Tecno Camon 18 Premier ni simu bora ya Tecno ambayo imetoka mwishoni mwa mwaka 2021
Ubora wake unaifanya bei ya Tecno Camon 18 Premier kuzidi shilingi laki saba kwa mikoa mingi Tanzania
Ubora wa camon 18 premier uko wazi kwa kuzitazama sifa zake muhimu zipatazo nane
Kwenye hii post utajua bei yake, ubora wa kioo, chaji na nguvu kubwa ya utendaji ya hii tecno mpya
Bei ya Tecno Camon 18 Premier Tanzania
Kwa maduka ya simu ya kariakoo bei ya tecno camon 18 premier yenye ukubwa wa GB 256 na RAM ya 8GB ni shilingi 750,000/=
Ukiendelea kusoma makala utagundua kuwa camon 18 premier ina kasoro chache
Kwa hiyo haishangazi bei yake kuwa kubwa
Fuatilia sifa za simu hii kwenye kila nyanja uelewe ubora wa tecno hii ya 2021
Sifa za Tecno Camon 18 Premier
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS ,256GB,RAM 8GB, |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 760,000/= |
Upi ubora wa simu ya Tecno Camon 18 Premier
Ubora wa simu aina ya tecno camon 18 premier upo kwenye kamera, chaji na betri, kioo na ukubwa wa memori
Kioo cha simu ni chepesi hasa ukiwa unacheza magemu
Chaji yake inawahi kujaza betri kwa haraka ndani dakika chache
Kamera yake imewekewa mfumo wa kipekee wa kutuliza video wakati wa kurekodi
Network ya simu inaweza kudownload mafaili makubwa kwa spidi kubwa
Kuna vitu ambavyo tecno wameviweka vinavyoongeza uwezo mkubwa wa simu
Fuatilia maelezo yote uvifahamu hivyo vitu
Uwezo wa Network
Camon 18 premier ni simu yenye 4G aina ya LTE Cat 13
Cat 13 ina spidi ya kudownload inayoweza kuzidi 600Mbps
Kama simu inadownload faili la ukubwa wa 1.2GB basi simu itachukuwa sekunde kama 10 kudownload faili lote.
Ila kwa bahati mbaya mitandao ya Tanzania haina spidi kubwa ya 4G
Kwa mfano halotel kwa maeneo mengi spidi yake ya juu ya kudownload ni 42Mbps
Premier inasapoti intaneti ya 4G ya mitandao yote nchini
Ubora wa kioo cha Tecno Camon 18 Premier
Kioo cha tecno camon 18 premier ni kioo kinachoonyesha vitu kwa rangi halisi kwa kiasi kikubwa.
Hiyo inatokana na kuwa na kioo cha amoled
Uzuri wa kioo pia umeongezwa na kuwa refresh kubwa ya 120Hz
Simu ikiwa na refresh inayozidi 90Hz inakuwa nyepesi sana wakati wa kutachi(ku-scroll)
Na inafanya simu kucheza gemu kwa ustadi
Tecno hii ina resolution kubwa ambayo inaongeza ubora wa muonekano wa vitu.
Resolution yake ni 1080 x 2400 pixels
Kiujumla camon premier ina kioo kizuri
Nguvu ya processor MediaTek Helio G96
Simu ya tecno camon 18 premier inatumia chip ya mediatek helio g96 kufanya kazi zake
mediatek helio g96 ni processor ya daraja la kati ambayo utendaji wake ni mkubwa.
Ni processor inayoweza kucheza gemu la Call of Duty: Mobile kwa spidi ya 42fps
Geekbench inaipa alama nyingi zipatazo 536 kwenye core moja.
