SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu za itel na bei zake 2022(Chini ya Laki mbili)

Brand

Sihaba Mikole

March 3, 2022

Kwa mtumiaji wa simu mwenye bajeti ndogo kabisa basi itel inaweza ikakupa simu kwa kiasi kidogo cha pesa ulicho nacho.

Simu za itel nyingi ni simu za bei rahisi.

Lakini unafuu huo wa bei unatokana na sifa za simu husika.

Na simu nyingi za itel utakazoziona hapa ni simu za laki mbili na kushuka chini.

Itel huuza simu za daraja la chini kwa kiingereza hufahamika Lower End.

Si smartphone bora sana ukilinganisha na simu za vivo, xiomi, nokia, samsung, iPhone, oppo, Infinix, Tecno,Sony na nyinginezo.

Ila ni simu zinazoweza saidia matumizi ya kawaida kama kuingia kwenye mitandao ya kijamii.

Hapa kuna ya simu za itel za bei nafuu kwa mwaka 2022.

Kwa kiasi fulani hizi simu zinaweza kukusukuma.

Kabla ya kuamua kipi cha kuchukua simu yoyote iliyopo hapa.

Ni jambo la msingi sana kufahamu sifa za simu husika kwanza.

Simu ya iTel A58

Simu ya iTel ni simu ya 3G yenye android ambayo inayotumia mfumo endeshi wa Android 11 aina ya Go Edition.

Android ya Go Edition ni toleo la android kwa ajili ya simu zenye RAM ndogo chini ya 2GB

Ndio maana bei ya iTel A58 inaanzia shilingi laki moja na sitini(mpaka 180,000)

Mara nyingi simu zenye RAM ndogo zinakuwa na utendaji wa chini.

simu ya itel a58

Ili kuimarisha utendaji wa simu mfumo endeshi mwepesi wenye vitu vichache kama Android Go hutumika.

Processor ya simu ya iTel A58 ni Spreadtrum Unisco Sc7731E.

Unisco Sc7731E inatumia muundo wenye nguvu ndogo sana wa Cortex A7 kwenye core zote nne(Quadcore).

Kwa maana hiyo baadhi ya app zitashindwa kufunguka kwenye itel a58

Mfano wa applikesheni ambayo inaweza isifunguke ama ikakwama ni gemu la PUGB 2108.

iTel a58 haitumii display ya Amoled ambayo huwa haipotezi ubora wa rangi wa picha.

Mfumo wa memori wa iTel A58 unasafirisha data kwa kasi ndogo.

Na ram yake haina uwezo wa kusafirisha data nyingi na spidi yake ni ndogo.

Simu inaweza chukua muda kuwaka na baadhi ya app kuchelewa kufunguka

Mfumo wake wa kamera una kamera mbili pekee zenye resolution ndogo.

Hazina teknolojia yoyote ya autofocus wala OIS.

Pitia ukura huu uelewe umuhimu wa autofocus. autofocus kwenye simu za iphone

Mfumo wake wa chaji haupeleki umeme mwingi hivyo betri la iTel A58 lenye ujazo wa 4000mAh litachukua masaa mengi kujaa.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g
Processor(SoC)
  • CPU – Spreadtrum UNISOC SC7731E
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.3GHz Cortex-A7
  • GPU-Mali T820 MP1
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 11
  • Go Edition
Memori  16GB na RAM 1GB
Kamera Kamera mbili

  1. 5MP,(wide)
  2. QVGA
  3. 5MP(selfie)
Muundo Urefu-6.6inchi
Chaji na Betri
  • 4000mAh-Li-Po
Bei ya simu(TSH) 182,490/=

Simu ya iTel A17

Simu ya iTel A17 ni simu ya bei nafuu ambayo inauzwa chini ya laki moja na nusu.

Bei hii inachagizwa na sifa za simu ambazo ziko tofauti na simu za vivo za bei rahisi.

Kwa nini iTel A17 inauzwa bei rahisi?

Ni simu ya android yenye android toleo la kumi aina ya Go Edition.

simu ya itel a17

Go Edition hutumika sana kwenye simu zenye uwezo mdogo.

Processor ya itel A17 ina nguvu ndogo ambayo inafaa sana kwa app ambazo zinahitaji nguvu ndogo.

Processor hiyo ni SpreadTrum Unisoc Sc9831 yenye muundo wenye utendaji mdogo aina Cortex A53 kwenye core zote nne.

Inatumia kioo cha IPS LCD na hakina refresh rate kubwa ya 90Hz na kuendelea ya kufanya simu kuwa nyepesi.

Simu ina Ram ndogo ya 1GB na haiwezi kuhifadhi mafaili ya kutosha sababu ina ukubwa wa 16GB pekee.

Saizi ndogo ya ROM inalazimisha mtumuaji wa iTel A17 kununua memory card ya ziada.

Simu ni fupi na betri yake ni ndogo ambaloe haliwezi kutunza chaji muda mrefu hasa data ikiwa haijazimwa.

