Kama unataka Tecno macho matatu basi ni simu ya Tecno Camon 17 ya mwaka 2021
Uzuri ni kuwa bei ya Tecno Camon 17 kwa Tanzania haizidi shilingi laki nne kwa maeneo mengi.
Ila bei yake inaonekana kuwa juu kiasi linapokuja ubora na uwezo wa simu kiutendaji.
Hivyo baada ya kufahamu bei yake itakulazimu kupitia sifa moja baada ya nyingine ya Camon 17
Muongozo uliopo hapa utakujulisha ubora na udhaifu wa Camon 17 baada ya kuona sifa zake zote
Bei ya Tecno Camon 17 Tanzania
Kwenye maduka ya simu kariakoo bei ya Tecno Camon 17 ya 128GB na Ram ya 4GB ni shilingi 400,000/=
Maduka mngine wanaiuza simu kwa bei ya shilingi 440,000/=
Hii ni bei inayovumilika japo kwa mtu anaependa simu yenye uwezo mkubwa ataona bei kuwa ni kubwa
Hivyo itamlazimu kuangalia machaguo mbadala utakayoyaona baadae kwenye makala hii.
Kwa kuzingatia sifa zake laki nne ni bei kubwa kidogo
Sifa za Tecno Camon 17
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | 128GB na RAM 6GB,4GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 440,000/= |
Upi ubora wa Tecno Camon 17
Ubora wa tecno camon 17 upo kwenye utendaji, kioo na memori kubwa
Pia uwezo wake wa kupokea toleo jipya la android 12.
Ni nadra kukuta simu ya tecno ikipata android mpya
Kioo cha hii simu ni chepesi wakati wa kutachi
Na uwezo wake wa kukaa na chaji masaa mengi ni mkubwa.
Ufanisi wa sehemu zingine unatofautiana kiuwezo, fuatilia zaidi uwezo,ubora wa nyanja zote za hii simu
Uwezo wa Network
Simu ya Tecno Camon 17 ni simu ya 4G aina ya LTE Cat 7
LTE Cat 7 inaweza kudownload faili kwa spidi inayofikia 300Mbps
Ni spidi inayoweza kudownload faili kwa sekunde chache kama mtandao wa simu unatoa spidi hiyo
4G yake ina masafa yote yanayotumika na mitandao ya simu ya Tanzania
Ni simu ambayo haina 5G ila kwa Tanzania hakuna laini ya simu inayotumia 5G kwa sasa
Ubora wa kioo cha Tecno Camon 17
Kioo cha tecno camon 17 ni cha ips lcd chenye refresh rate ya 90Hz
Refresh rate ya 90Hz inakifanya kiookuwa kilaini unapoperuzi vitu kama orodha ya meseji
Ila ubora wa kioo chake umepunguzwa na resolution ndogo ya 720 x 1600 pixels
Na pia ips lcd huonesha rangi chache tofauti na kioo cha samsung galaxy s9 aina ya amoled
Uangavu wake wa kioo una nits 450.
Huu uangavu unaweza usioneshe vitu vizuri simu ikiwa kwenye jua kali sana
Nguvu ya processor MediaTek Helio G85
Tecno camon 17 inatumia chipset ya Helio G85 katika kufanya kazi zake.
Helio G85 inafanana na processor ya Helio G75 ambayo imetumika kwenye Infinix Hot 11
Ni chip aina ya octa core kwa maana ina core nane
Ina uwezo wa wastani kiutendaji
Geekbench inaipa alama 358
Processor hii inajitahidi kucheza gemu nyingi kutokana na aina na uwezo wa core kubwa.
Uwezo wa core kubwa
Helio G85 ina jumla ya core kubwa mbili zenye spidi inayofikia 2.0GHz
Core zake zimeundwa kwa muundo wa Cortex A75
Cortex A75 ina utendaji wa kufanya kazi karibu bilioni 6 kwa wakati mmoja
Ila ni muundo wenye uwezo wa kati
Uwezo wa core ndogo
Core ndogo zipo sita aina ya cortex a55 kwenye Mediatek helio g85 zenye spidi inayofikia 1.8 GHz
Tecno Camon 17 inatumia cortex a55 kwa ajili ya kazi ndogo kama kutuma meseji au kupiga simu.
