SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Vivo Y02t na Sifa Zake

Bei Nafuu

Sihaba Mikole

November 20, 2023

Vivo Y02t ni simu ya bei nafuu ambayo imetoka katikati ya mwaka 2023

Bei ya vivo y02t haizidi laki tatu kwa hapa Tanzania kutokana na aina ya sifa ambazo simu inakuja nazo

Bei yake na sifa zake inaendana sana na simu ya OPPO A17K

vivo y02t

Ukitazama sifa za vivo y02t utagundua kuwa ipo katika kundi la daraja la chini

Kwa maana ni simu mahsusi kwa watu wenye matumizi ya kawaida na si matumizi makubwa ya simujanja

Bei ya Vivo Y02t ya GB 64

Kwa Tanzania bei ya hii simu ni shilingi 300,000/= yenye ukubwa wa GB 64

Vivo Y02t sio simu inayolenga mtumiaji mwenye uhitaji wa vitu vyenye ubora mkubwa

Yaani mtumiaji anaelengwa hapa ni yule anaetumia mitandao ya kijamii kidogo na vitu kama kupiga simu

Kwa mahitaji hayo simu huja na vitu vyenye ubora mdogo

Kitu kinachopelekea bei kuwa ndogo ukilinganisha na iphone 15 pro max kama utakavyoona kwenye jedwari la sifa za simu

Sifa za Vivo Y02t

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio P35
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.35 GHz Cortex-A53
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.8 GHz Cortex-A53
  • GPU-PowerVR GE8320
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 13
  • Funtouch 13
Memori eMMC 5.1, 64GB,32GB na RAM 4GB
Kamera Kamera moja

  1. 8MP
Muundo Urefu-6.51inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-10W
Bei ya simu(TSH) 300,000/=

Upi ubora wa Vivo Y02t

Betri yake ni kubwa inayoweza kukaa na chaji muda mrefu

Inasapoti mtandao wa 4G hivyo unapata mtandao wa wenye kwa kutumia kifaa cha bei nafuu

Hii ni simu yenye matumizi madogo ya umeme kwenye kazi ndogo ndogo

Nyanja zingine ni za kawaida zenye ubora wa kawaida pia

Uwezo wa network

Vivo Y02t inasapoti mpaka mtandao wa 4G aina ya LTE Cat 7

Kasi ya kupakua vitu ya LTE Cat 7 inafika 300Mbps

Kwa maana kama ukiwa unadownload faili la ukubwa wa MB 375 simu inaweza kuchukua sekunde 10 kumaliza

Ila kumbuka kwa hapa Tanzania huwezi kupata kasi hii kama hutumii mtandao wa 5G

Na kasi hiyo kuipata pia itahitaji gharama za ziada

Kiujumla uwezo wa network ni mzuri kiasi chake

Ubora wa kioo

Kioo cha vivo y02t ni cha IPS LCD chenye resolution ya 720 x 1600 pixels

Hii sio resolution kubwa lakini vitu kwa kiasi vitaonekana vizuri japo si kama muonekano wa vioo vya AMOLED au OLED

Vioo vya amoled vina faida ya kuwa na resolution kubwa na kina kikubwa cha rangi

Kwa bahati mbaya kioo cha hii vivo haina teknolojia ya kuongeza kina chqa rangi

Kwa maana hakisapoti HDR ama dolby vision

Hata hizi teknolojia hutumika sana kwenye simu za bei ghari

Usitarajie simu ya bei ya chini kuwa nazo

Nguvu ya processor Mediatek helio P35

Vivo Y02t inapewa nguvu na chip ya mediatek helio P35

Uwezo wa helio P35 wa kiutendaji ni mdogo kwa sababu muundo uliotumika ni wa Cortex A53 kwenye sehemu zote nane za hii chip

Cortex A53 mara hutumika kwa ajili ya kazi zinazohitaji nguvu ndogo

Ukiangalia simu mfano wa Google Pixel 8 Pro, processor yake ina sehemu zenye nguvu kubwa na nguvu ndogo

Ambapo sehemu zenye nguvu ndogo imetumia Cortex A510 na bado google imelalamikiwa kwa utendaji duni ukilinganisha na washindani wake

Hii inamaanisha kuwa vivo y02t haifai kucheza gemu kubwa zinazotumia nguvu kubwa ya processor

