Simu ya Redmi note 10 pro ni simu ya android ambayo ilitoka mwanzoni mwa mwaka 2021.
Mpaka kufikia sasa, hii simu inazizidi matoleo mapya mengi ya simu ikiwemo infinix note 11 pro
Pitia kwa umakini na tazama ubora wake kwenye display, memori, chaji na betri na utendaji wa processor.
Jambo utakaloliona ni kuwa redmi note 10 pro inazipita simu nyingi za android 11 na 12 zilizotoka 2022
Bei yake inavumulika sana kwa kutazama sifa za simu.
Kwani bei ya redmi note 10 pro ni chini ya laki sita kama ikinunualiwa toka nje ya nchi ila sio Tanzania
Bei ya Redmi Note 10 Pro Tanzania
Bei ya redmi note 10 pro kwenye maduka ya mitaa msimbazi kariakoo ni shilingi 850,000/=
Hii ni kwa redmi ya GB 128 na ram GB 6
Bei inashuka zaidi kama utainununua kwenye mtandao wa aliexpress
Kwani utaipata simu hii kwa bei ya shilingi 562,000/=
Na note 10 pro ya gb 128 na ram gb 8 inapatikana kwa 593,000/=
Ikiwa hauna haraka agiza redmi note 10 pro aliexpress ni rahisi sana
Sifa za Redmi Note 10 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 128GB,64GB na RAM 8GB,6GB |
Kamera | Kamera nne(redmi macho manne)
|
Muundo | Urefu-6.67inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 562,000/= |
Upi ubora wa simu ya Redmi note 10 pro
Ubora wa simu aina ya redmi note 10 pro upo kwenye utendaji wa processor.
Simu ina processor yenye nguvu ya kufungua app yoyote kiurahisi.
Ina kioo kizuri kinachokoleza rangi kwa kiwango stahiki kinachoonyesha vitu kwa uhalisia
Kioo chake ni chepesi sababu ya kuwa na refresh rate kubwa
Chaji yake inajaza simu kwa dakika chache
Bei yake ni rafiki na na simu yenye vitu ambavyo zamani vilipatikana kwenye simu za daraja la juu
Ina utendaji mkubwa wa memori kwani inasafirisha data kwa kasi
Uwezo wa Network
Simu ya redmi note 10 pro inakubali aina zote za network kasoro mtandao wa 5G ambao haupo hapa Tanzania kwa sasa
Aina ya 4G simu inayokuja nayo ni LTE Cat 15
4G ya LTE cat 15 inaweza kudownload faili kwa kasi inayofikia 800Mbps ambayo ni sawa na 100MB/s
Kama mtandao wa simu unakupa spidi hii basi inachukua sekunde 1.3 kupakua faili la ukubwa wa 1300MB
Simu ina network bands za 4G zipatazo 13
Na inakubali mitandao yote ya simu ya Tanzania unapotumia intaneti ya 4G
Ubora wa kioo cha Redmi note 10 pro
Amoled ndio kioo cha redmi note 10 pro ambacho hukoleza rangi kwa ustadi.
Amoled ni aina ya vioo vilivyo na contrast kubwa.
Contrast kubwa inafanya kioo cha simu kuwa na rangi nyingi
Hivyo vitu vinaonekana kwa uhalisia kwa kiasi kikubwa.
Kioo chake pia kina mfumo wa HDR10.
HDR10 huboresha muonekano wa rangi za vitu
Kiasi cha kuisadia simu kuweza kuonyesha vitu kama vinavyoonekana na jicho la binadamu
Na amoled ya hii simu ina resolution nzuri na kubwa yenye pixels 1080×2600
Unaposcroll(kuperuzi) kioo kipo fasta kwa sababu ya kuwa na refresh rate inayofikia 120Hz
Nguvu ya processor Snapdragon 732G
Ubongo wa simu ni processor.
Simu inayotumia processor yenye nguvu huwa bora kwenye nyanja karibu zote
Redmi note 10 pro inatumia processor ya snapdragon 732G
Ni processor ya daraja la kati inayoipita utendaji Helio G95 ya infinix note 10 pro
Na inaipita pia snapdragon 675 ya redmi note 10
Kwani alama zake kwenye app ya Geekbench zinafika 570 kwenye core moja
Kiujumla ni processor yenye core nane iliyogawanyika sehemu mbili
Ina core kubwa na core ndogo
Uwezo wa core kubwa
Kiutendaji, core kubwa inapiga mzigo kwa nguvu kubwa sana.
Nguvu inayoifanya simu kuweza kucheza gemu nyingi na za aina yoyote.
Hii inasababishwa na uwepo wa core mbili zenye nguvu ambazo zina spidi inayofikia 2.3GHz
Na nguvu kubwa kiutendaji inachangiwa na kutumika kwa muundo wa Kryo 460 ambao ni Cortex A76 iliyoboreshwa.
Cortex A76 ni core zenye nguvu na matumizi madogo ya chaji.
Japokuwa kiuwezo ipo nyuma ya processor ya simu aina ya MediaTek Dimensity 1200
MediaTek Dimensity 1200 ina Cortex A78 na imetumika kwenye simu ya vivo v23 pro
Uwezo wa core ndogo
Kuna jumla ya core ndogo sita.
Core ndogo zinamatumizi ya chini ya betri.
