SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu ya Tecno Camon 18 na Sifa Muhimu (2022)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

April 30, 2022

Tecno Camon 18 ni tecno macho matatu ya mwaka 2021 iliyoborehswa ubora kutoka kwa Camon 17

Ubora uliongezeka unaifanya bei ya tecno camon 18 kuzidi shilingi laki nne.

Lakini upande wa sifa za msingi unaifanya bei yake ionekane kubwa

muonekano wa tecno camon 18

Kwenye hii posti utafahamu bei camon 18 na sifa zake kwenye idara muhimu.

Ukijua sifa za simu itakusaidia kujua ubora wake na kufanya maamuzi sahihi

Bei ya Tecno Camon 18 Tanzania

Kwa dar es salaam maeneo ya kinondoni bei Tecno camon 18 ya ukubwa wa ukubwa GB 128 na ram GB 4 ni shilingi 445,000/=

Maduka ya simu ya kariakoo yanaiuza simu kwa 460,000/=

Ongezeko la bei linachangiwa na maboresho ya kwenye utendaji, kamera na kimo cha simu.

Lakini ukizitazama sifa za camon 18 kiundani utangundua kuwa ni simu moja na camon 17

Zifuatilie kwenye jedwari na ufafanuzi wake

Sifa za Tecno Camon 18

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
 • CPU – MediaTek Helio G88
 • Core Zenye nguvu(2) -2×2.0 GHz Cortex-A75
 • Core Za kawaida(6) – 6×1.8 GHz Cortex-A55
 • GPU-Mali-G52 MC2
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
 • Android 11
 • HIOS 8.0
Memori 128GB, RAM 6GB,4GB
Kamera Kamera TATU

 1. 48MP,PDAF(wide)
 2. 2MP(macro)
 3. 2MP(depth)
Muundo Urefu-6.8 inchi
Chaji na Betri
 • 5000mAh-Li-Po
 • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 460,000/=

Upi ubora wa Tecno camon 18

Ubora wa simu ya tecno camon 18 upo kwenye maboresho ya software, kamera na processor.

Camon inakuja na toleo jipya la HiOS.

Utendaji wa simu umeongezeka ukifananisha Camon toleo la 17

tecno camon 18 SUMMARY

Simu ina betri inayokaa na chaji masaa mengi

Resolution za kamera zimeongezwa ubora

Simu ni ndefu na ina muonekano wa kuvutia macho

Lakini sehemu zingine hazina tofauti na mtangulizi.

Fuatilia ufafanuzi wa kila sifa kuielewa camon 18 na 17 ufanano wao

Uwezo wa Network

Moja ya simu ya 4G aina ya LTE Cat 7 ni Camon 18

Simu yenye Cat 7 ina uwezo wa kudownload faili kwa spidi ianyofikia 300Mbps

tecno camon 18 network

4G yake inakubali intaneti ya 4g ya mitandao yote ya Tanzania.

Kwa sababu ina masafa yanayotumika hapa nchini

Ubora wa kioo cha Tecno camon 18

Kioo cha Tecno camon 18 ni cha aina ya IPS LCD chenye refresh rate ya 90Hz

Ni kiasi kinachoifaya simu kuwa fasta ukiwa unaigusa kwenda chini na juu (ku-scroll)

Ubora wa kioo unanogeshwa na resolution kubwa ya 1080 x 2460 pixels

Hivyo vitu vitaonekano kwa uzuri japo simu haina HDR10

Uangavu wake sio mkubwa kiasi cha konyesha vitu kwa ustadi simu ikiwa juani

Kiujumla kioo cha ips lcd huwa na ubora mdogo ukifananisha na vioo vya oled vya simu za sony xperia

Nguvu ya processor MediaTek Helio G88

Utendaji wa simu ya Tecno camon 18 unaweza kucheza gemu kubwa nyingi.

Hilo inasababishwa na simu kutumia chip ya Helio G88.

Helio G88 ni processor ya simu yenye core nane zilizo gawanyika katika sehemu mbili.

Sehemu za core kubwa ndio inachangia simu kuwa na uwezo mzuri kiutendaji.

Na sehemu ya core ndogo unaifanya simu kuwa na matumizi madogo ya betri

Core kubwa zina spidi inayofikia 2.0 GHz na ni za aina ya Cortex A75

Na core ndogo zina spidi inayofikia 1.8 GHz na za aina ya Cortex A55

Cortex A75 ina uwezo mkubwa wa wastani.

Kama unataka kujua aina ya processor, basi pitia hapa jinsi ya kujua uwezo wa processor za simu

Uwezo wa betri na chaji

Camon 18 ina betri kubwa lenye ujazo wa 5000mAh

Hili ni aina ya betri linalokaa na chaji muda mrefu

Ila chaji yake haipeleki umeme mwingi.

Kwani unajaza chaji kwa wati 18.

Hivyo simu inaweza kuchukua muda mwingi mpaka kujaa kwa asilimia 100

Ukubwa na aina ya memori

Kuna matoleo ya aina mbili ya Tecno hii zenye ukubwa wa GB 128

Kinachotofautiana ni ukubwa wa RAM

Kwani ipo yenye ram ya 4GB na ram ya 6GB

Lakini haijainishwa aina ya memori kama ni eMMC 5.1 au UFS 2.1

Uimara wa bodi ya Tecno Camon 18

Bodi ya simu imeundwa kwa plastiki upande wa nyuma

Na kwenye display kuna glasi lakini sio kioo cha gorilla

Pia simu inakosa uwezo wa kuzuia maji kupenya kama ikizamishwa kina kirefu

Simu ni ndefu, upana na urefu wake ni inchi 6.8

Ubora wa kamera

Tecno camon 18 ina kamera zipatazo tatu.

Huku kamera kubwa ikiwa na resolution ya 48MP

Na inatumia teknolojia ya ulengaji aina ya PDAF

tecno camon 18 camera

PDAF hailengi vizuri vitu vinavyotembea kwa kasi ukilinganisha na dual pixel pdaf

Kamera nyingine ya depth ina pixel chache.

Hii ni kamera inayotumika kukadiria umbali kati ya simu na kitu kinachoigwa picha

Na pia simu ina kamera ya macro kwa ajili ya kupiga picha vitu vya karibu sana na kamera

Kiujumla kamera zake si nzuri sana hasa upande wa kurekodi video

Kwani inarekodi video za full hd pekee na hazina OIS

Ubora wa Software

Camon 18 inakuja na toleo la android 11 lenye mfumo wa HIOS 8.0

HIOS 8.0 inakupa kitu kinaitwa “Always On Display”

Always On Display huonyesha taarifa ya baadhi ya app bila kufungua simu.

Kama kuna meseji mpya basi screen itaonesha idadi ya meseji zilizoingia

Yapi Madhaifu ya Tecno camon 18

Simu haina kamera ya kupiga eneo pana sana kwa nyuzi 120

Hizi ni kamera zinazofahamika kama ultrawide.

Pia Tecno wameendelea kutumia ulengaji aina ya pdaf

Simu inaweza kuingia maji kwani haina ulinzi hata wa kuzuia maji tiririka

Kioo chake kinakosa uwezo wa kuboresha muonekano wa vitu kwa maana haina HDR10

Kamera za hii simu haziwezi kurekodi video za 4K

Utendaji wa processor bado ni wa wastani wakati huo bei yake imepanda kidogo

Neno la Mwisho

Tecno Camon 18 ni simu nzuri ya Tecno kati ya tecno mpya za 2021 na 2022.

Ila bei yake inamshawishi mtumiaji kutafuta simu mbadala

Kuna simu kama ya Vivo t1 5g inaendana bei na camon 18

Lakini camon 18 haisogei kiubora kwa vivo t1

Hivyo tecno wanapaswa waishushe bei ya simu.

Lakini kwa mtu anaejali ukubwa wa memori pekee basi simu ina bei rafiki sana

 

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

Bei ya Tecno Spark 20 Pro+ na Sifa zake

Simu ya Tecno Spark 20 Pro+ ilitoka rasmi desemba ya mwaka 2023 ila kwa Tanzania imeanza kupatikana miezi ya karibuni Kwa Tanzania bei ya juu kabisa ya Tecno Spark 20 […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

Bei ya Tecno Spark 20 na Sifa Zake Muhimu

Tecno Spark 20 ni toleo la Tecno lilotoka mwishoni mwa mwaka 2023 hivyo ni simu inayofaa hata kwa mwaka 2024 Bei ya Tecno Spark 20 yenye ukubwa wa memori ya […]

No Featured Image

Bei ya Tecno Spark 4 na Spark 3 Pro na sifa muhimu 2023

Simu za Tecno Spark 4 na Spark ni simu za daraja la chini za mwaka 2019 Spark 3 ilitangulia kabla ya spark 4 Kiteknolojia, hazina vitu vizuri na hivyo basi […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram