wa wati 100
Kiwastani ndani ya nusu saa simu inaweza kujaa kwa 100%
Moja ya kamera yake inatumia teknolojia ya Laser AF kwenye ulengaji
Hii inasaidia kamera kutambua vizuri kitu kinachopigwa picha kikiwa hata kwenye mwanga mdogo
3. OnePlus 12
Bei ya OnePlus 12: 2,500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 512GB, RAM: 16GB
Simu ya OnePlus 12 ni toleo ambalo lilitoka mwezi desemba 2023
Ina ubora mkubwa kwenye kila idara kiasi cha kuwa na sifa nyingi zinazoendana na Samsung Galaxy S24 Ultra
Utendaji wa OnePlus ni mkubwa kwa sababu inatumia processor yenye nguvu ya Snapdragon 8 Gen 3
Kioo chake cha LPTO AMOLED kinaongezewa ubora na teknolojia ya HDR10+
Pia betri yake kubwa ina mAh 5400 na chaji yake ina kasi pia kwa maana ina wati 100
4. OnePlus Ace 3
Bei ya OnePlus Ace 3: 900,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 12GB
Simu ya OnePlus Ace 3 ilianza kuuzwa rasmi mwezi wa kwanza 2024
Utendaji wake ni mkubwa kwa ina chip ya Snapdragon 8 Gen 2
Na yenyewe inakuja na betri kubwa ya kukaa na chaji masaa mengi
Betri yake ina ujazo wa 5500mAh na haitoshi kuwa chaji inasapoti wati 100
Ina kamera tatu na kamera kuu ina OIS
OIS inasaidia kutuliza kamera ukiwa unarekodi video huku ukiwa unatembea
5. OnePlus Open
Bei ya OnePlus Open: 3,800,000/= ,Ukubwa wa Memori: 512GB, RAM: 16GB
OnePlus Open ni simu ya kufunika na kufunua
Pia upande wa nje una kioo na ukifunua pia kuna vioo kushoto mpaka kulia
Utengeneza wa simu wa aina unachangia simu kuwa na gharama kubwa
Ukizingatia OnePlus Open inatumia kioo cha amoled chenye teknoljia ya Dolby Vision
Betri yake inatosheleza kukaa na chaji muda japo ni 4800mAh
Na chaji yake inapeleka umeme wa wati 67
6. OnePlus Pad Go
Bei ya OnePlus Pad Go: 700,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 8GB
OnePlus Pad Go ni kishikwambi ambacho kina upana wa inchi 11.35
Hiki ni kipana zaidi ya vishikwambi walivyopatiwa walimu hapa Tanzania
Kioo chake ni cha aina IPS LCD chenye refresh rate ya 90Hz
Ina bonge la betri ambayo ni 8000mAh
Hivyo kukaa na moto muda mrefu ni swala la kawaida
Ila kamera yake sio nzuri na ina kamera moja pekee
7. OnePlus Ace 2 Pro
Bei ya OnePlus Ace 2 Pro: 1,100,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 12GB
OnePlus Ace 2 Pro ni simu ya mwaka 2023 na yenye utendaji wa kuridhisha
Kama ilivyo ada kioo chake ni cha AmOLED chenye rangi 1 Bilioni
Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh
Moja ya kitu cha kustaajabisha ni kasi yake kubwa ya kuchaji
Hii simu chaji yake inapeleka umeme wa wati 150
Simu inaweza kujaa ndani ya dakika 15
8. OnePlus Nord CE3
Bei ya OnePlus Nord CE3: 800,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 8GB
Simu ya OnePlus Nord CE3 ni simu ya daraja la kati yenye sifa nyingi nzuri
Ina macho matatu na kamera kuu ina megapixel 50
Na inaweza kurekodi video za 4K
Utendaji wake ni wa wastani kutokana na kutumia chip yenye nguvu za wastani
Chip hiyo ni Snapdragon 782G
9. OnePlus Nord 3
Bei ya OnePlus Nord 3: 1,10,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
