Hii ni orodha ya kampuni bora za simu ambazo zimefanya vizuri kimauzo toka mwezi wa kwanza mpaka wa tano 2022.
Katika orodha kuna kampuni za simu kutoka Marekani, Korea Kusini na China pia Japani
Hapa kuna takwimu za idadi ya simu janja zilizouzwa tangu mwaka uanze
Na utaelewa maneneo na aina za simu ambazo zimeongoza kuuza sana
Tuziangazie takwimu za mauzo kwa undani wake
Samsung
Samsung ni kampuni kubwa zaidi nchini korea ambayo ndio imeuza simu nying mpaka sasa
Simu za samsung zimenunuliwa kwa 28.5% kati ya simu zote duniani kote
Kampuni hii ya korea inatengeneza simu za aina tatu aina ya galaxy
Na simu zake zinazofanya vizuri ni zile zinazotumia mfumo wa Android
Zipo samsung za bei rahisi, bei ya kati na bei kubwa
Galaxy ambazo zinauza sana ni matoleo ya Samsung A-Series
Ambapo katika simu milioni 74.5 zilizouzwa na samsung, Samsung Galaxy A12 na Galaxy A32 ndio zinaongoza kwa mauzo
Hii ni tofauti na apple wanauouza sana simu za daraja la juu
Pamoja na mauzo mengi, samsung inaachwa nyuma kimapato na apple
Kwani mapato ya samsung upande wa simu ni dola bilioni 21
Zifuatalie hapa, samsung za bei rahisi zenye soko kubwa
Apple
Apple ni kampuni ambayo inashika nafasi ya pili kimauzo ya simu duniani
Kabla ya mwezi machi simu za iphones zilikuwa zinaongoza kwa kununuliwa zaidi
Kwani apple iliuza simu kwa zaidi ya 29% mpaka mwezi januari
Lakini baaada ya Samsung kuja na matoleo mengi mapya, apple ikawa inashika nafasi ya pili kwa mauzo ya 27.83%
Simu ambazo ziliifanya apple kushika usukani ni matoleo ya iPhone 13
Kumbuka kuwa apple hutengeneza simu janja za daraja juu pekee
Hizi simu hupatika kwa bei kubwa
Hivyo inaifanya iphones kuipatia mapato kampuni ya Apple Inc yanayofiki dola bilioni 97 kwa miezi minne ya mwanzo 2022
Apple inaweza kurudi nafasi ya kwanza kama watazindua smartphone mpya
Masoko makubwa ya iphones ni nchi zilizoendelea
Unaweza kutizama mlinganisho hapa kati ya samsung s22 ultra vs iphone 13 pro max
Xiaomi
Xiaomi ni kampuni ya china inayotengeneza simu za xiaomi, redmi na pocco
Hii ni kampuni inayofanya vizuri sana katika mauzo ya simu za kundi la kati
Kwa mwaka 2022, watengenezaji wa simu za redmi wanashikilia soko kwa mauzo ya 12%
Kwa kutazama, xiaomi bado ina safari ndefu kufikia nafasi za samsung na apple
Hata hivyo xiaomi wanajitahidi
Kwani kabla, huawei ilikuwa inaipita xiaomi kimauzo
Lakini tangu vikwazo vya Marekani iikumbe huawei imefanya kampuni zingine toka china kupanda juu
Kwa mwaka 2022 Xiaomi wameachia simu za gharama aina ya matoleo Xiaomi 12
Lakini soko la China linatawaliwa sana huawei na oppo huku xiaomi yenyewe ikishika nafasi ya tano
Pitia hapa kufuatalia simu za xiaomi na bei zake
Huawei
Kabla ya mwaka 2020, Huawei ilikuwa imeshaipiku Apple kimauzo
Na hivyo kushika nafasi ya pili huku ikiwa inatawala kwa kiasi kikubwa nchini China kwa mauzo yanayozidi 39%
Aliyekuwa raisi wa USA bwana Trump aliishitumu Huawei kuhusu ukusanyaji wa taarifa za watu
Basi huawei ikapitia vikwazo vya USA vilivyoizuia simu zao kutokutumia huduma za google na Android
Taratibu huawei ikaanza kuanguka mpaka kushika nafasi ya nne
Huku kampuni tanzu ya huawei ikifahamika Hornor ikiwa ndio muokozi wa Huawei kwa sasa
Kwa sasa huawei soko lake lina 6% pekee
Huku simu za hornor zikiwa zinaongoza kwa mauzo nchini China
Kumbuka huawei ni simu zinazotoa picha kali
Angalia hapa kuona picha ambazo zimepigwa na simu ya huawei
Oppo
Oppo ni kampuni ya smartphone iliyo chini ya kampuni ya BBK Electronic
Katika robo muhula wa kwanza oppo imeuza nakala za simu zipatazo milioni 30
Ambayo ni sawa na 5%
Mauzo ya oppo ni makubwa kwa sababu inatengeneza sana simu za daraja la kati na la chini
Japokuwa oppo pia huuza simu za gharama kama matoleo ya Oppo Find x
Lakini soko lake linapata shida kufikia simu za iphone na samsung
Oppo ina soko kubwa huko kwao china kuliko sehemu zingine
Na pia oppo hupatikana kwa wingi india
Vivo
Kampuni ya BBK Electronic ya China pia inaimiliki kampuni ya Vivo Communication Technology Co. Ltd.
Vivo Communication Technology ndio watengenezaji simu zote za vivo
Kwenye soko la mauzo ya simu duniani vivo ina 4%
Xiaomi inaizidi vivo kwa zaidi ya mara tatu wakati Samsung na Apple zinaizidi vivo karibu mara saba
Simu za vivo hazijaenea sana duniani
Japokuwa na wenyewe huwa wanatengeneza simu za madaraja yote
Kwa mfano Africa vivo inaachwa kimauzo na simu za infinix
Ila kiubora, smartphone nyingi za vivo ni nzuri kuliko za Infinix na tecno
Moja ya simu za vivo zinazofanya ni Vivo X70 Pro+ ambayo ina kamera kali
Realme
Simu za realme zinashika nafasi ya nane kimauzo kwa 3%
Hii inatengenezwa na kampuni toka china ambayo ipo chini ya oppo
Mauzo mengi ya realme yapo china na india
Na yenyewe haijasambaa sana duniani kama ilivyo kwa simu za redmi
Baadhi ya simu ya realme Realme 9 5G na Realme C21
Hii kampuni hutngeneza kwa asilimia kubwa simu za madaraja ya chini na ya kati
Motorola
Motorola Mobility ni kampuni ya Marekani ambayo kwa sasa ipo chini ya Lenovo
Motorola ni moja ya kampuni inayotengeneza simu nyingi
Mwaka huu tu kwa mfano imeshazindua simu karibu nne mpya
Lakini ukubwa wa motorola sio kama zamani
Kwani mauzo yao kidunia ni 2.4%
Baadhi ya simu ambazo motorola inatengeneza ni Morola Moto G62 5G
Pia motorola ni tofauti na apple
Kwani inatengeneza vile vile simu za matoleo ya daraja ya chini mpaka ya juu
LG
LG hufahamika zaidi kwenye uundaji wa tv na vitu vya majumbani kama mafriji
Lakini pia kuna smartphone nyingi tu ambazo LG wanatengeneza
Kwa bahati mbaya hii kampuni imeshindwa kuhimili usindani mkubwa
Hivyo wameamua kusitisha kutengeneza simu
Pamoja na hayo, LG inashika nafasi ya tisa na kuziacha simu za Nokia na Sony kimauzo
Kampuni hii ya korea kusini bado inashikilia soko kwa mauzo ya 1%
Moja ya LG ambazo zilifanya vizuri ni simu ya LG G8 ThinQ
Kampuni nyingine
Kampuni zingine za simu ambazo hazikutokea kwenye orodha zinauza chini ya 1%
Mfanno mzuri ni kampuni ya sony
Wakati huo kampuni zingine za simu zimejikita kwenye soko la maeneo machache
Kwa mfano infinix, tecno na itel wamejikita kwenye baadhi ya nchi za Afrika na Asia
Hivyo inakuwa na ngumu kutokea kwenye list
Maoni 14 kuhusu “Kampuni 10 Bora za Simu Kimauzo Duniani (2022)”
Nilikuwa nauliza kati ya Infinix hot 10 na oppo A57 ipi nzuri
oppo a57 ya 2022 ni kali zaidi
Nilikuwa nauliza kati ya Infinix hot 10 na oppo A57 ipi nzuri pamoja na Samsung S10 na
kiutendaji oppo a57 2022 ina nguvu kiasi ila overall samsung s10 bado ni nzuri zaidi
Tuambiwe kampuni inayotengeneza simu zenye ubora kiutendaji na siyo KATIKA mauzo.
Sawa kiongozi tunalifanyia kazi
Ninaulizia simuzuli oppo inabei ngani inayosapoti 5G
Kuna oppo reno8 rg inauzwa 1,200,000 ya gb 256
https://simunzuri.com/bei-ya-simu-oppo-reno8/
Ninaulizia beinya sm oppo inanyosapoti 5G
Galaxy note 10+ ni zaidi ya S21 plain. Ukibisha basi hujanitumia hiyo kitu
Naomba kujua Kati ya Samsung A57 na Google pixel 8 pro ipi ni nzur naomba na sifa zake kwa upande wa storage gb nakadharika na Bei pia bosss
Google pixel 8 pro ni Bora zaidi
Huawei kwa sasa naona wanarudi kwa kasi je awawezi kuipiku sumsang apple na xaomi ?
Kwa china inawezekana kwenye soko la dunia bado ni changamoto