Wapenzi wa simu za bei ndogo chini ya laki mbili vivo y66 inaweza ikawa ni simu nzuri
Ni simu ambayo imetoka mwaka 2017, miaka sita imepita sasa
Kwa nyakati za sasa yaani 2023 ubora wa hii simu ni mdogo ukilinganisha na simu ya vivo y22
Hivyo bei yake ni chini ya laki mbili kwa maeneo mengi Tanzania na nyingi ni used
Bei ya Vivo Y66 ya GB 32
Vivo Y66 ya GB 32 kwa Tanzania ni shilingi 150,000/=
Ila unapochukua hii simu uwe na akili kichwani kuwa ni toleo la zamani
Ni ngumu kupata mpya kwa mwaka 2023
Hivyo vitu vingi havina ubora mkubwa kuanzia utendaji hadi ubora wa kamera
Na haina uwezo wa kupokea toleo jipya na betri yake si kubwa
Ndio maana bei yake ni laki moja na nusu
Sifa za Vivo Y66
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | ,32GB na RAM 3GB |
Kamera | Kamera MOJA
|
Muundo | Urefu-5.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 150,000/= |
Uwezo wa Network
Hii simu inakubali mtandao wa 4G na mitandao mingine
Kuna taarifa finyu kuhusu processor iliyotumika
Hivyo ni ngumu sana kujua aina ya 4G ambayo inatumia
Kwa miaka ya 2017 4G za simu nafuu ilikuwa ni LTE Cat 4 yenye kasi ya 100Mbps ambayo ni sawa na 12.5MBps
Kwa maaana kama unapakuwa kitu cha GB 1.2 itachukua karibu mbili kumalizika
Kwa miaka ya sasa ni spidi ya kawaida, ina masafa yote yanayotumiwa na mitandao ya simu Tanzania
Ubora wa kioo cha Vivo Y66
Kioo cha vivo y66 ni cha IPS LCD chenye resoution ndogo ya 1280 x 720 pixels
Teknolojia imebadilika, kioo cha lcd huwa sio kizuri kama kioo cha amoled
Na pia kiwango kidogo cha resolution pia inafanya muonekano wa vitu usiwe wa kuvutia sana na wenye kukolea
Hata hivyo ni simu ambayo imepita muda kidogo tangu itoke
Hivyo huwezi ukatarajia teknolojia ya sasa iwepo kwenye kifaa cha miaka sita nyuma
Nguvu ya processor
Vivo y66 inatumia chip yenye idadi ya core zipatazo nane
Hakuna ufafanuzi kuhusu chip ambayo simu inatumia ila ni chip yenye nguvu ndogo
Kwa maana uwezo wa kufanya vitu vikubwa kama kucheza magemu simu haina
Ni vizuri vizuri ukafikiria toleo anagalau la Tecno Spark 9 kama unapenda sana magemu
Uwezo wa betri na chaji
Simu inakuja na betri yenye ujazo wa 3000mAh
Ni betri ndogo ambayo haiwezi kukaa na chaji masaa mengi kama ukiwa unatumia intaneti masaa yote mfululizo
Ila mwaka 2017 betri hii ilikuwa ni kubwa na inayotosheleza
Simu haina chaji inayopeleka umeme kwa kasi kubwa
Hivyo utakapokuwa unaichaji itakuwa inachukua muda hata kama betri yake ndogo
Ukubwa na aina ya memori
Vivo y66 ina toleo moja tu upande wa memori ambalo lina ukubwa wa GB 32 na RAM GB 3
GB 32 kwa nyakati hizi ni ndogo na simu inaweza ikajaa kwa haraka
Hivyo utalazimika kuwa unaweka memori kadi kubwa ili kupunguza mafaili pale memori ya simu inapokaribia kujaa
Haina uwezo wa kuongeza ukubwa wa RAM kama ilivyo baadhi ya simu za siku hizi
Uimara wa bodi ya Vivo Y66
Vivo Y66 ina bodi ya plastiki na haiwezi zuia maji kama simu ikizama kwenye kina kikubwa
Kwa maana ni vizuri ukawa unaitumia simu kwa tahadhari ya kutoiangusha kizembe
Na utalazimika kuweka screen protekta kwa ulinzi wa kioo
Kiujumla simu haina bodi imara kiivyo
Ubora wa kamera
Simu ina kamera moja tu ambayo haina PDAF
Ina uwezo wa kurekodi video za hd
Haina kamera zingine kama ultrawide na telephoto
Selfie kamera yake ina ukubwa wa megapixel 16
Kitu cha kuvutia angalau ni kuwa kamera yake ina HDR ila sio kamera inayoendana na viwango vya leo
Ubora wa Software
Vivo y66 inakuja na toleo la kitambo sana la Android 6 na Funtouch Os 3.0
Kwa sasa toleo jipya la Android ni Android 13 na hivi karibuni la 14 litatoka
Hata hivyo applikesheni nyingi bado zinasapoti android 6 hivyo utapata app karibu zote za muhimu
Ila baada ya miaka kadhaa mbeleni inaweza isiwe hivyo
Yapi Madhaifu ya Vivo Y66
Simu ni ya dhamani hivyo ukilinganisha na matoeo ya simu mpya ni kuwa simu ina mapungufu mengi
Ila kubwa ni kuwa utendaji wake ni mdogo na kamera yake haina uwezo mkubwa
Kioo chake kina resolution ndogo vilevile
Neno la Mwisho
Je Vivo Y66 ni simu ya kuwa nayo 2023?
Hapana sikushauri kununua hii simu kwa sasa labda kama bajeti yako ni ndogo sana
Hii simu itakuletea shida ikiwemo ukosefu wa matoleo mapya ya android na ukaaji wa chaji mdogo
Maoni 2 kuhusu “Bei ya Vivo Y66 na Ubora Wake 2023”
je ni simu gani bora kwa sasa kui nunu kwa bei ya laki 3
Hot 20i, Samsung 04, Redmi 12c