Hivyo inafanya simu kutumia umeme kidogo wakati wa kupiga simu
Kwa sababu kazi ndogo hutumia hizi core sita
Na matumizi madogo ya umeme yanachangiwa na kutumika kwa core aina ya Cortex A55.
Na pia core ndogo kuwa na kasi ya chini isiyozidi 1.8GHz
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya redmi note 10 pro inaweza kukaa na chaji kwa takribani masaa 118 endapo simu haitumiki mara kwa mara
Na ikiwa inatumia intaneti masaa yote simu inakaa na chaji masaa 14
Jifunze: ukaaji wa chaji wa redmi note 10 pro
Betri yake inapeleka umeme kwa kasi inayofikia wati 33
Kwenye simu hii, kasi ya wati 33 inajaza betri kwa 100% ndani ya dakika 81
Ni fasti chaji hii.
Ukubwa na aina ya memori
Memori ya redmi note 10 pro inasafirisha data kwa kasi kubwa inayoifanya simu kuwaka kwa haraka
Hii inasababishwa na memori aina ya UFS 2.2 ambayo ina spidi ya kuandika inayofikia 1200MB/s
Utendaji wa simu unategemea pia kasi ya memori kuandika na kusoma data kifupi kusafirisha data
Simu imegawanyika katika aina tatu upande wa memori
- Redmi note 10 pro ya GB 64 na RAM GB 6
- Redmi Note 10 Pro ya GB 128 na RAM GB 6
- Redmi Note 10 Pro ya GB 128 na RAM GB 8
Memori kubwa maana yake utahifadhi vitu vingi.
Ram kubwa inaongeza ufanisi kiutendaji wa simu
Uimara wa bodi ya Redmi note 10 pro
Bodi yake ni imara na ngumu kuharibika ama kupasuka kirahisi.
Ugumu wa bodi unachangiwa na simu kuundwa kwa vioo vya Gorilla Glass 5
Vioo vya gorilla 5 vinaweza visipasuke kabisa kama simu ikianguka kwa kimo cha mita 1.2 kutoka juu
Hutohitaji kuwa na screen protector wala kava.
Kwa sababu upande wa nyuma unalindwa pia na kioo cha gorilla glass
Binafsi, nimesoma materio yaliyounda kioo cha gorilla na kutazama majaribio ya kudondosha simu na maoni mengi ya watu.
Simu zenye vioo vya gorilla huwa ni imara na ngumu
Pia simu inaweza kuzuia maji yanayotiririka na vumbi pia kwani ina IP53
Ubora wa kamera
Hii ni simu ya redmi ya macho manne.
Kamera moja ina sensa kubwa kiasi cha 108MP
Kitu kinachopunguza ubora wake wa kamera ni kutumia teknolojia ya ulengaji ya PDAF
PDAF ni nzuri lakini haiwezi kutoa picha nzuri sana kwa kitu kinachotembea kwa kasi kikiwa kinapigwa picha kama ndege mnyama
Simu inatoa picha nzuri za mchana na usiku
Japo nyakati za usiku kuna uwepo kiasi kidogo cha noises
Zitazame picha zilizopigwa na simu ya redmi note 10 pro
Pia fuatilia, simu zenye camera bora
Ubora wa Software
Redmi note 10 pro ni simu ya android 11 inayokuja na mfumo wa MIUI 12
Simu inakubali toleo jipya la android 12 na MIUI 13
Kama ukifanikiwa kuweka android mpya utapata vitu vya ziada kama uwezo wa kuonyesha app zinazotumia mic.
Na utaweza kutambua app zinazokutraki
Yapi Madhaifu ya redmi note 10 pro
Simu haziwezi kuzuia maji endapo umeizamisha kwenye kina cha mita moja
Maji lazima yaingie ndani ya muda mfupi
Xiaomi hawajazingatia kutumia dual pixel pdad kuboresha uwezo wa kamera
Lakini pia kamera zake hazina OIS(Optical Image Stabiliztion)
Kama unarekodi video na mkono ukawa unatisika basi video inaweza kutokea vibaya
Neno la Mwisho
Bei ya redmi note 10 pro inaifanya simu kuwa ya bei nafuu huku ikiwa na ubora mwingi
Lakini kuna washindani wenye sifa nzuri nyingi kuliko hii redmi
Kwa mfano, simu ya samsung a52 ina mengi inayofanana na redmi note 10 pro
Wakati samsung galaxy a52 inauwezo wa kuzuia maji kupita ndani ya simu endapo ikidumbukia kwenye kina cha mita moja kwa muda wa nusu saa
Wakati huo bei ya samsung a52 inaendana na bei ya redmi tunayoizungumzia
Ila kiujumla redmi hii ni nzuri kuwa nayo
Maoni 4 kuhusu “Ubora na bei ya Redmi Note 10 Pro (2022)”
Mimi nipo na redmi not 10 imepasuka bodi yake ilianguka iakakanyagwa na gari ila mashine ndani ni nzima ikabid ninunue kioo kingine ila bodi sija bahatiwa kuipata nitaipataje hapa Dae es salaam ?
nitakuangalizia
Mimi nina redmi not 10 pro ilivujia wino nikanunua kioo kingine ila sio og je nitapataje na ni bei gani
Vioo vya amoled unaweza kuvipata Kwa bei nafuu AliExpress