Hivyo camon 18 premeier ina nguvu zaidi kuliko camon 17 na 18
Kinachoipa helio g96 ni muundo wa kiuwezo wa core kubwa na core ndogo
Uwezo wa core kubwa
Helio G96 ina core kubwa zenye nguvu sana zipatazo mbili
Spidi ya kila inaweza kufika 2.05 GHz
Na zinatumia muundo wa Cortex A76
Cortex A76 inaweza kufanya kazi nne kwa mzunguko mmoja kwa kila sekunde
Wakati huo processor inafanya mizunguko bilioni 2.05 kwa sekunde
Kwa maana hiyo processor inaweza kupiga kazi kubwa kuliko Cortex A75 ambayo ipo kwenye Infinix Hot 11
Uwezo wa core ndogo
Processor inatumia core ndogo zipatazo sita zenye spidi ya 2.0 GHz
Zimeundwa kwa mtindo wa Cortex 55
Ni muundo ambao unatumia nguvu ndogo
Processor ya Helio G85 inatumia muundo huo ila utendaji wake sio mkubwa kama Helio G96
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya camon 18 premier ina ukubwa wa 4750 mAh aina ya Li-Po
Betri inajaa kwa haraka kwa sababu inatumia chaji inayopeleka umeme mwingi wa wati 33
Mara nyingi chaji ya 33W hujaza betri chini ya masaa mawili
Simu inakaa na chaji masaa yapatayo 112 kama ikiwa haitumiki mara nyingi
Ukubwa na aina ya memori
Kuna toleo la aina moja tu la tecno camon 18 premier kwenye memori
Memori yake ina ukubwa wa 256GB aina ya UFS 2.2
Memori yake inaiongezea simu uwezo wa utendaji
Kutokana na uwezo wake wa kusafirisha data kwa kasi kubwa
Uimara wa bodi ya Tecno Camon 18 Premier
Hii ni moja ya simu ya tecno ambayo inewekewa glassi upande wa nyuma.
Tecno hawajaonesha kampuni iliyounda kioo chake.
Lakini kiujumla bodi ya kioo inaipa ulinzi wa ziada simu hasa kutoka kwenye michubuko
Na kioo pia kimewekewa glassi
Kama utakuwa huaimini simu sana unaweza kununua screen protector
Ubora wa kamera
Smartphone ya Tecno camon 18 premier ni tecno macho matatu
Kamera yake ya ultrawide imewekewa gimbal OIS
Hivyo kuna utulivu wa kurekodi video ukiwa unatembea
Simu inatumia teknolojia ya ulengaji ya pdaf ambayo sio bora sana kama dual pixel
Kizuri cha tecno premier ni kutokutegemea digital zoom (zoom ya app) pekee bali ina kamera ya Telephoto
Telephoto ni kamera inayopiga picha kwa umbali mrefu bila kupoteza pixels.
Camon inaweza kuzoom mara tano kama unatumia telephoto
Simu inaweza kurekodi mpaka video za 4k
Ubora wa Software
Simu inakuja na mfumo endeshi wa android 11 na software ya HIOS 8.0
HIOS 8.0 ina mpangilio mzuri kwenye settings
Settings ni rahisi kufikika na ina icon zinazomuelewesha kwa uzuri mtumiaji wa simu
Yapi Madhaifu ya Tecno Camon 18 Premier
Simu haina viwango vya IP53 wala IP68
Hii inamaanisha haina uwezo wa kuzuia maji kupenya ndani ya simu
Tecno walipaswa kutumia processor yenye nguvu zaidi ya Helio G96
Kwa sababu utendaji wa G96 hauendani na ubora wa kiujumla wa simu
Neno la Mwisho
Kama unatafuta simu bora ya tecno kwa 2022 basi ni Tecno Camon 18 Premier.
Japokuwa utendaji wa chip unaweza kuifanya bei yake iwe kubwa lakini ni simu nzuri ya tecno ya kuwa nayo
Camon premier inaweza kushindana na matoleo mengi mapya ya daraja la kati kutoka vivo, redmi, oppo na samsung
Wazo moja kuhusu “Bei ya Simu ya Tecno Camon 18 Premier na Sifa Zake Muhimu (2022)”
Nice