Simu ya iPhone 12 Pro Max ni simu ya daraja la juu iliyotoka mwaka 2020
Japo ina miaka miwili ila bado inapokea matoleo mapya ya iOS
Kitu kinachoifanya simu kuendelea kuwa na thamani
Kwani bei ya iphone 12 pro max kwa Tanzania inakaribia shilingi milioni mbili
Na hapo nyingi ni used sio mpya
Sifa za iPhone 12 pro max bado ni kubwa mno ukilinganisha na simu nyingi mpya za mwaka 2022 kama Tecno Camon 19 Pro 5G
Bei ya iPhone 12 Pro Max ya GB 128
Kwa Tanzania, iPhone 12 Pro Max yenye ukubwa wa GB 128 inapatikana kwa shilingi milioni 1.9
Hii ni simu janja ambayo imekamilika kila idara na inachuana na simu kama Xiaomi 12 Pro
Bei yake bado ni kubwa hata kwenye mtandao wa ebay na amazon
Sababu kubwa sifa zake nyingi bado zinaendana na wakati uliopo
Sifa za iPhone 12 Pro Max
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED, |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 256GB,128GB,512GB na RAM ,6GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,900,000/= |
Ni upi ubora wa simu ya iPhone 12 Pro Max
Ni simu inayokubali mtandao wenye kasi kubwa kwa maana 5G
Ni moja ya simu yenye kamera inayotoa picha nzuri katika kamera zake zote tatu
Ina uwezo wa kupokea toleo jipya la mfumo endeshi wa iOS
Ina memori zinazosafirisha data kwa kasi
Utendaji wa simu ni mkubwa unaozipita processor nyingi mpya za simu
iPhone 12 Pro Max ina uwezo wa kuzuia maji kupenya
Ina bodi ngumu kuvunjika na kuchunika pia
Uwezo wa Network
iPhone 12 Pro Max ni simu ya 5G inayokubali aina zote za 5G ikiwemo ile yenye kasi kubwa zaidi
Kwa maana ina 5G yenye kasi inayozidi 1000Mbps
Kwa Marekani, kasi 5G kwa mtandao wa T-Mobile inafika 1058Mbps verizon inazidi 2000Mbps
Yaani kama unadownload faili la 1200MB, simu itamaliza kudownload baada ya sekunde 9 tu
Ni kama ndoto ila ndio uhalisia ambao kwa Tanzania bado haupo
Na 4G yake ina masafa zaidi ya 30 hivyo mitandao ya 4G karibu yote duniani itafanya kazi kwenye hii simu
Aina ya 4G inayotumia ni LTE Cat 18 yenye kasi inayofikia 1200Mbps
Ila Tanzania hakuna mtandao unaoweza kukupa kasi hii
Ubora wa kioo cha iPhone 12 Pro Max
Katika kuonyesha vitu kiustadi iPhone huwa ina vioo vinavyojitahidi kuonyesha vitu kwa uharisia
Inatokana na simu kuwa na kioo aina ya OLED
Hivi vioo huwa vinaonyesha rangi nyingi na kwa usahihi
Ubora wake wa kioo unachagizwa na uwepo wa resolution kubwa ya 1284 x 2778 pixels
Na pia kioo kuwa na HDR10, dolby vision na uangavu unaifikia nits 800 hadi 1200
HDR10 na Dolby Vision hizi ni teknolojia za vioo ambavyo hujaribu kurekebisha muonekano wa vitu uendane kama jicho la binadamu linavyoona kwenye mazingira halisi
Basi kioo chenye hivyo hdr au dolby vision huonyesha picha kwa uzuri zaidi kuliko simu zisikuwa nazo
Nguvu ya processor Apple A14 Bionic
Katika orodha tano ya processor za simu zenye nguvu Apple A14 Bionic imo
iPhone 12 Pro Max inatumia chip ya Apple A14 Bionic ambayo ina core sita
Core zenye nguvu zipo mbili hufahamika kwa jina la Firestorm
Na core zinatumika kwenye kazi ndogo ndogo huitwa Icestorm
Utendaji wa apple a14 bionic unaweza kusukuma gemu ya PUGB Mobile 2018 kwenye resolution kubwa kwa kasi ya fremu 58 fps
Video zenye “graphics effects” kubwa kama Manhattan Offscreen zinacheza kwa fremu 180fps
Hii ni tofauti na MediaTek Helio G70 ambayo inacheza video hiyo hiyo kwa fremu 27fps
Helio G70 imetumika kwenye simu ya infinix hot 10t
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya apple iphone 12 pro max inapeleka umeme wa wastani wa wati 15 tu
Betri yake ina ukubwa wa 3687mAh Li-Ion hivyo betri inaweza isichukuwe muda mwingi kujaa
Ukaaji wa chaji wa iphone macho matatu ya 2020 ni wa kiwango kikubwa pamoja na kutokuwa na betri ya 5000mAh
Kwani ukiwa unaperuzi intaneti masaa mengi mfululizo simu inachukua masaa 14 chaji kuisha
Hiki ni kiwango cha simu ya Redmi Note 10 yenye betri ya 5000mAh
Ukubwa na aina ya memori
Apple iPhone 12 Pro Max ina matoleo ya aina tatu upande wa memori
Kuna ya GB 128, 256 na 512
Mfumo wa memori unaotumiwa na simu za apple ni NVMe
NVMe ina kasi ya kusafirisha data inayofikia 3GBps, ni mara tano ya mfumo wa eMMC 5.1
Simu ikiwa inatumia intaneti yenye kasi inahitaji kasi kubwa ya memori kwenye kuandika na kusoma data za faili
Vinginevyo uwezo wa simu utakuwa ni mdogo na faida ya intaneti yenye kasi hutoiona
Uimara wa bodi ya iPhone 12 Pro Max
Bodi ya iPhone 12 Pro Max haipitishi maji kama simu ikidumbukia kwenye kina cha maji ya mita sita kwa muda wa nusu saa
Hii inatokana na simu kuwa na viwango vya IP68
Upande wa nyuma simu imewekewa kioo cha gorilla glasi japo haijainishwa ni toleo lipi
Ila vioo vya gorilla huwa ni vigumu kuchunika na kupasuka
Upande wa pembeni imewekewa chuma wenyewe wanaibrandi kama Stainless Steel Frame
Hii simu haina sehemu ya memori kadi wala sehemu earphone
Kiuhalisia simu ni ngumu na imara
Ubora wa kamera
Linapokuja swala la kamera simu za apple huwa zina ubora mzuri wa picha
Kwenye picha za mchana, iphone 12 pro max inatoa picha safi na kwa uwiano wa rangi ulio sahihi
Hata ukizoom kitu kilicho mbali bado vitu vinaonekana kwa kutambulika na kama inavyotakiwa
Pitia na itazame: picha zilizopigwa na simu ya iPhone 12 Pro Max
Ubora wa picha unachangiwa na simu kuwa na ulengaji wa dual pixel pdaf kwenye kamera ya wide
Na kamera za ultrawide na telephoto zina OIS, ambayo hufanya video kurekodiwa kwa kutulia wakati unarekodi huku unatembea
Kamera zake zinaweza kurekodi mpaka video za 4k kwa fremu za 30fps na 60fps
iPhone 12 Pro Max inarekodi video na zinatokea vizuri kwa sababu ya kuwa na Dolby Vision HDR
Pitia Hapa kuelewa: Maana ya HDR na Umuhimu wake kwenye simu
Ubora wa Software
Kama utaipata simu ikiwa mpya basi kwa mara ya kwanza utakutana na mfumo endeshi wa iOS 14
iOS 14 ulikuwa ni mfumo wa mwanzo wa apple uliokuwa na kitu kinachofahamika kama app library
Apple library ni mtindo ambao unazikusanya app zinazofanana katika kundi moja
Kwa mfano app ambazo umeziongeza kwenye simu kwa nyakati zinazoendana zinaenda kwenye folder moja
App za mitandao ya kijamii na zenyewe mfumo unaziweka sehemu moja
Inasaidia kuweza kuipata app unayoitafuta kwa haraka
Yapi Madhaifu ya iPhone 12 Pro Max
Apple wamepuuzia kuweka radio kwenye simu zao ikiwemo hii
Kama utahitaji kusikilizia kipindi cha redio itakulazimu utafute app kama tunein
Kitu kinachoongeza gharama za kununua data
Pia apple inaongeza gharama nyingine ya kununua earphone za bluetooth
Kwa sababu iphone 12 pro max haina sehemu ya kuchomeka waya wa earphone
Chaji ya apple ni ndogo inayojaza simu kwa dakika 92
Wakati simu kama Mi 10 Ultra inajaza betri kwa dakika 27 tu
Kibaya kingine ni simu kutokuwa na sehemu ya memori kadi
Japokuwa simu zina ujazo mkubwa, lakini vitu vinaweza kujaa hasa kwa ile yenye GB 128
Neno la Mwisho
Kama unahitaji simu iliyo kamili kwenye idara nyingi basi bei ya iphone 12 pro max haiwezi kukutisha
Kwa sababu utakuwa unamiliki simu inayoweza dumu muda mrefu na yenye kupokea maboresho mengi ya iOS
Kwani sasa iPhone 12 Pro Max inaweza kupokea toleo la iOS 16
Maoni 5 kuhusu “Bei ya iPhone 12 Pro Max Tanzania na Sifa Zake (2022)”
Ninafurahi kupata elimu ktk platform hii napongeza Kwa jitihada
ntajuaje iphone origional na fake?
ntawezaje kutambua iphone origional na fake?
I am impressed with the quality of your phones
Nitajuaje kama Iphone 12 feke