Kampuni ya Tecno imeingia katika ushindani wa simu za 5G kwa kuzindua simu mpya ya Tecno Camon 19 Pro 5G
Bei ya Tecno Camon 19 Pro 5G inazidi laki saba kwa Tanzania kutokana na simu kuja na teknolojia imara zenye utendaji mkubwa
Hii ni simu ambayo imezinduliwa mwezi wa saba mwaka 2022
Ukizifuatilia sifa zake zitakuonyesha jinsi Tecno inavyoimalika katika kutengeneza simu
Baadhi ya sifa za CAMON 19 Pro 5G zinashindana na simu za Redmi na Oppo ambazo zinashika hatamu siku baada ya siku
Bei ya Tecno Camon 19 Pro 5G Tanzania
Tecno Camon 19 Pro 5G yenye GB 256 na RAM ya GB 8 inauzwa shilingi 760,000/= kwa maduka ya Dar Es Salaam
Bei inaweza ikawa isiwe moja na ikatofautiana kutoka duka moja hadi lingine
Lakini kiasi kilichotajwa ndicho sahihi
Kwa kuziangazia sifa za hii simu kuna maeneo inafanya vizuri
Kuna nyanja simu haijatendewa haki kiasi kinachofanya bei yake kutoendana na ushindani
Zitazame sifa za camon hii mpya kwenye jedwari.
Sifa za Simu ya Tecno Camon 19 Pro 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB, na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.8inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 760,000/= |
Ni upi wa simu aina ya Tecno Camon 19 Pro 5G?
Ubora mkubwa wa Camon 19 Pro 5G ni kuwa na utendaji mkubwa
Utendaji ambao umeifanya simu kuwa na sapoti ya mtandao wa 5G
Pia kioo chake ni kizuri kwa kucheza gemu
Kwa sababu kina refresh rate kubwa inayofanya simu kuwa nyepesi
Ina uwezo wa kupeleka chaji kwa haraka na betri kujaa kwa dakika chache
Na ukaaji wa chaji ni mkubwa kwani betri ya simu ni kubwa kiujumla.
Uwezo wa Network
Upande wa network simu inakubali kutumia mtandao wa 5G
Aina ya mtandao wa 5G simu inayotumia ni SA na NSA
SA kirefu chake ni Stand Alone na NSA inamaanisha Non Stand Alone
Unaweza kupitia: maana ya 5G kujua aina mbalimbali za 5G
Upande wa 4G haijainishwa aina ya masafa simu iliyonayo
Kutokana na aina ya processor simu inayotumia, kasi yake ya 4G inaweza kufika 1200Mbps
Kwa sababu chip yake huwa ina lte aina ya LTE Cat 18
Na simu pia ina GPS ya aina moja aina ya A-GPS (GPS ya Marekani)
Pitia: Kazi ya GPS kwenye simu na ufanyaji kazi wake
Ubora wa kioo cha Tecno Camon 19 Pro 5G
Kioo cha Tecno Camon 19 Pro 5G ni cha IPS LCD chenye resolution ya 1080 x 2460 pixels
Kioo chenye resolution kubwa huonyesha picha na video kwa ustadi mzuri
Ila vioo vya IPS LCD huwa vina rangi chache ukilinganisha na amoled
Hivyo basi baadhi ya vitu havitoonekana kwa rangi zake halisi
Hasa rangi nyeusi
Kuna uzuri kwenye screen ya camon kwani kuna refresh rate inayofika 120Hz
Tazama video hii inavoonyesha utofauti wa 120Hz(kushoto) na 60Hz(kulia)
Refresh rate ikiwa kubwa inasaidia screen ya simu kuwa nyepesi
Chukulia umefungua app ya meseji na ukakuta kuna meseji nyingi
Kisha ukaanza kutafuta meseji unayotaka kuisoma kwa ku-scroll (kutachi simu kwa kwenda juu au chini)
Kioo cha 120Hz kitakuwa kinascroll kwa haraka na kuifikia meseji ndani ya muda mfupi
Changamoto yake ni utimiaji wa moto mwingi
Nguvu ya processor MediaTek Dimensity 810
Kumbuka ukiwa na simu yenye processor dhaifu basi jua simu itakuwa dhaifu kwenye kila sehemu.
Ila sio MediaTek Dimensity 810 ambayo inaipa nguvu Tecno Camon 19 Pro 5G
Hii ni chip ya simu yenye utendaji mkubwa kutokana na muundo mzima wa core kubwa na core ndogo.
Ina jumla ya core zipatazo nane, core kubwa zipo mbili na core ndogo zipo sita
Uwezo wa Core Kubwa
Dimensity 810 ina core mbili ambazo hutumika pindi simu ikiwa inafanya kazi nyingi na kubwa kwa wakati mmoja
Mfano ukiwa unarekodi video za 4K au kucheza gemu basi core hizi mbili ndizo zitakazokuwa zinachakata kazi zote
Utendaji wake mkubwa unatokana na core kutmia muundo wa Cortex A76
Cortex A76 inaweza kufanya kazi 4 kwa mzunguko mmoja ndani ya sekunde
Izingatiwe clock spidi ya dimensity 810 ni 2.4GHz (mizunguko bilioni mbili nukta nne kwa sekunde)
Kutokana na nguvu hii, vipimo vya app geekbench inaipa chip alama zaidi ya 600
Na pia inafanya simu kuweza kucheza gemu ya Call of Duty: Mobile kwa resolution kubwa na kwa kasi ya 42fps
Hivyo picha za gemu zinaoonekana vizuri na bila simu kupata joto jingi
Uwezo wa Core Ndogo
Core ndogo zipo sita ambazo hufanya kazi pindi simu ikiwa inafanya kazi ndogo kama kupiga simu
Hizi ubora wake hupimwa kwa matumizi madogo ya umeme
Na huwa na utendaji mdogo kwa sababu zinatumia muundo wa Cortex A55
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Tecno Camon 19 Pro 5G ina ukubwa wa 5000mAh
Hivyo ukaaji wa chaji lazima uchukue masaa mengi hata ukiwa umewasha intaneti muda wote
Simu inakuja na chaji inayopeleka umeme wa wati 33
Ni kiasi kinachoweza kujaza betri ya simu ndani ya dakika 75
Hutokuwa na wasi pindi simu inapoisha chaji na ukiwa na haraka ya kuchaji
Ukubwa na aina ya memori
Upande wa memori kuna aina mbili za camon iliyopo kwenye posti hii.
Kuna camon ya GB 128 na Camon ya GB 256
Zote zinakuja na RAM ya GB 8
Kitu kichoisadia simu kufungua vitu vingi kwa wakati mmoja bila kukwama
Tecno hawajasema aina ya memori ambazo simu inatumia
Uimara wa bodi ya Tecno Camon 19 Pro 5G
Simu ina kimo cha inchi 6.8
Ni kimo kikubwa japo kuna baadhi ya watu wanapendelea simu ndogo
Hakuna pia taarifa kuhusu aina ya bodi simu inayotumia
Lakini kiujumla haina vioo vya gorilla ambavyo huwa ni vigumu kupasuka
Mfano ni kioo cha Gorilla Victus kilichopo kwenye simu mpya ya Xiaomi 12S Ultra
Ubora wa kamera
Hii simu unaweza kuita Tecno Macho Matatu
Kwani ina kamera za wide, macro na depth
Lakini ni kamera moja tu ndio yenye ubora unaotakiwa
Kamera za macro na depth zina resolution ndogo ya 2MP
Hivyo utoaji wa picha utakuwa wa kiwango cha chini na kibaya hazina aufocus wala OIS
Kumbuka macro ni aina ya kamera kwa ajili ya kupiga vitu ambavyo ni vya karibu sana na kamera
Kamera ya depth hutumika kutambua kitu au eneo linalotakiwa kuonekana kwa kiasi kikubwa
Hivyo kitu au eneo ambalo halitakiwi hutokea ukungu kwa nyuma
Ila ni simu ambayo haizwezi kurekodi video za 4k japokuwa simu ina processor yenye nguvu
Ubora wa Software
Tecno Camon 19 Pro 5G inakuja na Android 12 na mfumo wa HiOS 8.1
Ukiwa na HiOS 8.1 utaweza kutengeneza video yenye mkusanyiko wa picha zako
Pia ni mfumo ambao una app inayoitwa Phone Cloner
Phone Cloner inasaidia kuamisha vitu kutoka simu moja kwenda nyingine kwa haraka
Na pia tecno wameboresha mfumo wa kuscreenshot dokumenti
Yapi Madhaifu ya Tecno Camon 19 Pro 5G
Tecno Camon 19 Pro 5G haina mfumo wa kamera nzuri
Ukizingatia bei yake ni kubwa simu ilikuwa inastahili kuweka kamera inayoweza kurekodi video za 4k
Kwani kuna simu za laki nne ambazo zina kamera zinazorekodi video za 4K kwa kasi ya 60fps
Simu haina ulinzi wa vioo vya gorilla na pia bado inatumia kioo cha IPS LCD
Kamera zake zinatumia HDR ya kawaida badala ya angalau HDR10
Neno la Mwisho
Tecno Camon 19 Pro 5G inawafaa zaidi watu wanaotegemea simu kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja
Kama kamera na kioo sio kigezo kwako hii simu inafaa kuimiliki
Ila bei ya tecno camon 19 pro 5G ni kubwa
Kwa sababu simu ya Redmi Note 11 Pro 5G inapatikana chini ya laki saba
Kiubora Redmi inaicha Camon pakubwa
Maoni 8 kuhusu “Bei ya Tecno Camon 19 Pro 5G na Sifa Zake (Tecno Mpya)”
iko bomba sana
Tecno camon 19 ni simu ya gharama kubwa sana,hivo basi inatakiwa kuwa na ubora unaoendana na bei ya simu,64mp ni kubwa ila muonekano wa kamera haufanani na 64mp,maoni yangu waongeze ubora wa kamera
Nimefurahia uchambuzi wa kina kabisa, barikia! Vipi hakuna simu yenye betri ya 6000mah ya bei ya laki nne?
Zipo kuna za infinix na vivo
Maelezo yako yaeleweka mno, safi sana.
Mimi natumia camon 19 lakini mbona camera yake ipo quality sana kuliko hata samsung s9 na baaz ya googl pixel na nilishawah kushindanisha
Unaangalia vitu gani kutambua kuwa simu moja ina quality kuliko nyingine, na pixel ipi uliyoshindanisha.
Sim nzuri Sana mm natumia pamoja na mke wangu wote tu natumia camon 19