SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu 10 za Samsung za Bei Rahisi 2022 (Ubora na Mapungufu)

Bei Nafuu

Sihaba Mikole

April 23, 2022

Hii ni orodha ya simu kumi za samsung za bei rahisi kwa mwaka 2022.

Orodha hii inahusisha samsung za daraja la kwanza, la kati na daraja mwisho.

Utaona simu aina ya samsung zilizotoka kati ya mwaka 2015-2022

Bei zake zinavumulika kwa watu wenye bajeti ndogo

Samsung Galaxy M12

Simu ya samsung galaxy m12 ni simu iliyotoka mwaka 2021

Simu ina kimo kirefu kiasi cha inchi 6.5

Utendaji wake ni mdogo kwa sababu inatumia processor ya daraja la chini ya Exynos 850

Katika kuimarisha utendaji mzuri samsung wameiwekea simu mfumo wa One UI 3.1 Core

Simu ina betri la ukubwa wa 5000mAh ambalo linaweza kukaa na chaji kwa masaa 14 simu ikiwa kwenye intaneti

M12 ni samsung ya macho manne zenye kamera za ubora wa wastani

Kioo cha samsung m12 na pls lcd chenye refresh rate ya 90Hz inayofanya simu kuwa nyepesi wakati wa kutachi

Bei ya samsung m12 Tanzania

Bei ya samsung m12 kwa masoko ya dunia inafika shilingi 320,000/=

Kwa mtanzania anayenunua simu hii maduka ya kariakoo anaweza kuipata kwa zaidi ya shilingi 350,000/=

Samsung Galaxy A02S

Simu ya samsung galaxy a02s ilitoka mwanzoni mwa mwaka 2021.

Ni simu yenye kioo cha aina ya IPS LCD ambacho kina resolution ndogo

Ni simu ya 4G yenye network bands zipatazo 10 zinazokubalika na mitandao yote ya simu Tanzania

Utendaji wake wa processor kwenye kucheza gemu ni mdogo kutokana na kutumia chip ya Snapdragon 450 yenye nguvu ndogo

Ina betri kubwa yenye 5000mAh

Hivyo hii ni simu inayotunza chaji muda mrefu ila chaji yake haijazi betri kwa haraka

Kwani ina spidi ndogo ya 15W

Bei ya Samsung Galaxy A02S

Bei ya samsung galaxy inafika shilingi 320,000/= kwenye masoko ya nchi nyingi.

Kwa Tanzania kuna mtindo wa kuuza simu za samsung kwa bei ya juu.

Hivyo tarajia kuipata simu kwa zaidi ya 350,000/= japo ina ubora mdogo

Samsung Galaxy S10 Plus

Simu ya samsung galaxy s10 plus ni simu ya daraja la juu ya mwaka 2019

Galaxy S10 Plus utakayoipata kwa sasa itakuwa ni used(imetumika)

Kioo cha samsung galaxy s10 plus ni aina ya amoled chenye resolution kubwa 1440 x 3040 pixels

Ni simu ngumu isiyopitisha maji hata kama ikizamishwa kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa nusu saa

Kioo chake ni kigumu kwani kimewekewa gorilla glass 6

Utendaji wake una nguvu kuanzia network mpaka uchezaji wa magemu yanatumia graphics kubwa

Hii inasababishwa na simu kutumia chip ya Snapdragon 855

Simu ina android 9 lakini inaweza kupokea toleo jipya kabisa la android 12

Bei ya Samsung Galaxy S10 Plus

Kwa sasa bei ya sasmung galaxy s10 plus ni shiling 615,330/= kwenye mtandao wa amazon

Lakini kwa Tanzania hasa maduka ya simu ya Dar Es Salaam Galaxy S10 Plus bei yake ni 730,000/=

Bado ni bei nzuri ukichukulia ubora wa simu yenyewe

Samsung Galaxy A22 5G

Samsung Galaxy A22 5G ni simu ya 5G iliyoingia sokioni mwaka 2021

Ni ya 4G pia yenye network bands zipatazo 11

Kioo cha samsung galaxy a22 5g ni cha ubora wa chini aina ya TFT LCD ambacho kina refresh rate ya 90Hz

Ila kioo kina resolution kubwa ya 1080 x 2400 pixels

Simu ina utendaji mzuri unaoweza kusukuma app nyingi za kila aina.

Utendaji wa kuridhisha unachangiwa na processor ya MediaTeK Dimensity 1200

Simu ina betri ya ukubwa wa 5000mAh inayokaa na chaji masaa mengi kutokana na utendaji wa simu wa wastani

Na chaji inapeleka umeme wa wati 15 ambao utajaza betri muda mrefu

Bei ya Samsung A22 5G Tanzania

Bei ya samsung galaxy a22 5g kwa masoko ya duniani ni shilingi 485,298.00/=

Kwa Tanzania, hasa dar es salaam bei inaweza kuwa kubwa zaidi ya laki tano

Samsung Galaxy A03S

Simu ya samsung galaxy a03s ni smartphone ambayo imetoka mwaka 2021 yenye viwango vya kutumika hata mwaka 2022

Hii ni simu ya 4G aina ya LTE Cat 7 yenye spidi kubwa ya kudownload.

Spidi yake inaweza kufika kiwango cha juu cha kudownload cha 300Mbps (inategemea na nguvu ya mtandao)

Utendaji wa simu ni mdogo kwa sababu inatumia processor yenye nguvu ndogo

Processor hiyo ni MediaTek Helio P35

Kioo cha samsung galaxy ni cha ips lcd chenye resolution ndogo(720 x 1600 pixels) kwa nyakati za sasa

Kamera kubwa ina resolution ya 13MP na kamera zingine zina 2MP

Japokuwa samsung galaxy a03s ni simu ya macho matatu ila haina kamera nzuri

Simu inakaa na chaji muda mrefu kwani betri lake lina 5000mAh

Bei ya samsung Galaxy a03s Tanzania

Bei ya samsung galaxy a03s ya GB 64 ni shilingi 362,232/= za Tanzania kwa masoko ya ebay

Kwa maduka ya simu ya Dar Es Salaam na Mwanza simu inauzwa kwa wastani wa shilingi 380,000/=

Kama utaona bei ni kubwa inabidi uinunue simu kwenye mtandao wa ebay.

Samsung Galaxy S9

Simu ya galaxy s9 ni simu iliyo na ubora wa hali ya juu kwenye sehemu nyingi za simu

Japokuwa ni simu ya mwaka 2018, inazizidi simu nyingi za android mpya

Simu ina processor yenye nguvu inayofanya galaxy s9 kufungua app yoyote kiurahisi

Chip yake ni aina ya Snapdragon 845 au Exynos 9810

Ina kioo kizuri upande wa rangi na angavu.

Kwani kioo cha samsung galaxy s9 ni cha super amoled chenye HDR10

Kasoro kubwa ya galaxy s9 ni kukaa na chaji masaa machache hasa ukitumia intaneti muda mrefu

Hii inasababishwa na simu kutumia betri dogo la 3000mAh

Bei ya samsung galaxy s9

Bei ya samsung galaxy s9 ya GB 64 inafika shilingi 390,000/= kwa maduka ya simu ya kariakoo

Kumbuka simu za galaxy s9 nyingi ni used hakuna mpya

Bei inaongezeka na kuwa kadri ukubwa wa memori unavyoongezeka.

Samsung Galaxy A22

Simu ya samsung galaxy a22 ni simu iliyotoka katikati ya mwaka 2021.

Ni simu nzuri upande wa kamera kwa sababu ina OIS(Optical Image Stabilization)

Hii ni samsung ya macho manne yenye kamera inayopiga picha kwa upana mkubwa wa nyuzi 123

Utendaji wa simu ni wa wastani kwa sababu ina chip ya Helio G80 na memori aina ya eMMC 5.1

Kioo cha samsung a22 ni cha aina ya Super AMOLED chenye resolution ndogo ya 720 x 1600 pixels

Galaxy a22 inakaa na chaji masaa mengi hata ukiwa unatumia intaneti

Kwani betri lake lina ukubwa wa 5000mAh

Bei ya Samsung Galaxy A22 Tanzania

Bei ya samsung galaxy kwenye maduka ya simu ya dar es salaam inaanzia shilingi 500,000/=

Hii ni ya galaxy a22 ya GB 64

Hata ukinunua mtandaoni bei yake inaendana na hapa Tanzania

Samsung Galaxy A10

Samsung galaxy a10 ni simu ya mwaka 2019 yenye android 9

Na inaweza kupokea toleo la andriod 10 japo kwa sasa kuna toleo la android 12

Ubora wa galaxy a10 upo kwenye sehemu chache sana.

Kwa kiasi kikubwa sio simu nzuri hivyo bei yake inakuwa ndogo zaidi

Bei ya Samsung Galaxy A10

Bei ya samsung galaxy a10 mpya kabisa ya gb 32 ni shili ngi 284,417.14/=

Ila ukipata simu used ya galaxy a10 bei yake inakuwa ni shilingi 150,000/=

Samsung Galaxy A13

Simu mpya ya samsung galaxy a13 imetoka mwanzoni mwa mwezi machi 2022

Ni simu yenye mfumo endeshi mpya wa Android 12

Utendaji wake ni wa chini kwa sababu ina chip yenye nguvu ndogo aina ya Exynos 850

Ila ni simu imara na ngumu kupasuka kwa sababu ina vioo vya gorilla 5

Uwezo wa kukaa na chaji ni wa juu.

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh

Ni simu ya macho manne inayoweza kupiga eneo pana sana kwa nyuzi 123

Bei ya Samsung Galaxy A13

Bei ya samsung galaxy a13 ya gb 32 inafika shilingi 400,000/=

Kwa kuzingatia ubora wa simu, bei yake ni kubwa

Kwani bei hii inaweza kununua simu ya Redmi Note 10 5G yenye ubora mkubwa zaidi ya galaxy a13

Samsung Galaxy A10S

Simu ya samsung galaxy a10s ni toleo la mwaka 2019

Pamoja na umri mkubwa wa simu ila bado inafaa kwa nyakati hizi

Kwa sababu inakubali kupokea toleo la android 11

Simu nyingi mpya hasa za daraja la chini zinakuja na android 11

Lakini kwenye upande wa kamera na processor simu ina uwezo mdogo

Hata betri yake si kubwa sana kwani lina 4000mAh

Bei ya samsung galaxy a10s

Bei ya samsung galaxy a10s mpya ya GB 32 inafika shilingi 332,046/=

Maoni 4 kuhusu “Simu 10 za Samsung za Bei Rahisi 2022 (Ubora na Mapungufu)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A35 na Sifa zake

Samsung Galaxy A35 ni toleo jipya la samsung lilotoka mwezi machi 2024 Ni simu ya daraja la kati iliyochota baadhi ya sifa muhimu kutoka kwenye galaxy yenye bei kubwa Ndio […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

samsung s24 plus thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy S24+ na Sifa Zake

Kisifa Samsung Galaxy S24 Plus ina sifa nyingi zinazoendana kwa kiasi kikubwa na Samsung Galaxy S24 Ultra Kwa maana Galaxy S24+ ubora wake unazipita simu nyingi na mkubwa, hivyo bei […]

samsung s24 ultra thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy S24 Ultra na Sifa zake

Hivi karibuni simu mpya ya Samsung Galaxy S23 Ultra imeingia sokoni huku bei yake ikiwa haitofautiani sana na Apple iPhone 15 Pro Max Kwenye soko la dunia bei ya samsung […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram