Simu ya samsung galaxy s22 ni simu mpya ya daraja la juu ambayo imetoka mwaka 2022
Kitu ambacho kinafanya bei ya samsung galaxy s22 kuzidi milioni hapa Tanzania na duniani kiujumla
Kikubwa utakachokijua kwenye hii post ambacho kinasababisha simu kuwa na bei kubwa ni ubora wake wa processor.
Si processor pekee bali ubora wa galaxy s22 upo kwenye sifa karibu zote.
Hivyo ukielewa sifa muhimu za galaxy s22 ndio utafahamu kiundani sababu ya bei yake kubwa.
Bei ya Samsung Galaxy S22 Tanzania
Bei halisi ya samsung galaxy s22 kwenye soko la dunia(amazon) ni shilingi 1,627,500.00/=
Lakini maduka mengi ya simu dar es salaam wanauiza samsung s22 kwa shilingi 2,200,000/=
Swali lakujiuliza,
Bei yake ya zaidi milioni inaendana na ubora wake?
Kwa kutazama sifa za galaxy s22 upande wa kioo, bodi, kamera, chipset, network na mengine bei yake inaakisi ubora
Fuatalia sifa na maelezo yake kwenye hii post uweze kujua ubora wa galaxy s22 upo wapi hasa
Sifa za samasunga galaxy s22
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Dynamic AMOLED 2X, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 256GB, 128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera tatu (samsung macho matatu)
|
Muundo | Urefu-6.1inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,200,000/= |
Upi ubora wa simu aina ya Samsung Galaxy S22
Simu ya samsung galaxy s22 ina ubora mkubwa hasa kwenye utendaji wa processor
Simu ina kioo kinachoonyesha vitu kwa uhalisia kwa kiasi kikubwa
Chaji yake ni fast chaji inayojaza betri kwa dakika chache
Ni samsung macho matatu inayotoa picha nzuri hata kwenye mwanga hafifu
Ni simu yenye network ya 5G
Mfumo wake wa memori una kasi kubwa ya kusafirisha data nyingi kwa wakati mmoja
Ina GPU nzuri inayoweza kucheza gemu kwa ubora wa juu kwa urahisi
Uwezo wa Network
Samsung S22 ni simu ya 5G na inasapoti mtandao wa 4G pia
Aina ya LTE inayotumia ni LTE Cat 20
Spidi ya juu kabisa ya kudownload ya Cat 20 ni 3000Mbps
Ni spidi inayokaribia 5G
Network ya 4G ya galaxy s22 ina masafa yapatayo 22 yakiwemo yanayotumiwa na mitandao ya simu nchini Tanzania
5G yake pia ina masafa mengi
Kufahamu masafa ya mitandao ya simu ya 4G pitia, jinsi ya kujua ubora wa simu yoyote
Ubora wa kioo cha samsung galaxy s22
Samsung galaxy s22 inatumia kioo aina ya dynamic amoled
Dynamic amoled ni tofauti na super amoled.
Dynamic ina ongezeko la rangi na uangavu wake ni mkubwa zaidi
Hivyo mwanga wa kioo ukiwa mdogo screen inaonyesha vitu ukilinganisha na super amoled
Tazama video hii inayoonyesha utofauti wa super amoled na dynamic amoled
Ubora wa kioo cha samsung unachagizwa na uwepo wa HDR10+ na refresh rate kubwa ya 120Hz
HDR10+ inarekebisha muonekano wa picha au video kuendana na jinsi kitu kinavyoonekana kwenye mazingira yake halisi
Refresh ya 120Hz inaifanya simu kuwa nyepesi wakati wa kucheza gemu za simu
Na kikubwa, uangavu wa kioo unafika nits 1300
Hivyo hautopata tabu pindi simu inapotumika kwenye jua kali
Nguvu ya processor Exynos 2200
Kuna matoleo mawili ya samsung mpya ya galaxy s22 upande wa processor.
Samsung za marekani zinatunia chip ya snapdragon 8 gen 1
Wakati za nchi zingine zinatumia Exynos 2200
Makala hii inaangazia uwezo wa chip ya Exynos 2200
Exynos 2200 ni chip yenye nguvu ambayo inashika nafasi ya tatu kwa sasa
Kwenye geekbench ina alama zaidi ya 1100
Ni alama nyingi ukifananisha na chip iliyotumika kwenye simu ya Tecno Camon 18 Premier
Nguvu kubwa ya exynoss 2200 inachangiwa na muundo mpya wa core kubwa na core ndogo
Ni miundo inayoipa processor uwezo wa juu
Uwezo wa core kubwa
Exynos 2200 ina jumla ya core nne zenye nguvu ambazo zimegawanyika mara mbili.
Kuna core moja yenye nguvu sana ambayo inatumia muudo wa Cortex X2
Spidi ya core hii inafika 3.00 GHz kwa maana chip inaweza kufanya maelekezo kwa mizunguko bilioni tatu kwa sekunde
Kila mzunguko mmoja unaweza kufanya kazi 10 kwa wakati mmoja
Hii core ina ulaji mkubwa wa chaji lakini ufanisi ni mkubwa
Core tatu kubwa zingine zina spidi ya 2.4 GHz na zinatumia pia Cortex X2
Uwezo wa core ndogo
Chip ina jumla ya core zenye nguvu ndogo zipatazo nne
Core ndogo zinatumia muundo wa Cortex A710
Hizi core huwa na mizunguko michache ipatayo bilioni moja na laki saba kwa sekunde
Cortex A710 inatumia umeme mdogo na nguvu yake ni kubwa kuliko Cortex A55 ambayo imetumika kwenye simu nyingi za android ikiwemo Redmi note 11 pro plus 5g
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya samsung galaxy s22 ina ukubwa wa 3700 mAh
Ukubwa wa betri ni wa wastani unaoifanya simu kukaa na chaji masaa 87 kama ikiwa haitumiki mara kwa mara
GSMArena wanadai galaxy s22 inakaa na chaji masaa 11 simu ikiwa kwenye intaneti muda wote
Chaji inajaza betri kwa 100% kwa dakika zipatazo 63
Hivyo simu inachukuwa muda mchache sana kujaa
Spidi kubwa ya kuchaji inasababishwa na umeme wa wati 25 ambao chaji inaweza kupeleka kwenye betri
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo ya aina mbili ya galaxy s22 upande wa memori
Kuna galaxy ya ukubwa wa 128GB na nyingine ina ukubwa wa 256GB
Zote zina RAM yenye ukubwa wa RAM 8GB
Aina ya memori ambazo samsung imetumia ni UFS 3.1
UFS 3.1 huwa ina kasi kubwa sana kusafirisha data
Hivyo inafanya simu kuwaka na kufungua app kwa haraka
Na memori yenye kasi inaongeza utendaji mkubwa wa simu
Uimara wa bodi ya samsung galaxy s22
Samsung galaxy s22 ina bodi ngumu kuvunjika
Uimara wake unasababishwa na simu kutumia vioo vya gorilla glass victus+ upande wa nyuma na kwenye display
Na upande wa pembeni simu imewekewa fremu za aluminiamu
Vioo vya gorilla glass victus+ vinaipa simu uwezo kutokupasuka kama ikianguka kwa kimo cha mita mbili toka juu
Na pia ni vioo ambavyo ni vigumu kuchunika
Kiufupi tu, hutohitaji kuweka kava wala screen protector kutokana na ugumu wa kioo
Ubora wa kamera
Samsung galaxy s22 ina kamera tatu ambapo kamera kubwa ina resolution ya 50MP
Kwa picha nyingi ambazo nimeziona, kamera ya samsung inatoa picha nzuri iwe usiku ama iwe mchana
Hii inasababishwa na simu kutumia autofocus nzuri aina ya dual pixel pdaf
Nyakati za mchana kamera ina balansi rangi vizuri na kwa usahihi hivyo tone ni ya kuridhisha
Nyakati za usiku kuna noise ya kiasi kidogo sana
Zitazame picha zilizopigwa na galaxy s22 hapa, ubora wa picha za kamera ya galaxy s22
Pia jifunze; jinsi ya kujua simu yenye camera nzuri
Ubora wa Software
Galaxy S22 inakuja na mfumo endeshi wa android 12
Android 12 ina ongezeko wa vitu kama uwezo kuonyesha app zinazotumia mic na kamera
Hivyo inakupa fursa ya kufahamu app ambazo zinakutrack
Lakini pia android ina kitu kinaitwa Corol Extraction
Yaani muonekano wa rangi wa vitu vingine unakopi rangi ya wallpaper unayoitumia kwenye simu
Yapi Madhaifu ya samsung galaxy s22
Udhaifu mkubwa wa galaxy s22 ni uwezo wake wa kukaa na chaji masaa machache
Samsung s22 inazidiwa na simu ya iphone 13 pro max kwenye upande wa ukaaji na chaji
Hilo linachangiwa na simu kuwa na betri dogo sana
Neno la Mwisho
Matoleo mapya ya samsung galaxy s-series kwa mwaka 2022 ni matoleo yanayohusisha simu bora
Kwa mwenye bajeti kubwa na ya kutosheleza anaweza akamiliki hii simu na kufurahia ubora wake
Ila kama bajeti ni ndogo unaweza kutazama machaguo mengine kama realme, vivo,oppo na sony
Maoni 2 kuhusu “Bei ya Simu ya Samsung Galaxy S22 na Sifa Muhimu”
Hizi cm Zina copy zake kwani maana ninayo hapa Ina GB250 lakin inajaa vitu hata havina GB 5 inaandika imejaa pia camera haitoi vizuri na kingine fringprint yake inatolewa na mtu yeyote hatakama hajaweka
Hiyo bila Shaka ni feki ndugu yangu