Tecno Camon 20 ni simu ya mwaka 2023 ambayo imeingia sokoni mnamo mwezi Mei
Kiubora ni simu inayoweza kuwekwa kwenye kundi la kati hivyo bei yake sio sawa na matoleo ya Spark
Kwani bei ya tecno camon 20 kwa Tanzania inazidi laki tano
Ukimiliki hii simu kitu kimoja wapo utakachoweza kunufaika nacho ni kioo kizuri na kamera yenye lenzi kubwa
Unapaswa uifahamu hii simu kiundani ujue inavyotofautiana na Tecno Camon 20 Pro 5G
Bei ya Tecno Camon 20 ya GB 256
Tecno ambayo ukubwa wake unafika GB 256 kwa Tanzania inauzwa shilingi 600,000/=
Kwenye nyanja ya kioo, uimara wa bodi, ukubwa wa memori na hata kamera ina ubora unaoshahibiana kwa kiwango kikubwa na bei yake
Kwa hiyo kiwango hiki cha bei ni shindani japo simu itakumbana na changamoto kutoka kwa washindani wengine
Simu zenye bei sawa na hii baadhi huja na vitu vya ziada ikiwemo 5G ambayo haipo kwenye camon 20
Utaona washindani wake na utofauti uliopo baina yao
Sifa za Tecno Camon 20
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Amoled |
Softawre |
|
Memori | 256GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.67inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 600,000/= |
Upi ubora wa Tecno Camon 20
Camon 20 inakuja na chaji inayojaza betri kwa haraka ndani ya muda mfupi
Betri yake ni kubwa na inakaa na chaji masaa mengi
Inakuja na memori kubwa inayotosheleza kujaza vitu na kuweka applikesheni za kutosha
Ina kioo chenye uwezo wa kuonyesha rangi kwa usahihi mkubwa
Kamera zake zinatoa picha nzuri hasa kwenye mwanga mwingi
Uwezo wa Network
Upande wa network simu inaendana na toleo la Tecno Spark 10 Pro
Kwa sababu camon 20 inasapoti mpaka mtandao wa 4G aina ya LTE Cat 7
Kasi ya LTE Cat 7 ni 300Mbps sawa na 37.5MBps yaani kama unapakuwa faili la ukubwa wa MB 750 simu itachukua sekunde 20 tu kumaliza
Pia kasi ya ku-upload(kupakia) ni 100Mbps, bado ni kubwa kwa viwango vya spidi za network hapa nchini
Sio rahisi kwa hapa nchini kuweza kupata kasi hii kwenye simu za mkononi
Kwa sasa kasi hii inawezekana ukiwa na mtandao wa 5G lakini kumbuka 5G bado haijasambaa maeneo mengi
Pia simu ina masafa yote yanayotumiwa nchini hivyo laini zote zitafanya kazi
Ubora wa kioo cha Tecno Camon 20
Tecno Camon 20 inatumia kioo cha AMOLED ambacho kina resolution ya 1080 x 2400 pixels
Kiubora, vioo vya amoled huwa vina usahihi na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi
Pia ubora wake unachagizwa na kuwa na resolution ya kiwango kikubwa
Kwa maana muonekano wa vitu ni mzuri na wa kuvutia
Pamoja na kwamba kioo chake hakina HDR10+ ama Dolby Vision bado muonekano wa vitu ni mzuri
Kama hufahamu HDR10+ unaweza pitia hapa, maana ya hdr na umuhimu wake
Nguvu ya processor MediaTek Helio G85
Processor inayotumiwa na Tecno Camon 20 katika kazi zake ni mediatek helio g85
Utendaji wake ni wa wastani kwa maana haiwezi kuwekwa kwenye kundi la chip zenye nguvu
Sababu kubwa ni aina ya muundo unaotumiwa kwenye core mbili zenye nguvu sana
Muundo uliotumika ni Cortex A75 tofauti kabisa na Camon 20 Pro 5G inayotumia muundo wa Cortex A78
Cortex A75 una matumizi madogo ya umeme lakini utendaji unakuwa unapungua
Ndio maana gemu kama PUBG linacheza kwa resolution sio kubwa sana kwa kiwango cha 45fps
Ambapo kwa simu zenye nguvu zaidi inafika 85fps
Hata hivyo vitu vingi vitafanya kazi bila tatizo
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya hii simu ni kubwa kwani ina ujazo wa 5000mAh
Na chaji ina kasi ya wati 33 ambayo inajaza hii betri kwa muda wa dakika 70 (kutoka 0% hadi 100%)
Kwa ukubwa wa betri hii simu inakaa na chaji kwa masaa yanayozidi 14 kama ikiwa intaneti muda wote
Na kwa matumizi ya kawaida inaweza chukua hata siku bila kuisha chaji
Aina ya chaji iliyonayo ni zile usb type c(chaji zenye kichwa kipana)
Ukubwa na aina ya memori
Aina ya memori haijaainishwa kwa sababu chip iliyonayo ina sapoti UFS na eMMC hivyo ni ngumu kusema
