Simu ya samsung galaxy a33 5g ni simu ya daraja la kati inayoundwa na kamera nne.
Kwa jina lingine simu ya macho manne.
Galaxy A53 ni simu mpya ambayo imeingia sokoni aprili 2022
Simu ina ubora mwingi kwenye display, utendaji wa processor na uimara wa kuzuia maji kupenya
Kiujumla, sifa zake zina ubora kwenye nyanja zaidi ya tano kama utakavyoona kwenye posti hii.
Bei ya Samsung Galaxy A33 5G Tanzania
Bei ya samsung galaxy a33 kwa baadhi ya nchi za asia inaanzia shilingi 825,ooo/=
Kwa Tanzania bei inaweza ikazidi kidogo pindi hizi simu zitakopoingia kwa wingi
Bei isikushtushe sana.
Kwa sababu ni samsung ya a-series yenye ubora kwenye sehemu nyingi karibu zote.
Ila kuna vitu simu inavikosa kama vinavyojionyosha kwenye jedwari linoloonyesha sifa
Sifa za Samsung Galaxy A33 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super AMOLED, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | 128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.4inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 824,512.40/= |
Upi ubora wa Samsung Galaxy A33 5G
Kuujua ubora wa simu mpya ya samsung galaxy a33 5g tazama kioo chake.
Kioo cha simu kinazalisha rangi nyingi
Betri yake inakaa na moto muda mrefu
Simu ina utendaji wa kiwango cha kutosheleza
Ina ulinzi madhubuti kwenye screen, ulinzi unaoifanya simu kuwa ngumu
Hata sehemu zingine za simu zina ubora wa kuridhisha
Jifunze, vitu vya kuzingatia unaponunua simu yoyote
Kiubora, galaxy a33 inafanana vitu vingi na simu ya samsung galaxy a53 5g
Network
Samsung galaxy a33 inasapoti mitandao ya aina yote ikiwemo 4g na 5g
Simu ina network bands 15 za 4g ikiwemo bands zote zinazotumiwa na mitandao ya Tanzania
Zitambue: network bands za Tanzania za 4G
Kasi ya juu kabisa ya kudownload upande wa 4g inafikia 2Gbps
Na mtandao wa 5g una network bands 12.
5G ya samsung galaxy a33 inatumia 5g aina ya sub-6
Sub-6 hutumia miundombinu ya 4G kusafirisha data
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A33 5G
Kioo cha samsung galaxy a33 5g ni cha aina ya super amoled.
Samsung imepunguza refresh rate mpaka kufikia 90Hz
Wakati samsung galaxy a53 refresh rate yake ni 120Hz
Hata hivyo 90Hz inatosha kusukuma gemu kwa spidi inayoridhisha
Resolution yake pia ni nzuri aina ya FHD+(Full hd plus)
FHD+ ina pixel 1080 x 2400
Nguvu ya processor Exynos 1280
Exynos 1280 ni processor yenye nguvu kubwa.
Na gemu nyingi inasukuma bila simu kupata joto jingi.
Ila kuna magemu yenye graphics kubwa yanasababisha simu kupata joto.
Tazama hii video
https://www.youtube.com/watch?v=NXSFYISsZHU
Tumeifafanua hii processor kinaga ubaga kwenye kurasa ya galaxy a53
Uwezo wa betri na chaji
Simu ya samsung galaxy a33 5g inatumia betri kubwa la aina ya Li-Po
Betri ina ukubwa wa 5000mAh
Na simu inaweza kupitisha umeme mwingi wa wati 25
Kwa bahati mbaya simu haiji na chaji.
Hivyo ukinunua itakulazimu kununua chaji yake.
Sababu wanazozisema Samsung ni ulinzi juu ya mazingira.
Binafsi, haingii akilini bali ni mbinu mpya ya biashara
Ukubwa na aina ya memori
Ipo aina moja tu ya samsung galaxy a33 5g upande wa memori
Samsung a33 utakayoimiliki itakuwa na ukubwa wa GB 128
Na ram yenye ukubwa wa 8GB
Ni sazi inayotosha kuhifadhi mafaili na app nyingi
Na ram ya GB 8 inasaidia simu kufungua mafaili mengi kwa wakati mmoja kwa urahisi
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A33 5G
Upande wa screen simu ina kioo cha gorilla 5
Kwa mujibu wa corning waundaji wa vioo vya gorilla, gorilla 5 ni kioo kigumu kuvunjika endapo simu ikidondoka kwa urefu wa mita 1.2
Upande wa nyuma kuna plastiki.
Hii ni simu mpya nyingine ya 2022 isiyopitisha maji kwa muda wa nusu saa endapo ikizamishwa kwenye maji ya kina cha mita moja
Kiuhalisia galaxy a33 ina bodi ngumu na imara inayoweza kudumu muda mrefu
Ubora wa kamera
Simu ina kamera nne
Kati ya kamera hizo ni moja tu yenye teknolojia ya OIS
Na simu inatumia autofocus ya kawaida aina ya PDAF
Kwa bahati mbaya kamera za samsung galaxy a33 hazina kamera ya telephoto.
Hivyo mtumiaji wa simu atategemea digital zoom inayoweza kuzoom mara 10.
Changamoto ya digital zoom ni picha kupungua resolution
Upande wa video simu inaweza kurekodi video aina za 4k na full hd kwa spidi ya kawaida
Ubora wa Software
Simu inatumia android 12 na skin ya One UI 4.1
Ukiwa na one ui 4.1 utaweza kuongeza ram (2gb, 4gb, 6gb au 8gb)
Waakti android 12 imeongeza kitu kipya kwenye kuscreenshot.
Utaweza ku-screenshot ukurasa mzima kwa ukubwa utakaotaka
Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy A33 5G
Simu haiji na chaji hivyo utalazimika kununua chaji kutoka kwa samsung kama hauna chaji aina ya USB C
Pia samsung galaxy a33 haina sehemu ya earphone.
Hivyo utalazimika kununua adapter kama utahitaji kutumia earphone
Kamera zake hazitumii teknolojia bora za autofocus aina dual pixel pdaf au multidirection pdaf
Haina kamera aina telephoto na wala haina optical zoom
Neno la Mwisho
Simu ya samsung galaxy a33 5g ni moja ya simu bora ya daraja kati
Lakini mapungufu iliyonayo machache yanamshawishi mtu kutazama chaguao lingine.
Kwa mfano simu ya redmi note 11 pro+ 5g inachuana na matoleo mapya ya samsung kwenye kila kitu
Lakini ukitaka simu imara kwenye kila nyanja na ya bei rahisi, samsung galaxy a33 5g ni simu ya kuimiliki
Maoni 7 kuhusu “Ubora na bei ya simu ya Samsung Galaxy A33 5G[Simu Mpya]”
Asante kwa elimu unayotoa ili tuzifahamu simu, je kuna simu isiyokuwa na mapungufu ?
Haipo maana preference za watu hazipo sawa ndio maana kila mwaka kuna maboresho ya software na matoleo Malta yanakuja na vitu Bora zaidi
Naipata wapi mkuu?nikuje chapu
Naipata wapi mkuu,duka?
Upo mkoa gani?
Niko kahama nahitaji a53
Zipo zenye line 2 na mbona kuja nyingne adroid 13