Simu nzuri za bei rahisi nyingi huuzwa kuanzia 250,000 , 300,000 na kuendelea.
Ni ngumu kupata smartphone yenye uwezo mkubwa chini ya laki mbili labda iwe simu ya zamani.
Unapozungumzia simu nzuri lazima uongolee vitu vifuatazao.
Processor yenye uwezo wa kufungua app yoyote, simu inayokaa na chaji muda mrefu ikiwa inatumia intaneti, Kioo(display) kizuri, bodi imara inayozuia maji kupenya, simu inayopokea matoleo mapya ya android.
Na mengineo mengi ambayo yapo kwenye simu bora zifuatazo.
Na ukitaka kujua kwa nini hakuna simu nzuri ya bei nafuu fuatalia mlinganisho wa Samsung galaxy S22 ultra vs iPhone 13 Pro Max.
Kwenye post hii kuna simu za bei nafuu za Samsung, Tecno, Infinix, Xiaomi, Oppo na Vivo
Simu nzuri za bei nafuu
Samsung Galaxy A03S
Bei ya simu ya samsung galaxy A03S ni shilingi 346,350/=.
Hii ni bei ya wakati imezinduliwa mwaka 2021 mwezi wa nane .
Galaxy A03s inaweza ikaendelea kushuka bei chini ya hapo.
Galaxy a03s inatumia processor iliyotengenezwa na MediaTek.
Processor hiyo ni Helio P35.
Helio P35 ni chipset yenye nguvu ndogo kutokana na kuwa na muundo yaani core ya Cortex A53.
Kwa maana hiyo network ya 4G ya galaxy a03s ina spidi ya wastani.
Uwezo wa kucheza gemu inao ila si mkubwa.
Galaxy A03s haiwezi kucheza gemu la Call of Duty Mobile kwenye resolution kubwa(Full HD na ULTRA HD).
Jambo kubwa lililopo kwenye samsung hii ni kukaa na chaji muda mrefu.
Kwa sababu ina betri kubwa la 5000mAh.
Hii ni moja ya simu ya android inayotumia Android 11 na software ya samsung One UI 13.
Galaxy a03s zipo za aina mbili upande wa memori ambazo ni 32GB na 64GB zote aina eMMC.
Fuatalia kuhusu aina za memori kwa kutazama memori iliyopo kwenye samsung, sony na iphone.
Upande wa RAM zipo za 2GB, 3GB na 4GB
Samsung galaxy ni smartphone inayokaa na chaji na inamfaa mtumiaji mwenye matumizi madogo ya simu.
Kitu kimoja ambacho kimesahaulika kwenye posti ni kamera.
Kamera za hii simu si nzuri zinakosa dual pixel pdaf na OIS.
Na haziwezi piga picha na video za 4K.
Kwa mpenzi wa simu zenye kamera nzuri, ipuuzie hii simu kisha fuatilia simu zinazofuata ujue ipi ina unafuu.
Oppo A11s
Bei ya simu ya oppo A11s ni shilingi 363,792 bei ya mwaka 2021.
Matoleo ya mwaka 2021 bei za simu hushuka.
Ni simu nzuri ya bei nafuu ukilinganisha na Samsung A03s.
Oppo A11s inatumia processor iliyotengenezwa na Qulcomm.
Chip hiyo ni Snapdragon 460.
Snapdragon 460 ina nguvu ya wastani kutokana na kuwa na muundo wa Cortex A73 kwenye core zenye nguvu.
Hivyo 4G ya Oppo A11s ina kasi kubwa ya kudownload kwa spidi inayofika 600Mbps endapo mtandao ni mzuri.
Oppo a11s inaweza kucheza gemu la Call of Duty Mobile kwenye resolution kubwa ya Full HD.
Hii inasababishwa na kutumia gpu nzuri ya Adreno 610.
Simu hii ya oppo inakaa na chaji muda mrefu kwa sababu ya kuwa na betri kubwa 5000
Oppo a11s zipo za 64GB na 128GB zote ni eMMC 5.1.
Upande wa ram zipo za 4GB na 8GB.
Kamera zake tatu zinakosa vitu vya msingi yaani dual pixel PDAF na OIS.
Kwa mpenzi wa kamera usitarajie picha kali.
Nokia g10
Bei ya simu ya Nokia g10 ni shilingi 330,000/=
Ni bei ya mwaka 2021.
Hivyo simu ya Nokia g10 inaweza patikana chini ya bei ilitotajwa.
Nokia g10 inatumia processor ya MediaTek ya Helio P25.
Helio P25 ni chipset yenye nguvu ndogo.
Hivyo spidi ya simu ya mtandao wa 4G ni ndogo ambayo inaweza kufika 300Mbps kudownload.
Na app zinazohitaji nguvu kubwa kama gemu zinafunguka taratibu ama kwa shida.
Mfano gemu ya Call of Duty Mobile inakubali kucheza kwenye resolution ndogo.
Nokia g10 ina betri kubwa ya kudumu muda mrefu na chaji.
Ni simu ya bei bafuu ambayo ina Android 10.
Lakini simu inakubali kubadili android na kuweka toleo jipya la Android 11.
Kama ilivyo simu nyingi za bei nafuu, Kamera yake sio nzuri na haziwezi kurekodi video za 4k.
Na pia kamera ya nokia g10 inakosa teknolojia ya dual pixxel PDAF na optical zoom bila kusahau OIS.
Nokia g10 zipo za 32GB na 64GB zote aina ya eMMC 5.1
Na RAM zipo za 3GB na 4GB.
Bei zinatofautiana.
Kwa mpenzi wa magemu unaweza pia kuipuzia simu na kufautulia zingine zilizopo kwenye orodha.
Infinix hot 11s
Bei ya simu ya infinix hot 11s inaanzia shilingi 345,800/=
Infinix hot 11s inatumia processor yenye nguvu ya MediaTek Helio G88.
Helio G88 inaweza kusukuma application nyingi kwa sababu ya kutumia core zenye muundo wa Cortex A75.
Chipset Helio G88 kwa bahati mbaya ina modem ya 4G yenye spidi ya wastani.
Chipset hii inacheza gemu nyingi kwenye kila resolution.
Kwa mfano gemu PUGB Mobile linacheza kwenye resolution za Full HD na Ultra HD kwa spidi ya kuridhisha.
Bei ya infinix hot 11s inatofautiana kulingana na ujazo wa memori.
Infinix hot 11s ya 128GB yenye ram 6GB bei yake inafika shilingi 459,900
Zipo infinix 11s za 64GB na 128GB zote memori zake aina ya eMMC 5.1
Na pia ram zipo za 4GB na 6GB.
Kioo cha infinix hot 11s kina resolution kubwa ukilinganisha simu zilizotangulia.
Resolution yake ya 1080×2480 pixels inafanya screen ionyeshe picha safi.
Kamera yake si nzuri ila unafuu angalau kutokana na uwezo wa kurekodi video za resolution 1440p
Lakini inakosa vitu vya muhimu pamoja na kuwa na megapixel kubwa.
Kwa mpenzi wa kamera, unaweza kuifikiria Infinix hot 11s, lakini pia ipo simu nyingine ya bei nafuu unaweza kuifikiria zaidi ambayo ipo kwenye orodha.
Tecno Spark 7
Bei ya simu Tekno spark 7 inaanzia 230,000/= kwa maduka ya kariakoo na kinondoni.
Tecno spark 7 inatumia chipset ya MediaTek Helio A25.
Kwenye orodha ya simu iliyopo Helio A25 ndio processor yenye nguvu ndogo zaidi.
Baadhi ya application zitafunguka kwa taratibu
Na wakati mwingine simu inaweza kuanza kuchemka kadri inavyotumika sana tena kwa kazi ndogo.
Spidi ya 4G ya tecno spark 7 ni ndogo ambayo 150Mbps ni spidi ya juu kabisa.
Spidi ya 150Mbps inatosha sana tu kwa kuangalia video za youtube na mitandao ya kijamii.
Lakini si simu nzuri kucheza gemu kama la PUGB
Bei ya tecno spark inapanda kulingana na ukubwa wa memori ya simu
Bei itakuwa kwa spark 7 za 64GB inayotumia ram ya 3gb au 4gb.
Na bei ni ndogo kwa spark 7 za 32GB zinazotumia ram ya 3GB.
Kwa mpenzi wa kamera hii simu haifahi.
Inakosa teknolojia ya autofocus na ina kamera mbili.
Kama unataka kuchukua picha ya eneo pana tecno spark 7 haiwezi
Simu ya Tekno spark 7 inatumia mfumo endeshi wa android 11 na HIOS 7.5
Kwa watumiaji wanaohitaji simu inayotunza chaji basi spark 7 inafaa sana.
Ina betri kubwa la 6000mAh.
Kwenye orodha ipo simu yenye betri kubwa na ina uwezo mkubwa kwenye nyanja nyingi.
Fuatilia zaidi.
Redmi 9a
Bei ya simu ya xiaomi redmi 9a inaanzia shilingi 245,000/=
Bei inatofautiana kulingana na ukubwa wa memori na RAM
Kwa mfano.
