Tecno Spark 9 ni simu ya mwaka 2022 ambayo haina tofauti sana na Tecno Spark 10 ya 2023
Ni simu ya bei nafuu hata kwa mwaka huu ikizingatiwa ina toleo la android 12
Bei ya Tecno Spark 9 kwa Tanzania haizidi laki tatu na nusu kulingana na eneo na ukubwa wa memori
Unafuu wa bei unasababishwa na simu kuwalenga watu ambao hawatumii simu kwa vitu vinavyohitaji nguvu kubwa
Hivyo tarajia sifa nyingi zenye ubora wa kawaida sana
Bei ya Tecno Spark 9 ya GB 128
Tecno Spark 9 ya GB 128 kwa Tanzania inauzwa kwa shilingi 340,000
Ni mara chache kukuta simu yenye ukubwa wa GB 128 kuuzwa kwa bei ya chini ya laki nne
Zipo sababu nyingi hasa za kuitendaji, spark 9 ni simu ya toleo la daraja la chini
Uwezo wake hauwezi ukawa mkubwa kama Tecno Spark 10 Pro au simu ya Vivo Y22
Kuna watu matumizi yao ya simu ni kwa ajili ya mitandao ya kijamii na mawasiliano
Aina hii ya watumiaji ndio hii simu inawalenga, zifuatilie sifa zake uifahamu kiundani
Sifa za Tecno Spark 9
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 64GB,128GB na RAM ,6GB,3GB, 4GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 340,000/= |
Upi ubora wa Tecno Spark 9
Simu inakuja na kioo chenye refresh rate kubwa hivyo unapotachi inakuwa na mwitikio mzuri
Betri yake ni kubwa inayoweza kukaa na chaji muda mrefu bila kuisha haraka
Ina kioo na chip ambazo zinatumia umeme kidogo wa betri
Ina bei inayovumilika kwa watu wengi wenye bajeti ndogo ya kununua simu
Memori yake ni kubwa inayoweza kuhifadhi mafaili mengi
Ni simu ya 4G hivyo nguvu ya intaneti si mbaya
Sifa zingine ni za kawaida ama za chini kama utakavyoona kwenye hii post
Uwezo wa Network
Tecno Spark 9 ina uwezo wa kutumia network mpaka ya 4G
Aina ya 4G inayotumia ni LTE Cat 7 yenye kasi ya 300Mbps ambayo ni sawa na 37.5Mbps
Kama unadownload gemu ya Call of duty ya GB 2 kule playstore simu itachukua sekunde 54 kumaliza kudownload
Kitu cha kuzingatia ni kuwa ili upate kasi hii basi kampuni ya mtandao wa simu inabidi uwe una kasi kubwa
Kwa Tanzania sio rahisi kuipata 4G yenye kasi hii
Simu ina masafa yote ya mitandao ya simu iliyopo hapa nchini
Hivyo laini zote zinafanya kazi bila tatizo linapokuja swala la intanet
Ila ukilinganisha na simu kama ya oppo A78 kwenye network, utofauti ni mbingu na ardhi
Ubora wa kioo cha Tecno Spark 9
Spark 9 inatumia kioo cha IPS LCD chenye refresh rate ya 90Hz
IPS LCD ni vioo ambavyo huwa zina taa kwa nyuma zinazosaidia screen kuonyesha vitu
Tofauti na vioo vya amoled ambavyo huzalisha mwanga vyenyewe bila kutumia taa
Ndio maana rangi nyeusi kwenye amoled hukorea sana tofauti na IPS LCD
Resolution ya simu ni ndogo pia kwani ni 720 x 1600 pixels
Kwa miaka ya karibuni simu za kawaida huwa zinakuja na 1080 x 1600 pixels ambayo huwa na muonekano wa rangi za vitu uliokolea vizuri
Ila kumbuka spark 9 ni simu ya bei nafuu sio rahisi kuwa na vitu vingi vya kuvutia
Nguvu ya processor MediaTek Helio G37
Kwenye ufanyaji kazi, spark 10 inatumia processor mediatek helio g37 toka kampuni ya mediatek
Processor ndio ubongo wa vifaa vya kielektronik kama simu na kompyuta
Mediatek helio g37 ina core nane, nne za mwanzo zina kasi inayofika 2.3ghz na zingine nne zina 1.8ghz
Ila zote zinatumia muundo wenye utendaji mdogo wa Cortex A53
