SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu Bora Zenye Kamera Nzuri Kwa Sasa na Bei Zake(2026-2027)

Miongozo

Sihaba Mikole

November 18, 2026

Hii ni listi(orodha) ya simu zenye kamera nzuri kwa wakati

Kiuhalisia hizi simu zinaenda kutamba hata mwaka 2027

Kwa hapa tutaorodhesha simu tano (5) tu

Orodha kamili ya simu zote 15 zipo katika hii video

Orodha hii imetokana na tovuti ya DXOMARK na uchambuzi niliofanya kwa kutazama ubora wa picha na video wa simu zipatazo hamsini

Twende kazi

1-Huawei Pura 80 Ultra

Huawei Pura 80 Ultra ina kamera zipatazo nne

Kamera kubwa zaidi ina megapixel 50, kwa asiefahamu anaweza shangaa maana zipo za 200MP

Kitu kikubwa zaidi hii simu ina sensa kubwa sana

Hii sensa imeafanya simu kutoa picha nzuri katika mazingira yote

Itazame moja ya picha iliyopigwa na hii simu kwenye hiyo video juu

Kamera inaweza kuonyesha vitu kwa uhalisia wake

Hivyo eneo ambalo lina mwanga mdogo halijaweza kuzuia vitu visionekane kwa namna inavyotakiwa

Na hata mazingira ya mwanga kamera inatoa kila kitu kwa ubora ule ule

Na haina chengechenga kabisa mpaka uizoom mara nyingi

Bei ya huawei pura 80 ultra ni shilingi milioni tatu na nusu (3,500,000)

2-Motorola Signature 27

Hii ina kamera tatu na sensa zake ni kubwa vilevile

Bei yake ni shilingi milioni na laki sita (4,600,000)

Kwenye video hapo juu kamera yake imerekodi eneo la uwanja

Katika picha vitu ambavyo vipo mbali na kamera vinaweza kutambulika hata ukiizoom

Rangi ya uwanja haina tofauti kabisa na jinsi inavyoonekana na macho ya binaadamu

Hii simu kamera yake inaweza kuonyesha vitu hata katika mazingira ya mvua kubwa

Noises(chengachenga) zinaweza onekana kwenye kiza kingi na kwa kuikuza sana picha

3-Apple iPhone 18 Pro

iPhone 18 Pro ukubwa wa sensa yake inafanana na motorola

Lakini iPhone ina mapungufu kidogo kwa picha za kwenye hafifu

Vitu ambavyo vipo karibu na kamera vinaonakana vizuri na kwa utofauti wa rangi sahihi

Hii na kwa nyakati za usiku

Laki vile vitu ambavyo vimeathariwa sana na giza kunakuwa na kiwango kidogo cha chengachenga

Ndio maana hii ipo katika nafasi ya tatu

Na bei yake ni shilingi milioni tatu na nusu

4-Vivo X300 Pro

Kwenye video na picha niliyoichunguza sana ni ile iliyopigwa usiku ukumbini

Kutoka kwenye hiyo video hapo juu utaona mdada analinganisha hii simu na simu nyingine

Hii simu inaweza kurekodi kitu ambacho kipo mbali sana na kikatambuliko

Yaani mtu anayelengwa anaonekana

Na kitu ambacho kipo mbali na gizani kinaweza kutambuliko

Japo ukiikuza picha hasa za kwenye kiza kuna ubora unaopungua

Bei ya

5-OPPO Find X9 Ultra

Bei ya Oppo Find X9 Ultra kwa Tanzania ni shilingi milioni tatu na nusu

Upande wa kamera zipo nne

Uangavu wa picha ni mkubwa hasa kwenye mazingira ya mwanga mwingi

Na pia ina kiwango kidogo sana cha chenge chenga iwapo utaizoom picha mara nyingi

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

Bei ya iPhone Duo na Changamoto Zake Zilizoibuka

Apple kwa mara ya kwanza wamezindua simujanja za kujikunjua (folding phone) Imeleta hamsha hamsha nyingi kama ilivyo kawaida Japokuwa simu za folding zina miaka mingi tangu zilipotoka Bei yake ni […]

iphone 18 pro

Bei ya iPhone 18 Pro na Sifa Zake Muhimu

iPhone 18 Pro imetoka tangu mwezi wa tisa Imebadilika maeneo machache sana Kiasi cha kwamba unaweza usione tofauti na toleo la iPhone 17 Pro Hata hivyo bei ya iPhone 18 […]

No Featured Image

Matoleo ya iPhone 18 na Duo yathibitisha ubunifu umeisha

Apple mnamo mwezi wa tisa walizindua simu kali sana Simu kali zinamaanisha ubunifu Ila kwenye iPhone 18 hakuna upekee kwenye ubunifu Tutafafanua huu mtazamo wetu baadae Ila . . . […]

Hizi ndizo simu zenye uwezo mkubwa wa betri kupitiliza

Kuna teknolojia mpya ya betri imezipa betri za simu uwezo mkubwa sana Kwa sababu ya hii teknolojia simu zinakaa mpaka SIKU NNE bila kuchaji Na si siku nne ukiwa unaitumia […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company