Tuingazie simu ya daraja la chini ya Oppo A54 kutoka kwenye kampuni namba tano kimauzo duniani
Simu hii ilitoka mwaka 2021 mwanzoni kabisa
Sifa zake zinafanya bei ya Oppo A54 kuwa chini ya laki tatu na nusu (inategemea na ukubwa wa memori)
Kwenye hii posti utafahamu bei yake kama inaendana na sifa zake kwa mwaka 2022
Bei ya OPPO A54 ya GB 64
Oppo A54 ambayo RAM yake ni 4GB na memori ikiwa na ukubwa wa 64 GB inauzwa shilingi 328,084.29/=
Kwa baadhi ya maduka kariakoo bei ya simu inaweza kuwa kubwa zaidi
Lakini haipaswi kuzidi laki tatu na nusu
Bei ya hii simu ni kubwa ukifananisha na uwezo wake na sifa zake ambazo zimeorodheshwa chini
Kuna simu za Redmi na Vivo zenye bei sawa na A54 ya Oppo lakini kiubora A54 inazidiwa (utajua sababu)
Sifa za Simu ya OPPO A54
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, |
Softawre |
|
Memori | eMMC,128GB,64GB na RAM 6GB,4GB |
Kamera | Kamera tatu (macho matatu)
|
Muundo | Urefu-6.51inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 330,000/= |
Ni upi ubora wa oppo a54?
Ubora mkubwa wa oppo a54 ni kuhifadhi chaji kwa muda mrefu
Simu ina betri kubwa linalosaidia moto kukaa masaa ya kutosha
Lakini pia ina memori kubwa inayoweza kuchukua app na mafaili mengi
Lakini kwenye nyanja zingine(kama utakavoona) simu ina vitu vyenye ubora wa chini
Uwezo wa Network
Oppo hi ya 2021 ina network ya 4G aina ya LTE Cat 7
Simu inayokuwa na LTE Cat 7 inakuwa na uwezo wa kudownload faili kwa spidi inayofika 300Mbps
Lakini spidi kubwa pia inatokana na nguvu ya mtandao wa simu unaotumia
Ikizingatiwa 4G ya Tanzania haina spidi kubwa kwa laini karibu zote
Kwa bahati mbaya hii simu ililenga soko la India
Hivyo kuna baadhi ya masafa ya LTE yanayotumiwa na laini za simu hapa nchini oppo a54 haina
Masafa iliyo nayo ni 1, 3, 5, 8, 38, 40, 41
Tazama kwenye linki kujua masafa ya mtandao wa 4G yaliyopo Tanzania
Ubora wa kioo cha oppo A54
Oppo A54 inatumia kioo cha IPS LCD chenye resolution ya 720 x 1600 pixels
Kwa kutazama tu ubora wake kwenye kioo ni wa chini
Amoled huwa na ufanisi mkubwa kwenye kuonyesha vitu zaidi
Pia na uangavu wake si mkubwa
Nguvu ya processor ya MediaTek Helio P35
Fahamu kuwa simu inayozungumziwa kwenye kurasa huu ipo kwenye daraja la chini
Inatokana na kitendo cha simu kutumia chip ya MediaTek Helio P35
Nguvu ya Helio P35 ni ndogo sana
Kiasi cha kwamba ni ngumu kwa kamera ya A54 kurekodi video zanye ubora wa 4K
Kwenye app inayopima nguvu ya processor ya GeekBench, Helio P35 ina alama 171
Nguvu ndogo inasababishwa na processor kutumia muundo wa Cortex A53 kwenye core zote
Kama unacheza gemu kubwa kwa resolution ya juu simu inaweza ikawa inachemka sana
Ama kukwama kwama
Uwezo wa betri na chaji
Oppo A54 ni moja ya simu inayotunza chaji muda mrefu
Hii inasababishwa na simu kuwa na betri kubwa
Lakini pia kuwa na processor inayotumia umeme mdogo katika kufanya kazi zake
Uwezakano wa simu kukaa na chaji kwa masaa zaidi ya 14 ni mkubwa
Ila sasa simu hii lazima ichukue masaa mengi kujaa
Maana chaji inapeleka umeme wa wati 18
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo ya aina tatu upande wa memori na ram
Ukubwa wa memori unaanza GB 64 mpaka GB 128
Na RAM ya 4GB mpaka 6GB
Kwa bahati mbaya memori zake ni za aina ya eMMC 5.1
Inalazimika kutumia memori zinazofirisha data ndogo kwa sababu chip haina uwezo wa kuchakata data nyingi
Kwa hiyo OPPO A54 inaweza ikawa inachelewa kuwaka wakati wa kuwasha
Uimara wa bodi ya oppo A54
Karibu simu zote za daraja la chini huwa na bodi za plastiki
Pia hata hii oppo imeundwa kwa bodi za plastiki
Na ina sapoti laini mbili
Lakini pia inakubali memori kadi
Hivyo unapata uhuru wa kuitanua memori ya simu
Plastiki huwa ni rahisi kuchunika rangi
Kadri inavyotumika muda mrefu ndivyo ubora unavyopungua
Ubora wa kamera
Kama unataka oppo macho matatu ya bei nafuu basi A54 ipo
Ila jua kuwa ubora wa kamera zake tatu sio mkubwa
Kwani zinarekodi video za ubora wa ful hd pekee
Kamera kubwa ina ulengaji wa PDAF
Processor ya hii simu inachangia sana kamera kutokuweza kurekodi video ya 4K na kwa fremu nyingi
Aperture yake inapitisha mwanga mdogo kwani kipimo chake ni f/2.2
Hivyo basi ubora wa picha kwenye mwanga mdogo utakuwa ni mbaya
Ubora wa Software
Mfumo endeshi uliopo kwenye simu hii ni Android 10
Hakuna taaraifa iwapo oppo a54 inaweza kupokea Android 12
Haiwezi kushangaza kutokana na chip za MediaTek za daraja la chini kuwa na sapoti ndogo ya software
Lakini mtumiaji atanufaika na mfumo wa OPPO wa CorolOS 7.2
Oppo wanadai kuwa mfumo una kitu kinaitwa Super Power Saving Mode
super Power Saving Mode inaiongezea simu muda wa kutumika pale betri inapokuwa limebakiza chaji kidogo sana
Yapi Madhaifu ya oppo A54
Kutokana na simu kuwa kwenye kundi la chini inafanya kuwa mapungufu mengi
Kubwa zaidi ni nguvu ndogo ya utendaji
Inaondoa utamu wa kutumia applikesheni yoyote unayotaka kwa raha
Kioo cha ips lcd huwa na rangi chache
Kitu kinachofanya baadhi ya vitu kutoonekana kwa rangi halisi
Mfano rangi nyeusi
Neno la Mwisho
Kama bei ya oppo a54 ingekuwa ni chini ya laki tatu basi ingekuwa ni simu nzuri ya bei nafuu
Lakini bei yake kuzidi laki tatu kunaipeleka simu kwenye ushindani na simu ya Redmi 9
Redmi 9 ina utendaji wenye nguvu kiasi ukilinganisha na oppo iliyopo
Ila oppo wana mfumo mzuri unosaidia simu kukaa na chaji muda mrefu
Si simu mbaya kuimiliki kwa mwaka 2022
Wazo moja kuhusu “Bei ya Simu ya Oppo A54 na Sifa Zake Muhimu (2022)”
Kioo chake kina bei gani