Muundo huu unaifanya simu kukaa na chaji masaa ya kutosha
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya Tecno Camon 17 inapeka umeme wa kima cha kati wa kisi cha wati 18
Chaji yake ina uwezo wa kujaza betri kwa masaa yanayozidi matatu.
Hii inatokana na beti ya camon 17 kuwa na ukubwa wa 5000mAh aina ya Li-Po.
Ukubwa huu unaipa simu uwezo wa kukaa na chaji masaa zaidi ya 14 simu ikiwa inatumia intaneti muda wote
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo mawili ya Tecno Camon 17 yanatofautiana ukubwa wa memori kwenye RAM
Kuna camon 17 ya GB 128 na ram ya gb4 na nyingine ina ram ya gb 6
Haijaainishwa na Tecno aina ya memori iliyotumika
Kwani processor ya MediaTek Helio G85 inakubali memori ya eMMC 5.1 na UFS 2.1
Uimara wa bodi ya Tecno Camon 17
Moja ya sehemu inayofanya bei ya tecno camon 17 kuwa kubwa ni aina ya bodi ya simu
Simu imeundwa kwa bodi ya plastiki ambazo si imara sana hasa inapoanguka kimo kirefu cha mita mbili
Na pia haina viwango vyovyote vya IP .
Viwango IP(Ingression Protection) vinaonyesha uwezo wa simu kuzuia maji na vumbi
Urefu wa simu ni inchi 6.6 hivyo ni simu ndefu
Ubora wa kamera
Camon 17 ina kamera tatu.
Ni kamera moja angalau yenye ubora stahiki kutoa picha nzuri.
Hiyo ni kamera kuu yenye resolution ya 48MP
Lakini imetumia autofocus aina ya PDAF inayozidiwa ubora na dual pixel pdaf
Kamera ya tatu ni aina ya QVGA.
QVGA ni aina ya kamera za kizamani ambazo zina resolution ndogo kwa viwango vya kisasa
Kamera zake zinaweza kurekodi video za aina moja tu za full hd kwa spidi ya 30fps
jifunze, jinsi ya kuchagua kamera nzuri za simu
Ubora wa Software
Ukinunua camon 17 kwa mara ya kwanza utapata android 11
Lakini hii ni simu ya tecno inayoweza kupokea toleo jipya la android 12
Kitu kinachoifanya simu kuendelea kuwa mpya
HiOS 7.6 ya Tecno inaweza kukuonyesha hali ya hewa ya eneo ulilopo kwa wakati uliopo
Pia HiOS 7.6 ina app ya kuhariri video na kuzieguza jinsi unavyotaka zitokee
Yapi Madhaifu ya Tecno Camon 17
Kamera ya Tecno Camon 17 haina OIS ambayo hutumika kutuliza video wakati wa kurekodi
Bei ya simu haiendani na uwezo wa processor kiutendaji.
Kwani utendaji wake ni wa kiwango cha kati
Simu haina viwango vinavyoonyesha uwezo wa kuzuia maji tiririka.
Baadhi ya simu za laki nne zinatumia kioo cha amoled tofauti na camon 17 yenye ips lcd
Simu haina kamera ya ultrawide kwa ajili ya kuchukua eneo pana
Neno la Mwisho
Bei ya Tecno Camon 17 inaweza kununua simu aina ya Xiaomi Redmi Note 10T 5G
Wakati simu ya Xiaomi Redmi Note 10T 5G ina processor yenye nguvu na inakubali mtandao wa 5G
Na redmi note 10t 5g inalindwa ni kioo kigumu kuchubuka cha gorilla 3
Kwa nyakati za sasa bei ya tecno 17 inafaa kuuzwa kwa bei ya laki tatu na nusu
Maoni 4 kuhusu “Bei ya Simu ya Tecno Camon 17 na Sifa Zake Kiundani (2022)”
kama simu ukiirestore inamadhara gan
simu ya smartphone ukii restoro madhara yake n nn?
Madhara yake ni kupoteza data
CAMON BADOIPO CHINI