Kama unataka simu yoyote kwa bei ya chini hasa hapa Tanzania huna budi kujua jinsi ya kununua simu mtandaoni
Hapa kuna muongozo unaofafanua hatua za kununua simu kupitita mtandao wa Aliexpress
Nimelazimika kuelezea manunuzi ya vitu mtandaoni kwa sababu watumiaji wa tovuti ya simunzuri.com wamekuwa wakiuliza jinsi ya kupata simu mbalimbali kwa bei nafuu.
Mtandao wa aliexpress una simu za aina nyingi ambazo kwa Tanzania zinapatikana kwa bei ya juu kidogo
Kujiunga na aliexpress
Kitu cha kwanza ni kujiunga na aliexpress
Hivyo unapaswa uwe na email na namba ya simu inayofanya kazi
Kuna njia mbili za kuingia kwenye duka la mtandaoni la aliexpress
- Kutumia tovuti
- Kutumia applikesheni
Kutumia tovuti kwa maana unatumia Google kuingia kwenye linki ya aliexpress.com
Aplikesheni itakulazimu kuingia Google Playstore kwa android au Apple Appstore kwa simu za iPhone
Kujiunga kwa njia ya tovuti
Tembelea au google aliexpress.com
Ukifungua ukurasa wa tovuti hiyo itakuletea ukurasa unaoonyesha vitu mbalimbali vinavyouzwa humo
Kwa mtumiaji wa simu muonekano wa tovuti upo hivi
Na kwa mtumiaji wa kompyuta muonekano utakuwa kama ifuatavyo.
Kwenye kompyuta bonyeza Register(upande wa kulia) na kwa mtu mtumiaji wa simu bonyeza alama inayowakilisha akaunti
Kisha chagua “register”
Kwenye simu itakuja ujumbe ikikutaka uchague e-mail unayotaka kujisajilia
Na kwenye kompyuta inakuletea ujumbe unaokutaka ujaze nchi uliyopo (Tanzania), email na ujaze password (neno la siri) uitakayo
Kujisajili kwenye simu inachukua muda mchache ukiwa umechagua email au akaunti ya FB kama unayo
Ila ukijisajilia kwa kompyuta, aliexpress watatuma ujumbe kwenye email yako
Utabonyeza linki uliyotumiwa ili kukamilisha usajili
Ni vizuri kuzifanya hatua hizi kwa kutumia simu kama unayo
Hivyo download app ya aliexpress playstore na app ya aliexpress appstore kwa iphone
Hatua za kujisajili ni zile zile
Jinsi ya kutafuta simu unayoitaka
Baada ya kukamilisha, app itakuwa tayari kununua simu na kukufikia mpaka eneo unaloishi
Ili uipate simu unayoitaka, inakubidi uitafute simu kwenye sehemu ya kusachi
Andika jina simu kisha bonyeza kitufe cha kutafuta
Zitakuja picha za simu mbalimbali
Zipo zinazoendana na unachokitafuta wakati mwingine yatakuja matokeo tofauti (mara chache)
Picha za simu zitaonyesha bei ya simu unayoitafuta na gharama za kusafirisha
Utabonyeza ambaye unaona ana gharama nafuu kwako wewe
Na baada ya kuchagua muuzaji unayemtaka, app ya aliexpress itakuletea ukurasa kwa ajili ya malipo ambao una muonekano huu.
App ya aliexpress itakupa uhuru wa kuchagua aina ya toleo la simu unalotaka
Kwa mfano simu ya iphone 11 pro max iliyopo kuna ya GB 64 na GB 256
Tumechagua ya GB 64, na pia unapewa nafasi ya kuchagua rangi uitakayo (Color: Black)
Ikimaanisha tumechagua iphone 11 pro max nyeusi
Vile vile unaweza kuchagua kampuni unayotaka ikusafirishie mzigo
Mara nyingi msafirishaji wa uhakika huwa ni Aliexpress Standard Shipping
Pia wapo wanaosaifrisha bure ila mizigo huwa inachelewa sana
Ukiitazama picha ya pili kwenda juu kuna neno limeandikwa Service 75 day buyer protection
Haya ni makadirio ya siku mzigo unapaswa ukifikie ndani ya kipindi cha siku 75
Iwapo siku zikizidi unaweza kudai urudishiwe pesa yako
Jinsi ya kufanya malipo Aliexpress
Baada ya kujaza taarifa zote za simu hatua inayofuata ni kununua simu husika
Ili ununue simu janja aliexpress itakulazimu kulipa kwa Master Card au Visa Card
Huduma ya malipo kwa njia visa card inaweza kufanyika kwa kutumia M-Pesa Visa Card
M-Pesa Visa Card ndio njia rahisi zaidi kwa ambao hawana akaunti za benk
Jinsi ya kutengeneza kadi ya Visa Card kwa M-Pesa
Hatua za kufuata kwenye simu yako
- Bonyeza namba *150*00# kwenye laini ya Vodacom Tanzania
- Chagua namba nne (4) malipo kwa m-pesa
- Chagua namba sita (6) M-Pesa Visa Card
Itakuja menyu yenye machaguo sita
Utachagua namba moja (1) Tengeneza kadi kama hukuwahi kuwa nayo
Utasubiri sekunde chache kisha utaletewa ujumbe wenye taarifa tatu.
