Tangu mwaka 2023 umeingia, kuna matoleo mapya simu janja ambayo yametoka mwishoni mwa mwaka 2022 na mwanzoni 2023 na mengine yatatoka baadae.
Katika hizo simu mpya zipo za bei ndogo, kubwa, nzuri na mbaya
Hii post imeorodhesha simu nzuri matoleo mapya kwa mwaka huu wa 2023 na yale ya mwishoni mwa mwaka 2022.
Simu Nzuri maana yake ni simu ambayo imekamilika kila idara na yenye mapungufu kidogo sana.
Hivyo bei zake haziwezi kuwa ndogo lazima ziwe juu.
Fuatililia ufafanuzi kuanzia kwenye ubora mpaka bei za kila simu
iPhone 14 Pro
Simu ya iPhone 14 Pro imetoka mwezi wa tisa 2022
Kwa upande wa apple bado ni simu mpya kwani hakuna toleo jipya la iphone kwa mwaka 2023 mpaka mwishoni mwa mwaka
Utendaji wa iPhone 14 Pro ni mkubwa sana kwa sababu ina chip(processor) ya Apple A16 Bionic
Ukaaji wake wa chaji unafika masaa 14 ukiwa unatumia intaneti muda wote
Ina kioo chenye uangavu mkubwa, kioo hiko wanakiita LTPO Super Retina XDR OLED
Kamera yake inapiga picha kwa ustadi kwa mazingira yote ya mwanga hafifu na mwanga mwingi
Unaweza ifuatalia hii simu kupitia, ubora kuhusu iPhone 14 Pro
Bei ya iPhone 14 Pro
Bei ya sasa ya iPhone 14 Pro inafika shilingi 2,600,000/=
Bei itazidi kama utahitaji iphone 14 Pro yenye memori kubwa zaidi kwani yako matoleo kama matatu
Xiaomi 12 Pro
Xiaomi ni kampuni ya China inayosifika kwa kuunda simu kali na kwa bei nafuu
Mwishoni mwa mwaka 2022 walizindua toleo la Xiaomi 12 Pro simu yenye kamera tatu huku kila kamera 50MP
Hii ni simu yenye kioo kiangavu na chenye ufanisi wa uoneshaji rangi kwa usahihi
Kwani kioo chake cha LTPO amoled chenye refresh rate ya 120Hz, Dolby Vision na HDR10+
Xiaomi 12 Pro inakuja na chaji ya wati 120 ambayo inajaza simu kwa 100% ndani ya dakika 18 tu
Pia inauwezo wa kuchaji simu kwa “wireless” yaani bila kutumia waya wa chaji
Cha kufurahisha ni kuwa bei yake sio kubwa sana na inaendana na simu ya Oppo Reno8 5g ila oppo inazidiwa mbali
Bei ya Xiaomi 12 Pro
Xiaomi 12 Pro ya GB 128 inauzwa shilingi 1,200,000/= mpaka ikufikie hapa Tanzania
Gharama inaweza ikawa chini kabisa kama ukinunua kwa kuagiza nje yaani Aliexpress
Vivo X90 Pro
Vivo X90 Pro ni simu ya Android 13 ambayo imetoka imetoka mwezi novemba 2022
Hii ni simu bora kabisa ya vivo kwani ina utendaji wenye nguvu kutokana na kutumia chip ya Dimensity 9200
Kioo chake ni cha amoled chenye refresh rate ya 120Hz na resolution 1260 x 2800 pixels
Hivyo swala la muonekano wa vitu kioo kinanyesha kwa ubora mkubwa
Vivo X90 Pro iko fasta kwa sababu inatumia memori aina ya UFS 4.0
Mfumo wake wa kamera una kamera tatu ambazo ufanisi wa upigaji picha ni wa kiwango kinachoendana na iPhone 14 Plus au samsung galaxy s23