Sifa za iTel A17 kwa ufupi.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g
Processor(SoC)
  • CPU – UNiSOC SC9831E
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.3Cortex-A53
  • GPU-Mali-T820 MP1
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 10
  • Go Edition
Memori 16GB na RAM 1GB
Kamera Kamera moja

  1. 5MP,(wide)
  2. 2MP(selfie camera)
Muundo Urefu-5.0 inchi
Chaji na Betri
  • 2400mAh-Li-Ion
Bei ya simu(TSH) 140,910/=

Simu ya iTel P37 Pro

Simu ya iTel P37 Pro ni simu ya bei nafuu ya itel ambayo ina 4G.

Bei yake ni kubwa kidogo ukilinganisha na simu zilizotangulia.

Bei ya hii simu inaweza ikafikia laki mbili na themanini.

Kuna sababu chache amabzo zinasababisha hiyo bei.

simu ya itel p37 pro

Kwanza, Processor ya itel P37 pro ina core nane(octacore) ambazo zinatumia muundo wa Cortex A55 unaofahamika kwa matumizi madogo ya chaji.

Bado processor yake ya Unisoc SC9863A ina nguvu ndogo ambayo inaleta shida kwa baadhi ya app kufunguka.

Kioo chake ni cha IPS LCD  ambacho huwa kina rangi chache.

Memori ya iTel P37 Pro upande wa ram ukubwa umeongezeka.

Zipo P37 Pro za 32GB na 64GB na Ram 2GB na 3GB.

Betri ya itel p37 ni kubwa kwa ujazo wa 5000mAh.

Simu ina mfumo mbaya wa kamera ambazo hazina teknolojia ya OIS wala dual pixel autofocus.

Kamera zake haziwezi kurekodi video za 4k

Sifa za iTel P37 Pro kwa ufupi

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – UniSoC SC9863A
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×1.6 GHz Cortex-A55
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.2 GHz Cortex-A55
  • GPU-PowerVR GE8322
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 10
  • Go Edition
Memori  32GB,64GB na RAM 2GB,3GB
Kamera Kamera mbili

  1. 13MP,(main)
  2. 0.3MP(depth)
  3. 8MP(Selfie)
Muundo Urefu-6.8inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Ion
Bei ya simu(TSH) 274,890/=

Simu ya iTel P37

Simu ya iTel P37 ni moja ya simu ambazo hazina mtandao wa 4G.

Bei ya iTel P37 inafikia shilingi laki moja na themanini(180,000/=)

Simu ni ghari ukilinganisha na ubora wa simu na simu nyingi za android za bei rahisi

Kwa nini?

Processor ya iTel p37 ina nguvu ngodo sana kutokana na kutumia muundo wa Cortex A7.

simu ya itel p37

Processor ina core nne ambazo ni chache kwa nyakati hizi.

Haitumii vioo bora kwa sasa vyenye uangavu aina ya AMOLED bali vinatumia IPS LCD.

iTel p37 inaendeshwa na Android 10 Go Edition ambayo huwa na vitu vichache.

Ina ram ndogo ya 2gb na memori yenye kuhifadhi vitu vichache ya 32GB.

Mfumo wake wa kamera una kamera mbili zenye resolution ndogo.

Kamera haina dual pixel pdaf wala OIS.

Bodi ya iTel P37 imeundwa kwa plastiki na haina kioo cha gorilla glass.

Ina betri kubwa la 5000mAh linalofanya simu kukaa na chaji muda mrefu.

Mfumo wa chaji ya iTel P37 unapeleka umeme unaofanya betri kubwa kujaa masaa mengi.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g
Processor(SoC)
  • CPU – UniSoC SC7731E
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.3GHz Cortex-A7
  • GPU-Mali T820 MP1
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 10
  • Go Edition
Memori  2GB na RAM 32GB
Kamera Kamera mbili

  1. 8MP,(main)
  2. 0.3MP(depth)
  3. 8MP(selfie)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Ion
Bei ya simu(TSH) 177,870/=

Simu ya iTel A37

Simu ya iTel A37 ni simu ya android ya daraja la chini.

Sababu ya itel a37 kuwa kwenye daraja la chini ni kwa sababu ya sifa zake.

Processor ya smartphone ya iTel A37 ina nguvu ndogo kwa sababu inatumia muundo wa Cortex A7

Processor hiyo ni Spreadtrum UniSoC  SC7731E

simu ya itel a37

Inatumia android Go edition ambayo hutumika kwenye simu zenye uwezo mdogo.

Kioo chake ni aina ya IPS LCD ambacho huwa kinaonyesha rangi nyeusi ambayo sio halisi.

Simu ina uwezo wa kuhifadhi mafaili machache na applikesheni chache

Sababu kuu simu ina memori ndogo ya 16GB na RAM ya 1GB.

Kamera zake ambazo zipo mbili zina resolution ndogo na hazina teknolojia ya maana ya kulenga vitu kwa usahihi.

Uwezo wake wa kukaa na chaji ni mdogo kwa sababu inatumia  betri dogo la 3020mAh.

