Moja ya changamoto ya ununuaji wa simu nzuri ni kukumbana na wauzaji wasio waaminifu.
Hawa wauzaji wapo wengi maeneo maarufu ya uuzaji simu nchini hasa Dar Es Salaam na ikiwemo mtandaoni
Mara nyingi utakutana na tangazo simu used toka dubai au UK nk
Wanunuaji wa simu za Samsung aina ya S-series mfano wa Samsung Galaxy S20, Samsung Galaxy S23 huathirika zaidi
Hivyo huna budi kujua jinsi ya kuzitambua simu feki za Samsung iwapo unataka kununua samsung za bei ya juu
Zipo njia nyingi lakini hizi ziliowekwa hapa ni baadhi.
Kuangalia Mfumo Endeshi wa One UI
Samsung tangu 2019 zinatumia mfumo endeshi wa One UI ambao una apps za samsung
Hivyo hatua ya kwanza ni kujua kama mfumo endeshi wa hiyo simu ina One UI
Unapaswa kujua taarifa za simu kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo tovuti rasmi ya Samsung
Haihukikishii kuwa simu ni orijino ila ni hatua ya mwanzo kabisa ya kuifuata
Kwa sababu mfumo endeshi wa Samsung wenye android 11 unaweza kuwekwa kwenye simu zingine
Ili kujua toleo la One UI, ingia Settings ->About Phone -> Software Information
Kwenye orodha utaona namba ya toleo kwenye kipengele cha kwanza
Baada ya hapo india kwenye tovuti ya Samsung au GSMArena au SimuNzuri usome sifa za simu
Kisha linganisha kama zinaendana
Kutazama aina ya Processor ya Simu
Mbinu ya pili ni kuweka applikesheni ya CPU Z kwenye simu ya samsung unayotaka kununua
App ya CPU Z inaweza kusoma taarifa zote za simu husika
Taarifa ya muhimu unayoihitaji kuifahamu ni processor iliyotumika
Simu nyingi za Samsung zinatumia chip ya Exynos au Qualcomm Snapdragon
Iwapo taarifa za SoC (System On Chip) zinataarifu tofauti basi jua kuwa simu inaweza kuwa ni feki
Kwa mfano Simu ya Samsung Galaxy S10 toleo la Marekani zina SoC ya Snapdragon 855 na sehemu zingine duniani zinakuja na chip ya Exynos 9820
Hivyo CPU Z inapaswa ikuonyeshe mojawapo kati ya chip hizo mbili
Lakini taarifa za app zikiwa tofauti jua kuwa samsung uliyo nayo ni feki
Hakuna muuzaji atakayekubali uweke app kabla ya kununua lakini simu zote mpya huwa zina warrant
Tumia muda wa warant kuichunguza simu
Kutazama muonekano wa utoaji mwanga wa kioo
Karibu matoleo mengi ya S-Series hutumia vioo vya Amoled
Sifa kubwa ya amoled ni kutotumia taa bali kioo hutoa mwanga wenyewe
Hivyo inafanya rangi nyeusi kuonekana kwa usahihi kabisa
Kiasi cha kwamba kama simu ukiiwasha kwenye giza hakuna mwangaza unaoweza toka kwenye kioo
Ukienda kwa muuzaji muulize aizime na kuiwasha simu kisha aiweke sehmu simu yenye giza
Kioo cha amoled rangi nyeusi huonekana giza totoro
Kutumia IMEI namba
Kirefu cha IMEI ni International Mobile Equipment Identity ambayo inawakilisha namba ya kipekee ya kifaa unacho kimiliki
Kila simu huwa ina namba yake ya utambulisho ndio ukiibiwa simu polisi wanaulizia IMEI ya simu
Ukibonyeza kwenye simu namba *#06# utaona namba yenye tarakimu 15
Inakiri hiyo IMEI namba na kisha na kisha tembelea tovuti zenye mfumo wa kucheki IMEI
Tovuti za namna hiyo zitaitambua aina ya simu na zitakuonyesha taarifa za simu hiyo
Moja ya website hiyo ni, imei checker, unaingiza hizo namba kisha bonyeza check
Kama tovuti inaleta taarifa tofauti kabisa na samsung unayotaka kununua elewa kuwa hiyo simu yaweza kuwa ni feki
Ila njia hii sio ya uhakika sana
Kwa sababu IMEI namba zinaweza kubadirishwa japokuwa TCRA inapiga marufuku mafundi kubadiri IMEI za simu
Kuizamisha simu kwenye maji
Hii ndio njia ya uhakika kabisa japo inaweza kukustajahabisha
Samsung zote za bei kubwa zilizowahi huwa hazipitishi kwenye kina cha mita moja na nusu kwa muda wa nusu saa
Na hata ukiitoa simu nje ya maji simu inaendelea kufanya kazi kama kawaida
Hii inatokana na hizo simu kuwa na viwango vya IP68 vinavyoainisha kuwa simu inaweza kuzuia maji na vumbi
Kwa samsung toleo la S-Series inaweza kustahamili hali hii pasipokuwa na shaka
Kwa hiyo unaweza itumia hii njia baada ya njia zingine zote kuonesha usahihi
Kufuatiliatilia spidi ya chaji
Kasi ya chaji kupeleka umeme mwingi hutegemea na jinsi muundo wa simu ulivyoundwa
Kwenye sifa za simu huwa kunainishwa uwezo wa simu kupitisha chaji
Kwa mfano kasi ya chaji ya Samsung Galaxy S23 Ultra inafika wati 45
Maana yake ni kuwa simu husika inapaswa isome kiwango hiko pidi chaji yenye uwezo wa wati 45 inpowekwa
Kuna app kama AccuBattery ambayo inaweza kuonesha kiwango cha chaji kinachoenda kwenye simujanja
Samsung feki lazima iwe inapeleka chaji kwa kiwango tofauti na kilichoanishwa
Hitimisho
Hizi njia zote zinakuhitaji wewe mtumiaji kuifahamu simu kabla ya kuamua kuinnunua
Ndio maana kwenye tovuti ya simunzuri ikitajwa bei pia kuna maelezo ya simu husika
Usipofuatilia simu unaweza ukajikuta unamiliki samsung feki
Maoni 7 kuhusu “Zitambue Simu Feki za Samsung Kwa Njia Rahisi”
Nimenunua S21 5G ila nyuma ya siku imeandikwa galaxy na siyo samsung ni fake au
Maandishi ya nyuma kwenye hiyo simu yanapaswa yawe Samsung
Nimenunua S21 5g ila nyuma ya simu imeandikwa Galaxy na siyo samsung ni fake au?
Kuna huo uwezekano
nimenunua s23 ultra baada ya siki haisomi mtandao Wala laini ndani vp nimepigwa?
Inawezekana, download app inaitwa CPU X utaona taarifa za simu yako
Habari wadau,Je A14 5g 128 gb inapatikana kwa bei gani madukani na Je ina utofauti gani na A15?