- Namba ya visa card
- Tarehe ya kadi kuisha muda wake
- Namba ya cvv yenye tarakimu tatu
Baada ya kukamilisha zoezi la kuunda kadi ya malipo itabidi uiwekee kadi pesa kutoka kwenye akaunti ya M-PESA
Utafuata hatua za awali, ukifikia kwenye menyu ya visa card, chagua namba 3 (Weka Pesa Kwenye Kadi)
Hakikisha unaweka pesa inayoendana na bei ya simu aliexpress, pesa ya kusafirisha mzigo na makato ya mpesa visa card
Makato ya M-Pesa ni 4.3% ya pesa ya kitu unachokinunua na gharama ya usafiri
Kulipia simu na ujazaji wa anuani ya Makazi
Kitu kinachofuata ni kubonyeza kitufe kilichoandikwa “Buy now”
Itakuja peji itakayotaka ufuate hatua tatu za kukamilisha muhamala
Hatua hizo ni kama zifuatazo zinaoonekana kwenye picha
Kama uonavyoona, cha kwanza ni kujaza majina yako kamili kama yanavyoonekana kwenye kitambulisho chako cha URAIA au MPIGA KURA
Sehemu ya pili ni kuiingiza namba ya simu unayoitumia
Sehemu ya tatu ni kuingiza anuani yako ya posta
Kama hauna ingiza jina la WILAYA unayoishi (sio lazima kuwa na sanduku la posta)
Kisha unaweka nchi unayotokea (Tanzania) halafu sehemu inayofuata jaza MKOA unaoishi
Na baada ya mkoa jaza jiji (jina la mkoa tena)
Na sehemu ya mwisho namba ya postal code(posti kodi) ya kata unayoishi
Unaweza kuzipata posti kodi za kila wilaya na kata hapa Tanzania kwenye hii linki
Baada ya hapo itakuja ukurasa wa kuthibitisha kuwa unataka kununua hiyo simu
Hapo utabonyeza “Place order”
Kisha ukurasa unaotaka kujaza taarifa za viza kadi utakuja ukiwa na muonekano huu
Chagua hiyo sehemu iliyoandikwa “Add a new card”
Kisha ukurasa utakaojaza taarifa za kadi utatokea ukiwa na muonekano huu wa chini
Sehemu iliyoandikwa Card number utaweka namba za m-pesa visa card uliyotengeneza ambazo huwa zipo 16
Kwenye Cardholder name utaweka majina yako kamili kama yalivyo kwenye kitambulisho(au kadi ya benki) ulichosajilia simu
Sehemu iliyoainishwa kwa neno MM/YY inachukuwa tarehe ya kuisha kwa kadi (expire date)
Ambapo MM inawakilisha mwezi na YY inawakilisha mwaka
Mwezi na mwaka huandikwa kwa tarakimu mbili
CVV ni tarakimu tatu ambazo zipo kwenye kadi(unatumiwa kwenye sms pia), hizi hutumika kwa ajili ya usalama
Baada ya hapo bonyeza kitufe kilichoandikwa Pay Now
Ukifanikiwa basi kazi yako ni kusubiria mzigo ukufikie
Wapi pa kupokea mzigo kutoka aliexpress?
Mizigo mingi huwa inapokelewa kwa njia ya posta ya wilaya uliyoijaza
Kama unanunua simu mtandaoni kupitia aliexpress mzigo unaenda posta mara nyingi
Swali ni kwamba utajuaje mzigo wako umefika posta?
Posta Tanzania wana mfumo wao ambao unaweza kuutumia kutrack mzigo wako
Na pia mzigo ukiwa umefika wahudumu wa posta watakutaarifu kwenda kuchukua simu yako
Na pia kwenye app ya aliexpress utaweza kutrack simu yako wapi ilipofika
Ukienda posta lazima uwe na kitambulisho na malipo ya shilingi 2350/= ili upewe simu yako
Muda unaotumika mzigo kufika Tanzania
Kikawaida inaweza ikachukua wiki tatu (3) mpaka tano (5) mpaka mzigo ukufikie
Wakati mwingine mzigo unaweza kuchukua mpaka miezi mingi
Ila kama utachagua msafirishaji kuwa Aliexpress Standard Shipping mara nyingi mzigo unakufikia wiki tatu mpaka tano
Epuka kusafirisha mzigo na kampuni kama Canaio au China Post
Huwa wanachelewesha kusafirisha mizigo
Kuna nyakati mzigo unaweza usikufikie kabisa
Ila usiwe na wasi hela yako haitopotea.
Nini cha kufanya kama simu haijakufikia?
Kama nilivyosema wakati mwingine muuzaji wa simu aliexpress anashindwa kukuletea mzigo au anakuletea kitu tofauti
Aliexpress inakupa nafasi ya kudai kurudishiwa pesa yako
Hii inafanyika kwa kufungua malalamiko(open dispute) kwenye mfumo wa aliexpress
Muuzaji atayaona malalamiko yako kisha mtaelewana
Kama hamtofikia maelewaona mfumo wa aliexpress utakurudishia pesa yako ndani ya siku kumi tano
Kikawaida unaponunua kitu aliexpress pesa haiendi moja kwa moja kwa muuzaji
Bali inabaki kwa aliexpress mpaka simu itakapokufikia
Ni salama sana kununua kitu aliexpress ukiwa Tanzania.
Wakala wa Aliexpress Tanzania?
Mtandao wa aliexpress hauna wakala wala tawi hapa Tanzania
Njia pekee ya kufanya mawasiliano na aliexpress ni kwa kupitia app au tovuti yao
Izingatiwe kuwa aliexpress ni soko tu la mtandaoni linalojumuisha wauzaji na wanunuaji
Wauzaji wengi ni kutoka China
Hivyo usihangaike kutafuta wakala wa aliexpress Tanzania kwani hakuna kitu kama hiko
Angalizo
Unaponunua kitu(simu) aliexpress jitahidi kusoma reviews(maoni) ya watu waliowahi kununua kabla
Ni sehemu ambayo kuna matapeli pia na bidhaa feki zinapatikana kule pia
Hivyo kuwa mwangalifu ununuapo chochote
Hitimisho
Huu muongozo umefupishwa lakini umegusa sehemu nyingi
Ufupisho huu umekupa picha kiasi chake ya jinsi ya kununua simu mtandaoni kupitia alixepress
Pia unaweza kuutumia huu muongozo kununua vitu vingine aliexpress unaomilikwa na kampuni ya alibaba
Maoni 29 kuhusu “Jinsi ya Kununua Simu Mtandaoni (Hatua kwa Hatua)”
Je nikiwa nilipo kuna kata na kuna posta je naweza jaza kata au wilaya?
Jaza jina la wilaya, kata itatumbulika kwa kutumia post code(post kodi)
Je Naweza pia kuagiza pikipiki 1?
Mtandao wa Alibaba unaweza kuagiza chochote
Sas nikiagiza kwa mfano nipo kagera hapa naenda kuchukulia wapi.?
Posta ya wilaya uliyopo
Ali baba & AliExpress ni campun moja au vp
Kampuni ni moja na mmiliki ni mmoja, tofauti ni kuwa aliexpress ni B2C (business to consumer) yaani kwa ajili wateja wa kawaida, na alibaba ni kwa ajili ya wafanya biashara wanaochukua mzigo mkubwa yaani B2B
Je Kama sina kitambulisho cha kura ila nina namba tu ya nida je posta watanikabidhi mzigo kweli??
Watakubali
Nahukuru,Aliexpless imetufunulia dunia na imefaya dunia kuwa kama kijiji
Naweza kununua simu kutoka marekani? Na je naweza nunua kupitia aliexpresss? Nahitaji iPhone 14 promax original je kupitia aliexpress nitapata? Na je simu yangu ikifika kuna kodi nitatozwa? Kwa kumalizia nikushukuru kwa muongozo mzuri ambao hauna longolongo. Keep it up
Amazon, kwa usa nakushauri utumie amazon.com, kuhusu kodi huwa haitozwi ila kwa sasa sina uhakika, lakini huwa haitozwi
Mimi kila nkifikia hatua ya mwisho kunachangamoto ya mm/yy na kujirudia na pvv kisha natumiwa ujumbe kwenye simu yangu wa Transaction of tsh 560000.63 on card ending 0073 at www al declined due to1001 the voucher has expired at03:37 pm nini nakosea?
Jaribu kuweka pesa ya ziada unaweza kuta hela ni ndogo ukijumlisha makato
Je mfano nimeagiza simu alafu ikaja simu kimeo au wakaleta simu ambayo ni feki au simu ambayo sio niliyoichagua nafanyaje? maana hawa sio kama wale kikuu matapeli? unanunua simu unaletewa mataka taka ambayo hujayatarajia
Unafungua malalamiko kwenye sehemu imeandikwa dispute
Ikiwa mfano bidhaa niliyoletewa ni feki au siyo niliyoihitaji ….naweza fungua dispute ,nataka kujua je ile bidhaa nabaki nayo au nawarudishia aliexpress??
Je nikitaj inakuaje
Nimeagiza mzigo AliExpress lakini nimecofirm kimakosa kuwa nimepokea mzigo lakini sijapokea nafanyeje
Nipe muda nilifuatilie
Mko vizuri,vipi naweza kuagiza camera?
Inawezekana
Vp kama sina namba ya nida wala kitambulisho cha mpiga kura nafanyaje
Nadhani vitu kama Kadi za Benki zinaweza Saudia japo sina uhakika
nataka kununua samsung s24 ultra Alibaba je naweza letewa bidhaa yenyewe au copy ya hiyo bidhaa
Kuwa Malini kule
sijaelewa apo ulivyosem em nipe maelekezo kidogo ata labda kam ntawez kununua simu uko alibaba
Hujaelewa wapi kiongozi