Simu imetengenezwa kwa bodi ya plastiki na kioo sio cha gorilla glass hivyo screen protector ni muhimu.

Kuna simu huwa hazihitaji screen protector kabisa mfano ni samsung s22 ultra.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g
Processor(SoC)
  • CPU – UniSoC  SC7731E
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.3 GHz Cortex-A7
  • GPU-Mali T820 MP1
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 10
  • Go Editon
Memori 16GB na RAM 1GB
Kamera Kamera mbili

  1. 5MP,(main)
  2. 5MP(selfie)
  3. 0.2MP(depth)
Muundo Urefu-5.71inchi
Chaji na Betri
  • 3020mAh-Li-Po
Bei ya simu(TSH) 154,770/=

Simu ya iTel S16

Simu ya itel s16 ni moja ya simu nzuri ya itel ukilinganisha na simu nyingi zilizopo kwenye orodha hii.

iTel S16 inatumia android toleo la kumi aina ya Go Edition.

Bei ya itel s16 inafika mpaka shilingi 190,000/=(laki na tisini)

simu ya itel s16

Processor ya simu ina core nane aina ya Cortex A55 ambazo zina nguvu ndogo na zinatumia umeme mdogo.

Kioo cha iTel S16 na chenyewe ni cha IPS LCD

Vioo vya LCD huwa vinaonyesha rangi chache.

Hivyo baadhi ya vitu vinapoteza uhalisia wa rangi yake.

Tazama hapa tofauti ya picha kwenye kioo cha IPS LCD na AMOLED.

amoled-vs-ips-lcd

Mfumo wake wa kamera kuu una resolution kubwa japokuwa inakosa OIS na dual pixel pdaf.

Betri yake ni kubwa kiasi cha 4000mAh ila upelekaji chaji ni mdogo.

Ram na Rom ni 2GB kwa 32GB ambazo bado ndogo vile vile.

Kwa wakati huu simu nzuri lazima iwe na RAM 4GB na 64GB upande wa ROM.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – UniSoC SC9863A 
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×1.6 GHz Cortex-A55
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.2 GHz Cortex-A55
  • GPU-PowerVR GE8322 
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 10
  • Go Edition
Memori  32GB na RAM 2GB
Kamera Kamera tatu

  1. 48MP(main)
  2. 2MP(Macro)
  3. 0.3MP(Depth)
  4. 8MP(selfie)
Muundo Urefu-6.6inchi
Chaji na Betri
  • 4000mAh-Li-Po
Bei ya simu(TSH) 187,110/=

Simu ya iTel A36

Simu ya itel a36 inafanana vitu vingi na itel a37.

Hivyo haina haja kuifafanua kiundani.

Bei ya iTel A36 inafika 174,000/=

simu ya itel a36

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g
Processor(SoC)
  • CPU – UniSoC SC7731E
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.3GHz Cortex-A7
  • GPU-Mali T820 MP1
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 9
  • Go Edition
Memori 16GB na RAM 1GB
Kamera Kamera moja

  1. 5MP,(main)
  2. 5MP(selfie camera)
Muundo Urefu-5.5inchi
Chaji na Betri
  • 3020mAh-Li-Ion
Bei ya simu(TSH) 173,250/=

Hitimisho

Bei za simu za iTel ni ndogo na kila mtu anaweza kuimudu.

Lakini bei ndogo ya simu inaambatana kwa 100% na ubora mdogo wa simu.

Ukizipitia kila simu ya itel zilizoorodheshwa utaona kamera mbaya, simu zina memori ndogo, processor yenye nguvu hafifu, betri ndogo na mengineyo mengi.

Ila bado ni simu zinazofaa kwa matumizi madogo.

Maoni 5 kuhusu “Simu za itel na bei zake 2022(Chini ya Laki mbili)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

samsung a06

[VIDEO]-ubora wa picha na kiutendaji wa Samsung Galaxy A06

Hii ni video inayokupa nafasi kushuhudia sifa za ziada za samsung galaxy a06 hasa upande wa kamera Kama hujui, Galaxy A06 NI simu mpya ya daraja la chini ambayo imetoka […]

No Featured Image

Bei ya Samsung Galaxy A06 na Ubora wake

Samsung Galaxy A06 ina betri inayokaa na chaji muda mrefu na ni simu ya daraja la chini Hii inamaanisha watu wengi kwa hapa Tanzania wanaweza inunua Kwa sababu bei ya […]

No Featured Image

Bei ya Tecno Spark 30C na Sifa Zake Muhimu

Tecno wameleta toleo jipya la simu ya madaraja ya chini yenye maboresho Ina maboresho upande wa skrini(kioo) kuwa na refresh rate kubwa ambayo mara hupatikana kwenye simu za daraja la […]

thumbnail

[VIDEO]:Simu zote za iPhone za bei ndogo na zinazofaa

Kabla ya kununua iphone za bei rahisi ambazo mara nyingi huwa ni used, kitu cha kwanza cha kuangalia ni kama itakuwa inapata sapoti ya kupokea mfumo endeshi wa iOS Tofauti […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company