Uwezo wa betri na chaji

Chaji ya Vivo Y02t ina upelekaji moto kwa spidi ya wastani

Kwani kiasi cha juu kabisa cha umeme ni wati 10

Hii inachukua muda mrefu kidogo kujaza betri yake ambayo ina ujazo wa 5000mAh

Kitu kizuri cha mfumo wa chaji wa hii simu ni uwepo wa reverse charging

Yaani unaweza kuitumia vivo y02t kama power bank na kuchaji vifaa vingine

Kasi ya kupeleka umeme kwenye reverse charging ni 5W

Ukubwa na aina ya memori

Kuna toleo la aina moja la vivo y02t upande wa memori na RAM

Utapata vivo ya GB 64 na RAM 4

GB 64 kwa mtumiaji wa whatsapp na anaependa kupakua mafaili inaweza kuwahi kujaa

Kama haitosholezi unaweza kuongeza memori kadi kwa sababu sehemu ya kuweka memori ipo

Aina ya memori inayotumiwa na vivo y02t ni eMMC ambayo kasi yake huzidiwa mara na memori za UFS

Siku hizi simu za bei ndogo kutoka kampuni nyingi hutumia memori za UFS

Uimara wa bodi ya Vivo Y02t

Bodi ya Vivo Y02t ni ya plastiki

Haina viwango vya IP67 kwa maana haina uwezo wa kustahimili kuzuia maji pindi ikizama kwenye kina cha maji

Hii inakuhitaji kuwa makini unapoitumia katika mazingira ya mvua au sehemu ya maji

Na pia ni vizuri ukawa na skrini protekta kuimarisha ulinzi wa simu

Ubora wa kamera

Mfumo wa kamera wa Vivo Y02t ni wa kiwango cha chini

Kwani ina kamera moja tu upande wa nyuma

Na kamera yenyewe ina ukosefu wa teknolojia ya PDAF

Upande wa video vivo y02t inaweza kurekodi video za resolution ya 1080 kwa kiwango  cha 30fps

Ubora wa picha usitarajie makubwa kama kwa simu ya vivo v29 5G

Ubora wa Software

Vivo Y02t inakuja na mfumo endeshi wa Android 13 japo kwa sasa kuna ujio wa Android 14

Mbali na android 13, vivo hii pia inatumia mfumo wa Funtouch Os 13

Funtoch Os 13 inakupa uwezo wa kuchagua rangi za icon inayoendana na wallpaper unayotumia kwenye simu

Washindani wa Vivo Y02t

Kwenye kipengele cha simu za bei ndogo kuna washindani wengi sana kutoka tecno, infinix, samsung, xiaomi na oppo

Vivo y02t bei yake inaendana na samsung galaxy 04

Na kisifa hizi simu hazitofautiani pakubwa

Neno la Mwisho

Iwapo unataka kumnunulia mtu simujanja kwa mara ya kwanza hii simu inaweza kuwa toleo zuri kwake

Mtumiaji wa simu janja kwa mara ya kwanza huwa hana uhitaji wa vitu vingi sana

Kwa uwezo wa vivo y02t inaweza mtimizi hitaji lake

Ila mcheza magemu, mpenda kamera, na anayetumia simu kwa kazi nyingi vivo y02 sio chaguo sahihi

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

No Featured Image

Simu 14 mpya za Vivo za ubora mkubwa na bei zake (2024)

Tangu mwishoni mwa mwaka 2023 mpaka mwaka huu 2024 Vivo imeachia matoleo mengi ya simu Katika matoleo hayo yapo ya bei ndogo, bei ya kati na bei kubwa Kwa maana […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

No Featured Image

Bei ya sasa ya Oppo A17K na Sifa Zake

Oppo  A17K ni simu iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2022 mnamo mwezi oktoba Ni simu ya daraja nafuu ambayo haihitaji bajeti kubwa kuimiliki Kwani bei ya oppo A17K haizidi laki tatu […]

redmi 10a thumbnail

Bei ya Sasa ya Redmi 10A na Sifa Muhimu

Simu ya Redmi 10A iliiingia sokoni mwaka 2022 Ni aina ya simu inayolenga watu wenye matumizi ya kawaida kama sio machache Hivyo bei ya Redmi 10A ni chini ya laki […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram