SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu 14 mpya za Vivo za ubora mkubwa na bei zake (2024)

Simu Mpya

Sihaba Mikole

March 11, 2024

Tangu mwishoni mwa mwaka 2023 mpaka mwaka huu 2024 Vivo imeachia matoleo mengi ya simu

Katika matoleo hayo yapo ya bei ndogo, bei ya kati na bei kubwa

Kwa maana inalenga watumiaji wa simu wenye hali zote za kiuchumi

Hivyo basi hapa tunakuletea simu mpya za vivo na bei zake ambazo zimetoka kati ya desemba 2023 na mwaka 2024

Kuna simu zipatazo 15 kwenye orodha na nyingi ni nzuri kwa kiasi kikubwa

1. Vivo V30 Pro

Bei ya Vivo V30 Pro: 1,300,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  8GB

Simu ya Vivo V30 Pro ni simu iliyotoka februari 2024

Inatumia processor yenye nguvu ya wastani, chip hiyo ni Mediatek dimensity 8200

Kioo chake cha amoled kina utajiri wa rangi na kina HDR10+

Hii ni moja ya simu yenye kamera inayopiga nzuri kwenye kamera zote tatu

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh na kasi yake ya chaji ni wati 80

2. Vivo Y100t

Bei ya Vivo Y100t: 600,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  8GB

Simu ya Vivo Y100t iliingia rasmi februari 2024 kama ilivyo kwa Vivo V30 Pro

Inatumia chip ya dimensity 8200

Bei yake ni ndogo ukilinganisha na Vivo Y100t  inatokana na aina ya kioo chake na hata kamera

Kwani ina kamera mbili lakini kamera moja ndio nzuri zaidi

Na pia kioo chake sio cha Amoled bali ni IPS LCD ila hakina HDR10+

3. Vivo IQOO Neo9 Pro

Bei ya Vivo IQOO Neo9 Pro: 1,300,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  8GB

Hii ni simu ambayo na yenyewe imetoka mwezi februari 2024

Inatumia chip yenye nguvu kubwa kiutendaji ya Snapdragon 8 Gen 2

Kioo chake ni cha aina ya LTPO AMOLED na refresh rate yake ni kubwa inayofika 144Hz

Chaji yake inapeleka umeme wa kujaza betri ndani ya dakika 20 kutokana na kuwa na kasi ya wati 120

Ila ina kamera mbili tu huku kamera kubwa ikiwa na uwezo wa kurekodi video za 4K

4. Vivo Y200e

Bei ya Vivo Y200e: 630,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  6GB

Simu ya Vivo Y200e iliingia sokoni mwaka 2024 mwezi wa februari

Ina utendaji wa juu wa kuridhisha japo sio mkubwa sana kama IQOO Neo9 Pro

Hii inatokana na kutumia processor ya Snapdragon 4 Gen 2

Ina jumla ya kamera mbili tu huku kamera kubwa ikiwa na megapixel 50

Chaji yake inapeleka umeme wa wati 44

5. Vivo V30

Bei ya Vivo V30: 1,100,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  8GB

Kamera za Vivo V30 zipo tatu ambazo ni ultrawide, wide na ya tatu haijaainishwa

Utendaji wake ni wa kuridhisha kwa sababu inatumia chip ya Snapdragon 7 Gen 3

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh wakati huo chaji yake inapeleka umeme wa wati 80 unaoweza jaza simu kwa 100% ndani ya dakika 40

Kioo chake ni cha amoled na kina HDR10+

6. Vivo Y100(IDN)

Bei ya Vivo Y100(IDN): 630,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  8GB

Hii ni simu ambayo ilitoka mwezi januari mwaka 2024

Ni simu yenye sifa nzuri katika nyanja za utendaji, kioo na hata chaji na betri

Kioo chake kina HDR10+ na pia ni cha aina ya AMOLED

Chajji yake ina wati 80 inayojaza betri kwa dakika 45 pekee

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh hivyo inakaa na moto muda mrefu

7. Vivo Y28

Bei ya Vivo Y28: 450,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  4GB

Hii ni simu ya daraja la kati iliyotoka mwezi januari 2024

Utendaji wake ni wa wastani kutokana na kutumia chip ya mediatek dimensity 6020

Ubora wa kioo chake sio mkubwa kwa sababu resolution yake ni 720 x 1612 pixels

Kamera zake zipo mbili na zinarekodi video za full hd pekee na sio 4K

Betri yake ni kubwa ila kasi ya chaji yake ni wati 15 hivyo inachukua muda kujaa

8. Vivo G2

Bei ya Vivo G2: 450,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  4GB

Vivo G2 ni simu nyingine ya mwaka 2024 ambayo imetoka januari

Hii simu ina utendaji wa wastani na kuna baadhi ya sifa zina ubora wa chini

Kwa mfano kioo chake ni cha IPS LCD ambacho resolution yake ni ndogo

Kamera yake inaweza kurekodi video za full hd kwa kiwango cha 30fps

Na yenyewe ina betri kubwa ila chaji haina kasi kubwa kwani inapeleka umeme wa wati 15

