Hakuna kitu kigumu kama kupata simu yenye kamera kali kwa bei ndogo
Ukifuatilia simu zenye kamera nzuri utagundua kuwa zinauzwa kwa bei kubwa
Kiasi cha kwamba ni watu wachache wanaweza kumudu kuwa nazo kwa hapa Tanzania
Hapa imeorodheshwa orodha ya simu zenye nzuri na zinazouzwa kwa bei rahisi
Ubora wa picha wa hizi simu zilizopo si mkubwa ila ni ubora unaotoa picha ama video za kuweleweka.
Simu Zenye Kamera Nzuri za Bei Ndogo
Samsung Galaxy A23 5G
Samsung Galaxy A23 5G ni simu yenye kamera nne aina ya lenzi za wide, ultrawide, macro na depth
Hii ina maana kuwa Galaxy A23 inaweza kupiga picha eneo pana sana
Kamera kubwa ina ukubwa wa megapixel 50 huku ikiwa imewekewa OIS na ulengaji wa PDAF
OIS inaifanya simu kutulia wakati wa kurekodi video na ulengaji PDAF inaifanya kamera kulenga kitu kwa ustadi na picha kuwa “sharp”
Ila kamera zilizobaki zina megapixel ndogo na hazijaekewa teknolojia za ziada
Kamera zake pia hazina HDR ambazo husaidia kurekebisha muonekano wa vitu hasa maeneo yanapaswa kuonekana kiza na mwanga
Ubora wa picha wa wakati wa mchana ni wa kuridhisha sana
Na kwenye mwanga mdogo kamera inajitahidi kuonesha vitu na kwa kasoro ndogo sana
Bei ya Samsung Galaxy A23 5G ya GB 128 ni shilingi 640,000/=
Samsung Galaxy A14 5G
Hii ni simu yenye kamera tatu ambazo ni wide ina 50MP, Macro yenye 2MP na Depth pia ina 2MP
Macro na Depth huwa hazina umuhimu kihivyo
Hii simu inatumia ulengaji wa PDAF hivyo ina utambuaji wa haraka wa vitu vinaavyostahili kupigwa picha kinapotokea mbele ya kamera
Uwezo wa simu kurekodi video ni wa Full HD na haiwezi rekodi video za 4K
Wakati wa kurekodi utalazimika kutuliza mkono kwa sababu simu haina OIS
Pia kamera zake zina uwezo wa kukusanya mwanga wa kutosha
Hivyo kwenye mwanga hafifu kamera inapiga picha vizuri
Bei ya Samsung Galaxy A14 5G kwa sasa ni 470,000/=
Google Pixel 4
Google Pixel 4 ni simu ya mwaka 2019 yenye kamera mbili tu
Kamera hizo ni wide (kamera kuu) na kamera kwa ajili ya kupiga vitu vya mbali yaani Telephoto
Kamera zote zina resolution ya megapixel 12
Kamera zake zote ni nzuri kwani zinaweza kurekodi video za 4K na zina HDR (High Dynamic Range)
Kwa hiyo kamera za hii simu zina uwezo wa kutofautisha kiza(rangi nyeusi) na mwanga(nyeupe)
Kwenye ulengaji inatumia teknolojia ya juu zaidi aina ya dual pixel PDAF ambayo iko na kasi kubwa kukilenga kitu
Tembele hapa, kuangalia ubora wa picha wa kamera ya google pixel 4
Kwenye mazingira ya mwanga hafifu na mwanga mwingi muonekano wa vitu unaonekana kama yalivyo kwenye mazingira halisi
Bei ya pixel 4 kwa sasa ni 450,000/= na nyingi utakayopata ni used kwani ni miaka minne sasa tangu imetoka
Redmi Note 10
Simu ya Redmi Note 10 ni simu ya mwaka 2021 yenye kamera zipatazo nne
Kamera hizo ni ultrawide, wide, macro na depth huku wide ikiwa na lenzi ya 50MP
Hii simu ina ulengaji PDAF na pia ina HDR kitu kinachotoa uhakika wa kupata picha nzuri
Kwa bahati mbaya kamera zake hazina OIS
Ubora wa kamera ya hii simu ni kuwa inaweza kurekodi video kwa 30fps
Pia ina uwezo wa kukusanya mwanga mwingi kitu inachoiboresha simu kupiga vizuri kwenye mwanga mdogo
Bei ya Redmi Note 10 kwa sasa haizidi 400,000/= bei yake imeshuka sana
Realme 10
Realme 10 ina kamera mbili ila kiuhalisia ni kamera mbili kwa sababu depth huwa haipigi picha
Kamera kubwa ina ukubwa wa megapixel 50 na ina PDAF hivyo swala la ulengaji hakuna shida
Pia ina ukusanyaji wa mwanga wa kiwango kikubwa na lenzi yake ni kubwa.
Kwenye ubora wa picha, Realme 10 iko vizuri
Inapiga picha bila chengachenga wakati wa mchana ila nyakati za usiku ni changamoto
Chengachenga zinaonekana kwa uwazi kama ukiikuza picha
Haina uwezo wa kurekodi video za 4K na haina OIS kwa ajili kuchukua video kwa utulivu
Bei ya Realme 10 ni shilingi 480,000 za Tanzania
Infinix Note 12i
Infinix Note 12i ni simu ya kamera tatu ila ni kamera moja tu ndio inayopiga picha vizuri
Kamera mbili zingine zina resolution ndogo sana
Kamera yenye ubora unaotakiwa imewekewa PDAF lakini inakosa OIS
Uwezo wa kurekodi video ni wa aina moja pekee ambao Full HD PLus
FHD+ inaonyesha picha nzuri
Na pia kamera za hii simu ina HDR, hivyo uboreshaji wa muonekano wa vitu upo
Bei ya Infinix Note 12i ni shilingi 430,000/=
Japokuwa inaachwa mbali sana na infinix yenye kamera nzuri, ila infinix yenye kamera kali gharama
OnePlus 6t
Simu ya OnePlus 6t ni simu ya daraja la juu ya mwaka 2018 ambayo ina kamera mbili
Kamera za oneplus 6t ni za kiwango kikubwa
Kwa mfano kamera aina ya WIDE(kamera kubwa) ina megapixel 16 na ina OIS na PDAF
Tundu la kupitisha mwanga lina upana wa f/1.7 kwa maana kamera inaweza kukusanya mwanga wa kutosha
Inaweza kurekodi video za 4K na ina HDR bila kusahahu teknolojia ya kuongeza utulivu kwa ajili ya kurekodi video aina gyro-EIS
Simu inatoa kamera iliyokolea rangi kiasi fulani wakati wa mchana
Bei ya OnePlus 6t kwa sasa ni shilingi 480,000/=
Uzuri ni kuwa simu hii inaweza kupokea toleo la Android 11
Redmi Note 11
Unaweza ukadhani simu ya Redmi Note 11 ina kamera nzuri zaidi ya Redmi Note 11 ila sivyo ndivyo
Redmi Note 11 kamera yake inaachwa na mtangulizi wake
Hii simu ina jumla ya kamera nne ila kamera mbili tu ndio za msingi
Redmi Note 11 inaweza kurekodi video za full hd na haina OIS
Kwenye ulengaji simu inatumia teknolojia ya PDAF kama zilivyo simu nyingi zilizopo
Wakati wa mchana kamera inapiga vizuri na rangi za vitu vinaendana na uhalisia
Nyakati za usiku kamera haitoi picha za kuvutia kwani chengachenga zinaweza kuonekana iwapo ukiikuza picha
Bei ya Redmi Note 11 kwa mwaka 2023 ni shilingi 380,000/=
Pia pitia: Ubora wa simu ya Redmi Note 11 Pro+ 5G
Vivo Y22
Vivo Y22 inaweza ikawa ndio simu yenye kamera ya kawaida sana kwenye hii orodha
Ni simu ya mwaka 2022 yenye idadi ya kamera tatu ila moja ndio yenye ubora sahihi
Kwani ina megapixel 50 na ulengaji wa PDAF
Ila ni simu yenye kamera inayokosa teknolojia ya HDR
Hii inamaanisha kwenye giza simu inaweza kupata shida kutoa picha nzuri
Ila kwenye mwanga mwingi ubora wa picha ni wa kuridhisha
Bei ya Vivo Y22 ni shilingi 400,000/=
Google Pixel 3 XL
Linapokuja idara ya camera, simu za google Pixel lazima uzifikirie hata kama imetoka miaka mingi ya nyuma
Google Pixel 3 XL ni simu ya mwaka 2018 yenye kamera moja tu ambayo ni matata sana
Kamera ya hii simu ina teknolojia ya juu ya ulengaji aina ya dual pixel pdaf
Huwa iko fasta kuliko PDAF
Ina uwezo wa kurekodi wa video za 4K na pia ina OIS
Kwa hiyo kunakuwa na utulivu wakati wa kuchukua video
Bei ya sasa ya Google Pixel 3 XL ni shilingi 330,000/=
Lakini kwa wakati huu utapata simu used hivyo umakini unahitajika
Maoni 6 kuhusu “Simu zenye Kamera Nzuri za Bei Rahisi (2023)”
Kwani hzo Simu used nazo huwa zina box zake
* hvi hzo Simu used nazo huwa zina box zake au zina kuwa hazina box
Hizi huwa zipo kwenye box pia na zingine unakuta hazipo
Kati ya simu ulizotaja kuna nyeupe kwa mbele hasa sumsung
Naitaji cm mpya ambayo kamera zake ukipiga picha kamela inatoka nje ukimaliza inalud ndan ila sijafaam aina gan ya cm nazionaga kweny matangazo
duh