Kampuni ya Samsung ilizindua simu nzuri ya kundi la kati aina ya Samsung Galaxy A52 mwanzoni mwa 2021
Utendaji wa Galaxy A52 ni wa kiwango kikubwa unaochuana na simu nyingi za android 2022
Hivyo inafanya bei ya samsung galaxy a52 izidi shilingi laki nane ikiwa mpya
Japokuwa kisifa ni simu inayopaswa kuuzwa chini ya laki nane kwa sasa ili iwe shindani
Ila simu ina vitu vingi vinavyoshawishi kuinunua kama utakavyoona baadae kwenye makala hii
Bei ya Samsung Galaxy A52 ya GB 128
Kwa hapa Tanzania hasa Dar Es Salaam bei ya samsung galaxy a52 ikiwa mpya ni shilingi 860, 000/=
Wauzaji wanaoiuza ikiwa imetumika wengi wanaiuza kwa shilingi 560,000/=
Kwa bei isiyozidi laki sita inastahili zaidi kwa sasa kutokana na uwepo wa matoleo ya simu za xiaomi na Realme
Kuna simu mpya za laki nane za xiaomi ambazo zina sifa za ziada nyingi ambazo hazipo kwenye Samsung A52
Sifa za Samsung Galaxy A52
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super AMOLED, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.1: 256GB,128GB na RAM 8GB,6GB,4GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 860,000/= |
Ni upi ubora wa simu ya Samsung Galaxy A52?
Galaxy A52 ni simu inayoweza kuzuia maji kupenya ndani
Ina kamera inayoweza kupiga eneo pana
Chaji yake inawahi kujaza betri kwa muda mfupi
Utendaji wake ni mkubwa kutokana na kutumia chip yenye nguvu
Ina kioo chenye uwezo wa kuonyesha rangi nyingi hivyo vitu vitaonekana kwa ufanisi
Ina nafasi kubwa za kuweka applikesheni na mafaili mengi
Kioo chake ni chepesi(smooth) kutachi na kuchezea magemu
Uwezo wa Network
Samsung A52 ni simu ya 4G inayokubali masafa 13 yakiwemo yanayotumiwa na mitandao ya simu ya Tanzania
Aina 4G simu inayotumia ni LTE Cat 15
Spidi ya juu kabisa ya kudownload faili ya LTE Cat 15 ni 800Mbps
Kasi hii inaweza kudownload faili la ukubwa 1000MB kwa sekunde kumi tu
Lakini hilo inategemea na nguvu ya mtandao wa simu kwa kiasi kikubwa
Kwa mfano Halotel kwa baadhi ya maeneo kasi yake ni 27Mbps
Hii ni 3% ya uwezo wa simu ya samsung galaxy a52 iliyonayo kwenye network
Hivyo, kwa faili la 1000MB itachukua sekunde 294 sawa na dakika tano(kimakadirio) kumalizika kudownload lote
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A52
Kioo cha Samsung Galaxy A52 ni aina ya super amoled ambavyo huundwa na samsung wenyewe
Kwenye usahihi wa rangi, super amoled huwa ipo mbele ya vioo vya IPS LCD
Rangi nyeusi inaonekana kwa kukolea sana kwenye super amoled
Uzuri wa kioo cha galaxy a52 ni kuwa na refresh rate kubwa ya 90Hz
Refresh rate kubwa inatengeneza uwepesi wa kutachi simu na kucheza gemu
Ubora wake wa kioo unachangiwa pia na resolution kubwa ya 1080 x 2400 pixels
Nguvu ya processor Snapdragon 720G
Kila kitu kinachofanywa na Galaxy A52 kinachakatwa na processor ya Snapdragon 720G
Ni chip yenye jumla ya core zipatazo nane
Kati ya hizo core zenye nguvu zipo mbili na core zenye utendaji mdogo zipo sita
Core zenye nguvu kubwa zinaifanya simu kuweza kufanya kazi kubwa kwa urahisi
Kama unacheza la PUGB Mobile, processor itacheza kwa resolution kubwa na kwa kutoa 42fps
Ndio maana Geekbench inaipa chip alama 565 japo sio nyingi kama Apple A14 Bionic
Apple A14 Bionic imetumika kwenye simu ya iPhone 12 Pro Max
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya Samsung Galaxy A52 inapeleka umeme wa wati 25
Ni umeme unaoweza jaza simu kwa 50% ndani ya nusu saa