Ila kama ni UFS ndio itakuwa nzuri zaidi. UFS ni mfumo unaisukuma data nyingi na kwa kasi
Yaani kama ukiwasha simu utaona inafunguka kwa haraka
Kiuzoefu ni kuwa memori za eMMC huwa zinafanya simu kuwa nzito kadri muda unavyokwenda na kadi memori inavyojaa
Camon 20 ipo ya aina moja tu na ina RAM ya GB 8 na memori ya GB 256
Simu inaruhusu kuongeza ukubwa wa RAM kwa kiwango cha GB 5
RAM kubwa ni muhimu kwenye simu za android maana zinakulaga memori ya kutosha
Uimara wa bodi ya Tecno Camon 20
Kwenye matoleo ya Camon 20 tecno wamejitahidi kuimarisha bodi za simu na kudondokewa na maji maji
Maji ya kiwango cha kuchuruzika hayaingi ndani ya simu
Kwani ina viwango vya IP53 vinavyoosharia uwezo wa simu kuzuia vumbi na maji ya kiwango hiko
Ila haina uwezo wa kuzia maji kupenya kama ikizama kwenye kina kikubwa na kwenye maji mengi, na hata mvua kubwa
Hivyo hauna budi kuwa makini unapokuwa kwenye mazingira ya aina hiyo
Pia bodi ya hii simu ni ya plastiki ukiweka kava itakaa muda mrefu bila kupoteza ubora wa rangi
Ubora wa kamera
Hii simu ina jumla ya kamera zipatazo tatu
Kamera kubwa ina megapixel 64 na kiuhalisia simu ina kamera moja tu
Kw maana lenzi iliyoandikwa depth huwa haipigi picha bali kazi yake kubwa ni kufanya vipimo
Ubora wa kamera ni wa kuridhisha hasa kwenye mwanga mwingi
Ila ina changamoto ya kung’arisha kitu sana hivyo ile rangi halisi inakosekana
Kwa wapenda mitandao ya kijamii hii inaweza kuwavutia maana unaweza usihitaji app ya kamera kuweka uzuri kwenye sura yako
Upande wa video hauvutiii sana kwani inaweza kurekodi video za full hd pekee na haina OIS wala EIS kwa ajili ya kutuliza kamera wakati unarekodi huku ukiwa unatembea
Na pia ubora wa picha ni wa kawaida
Ubora wa Software
Hii simu inakuja na Android 13 na HIOS 13 kama ilivyo kwa Camon 20 Pro 5G
Hivyo kufahamu kiundani pitia, Software ya android 13 kwenye camon 20 pro 5g
Washindani wa Tecno Camon 20
Kama ilivyofafanuliwa mwanzoni Camon 20 bei yake inaipeleka simu kwenye ushindani mkubwa
Simu ya kwanza ni Redmi Note 10 yenye kioo cha amoled, kamera za ultrawide na macro na chaji ya 33W na pia kamera inayorekodi video za 4K
Wakati huo bei ya Redmi ni shilingi 400,000/=
Sifa hizi pia zinapatikana kwenye Redmi Note 12 5G ambayo bei yake ni chini ya shilingi laki sita
Simu nyingine ni Realme 10 Pro+ yenye kioo cha amoled na refresh rate ya 120Hz, HDR10+, kamera yenye gyro-EIS na processor yenye utendaji mkubwa kuliko Helio G85
Na bei ya Reame 10 Pro+ ni shilingi 521,000/= kwa hapa nchini
Na kuna matoleo mengine mengi ambayo hatuwezi kuelezea yote
Neno la Mwisho
Matoleo ya Camon yameendelea kuwa ni moja ya matoleo mazuri kwa tecno
Baadhi ya vitu muhimu ya camon 19 vimetumika pia kwenye camon 20 mfano ni processor
Kioo chake ni kizuri na kina ustadi mkubwa wa kuonyesha vitu
Ila bei yake inaizamisha simu kwenye ushindani na simu nyingi ambazo zina vitu vizuri zaidi ya hii
Maoni 23 kuhusu “Bei ya Tecno Camon 20 na Sifa Zake Muhimu”
Ni tuzo gani camon 20 imeshida kimataifa
Sipo aware nayo hii
camon 20 ilishinda tuzo gani ya kidunia?.
Bei halisi ya hiyo simu ni ipi
Bei alisi ya simu hii ni ipi?
ipo kwenye post imewekwa
Hongereni kwa kutoa simu nzuri. Niliona tangazo kuwa simu hii inaweza kukopeshwa, ni kweli? Na kama ni kweli vigezo ni vipi?
Je simu hii twapataje Kwa watu wa Arusha?
fundimadishi5@gmail.com
Bei gan
Cm hii picha yake iko wp ??
Simu nimeinunua ni nzuri
Hongera, kitu gani kikubwa ulichoipendea
Bei halisi ya hi cm ni ipi? Na Kuna uwezekano wa kukopeshwa? Na vigezo vyake
tunahitaji uwezo wa kamera kama pixel 6 or 7 maana ndio matumizi makubwa kwa wana habari madairect ambayo inaweza kuchua hdi movie
Vigezo kukopa
Hatuna hii huduma Kwa sasa
Nahitaji Infix Note 11 prom
Unapatikana wapi
Bei halisi ya simu hizi ni ipi?Nipo Dodoma naipataje?
Nilikua nahitaji Tecno spc 20 inayochomoza camera.
Nmezpenda naipataje
Naitaji ya mkopo sasa napaje
Naitaji ya mkopo sasa naipataje? Na bei ya kuanzia nishingap?