Redmi 9a 32GB 2GB inauzwa shilingi 245,000/=
Redmi 9a 32GB 3GB inauzwa shilingi 270,800/=
Redmi 9a 64GB 4GB inauzwa shilingi 291,700/=
Redmi 9a 128GB 4GB inauzwa shilingi 333,300/=
Redmi 9a 128GB 6GB inauzwa shilingi 354,100/=
Ukitizama bei zinavumulika.
Redmi 9a inatumia processor ya MediaTek Helio G25.
Chip ya simu aina ya Helio G25 ina nguvu ndogo na yenyewe kutokana na core zote nane kutumia muundo wa Cortex A53.
Hivyo spidi ya 4G ya redmi 9a si kubwa.
Kutokana na kutumia chipset yenye uwezo mdogo, simu haina uwezo wa kusukuma gemu nyingi kwenye resolution kubwa yaani Full HD na Ultra HD.
Ukipita hii linki inayoelezea GPU iliyopo kwenye chip ya Helio G25, utaona kuwa Redmi 9a itashindwa kucheza gemu za LEAGUE OF LEGEND na CALL OF DUTY kwenye Full HD.
Simu ina kamera moja nyuma na selfie camera moja.
Na mfumo wake wa kamera si wa kuvutia kiujumla.
Kwa watu wanaohifadhi mafaili mengi kwenye simu Redmi 9a.
Kwa wapenzi wa kamera wanapaswa kufuatilia simu zingine za bei nafuu zilizopo
Umidigi a9 pro
Bei ya simu ya Umidigi A9 Pro inaanzia shilingi 300,900 /=
Bei inatofautiana kulingana na ukubwa wa memori ya simu na ukubwa wa ram.
Umidigi a9 Pro 64GB 4GB inauzwa shilingi 300,900 /=
Umidigi a9 Pro 128GB 6GB inauzwa shilingi 360,000/=
Umidigi a9 Pro 128GB 8GB inauzwa shilingi 401,200/=
Jina la hii simu ni geni kwa wengi ila ni simu ya bei nafuu yenye sifa nzuri ukilinganisha na simu zilizopo kwenye orodha.
Umidigi a9 pro inatumia processor yenye nguvu ya wastani ya MediaTek Helio P60.
Helio P60 inaweza kusukuma application nyingi kutokana na kutumia muundo wa Cortex A73 kwenye core mbili zenye nguvu.
Hivyo modem yake ina spidi kubwa ya kuupload(kupakia) vitu mtandaoni.
Mfumo wake wa kamera una kamera za aina nne lakini zote zinakosa OIS na dual pixel pdaf.
Kwa kufananisha na simu zilizotangulia Umidigi ina kamera nzuri kiasi japokuwa haina uwezo wa kuchukua video za 4k
Mfumo wake wa memori ni aina ya UFS 2.2 ambao huwa unasafirisha data kwa kasi ukilinganisha na memori za eMMC.
UFS 2.2 inasaidia simu kuwaka kwa haraka na application kufunguka kwa upesi
Display yake ina resolution(2340*1080) kubwa inayoonyesha picha safi.
Simu inatumia android 10 sidhani kama inaweza kuupdate kuweka Android 11.
Kwa bahati betri yake si kubwa sana kwani lina ukubwa wa 4150mAh.
Kwa wanaojali pafomansi(nguvu) kubwa ya simu basi umidigi a9 pro ni simu ya bei nafuu yenye uwezo mkubwa.
Na hata kamera.
Hitimisho.
Kwa kuziangalia simu zilizoorodheshwa hapa asilimia kubwa ya simu za bei nafuu huwa zina uwezo mdogo.
Ni brand chache zinazoweka vitu ambavyo vinaboresha uwezo wa simu kiutendaji.
Simu za bei nafuu zinafaa kwa mtu mwenye bajeti ndogo ama anayeanza kutumia simu.
Processor nyingi za MediaTek ambazo zina uwezo mdogo zimetumika kwenye simu zilizopo.
Kama unataka simu nzuri ni lazima bajeti yako ikiongezeke ya kununua simi.
Simu za bei nafuu za itel hazipendekezwa hapa kwa sababu nyingi zina ubora mdogo.
Maoni 2 kuhusu “Simu Nzuri za Bei Rahisi Chini ya 350,000/-”
Kati ya infinix note 30 VIP na google pixel 5 ipi nzuri?msaada wenu jamani
Pixel 5 bila shaka, Ila infinix note 30 VIP ina utendaji mkubwa zaidi.