Betri yake ina ukubwa wa 4500mAh
Betri hii inaweza kuisha chaji baada ya masaa 14 simu ikiwa inatumia intaneti masaa yote mfululizo
Hivyo unapata simu yenye utendaji mkubwa na ukaaji wa chaji wa kuridhisha
Ukubwa na aina ya memori
Kuna Samsung Galaxy A52 za GB 128 na 256
Kinachotofautiana sana ni ukubwa wa RAM
Kwani zipo zenye RAM ya 4GB, 6GB na 8GB
Ukipata yenye RAM kubwa inamaanisha simu itakuwa na uwezo wa kufungua apps nyingi kwa urahisi zaidi
Ikizingatiwa aina ya RAM zake ni LPDDR4X yenye bandwidth ya juu kabisa 13Gbps
Aina ya memori zake ni UFS 2.1 ambazo usafirishaji wake wa data ni 1200MBps
Kwa maana kama unakopi faili la 2400MB kwenda kwenye simu basi itamalizika kukopi kwa sekunde mbili
Memori za UFS hufanya simu kufungua app kwa haraka
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A52
Hii simu inalindwa na kioo cha Gorilla 5 upande wa nyuma na mbele
Ni ngumu simu kupasuka kama ikianguka kwa kimo cha mita moja kwenye uso wa ardhi ulio flati
Lakini ikianguka kwa kimo cha 2m screen ya simu lazima ipasuke
Kioo cha gorilla ni kigumu pia kuchunika
Ukichukua sarafu ya shilingi mia na kuanza kuisugua kwenye kioo au nyuma hutoona mikwaruzo
Galaxy A52 ina viwango vya IP67
Hivyo hii ni simu ambayo haipitishi maji
Ukiingiza kwenye jagi la maji simu itaendelea kufanya kama kawaida ikiwa ndani ya maji
Ila kwa maji ya kina cha mita moja simu inavumilia kwa muda wa nusu saa
Ubora wa kamera
Ukilinganisha kamera ya iphone 12 pro max na ya Samsung Galaxy A52, utaona samsung ina ubora wa kawaida sana
Japo ukiitizama hii picha ambayo imepigwa na A52 inaonyesha inatoa picha zenye ubora mkubwa
Kama unalinganisha hii simu na simu ya Tecno Phantom X, utaona samsung pia ina kamera nzuri
Katika kamera nne kuna kamera moja tu yenye autofocus aina ya PDAF na OIS
Kwa maana kamera zingine hazitotoa picha nzuri ukiwa unapiga picha kitu kinachokimbia kwa kasi
Simu inaweza kurekodi video za 4K kwa kiasi cha fremu 30
Na video za full hd zinaweza kurekodiwa mpaka kwa fremu 60 kwa sekunde
Kwa kuwa kamera kuu ina OIS, basi video itatokea kwa kutulia wakati wa kurekodi huku ukiwa unatembea
Ubora wa Software
Samsung Galaxy A52 ni simu ya android 11
Na inaweza kupokea toleo jipya la android 12
Mbali na android simu inakuja na mfumo wa One UI 4.1
One UI 4.1 ina maboresho mengi ikiwemo Camera, Audio Connection na upande wa Gallery
Kamera imeongezewa uwezo wa kuzoom wakati wa kuchukua picha na kurekodi video
Kwani app ya kamera inaweza kuzoom mara 20 ukiwa unarekodi video
Na inaweza kuzoom mara 10 kama unapiga picha
Hivyo basi inakurahisishia kurekodi kitu ambacho kipo mbali na kamera ya simu
Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy A52
Udhaifu mkubwa unaweza ukawa upo kwenye kamera
Hasa kamera za ultrawide na macro hazijawekewa aina yoyote autofocus
Na pia hazina OIS kwa ajili ya kurekodi video kwa utulivu
Pia display ya galaxy haijaboreshwa zaidi
Kwani haina HDR10 wala dolby vision ambazo huboresha muonekano wa vitu
Neno la Mwisho
Kama unahitaji simu ya daraja la kati ambayo ina ubora kwenye maeneo mengi basi Samsung Galaxy A52 lazima iwepo kwenye listi
Hivyo bei yake inakupasa uwe na bajeti ya kueleweka kidogo
Na hata kama utapata iliyotumika, umakini ni muhimu kutokana na baadhi kuwa mbovu
Wazo moja kuhusu “Bei ya Simu ya Samsung Galaxy A52 na Sifa Muhimu (2022)”
Asante kwa maelekezo manzur