Kwa mpenzi wa magemu atapata wakati mgumu kucheza magemu makubwa kwa uzuri
Uwezekano wa simu kupata joto ni mkubwa unapocheza gemu la PUBG
Kutokana na uwepo wa Cortex a53 inafanya simu kutumia uememe mdogo
Kwa sababu haitumii nguvu kuwa
Uwezo wa betri na chaji
Simu inakuja na betri ya 5000mAh
Hiki ni kiwango kitakachofanya simu kukaa muda mrefu na chaji hata ukiwa unatumia intaneti
Ila simu haina fast chaji hivyo itachukua muda mrefu kujaa ukizingatia betri ya simu ni kubwa
Yote yote ukaaji wa chaji ni wa kiwango cha kuridhisha
Ukubwa na aina ya memori
Tecno spark 10 inatumia memori aina ya eMMC ambazo kasi zake sio kubwa kama UFS
Kuna matoleo matatu ya spark 9 upande wa memori
Matoleo mawili yana GB 64 na toleo moja lina GB 128 na mgawanyo wa RAM ni GB 3, 4 na 6
Kiwango cha memori kinatosheleza kabisa kuhifadhi mafaili mengi
Na hata kama ikijaa simu ina sehemu ya kuongeza memori kadi ya ziada
Uimara wa bodi ya Tecno Spark 9
Bodi ya tecno spark 9 ni plastiki upande wa nyuma na pembeni
Simu haina uwezo wa kuzuia maji iwapo ikidumbukia kwenye mkusanyiko wa maji mengi
Lakini pia uwezo wa kuzuia vumbi ndani ya simu haupo kutokana na kutokuwepo na viwango vya IP
Hivyo ni muhimu kuwa makini na simu hasa utumiapo kwenye mazingira yenye maji au mvua
Na ni vizuri ukaweka kava ili ubora wa plastiki usipungue kwa haraka
Ubora wa kamera
Simu ina kamera mbili ila kamera ya pili haijainishwa aina ya lenzi inayotumia
Ila kamera kubwa ina megapixel 13 bila uwepo wa teknolojia ya PDAF ambayo ni ya kawaida kwa simu nyingi siku hizi
Kiwango cha megapixel sio kibaya kwani simu kama iphone 13 pro max kamera yake ina megapixel 12 na inatoa picha nzuri
Hii ina maana megapixel sio kigezo pekee cha kamera nzuri kuna vigezo vingi ambavyo spark 9 inakosa
Kwa kuangalia mfumo mzima kwa kamera ya hii simu ni kuwa ina ubora wa kawaida
Upigaji wake wa picha hauwezi ukawa wa kiwango kikubwa kama Tecno Camon 19 Pro
Ubora wa Software
Tecno Spark 9 inakunja na mfumo wa Android 12 na HiOS 8.6
Ukiwa na HiOS 8.6 inakuwezesha kubadilisha video kuwa audio
Kwa mfano umepakuwa video ya wimbo wowote hutokuwa na haja ya kudownload app ya kubadilisha video kuwa audio kwa simu inakuja nayo
Kitu kingine ni HiOS 8.6 inakupa nafasi ya kuongeza ukubwa wa RAM
Kwa mfano kama unanunua spark 9 ya ram bg 3, hii ram sio kubwa lakini inaweza kuongezwa
Lakini haitoshi ni mfumo unaokuletea app ya kuhariri video utakazokuwa unarekodi kwenye simu yako
Changamoto ya mfumo huu ni kuwa una matangazo mengi ya notification.
Yapi Madhaifu ya Tecno Spark 9
Kama ilivyotangulia kuelezwa ni kuwa hii ni simu ya bei nafuu hivyo vipo vitu vingi vyenye ubora wa kawaida
Moja, ni chip kutokuwa na utendaji mkubwa hasa kwenye magemu
Kamera zake sio za kuvutia na haina kamera ya ultrawide
Simu inatumia aina ya memori ambayo kwa sasa wakati wake unapita
Siku hizi simu nyingi zinatumia walau UFS 2.1 na sio eMMC
Neno la Mwisho
Spark 9 ni simu janja ya mwaka 2022 ila bado inafaa hata kwa mwaka 2023
Ukiangalia matoleo mapya ya tecno spark 10 utaona kuwa kuna tofauti ndogo na tena unakuta kwa kiwango kikubwa zipo sawa
Basi kama bajeti yako ni ndogo sana sio mbaya ukajivutia hii simu kusukuma siku