Simu ya Google Pixel 8 Pro imezinduliwa mwezi wa kumi (oktoba) 2023
Ni simu ya daraja la juu kama ilivyo kwa iphone na samsung matoleo ya S-series
Kwa maana hiyo bei ya google pixel 8 pro inatarajiwa kuwa zaidi ya milioni mbili kwa Tanzania
Pixel 8 Pro ina ubora katika maeneo mengi kitu kinachosaidia kutimiza mahitaji ya mtumiaji kwenye kila nyanja
Ila kubwa zaidi simu za google huwa na kamera nzuri kuliko hata washindani wake
Ili kuielewa ubora wa hii simu itabidi uelewe sifa zake kila moja
Bei ya Google Pixel 8 Pro ya GB 128
Google Pixel 8 Pro yenye GB 128 inauzwa shilingi za Tanzania milioni 2 na laki nane
Kwenye duka la mtandaoni la Amazon bei yake inaanzia milion 2.6
Kuna tofauti ndogo kwa muhitaji asiye na haraka anaweza akaagaza kwa maana inachukua muda kidogo mpaka kukifikia
Bei ya simu inaendana sana na sifa zake japo baadhi ya chambuzi zimeonyesha mapungufu kwenye utendaji hasa upande wa magemu
Ila kitu unachopaswa kuzingatia ni kuwa Google wamejikita zaidi katika software kuliko hardware
Sifa za Google Pixel 8 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | LTPO OLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1,256GB,128GB,512GB,1TB na RAM 12GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,800,000/= |
Upi ubora wa Google Pixel 8 Pro
Kioo cha pixel 8 pro kina uwanda mpana wa uonyeshaji kiwango kikubwa cha rangi
Chaji yake inajaza betri kwa muda mfupi
Pia betri yake ni kubwa
Kamera zake zinapiga na kurekodi video kwa ubora mkubwa
Inatumia mfumo wa memori wenye kasi kubwa ya kusafirisha data
Utendaji wa simu kiujumla ni wa kuridhisha
Ni simu inayosapoti aina mbalimbali za network kwa maana hadi 5G
Uwezo wa network
Google Pixel 8 Pro ni simu ya 5G ambayo inasapoti pia aina nyingine za mitandao
Inakubali karibu masafa yote yanayotumiwa na simu mbalimbali duniani
Kw maana hiyo hata 5G za Airtel, Tigo na Vodacom zitafanya kazi vizuri
Hii simu inakubali mpaka 5G ya masafa marefu yenye kasi zaidi
Ikumbukwe kuwa mitandao ya Tanzania inatumia yenye masafa ya kati
Na kwa bahati mbaya sio mikoa yote yenye network 5G
Kwa sehemu network hii ipo Dar Es Salaam na Dodoma kwa airtel
Na Dar pia na kwa maeneo machache.
Ubora wa kioo cha Google Pixel 8 Pro
Kioo cha google pixel 8 pro ni aina ya LTPO OLED chenye refresh rate ya 120Hz
LTPO inasaidia kioo kutotumia refresh rate kila wakati
Kuna aina ya matumizi ambayo hayahitaji refresh rate 120Hz
LTPO inaweza kuyaainisha na kuseti kiwango kidogo cha refresh rate
Kioo cha hii simu kina uwezo wa kuonyesha rangi kutokana na uwepo wa HDR10+
Uangavu wa kioo ukiwa nje unaweza kufika mpaka nits 1400
Hivyo vitu vitaonekana vizuri tu ukiwa unatumia simu kwenye mazingira ya jua kali
Simu zenye uangavu mdogo humpa mtumiaji wakati wa kuona vitu kwenye kioo kama ukiwa juani
Uzuri ni kuwa kioo cha hii simu resolution ni kubwa pia ambayo ni 1344 x 2992 pixels
Nguvu ya processor
Simu za google kwa sasa wanatumia processor wanazounda wenyewe
Processor inayoiwezesha google pixel 8 pro kufanya kazi zake ni Google Tensor G3
Google Tensor G3 imegawanyika sehemu tatu na ina idadi ya core zipatazo tisa(9)
Processor nyingi za simu huja na core 8 lakini hiki sio kigezo cha chip kuwa na utendaji
Kwani Google Tensor G3 imeonyesha kiwango cha chini kwa baadhi ya gemu ukilinganisha na washindani wake ambao ni Snapdragon 8 Gen 2 iliyotumika kwenye Samsung Galaxy S23 Ultra na pia Apple A17 Pro iliyopo kwenye iPhone 15 Pro Max.