9. Vivo V30 Lite

Bei ya Vivo V30 Lite: 1,400,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  8GB

Simu ya Vivo V30 Lite ni simu ya mwaka 2023 iliyotoka desemba

Kwa maana hivyo bado ni simu mpya kwa mwaka 2024

Utendaji wake ni wa kiwango cha kati hii kwa sababu inatumia processor ya Snapdragon 695 5G

Chaji yake inapeleka umeme wa wati 44 hivyo betri lake la wati 4800mAh inajaa kwa haraka

Hii simu ina kamera tatu yaani macho matatu na moja ya kamera ina OIS kwa utulivu wakati wa kurekodi video ukiwa unatembea

10. Vivo IQOO Neo9

Bei ya Vivo IQOO Neo9: 1,200,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  8GB

Simu ya Vivo IQOO Neo9 ni simu ya vivo iliyotoka desemba 2023

Utendaji wake ni mkubwa kwani inatumia chip yenye nguvu ya Snapdragon 8 Gen 2

Ina jumla ya kamera mbili huku kubwa ikiwa na megapixel 50 na OIS

Chaji yake ya wati 120 inajaza simu kwa 40% ndani ya dakika 9

Na betri lake lina ukubwa wa 5160mAh

11. Vivo S18 Pro

Bei ya Vivo S18 Pro: 1,200,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  8GB

Vivo S18 Pro ni simu nyingine kali ya vivo ya mwaka 2023 ila ilitoka mwezi desemba

Inatumia processor yenye nguvu ya Mediatek Dimensity 9200+

Kioo chake ni cha AMOLED na kina refresh rate ya 120Hz

Kamera zake tatu na zinaweza kurekodi video za 4K

Chaji yake inapeleka umeme mpaka wa wati 80 na betri yake ina 5000mAh

12. Vivo S18

Bei ya Vivo S18: 850,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  8GB

Kwenye desemba 22 mwaka 2024 ndio mwaka ambao simu ya Vivo S18 iliingia rasmi sokoni

Nguvu ya kiutendaji ni ya kuridhisha japo sio kama simu ya Vivo S18 kwa sababu yenyewe inatumia chip ya Snapdragon 7 Gen 3

Pia kioo chake ni kizuri kwani cha Amoled

Ina kamera mbili tu na kamera kubwa ina megapixel 50

Chaji yake inapeleka umeme mwingi wa wati 80 na betri yake ina 5000mAh

13. Vivo S18e

Bei ya Vivo S18e: 780,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  8GB

Simu ya Vivo S18e ni simu ya daraja la kati ambayo ilitambulishwa mwezi desemba na kuanza kupatikana rasmi januari 2024

Inatumia chip ya Mediatek Dimensity 7200 ambayo nguvu yake ni ya wastani

Betri yake ina ukubwa wa 4800mAh na chaji ni wati 80

Ina kamera mbili tu huku kamera kubwa ina megapixel 50

Kioo chake ni cha amoled chenye refresh rate ya 120Hz

14. Vivo Y36i

Bei ya Vivo Y36i: 450,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  4GB

Hii ni simu ya daraja la kati ambayo ilianza kupatikana mwezi januari 2024 ila ilitangazwa mwezi desemba 2023

Inatumia processor ya Mediatek dimensity 6020

Ina kamera moja tu yenye megapixel 13 na ulengaji wa PDAF

Hii kamera inaweza kurekodi video za full hd yaani 1080

Ukubwa wa betri ni 5000mAh na chaji ina kasi ya wati 15

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

vivo y02t

Bei ya Vivo Y02t na Sifa Zake

Vivo Y02t ni simu ya bei nafuu ambayo imetoka katikati ya mwaka 2023 Bei ya vivo y02t haizidi laki tatu kwa hapa Tanzania kutokana na aina ya sifa ambazo simu […]

Jinsi ya Kutumia GPS kwenye Simu (Hatua kwa Hatua)

GPS kirefu chake ni Global Positioning System, ni mfumo wa utambuzi wa maeneo ambao unasimamiwa na Marekani Simujanja karibu zote zina huu mfumo Una faida kubwa sana hasa kama unajua […]

samsung fold 4 camera

Simu 10 Zenye Kamera Nzuri na Bora 2023

Mwaka 2023 yapo mateo ya simu yaliyoingia sokoni yakiwa na kamera nzuri na bora kwa kupigia picha na kurekodi video Kuna simu zenye kamera kali zaidi na mfumo mzuri kwenye […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram