Tecno Spark 50 Pro imekuja na vitu viwili vya kipekee
Na ndicho kinachotengeneza utofauti na toleo la tecno spark 40 pro
Ila kwa jicho la haraka unaweza kudhani sifa za spark 50 na spark 40 hazina tofauti ila utofauti upo hayo maeneo mawili
Kwanza tulinganishe bei na sifa zake
Bei ya Tecno Spark 50 Pro GB 256
Bei ya Tecno Spark 50 Pro ni shilingi laki tano (500,000)
Upande wa memori kuna toleo la aina moja tu lenye GB 256 na RAM ya GB 8
Hii inakupa nafasi kubwa na kutumia app nyingi kwa wakati mmoja sababu ya kuwa na RAM kubwa
Sasa jambo la muhimu ni sifa zake
Hizi zitakuonyesha utofauti wa toleo la sasa na lilopita
Sifa za Tecno Spark 50 Pro
| Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
|---|---|
| Network | 2g, 3g, 4g |
| Processor(SoC) |
|
| Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
| Softawre |
|
| Memori | 256GB na RAM 8GB |
| Kamera | Kamera moja
|
| Muundo | Urefu-6.78inchi |
| Chaji na Betri |
|
| Bei ya simu(TSH) | 500,000/= |
Kwa haraka kuna utofauti mdogo kati ya Infinix Hot 70 Pro na Tecno Spark 50 Pro
Uwezo wa network
Tecno Spark 50 Pro inasapoti mpaka mtandao wa 4G
Simu inatumia laini za kawaida na haiji na sapoti ya laini za eSIM
Baadhi ya simu siku hizi zimeacha kuweka FM Radio
Ila hii inayo na pia inasapoti NFC
Inayosaidia kufanya malipo bila kadi ya benki
Lakini matumizi ya NFC kwa Tanzania sio makubwa
Ubora wa kioo
Ubora wa kioo ni wa kawaida kiujumla
Maana imewekewa kioo chenye resolution ya 720p
Kwa bahati mbaya tecno spark 50 pro ni simu ndefu
Hivyo udogo wa resolution unapunguzwa na ukubwa wa kioo ambacho 6.78 inchi
Hii ni njia mojawapo kampuni zinapunguza gharama ili simu iwe nafuu kwa walengwa
Hata ina refresh rate inayofika 120Hz
Inayofanya kioo kuwa na mwatikio mkubwa unapotachi
Nguvu ya Utendaji
Kwa aina ya prosesa ya Tecno Spark 50 Pro utendaji wake ni wa kawaida
Ila inaweza kufanya vitu vingi ikizingatiwa RAM yake ni kubwa (GB 8)
Kwa aina ya walengwa hii simu inatosha
Lakini kama unamatumizi makubwa sana inaweza ikakuletea changamoto
Hata hivyo kwa aina ya matumizi ya watu wengi wanaweza wasione utofauti wowote
Uimara wa bodi
Kitu cha kufurahisha simu imewekewa waterproof
Kwa maana ina cheti cha IP64
Hiki cheti kinaashiria simu inaweza kuzuia maji iwapo imezama kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa nusu saa
Pia ina uimara wa kuhimili kupasuka ikianguka katika kimo cha mita 1.5
Mita 1.5 ni sawa na urefu wa kiuno cha mtu kutoka chini
Hii inaishiria ikianguka kwenye kimo kikubwa zaidi inaweza kuharibika
Hivyo umuhimu unahitajika
Ubora wa kamera
Simu ina kamera moja ya ukubwa wa megapixel 50
Ubora wa picha ni mzuri hasa katika mazingira ya mwanga mwingi
Hii kamera inarekodi mpaka video za full hd+
Bado uangavu ni mzuri na wa kuonyesha vitu kwa ustadi
Kiijumla kamera inatosheleza japokuwa simu haina kamera za ultrawide na telephoto
Hizi hufanya simu kuweza kupiga eneo pana zaidi na pia kitu ambacho kipo mbali na kamera
Uwezo chaji na betri
Tecno Spark 50 Pro ina bonge la betri
Ukubwa wake ni 6000mAh, kimakidilio ukaaji na wa chaji unafika masaa 14 ukiperuzi intaneti muda wote
Betri ili ijae haraka inahitaji fast chaji
Na hii simu ina chaji ya wati 60, ndani ya dakika 70 betri inajaa kutoka 0 hadi 100
Hii simu haitohitaji kuichaji mara kwa mara hivyo inaepusha betri kuharibika mara kwa mara
Ubora wa software
Tecno Spark 50 Pro inatumia mfumo wa Android 16
Ambapo ndani inaendeshwa na mfumo wa HIOS 16
HIOS 16 imeiwekea hii simu mifumo mingi ya AI
Kwa maana inajumuisha chatgpt, deepseek, gemini, nk
Kwa hiyo unaweza kuchagua unaoupenda
Washindani
Bei ya Tecno Spark 50 Pro inaenda kwenye ukanda wenye simu nyingi kali zaidi
Kwa maana bei hii inaweza kukupa simu kama Redmi Note 14 Pro
Lakini pia Samsung Galaxy A26
Na bila kusahau simu ya Infinix Hot 70 Pro
Kiuhalisia hapa pana machaguo mengi ya kwenda nayo
Neno la mwisho
Kwa sehemu Tecno Spark 50 Pro inafanana na toleo la mwaka jana
Ila tofauti mbili upande wa chaji na uimara wa bodi umeongeza kitu kikubwa