Moja ya kitu kinachoshangaza ni ufanisi wa matumizi ya betri
Google Tensor G3 inakula chaji zaidi ya snapdragon na apple a17 pro
Kwenye app ya kupima nguvu za processor inayoitwa Geekbench, Google Tensor G3 ina alama 1700 ambazo kwa levo yake ni ndogo
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Google Pixel 8 Pro ina ukubwa wa 5050mAh
Ukiwa mtumiaji sana wa simu kuanzia intaneti, kuangalia video za youtube, kucheza gemu na mambo mengine hii simu inaweza kudumu mpaka masaa kumi(10)
Ni masaa mengi kwa wastani ila ukitazama bei ya simu na washindani wake ambao ni Samsung Galaxy S23 Ultra na iPhone 15 Pro Max, betri ya google iko nyuma kwa zaidi ya masaa mawili
Sababu kubwa inasababishwa na processor yake ya Google Tensor G3 kuwa na ufanisi usioridhisha(tutaangalia kiundani)
Kwenye upande wa chaji, simu inasapoti chaji ya wati 30
Ambayo inaweza kujaza simu kwa 50% ndani ya nusu saa
Kimakadirio simu inaweza kujaa kwa 100% ndani ya dakika 80 yaani lisaa na dakika 20
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo manne ya pixel 8 pro upande wa memori
Unaweza kumiliki ya GB 128, 256, 512 na 1TB zote zikiwa na GB 12
RAM kubwa ni msaada sana kwenye simu kwani utaweza kufanya vitu kwa wakati mmoja pasipo kuganda ganda
RAM ikiwa ndogo kuna nyakati inawahi kujaa hivyo unalazimika kufunga baadhi ya app na huwa inakera
Kwa viwango hivi vya memori utaweza kuhifadhi mafaili mengi wala hutokuwa na wasiwasi wa whatsapp kujaza mapicha mengi kutoka kwenye magrupu.
Uimara wa bodi ya Google Pixel 8 Pro
Bodi ya Google pixel 8 Pro imeundwa kwa vioo vya Gorilla Victus mbele na nyuma
Ni vioo vigumu kupasuka na kuchunika (Ni stahimilivu kiujumla)
Ukiizamisha pixel 8 pro kwenye maji ya kiwango cha ndoo ya lita 20 au diaba kwa muda wa nusu saa maji hayatoingia ndani ya simu
Ina viwango vya IP68 vinavyoashiria uwezo wa simu kutopitisha maji wala vumbi
Kwa maana hivyo hutokuwa na wasi ukiwa unaitumia kwenye mvua kubwa
Simu inakuja na laini moja huku laini ya pili ikiwa ni eSIM
Ni mitandao miwili hapa Tanzania inayosapoti eSIM ambayo ni Vodacom na Airtel
Ubora wa kamera
Upande wa kamera Google Pixel 8 Pro inaziacha simu nyingi nyuma kwa ubora
Kwa kifupi ni kwamba simu ina jumla ya kamera zipatazo tatu
Huku kamera kubwa ikiwa na megapixel 50
Hata hivyo ukubwa wa megapixel sio kielelezo pekee cha ubora wa simu upande wa kamera
Pitia hapa kujua, vitu vinavyoifanya simu kuwa na kamera nzuri kwa kutazama iPhone 15 Pro
Uzuri ni kuwa kamera zake mbili zinatumia ulengaji wa dual pixel pdaf na kamera kuu inatumia multi-direction ambazo hutambua kitu kinachopaswa kupigwa picha kwa haraka
Kuhusu kamera ya google pixel 8 pro hii ni mada nyingine ya kuitazama kiundani
Ubora wa Software
Google Pixel 8 Pro inatumia toleo jipya kabisa la nadroid ambalo ni Android 14
Android 14 inakupa uwezo wa kuunda wallpaper kwa kuipa malelezo
Kwa mfano, nataka wallapaper yenye miti katikati ya miti barabara inapita
Cha kufanya hayo maelezo unayaandika kwa kusema, “tengeneza wallpaper yenye miti katikati ya miti barabara inapita”
Baada ya muda app itachakata na kukupa wallpaper unayotaka
Hii inaitwa artificial intelligence(akili bandia)
Washindani wa Google Pixel 8 Pro
Washindani wakubwa wa hii simu ni simu zote za madara ya juu
Hapa nazungumzia Samsung na iPhone
Pixel itakumbana na wakati mgumu kutoka kwa watu wanaotaka utendaji mkubwa
Hilo linatokana na bei yake kutendana na simu za madaraja ya juu na zenye uwezo mkubwa kwenye maeneo mengi sio kamera tu.
Neno la Mwisho
Google ubora wao mkubwa upo sana kwenye software
Kwa wapenda kamera nzuri hii ni bonge la simu kuwa nayo
Kwa wanaopenda kuona mapinduzi ya matumizi ya akili bandia(artificial intelligence) basi hii simu itakuonyesha mambo makubwa ya AI
Maoni 3 kuhusu “Bei ya Google Pixel 8 Pro na Sifa zake Muhimu”
Kati google na s23 ipi kali kiutendaji
Samsung s23 ni nzuri zaidi
Mwenye picha ya sm smsng s23 plz naomba nione