Inakuja na chaji yenye kupeleka umeme mwingi hivyo betri yake 4870mAh inajaa 50% kwa dakika 8 tu
Bei ya Vivo X90 Pro
Bei ya Vivo X90 Pro inafika shilingi milioni mbili (2,000,000/=) ya GB 256
Hii ni bei ya Aliexpress hivyo kwa hapa Tanzania bei inaweza kuwa juu kidogo
Sony Xperia 5 IV
Simu ya Sony Xperia 5 IV imetoka mwezi septemba mwaka 2022
Ila ni simu inayochuana na simu zingine uzionazo kwenye orodha
Inatumia chip yenye utendaji mkubwa ya Snapdragon 8 Gen 1
Hivyo kama unacheza gemu simu haitogandaganda
Ina betri kubwa ya kukaa chaji masaa mengi kwani ukubwa wake ni 5000mAh
Ni simu yenye uwezo wa kuzuia maji kuingia ndani ya simu kutokana na kuwa na IP68
Ina kamera tatu zenye 12MP ila picha zake ni kali na za kuvutia
Bei ya Sony Xperia 5 IV
Bei ya sony xperia 5 iv kwa hapa Tanzania inaweza fika 1,800,000/=
Ni bei inayoshahibiana na ubora wa simu kwenye kila kipengele
OPPO Reno8 T 5G
Oppo Reno8 T 5G ni simu ambayo imeingia sokoni mwezi februari 2023
Ni simu inayotumia kioo cha AMOLED chenye uwezo wa kuonyesha rangi bilioni moja
Maana yake ni kuwa kioo kitaonyesha kitu kwa rangi zake halisi kwa kiwango kikubwa
Kwenye upande wa kamera simu haivutii sana
Kamera kuu(wide) ni nzuri lakini kamera zengine kiuhalisia ziko kama pambo kwani zina megapixel 2 ambayo ni ndogo
Chaji yake inakuja na uwezo wa kupeleka wati 67, hivyo chaji itawahi kujaa haraka
Bei ya Oppo Reno8 T 5G
Bei ya OPPO Reno8 T 5G ni shilingi za Kitanzania 800,000/=
Ni kiwango kidogo ukilinganisha na simu ziliainishwa hapa
Ila bei inaweza kuwa kubwa sababu simu ina kasoro kadhaa
Tecno Phantom X2 Pro
Kama unatafuta simu nzuri zaidi ya Tecno basi Tecno Phantom X2 Pro ndio jibu sahihi
Kiubora inaweza kuachwa mbali na Vivo X90 au Xiaomi 13 Pro ila ni simu ya daraja la juu yenye utendaji mkubwa
Utendaji mkubwa unasababishwa na simu kutumia chip ya Dimensity 9000
Ni tecno inayotumia kioo cha amoled ambavyo ubora wa uonyeshaji rangi za sahihi vitu ni mkubwa\
Ina betri kubwa na chaji yenye kasi
Hata mfumo wa kamera umeboreshwa, kamera zake zinaweza kuchukua video za 4K
Bei ya Tecno Phantom X2 Pro
Tecno ya GB 256 inapatikana kwa shilingi 1,500,000/=
Ni nadra kukutana na Tecno ikiwa na bei kubwa kiasi hiki lakini hii simujanja yenye maboresho mengi toka Tecno
Samsung Galaxy S23 Ultra
Kwenye hii orodha hakuna simu yenye kamera nzuri kama Samsung Galaxy S23 Ultra
Hii ni samsung mpya ya mwaka 2023 ina kamera nne zinazoweza toa picha nzuri iwe usiku ama mchana
Betri yake ni kubwa na ukaaji wa betri uanfika masaa 12 ukiwa unatumia intaneti ya 5G
Inatumia kioo aina ya dynamic amoled, na vioo vya amoled huwa ni vizuri tu kiujumla
Utendaji wake ni mkubwa kwani unakaribiana na simu iPhone 14 Pro Max
Bei ya Samsung Galaxy Ultra