OnePlus Nord 3 inatumia chip yenye nguvu katika utendaji wake ambayo ni Mediatek Dimensity 9000
Inatumia kioo cha Amoled chenye HDR10+ na refresh rate ya 120Hz
Hii simu itakupa faida ya kuchaji simu kwa haraka kwani chaji yake inapeleka umeme wa wati 80
Kamera yake kuu viwango vyake ni vikubwa kwa kutazama teknolojia ilizoambatana nazo
Kwa kifupi kamera yake inaweza kurekodi video za 4K
10. OnePlus Nord CE 3 Lite
Bei ya OnePlus Nord CE 3 Lite: 680,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 8GB
Simu ya OnePlus Nord CE 3 Lite ni simu ya daraja la kati iliyotoka mwanzoni mwa mwaka 2023
Inatumia processor yenye nguvu ya wastani kiutendaji, chip hiyo ni Snapdragon 695 5G
Tukija kwenye swala la betri na yenyewe ina 5000mAh
Kamera zake zipo tatu ila kamera kuu ndio nzuri kwa kiasi fulani japo sio kama OnePlus Nord 3
Kama ilivyo kwa OnePlus zingine na hii chaji yake ina kasi ya wati 67
11. OnePlus Ace 2V
Bei ya OnePlus Ace 2V: 900,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 12GB
Simu ya OnePlus Ace 2V inatumia processor ya Mediatek Dimensity 9000
Pamoja na kwamba hii simu imetoka mwaka 2023 mwanzoni kabisa ila ni simu inayofaa hata kwa mwaka 2024
Na yenyewe ni simu ya macho matatu kwa maana ina kamera ya wide, ultrawide na macro
Kamera kubwa zaidi ina megapixel 108
Betri na chaji ina viwango vya kuridhisha maana betri ni 5000mAh na chaji ni 80W
12. OnePlus Pad
Bei ya OnePlus Pad: 1,500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 12GB
OnePlus Pad imetoka mwaka 2023 mnamo mwezi April
Hii ni kishikwambi chenye sifa nyingi nzuri kwenye kila idara
Mfano kioo chake ni IPS LCD ambacho kina HDR10+, Dolby Vision na refesh rate kubwa ya 144Hz
Yaani kwa mpenzi wa magemu ataburudika sana na muonekano mzuri wa picha za gemu
Ikizingatiwa utendaji wake ni wenye nguvu kwani inatumia chip ya Mediatek Dimensity 9000
13. OnePlus 11R
Bei ya OnePlus 11R: 1,200,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 8GB
OnePlus 11R ina mwaka mmoja sasa tangu ilipotoka rasmi mwenzi februari 2024
Hata hivyo sifa zake upande wa kamera, chaji, kioo na betri inaipa simu kuendelea kuwa ni simu bora pia kwa mwaka huu
Chaji yake inapeleka umeme wa wati 100
Na kioo cha OnePlus 11R ni cha amoled chenye HDR10+ na refresh rate ya 120Hz, ni kubwa sana
Kamera yake moja wapo ina ulengaji wa multi-direction pdaf
14. OnePlus Ace 2
Bei ya OnePlus Ace 2: 1,100,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 12GB
OnePlus Ace 2 ilitoka mwezi februari mwakwa 2023
Inatumia processor yenye nguvu ya Snapdragon 8+ Gen 1
Kioo chake ni cha Amoled chenye HDR10+
Kasi ya chaji yake ni 100W na betri ina ukubwa 5000mAh
15. OnePlus 11
Bei ya OnePlus 11: 1,800,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 8GB
OnePlus 11 ni simu nyingine ya mwaka 2023 iliyo na ubora kwenye idara nyingi
Kioo chake ni cha amoled
Na ina kamera tatu ambazo zote ni nzuri
Chaji ya oneplus 11 ina kasi wati 80
Hivyo betri yake ya 5000mAh inawahi kujaa kwa haraka