Inawezekana ukawa umewahi kuona sifa za simu upande wa kioo na kamera
Moja ya kitu utakachokiona kikianishwa ni HDR mfano mzuri ni simu mpya ya Samsung Galaxy S23+
Hivyo ikakufanya kutaka kujua maana ya HDR
Kama unajiuliza hdr ni nini basi hili ndio jibu
HDR ni tekniki (mbinu) ambayo kamera inatumia kutoa picha ambayo ina muonekano unaoendana na jinsi jicho la binadamu linavyoona hiko kitu kwenye mazingira halisi
Kirefu chake ni High Dynamic Range
Jinsi HDR inavyofanya kazi
Kama kamera ina uwezo wa kuchukua video au picha za HDR, kitu cha kwanza inachofanya ni kupiga picha nyingi kwa wakati kwa nyakati tofauti
Yaani unapobonyeza kitufe cha kupiga picha, kamera hupiga picha nyingi kwa kutofautisha kiasi cha mwanga
Kwa maana viwango vya exposure vintofautiana
Baada ya hapo, simu inaunganisha picha zote ambazo kamera imezipiga
Kuziunganisha picha kwa pamoja kunatengeneza muonekano mpya wa video au picha
Hiki kitendo kinafanyika ndani ya sekude chache
Aina za HDR
Mpaka sasa 2022 kuna aina sita za hdr ambazo ni
- HDR10
- HDR10+
- Dolby Vision
- HLG
- Technicolor
- Dolby Vision IQ
Tutazifafanua kwa ufupi HDR10 na HDR10+ pekee
HDR hutumia kitu kinaitwa “metadata” kutambua kiwango cha uangavu kinachohitajika
Hivyo kuna metadata inayotumia kiwango cha uangavu wa aina moja hufahamika kama static metadata
Lakini kuna metadata inayobadilika kulingana na kiwango cha uangavu wa eneo husika hii huitwa dynmic metadata
HDR10 yenyewe inatumia static metadata
Hivyo kama display ina rangi zaidi ya bilioni baadhi ya rangi zinaweza kuonekana zikiwa na giza kiasi
Hilo linarekebishwa na HDR10+ ambayo inapunguza ama kuongeza uangavu kutokana kiasi cha mwanga wa eneo husika
Kitu kinachofanya HDR10+ kuweza kuonyesha rangi nyingi kwa ustadi
Faida za kutumia HDR
Faida kubwa ya HDR ni uwezo wa kurekebisha muonekano wa vitu ambavyo vimepigwa kwenye mwanga hafifu
HDR hubalansi rangi za vitu kwa ustadi
Na inafanya kitu kionekane kwenye simu kama kinavyoonekana kwenye uhalisia wake
Japo kuna nyakati hilo halitokei
Udhaifu wa HDR
Kuna baadhi ya picha za hdr huongeza rangi ambazo hazipo
Kiasi cha kwamba uhalisia wa picha unakuwa haupo
Hii inatokana na hdr kukoreza rangi zaidi ya rangi ya kitu kinavyoonekana
Na baadhi ya vifaa vinachukua picha chache huku ikitumia hdr
Sasa picha ikiwa imechukuliwa kwenye exposure ya aina moja ubandia lazima utokee
Simu zenye kioo na kamera ya HDR
Simu zote za daraja la juu za mwaka 2021 na 2022 huwa na HDR10 au HDR10+
Ila kuna kamera za simu chache ambazo zinaweza kurekodi video za HDR10+
Kiufupi baadhi ya simu hizo ni samsung galaxy s22, iphone 13 pro max, xiaomi 12 pro, vivo x70 pro na nyinginezo
Gharama za simu za HDR10 na HDR10+
Ukitazama baadhi ya simu zilizotajwa unaweza kujua uhalisia wa bei
Kiuhalisia bei ya simu za HDR10+ ni zaidi ya laki tano
Hakuna simu ya bei rahisi yenye hdr10+
Wazo moja kuhusu “Ni nini Maana ya HDR (kwenye simu)?”
Kifupi nimependa maelezo yenu mlio fafanua kwa mapana na kwa weledi mkubwa nimependa sana kiufupi nimengi nimepata kujifunza kutoka kwenu hadi vitu ambavyo sikuwahi kutegemea kwamba nitakujaga kivifahamu Ahsante sana.