Kwa hapa Tanzania hii simu utaipata kwa zaidi ya shilingi milioni 2.9
Ni samsung yenye kasoro chache sana
Inahitaji mtu mwenye bajeti kubwa kuimiliki
Samsung Galaxy S23+
Hili ni toleo jipya lingine ambalo limetoka pamoja na Samsung Galaxy S23 Ultra
Kisifa ni kuwa Galaxy S23+ inaendana na mkubwa isipokuwa utofauti upo kwenye kimo na kamera
Samsung hii ina macho matatu na haiji na peni
Ila mfumo wake wa chaji unaweza kupokea wati 45 hivyo inafanya simu kujaa kwa dakika chache
Kwa mpenzi wa simu ya urefu wa wastajni, hili toleo linafaa
Unaweza ifahamu zaidi hii simu hapa, ubora uliopo kwenye Samsung Galaxy S23+
Bei ya Samsung Galaxy S23+
Bei ya Samsung S23+ inafika shilingi 2,400,000/= kwa toleo yenye memori ndogo
Ila bei itakuwa kubwa zaidi kwa S23+ za GB 512
Realme 10 Pro
Realme 10 Pro ni simu ya bei ndogo zaidi iliyotokea kwenye list
Ni simu ya 5G yenye utendaji wa wastani
Inatokana na Realme 10 Pro kutumia processor ya Snapdragon 695 5G
Ina kamera zipatazo mbili ila moja ndio inayoweza kutoa picha zinazovutia
Chaji yake inaweza kupeleka umeme wa wati 33
Si umeme mwingi sana ila unajaza simu kwa dakika chache
Utendaji wakw ni wa wastani
Bei ya Realme 10 Pro
Bei ya simu ya realme 10 pro inafika shiligni 610,000
Hii ni bei ya realme 10 pro ya GB 128 na RAM ya GB 8
Ukiiangalia ukubwa wa memori na sifa zake zingine, bei inaendana na ubora
Xiaomi 13 Pro
Xiomi 13 Pro iliingia sokoni mwezi desemba mwaka 2022
Ina miezi miwili na inatumia toleo jipya la android yaani Android 13
Kioo chake ni aina LTPO AMOLED chenye uwezo wa kuongeza au kupunguza refresh rate kutokana na matumizi
Ni simu inayokuja na chaji ya wati 120 hivyo ujaaji wa chaji ni wa dakika kadhaa.
Ina kamera tatu zote zenye 50MP na zinapiga picha nzuri kwenye mazingira yoyote
Pia zinaweza kuchukua mpaka ya kiwango cha 8k
Utendaji wake unaendana na simu za samsung s23 kutokana na kuwa na processor ya aina ya Snapdragon 8 Gen 2
Bei ya Xiaomi 13 Pro
Bei ya Xiaomi 13 Pro ni shilingi 2,000,000/=
Hiyo bei inaakisi kwa kiasi kikubwa vitu ambavyo simu inayo
Maoni 10 kuhusu “Simu Nzuri Matoleo Mapya na Bei Zake 2023”
Mimi ninahitaji kioo cha simu aina Samsung Galaxy m22
Je Tecno 8c bei
8c ni 240,000
Kwa Tanzania bei
Mkuu nimesoma maelezo yako yaneenda shule sana ila samsung naziogopa sana gharama ya kioo ni bei ya simu ingine napendezewa na Xi
Mkuu nimesoma maelezo yako yaneenda shule sana ila samsung naziogopa sana gharama ya kioo ni bei ya simu ingine napendezewa na Xiaomi japo hujagusia Google piexl
Naitaj infinix not 20 iwe na sitoreg 228 je naweza kuipta?
Storage ya 228 haipo
Hizo ndio sm Bora kidunia nzima au
Maelezo yenu yako poa sana ila hizi simu za SAMSUNG kioo kikizingua inabidi tu uiweke kwenye droo maana vibei sana