Ubora wa simu za xiaomi unatofautiana katika makundi matatu.
Kwenye haya makundi matatu kuna simu za xiaomi zenye ubora wa juu, ubora wa kati na ubora wa chini.
Bei inatofautiana kulingana na sifa za simu husika.
Xiaomi ina simu zenye brand ya Redmi, Xiaomi na Pocophone hufahamika kama poco.
Simu za redmi inahusisha simu la tabaka la kati na la chini.
Na simu za matoleo ya Mi ni simu za premium kwa asilimia kubwa na gharama zake huwa ni kubwa.
Matoleo ya pocophone yamegawanyka kwenye matabaka ya juu na ya chini.
Mara nyingi pocophone hulenga pafomansi.
Kuelewa kiundani ubora wa simu za xiaomi inakupasa kuzifuatilia simu za xiaomi moja moja
Unaweza kuzijua kupitia kurasa zifuatazo.
Simu za xiaomi kwa mwaka 2022.
Simu ya xiaomi redmi note 10 5g
Simu ya xiaomi ya bei nafuu ya Redmi 9A
Ubora wa simu za Brandi ya Xiomi Mi
Brandi ya simu ya Mi ni kwa ajili ya simu za tabaka la juu.
Bei yake pia ni kubwa.
Baadhi ya simu za mi ni zifuatazo.
- Mi 11 Ultra
- Mi 11i
- Mi 11 Lite 5G
- Mi 11
- Mi 10T pro
- Mi 10T
- Mi 10T Lite
- Xiaomi 11T pro
- Xiaomi 11T
- Xiaomi 11 Lite 5G NE
Sifa kubwa ya simu ambazo unazoona hapo juu ni kutumia processor yenye nguvu kubwa kwenye utendaji.
Hauwezi kukuta chip zenye nguvu ndogo kwenye simu za Xiaomi Mi.
Chipset ambazo zimetumika sana ni Snapdragon 888, MediaTek Dimensity 1200, Snapdragon 778 5G, Snapdragon 750 na Snapdragon 865.
Simu zinazotumia chips hizo mara nyingi huwa na uwezo wa hali juu.
Kama nilivyotangulia kuandika, inafaa kusoma sifa zote za kila simu kutokana na xiaomi kuwa na matoleo mengi.
Ubora wa simu za Brandi ya Redmi
Kwenye brandi ya simu za Redmi utakutana na simu mbaya na nzuri.
Simu zenye uwezo chini na simu zinazopiga kazi kubwa.
Redmi zenye neno Note mara nyingi huwa zina ubora wa kati.
Na huwa ni simu zenye vitu vizuri vingi.
Hapa utakutana na simu zifuatazo.
- Redmi Note 11 Pro 5g
- Redmi Note 11 Pro
- Redmi Note 11S
- Redmi note 11
- Redmi Note 10 5G
- Redmi Note 8 2021
- Redmi Note 10S
- Redmi Note 10
- Redmi Note 10 pro
Sifa kubwa ya matoleo ya simu za Redmi Note ni kutumia processor za tabaka la kati kiuwezo.
Utakuta baadhi zinatumia processor za Snapdragon ama MediaTek
Snapdragon zinaweza kuwa matoleo ya 6xx au 7xx.
Hizo ni processor zinazokuwa na nguvu.
Na processor za MediaTek zinaweza kuwa Helio Gxx.
Pia kuna Redmi ambazo zina ubora mdogo huuzwa kwa bei za chini.
Redmi hizi huwa hazina neno NOTE.
Mfano ni Redmi 9.
Unaweza tembelea kurasa rasmi zinazoorodhesha simu za redmi zote.
Ubora wa simu Brandi ya Pocophone
Upande wa simu Poco kuna smartphone kali zinazokusukuma vitu vingi.
Lakini zipo ambazo zina ubora wa kati.
Baadhi simu za brandi ya pocophone utazokutana nazo ni zifuatazo.
- Poco M3
- Poco X3 NFC
- Poco F2 Pro
Poco X3 NFC na Poco F2 Pro ni simu bora kwenye idara nyingi.
Wakati poco M3 ni simu yenye ubora wa kati yenye vitu vichache vinavyoongeza ubora wa simu.
Kiujumla si rahisi kueleza ubora wa simu za xiaomi bila ya kutaja simu husika.
Sababu kuu kuna simu za xiaomi nzuri na zingine mbaya kama ilivyo simu nyingi za android zinazotengenezwa na kampuni za kichina.
Xiaomi wana brandi za simu nyingi kama ilivyo kwa simu za vivo