Mwishoni mwa mwaka 2023 na mwanzoni mwa 2024 kuna matoleo mapya ya infinix yalitoka
Matoleo hayo mengi ni ya daraja la kati na la chini yaani yamegusa kila mtu kulingana na bajeti ya mnunuaji aliyonayo
Hivyo basi hapa kuna orodha ya simu kumi za infinix zinazotarajiwa kutamba na bei zake kwa mwaka 2024
Simu zote zilizoorodheshwa bei zake ni himilivu tofauti na orodha ya simu mpya zenye ubora mkubwa zaidi
Hizi ni baadhi
Infinix Smart 8 Plus
Bei ya Infinix Smart 8 Plus: 300,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Simu ya Infinix Smart 8 Plus imeingia sokoni mwezi februari
Hii ni simu yenye betri yenye 6000mAh ambayo inaipa simu muda mwingi wa kukaa na chaji
Chip yake Mediatek Helio G36 ambayo haina nguvu kubwa kwani ni maalumu kwa simu za madaraja ya chini
Kioo chaje hakina resolution kubwa na chaji yake inapeleka umeme kwa kasi ya kiwango cha 18W
Hii simu ina kamera moja yenye megapixel 50
Infinix Smart 8 Pro
Bei ya Infinix Smart 8 Pro: 300,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Simu nyingine ya daraja la chini ambayo imetoka mwezi februari 2024 pia
Ni tecno mpya inayotumia processor ya Helio G36 kama ilivyo kwa smart 8 plus
Sifa nyingi za hii hazitofoatiani na smart 8 plus
Isipokuwa ni kwamba hii betri yake ina 5000mAh
Mambo mengine yanalingana kwa kiasi kikubwa
Infinix Smart 8 HD
Bei ya Infinix Smart 8 HD: 250,000/= ,Ukubwa wa Memori: 64GB, RAM: 3GB
Katika smart 8 mpya za mwaka 2024, Infinix Smart 8 HD ina unafuu kidogo katika utendaji
Hii inatokana na kutumia chip ya Unisoc T606 ambayo core zake mbili zenye nguvu zinatumia muundo wa Cortex A76
Ila changamoto kubwa ni kuwa simu ina nafasi ya GB 64 na RAM ndogo ya GB 3
Kiwango kidogo cha memori kinaweza kurudisha chini utendaji wa simu
Ila ni infinix nzuri ya bei nafuu
Infinix Hot 40 Pro
Bei ya Infinix Hot 40 Pro: 600,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Infinix Hot 40 Pro ni simu ya daraja la kati iliyotoka desemba 2023
Inatumia chip ya Mediatek Helio G99 yenye nguvu ya wasatani katika utendaji wake
Hii simu ina kamera zipatazo mbili zinazofanya kazi na kamera moja ina 108MP
Betri yake inakaa na chaji kwani ni kubwa na chaji yake inapeleka umeme wa wati 33
Kioo chake kina resolution kubwa hivyo muonekano wa vitu ni mzuri
Infinix Hot 40
Bei ya Infinix Hot 40: 450,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 8GB
Infinix nyingine ya daraja la kati iliyotoka mwezi desemba mwaka 2023
Utenadaji wa infinix hot 40 ni wa wastani kutokana na kutumia processor yenye nguvu ya wastani
Betri yake ina 5000mAh kama ilivyo kwa simu nyingi za siku zilizopo
Chaji ina uwezo wa kupeleka umeme wa wati 33
Na ina kamera mbili zenye lenzi za wide na macro
Infinix Hot 40i
Bei ya Infinix Hot 40i: 400,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM: 4GB
Kiutendaji, infinix hot 40i inafanana na Infinix Smart 8 HD
Isipokuwa Hot 40i ni fupi ila memori na ram ni kubwa inayoweza kusaidia kuhifadhi vitu vingi
Simu ina kamera moja yenye megapixel 50
Ukubwa wa betri lake ni mAh 5000
Kasi ya chaji ni 18W hivyo simu itachukua muda kidogo kujaza betri
Infinix Zero 30 4G
Bei ya Infinix Zero 30 4G: 500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Kioo cha infinix zero 40 4G ni aina ya AMOLED ambavyo huwa na ubora wa uonyeshaji wa vitu kwa uhalisia wa rangi
Ina chaji yenye kujaza betri kwa haraka kwani chaji yake ina wati 45
Kamera zipo mbili na kamera kubwa ambayo ndio nzuri zaidi ina megapixel 108
Utendaji wa Infinix Zero 30 4G hauna tofauti na Infinix Hot 40 Pro
Kwa sababu zinatumia processor ya aina moja
Infinix Zero 30
Bei ya nfinix Zero 30: 680,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Infinix Zero 30 ni infinix yenye 5G iliyotoka mwezi Septemba 2024
Japo ina miezi saba tangu itoke ila ni moja ya simu bora za infinix kwa mwaka 2024
Utenadji wa hii ni mkubwa na wa kuridhisha ukiringanisha matoleo yote yaliyopo kwenye hii orodha
Inatumia processor yenye nguvu ya Mediatek dimensity 8020
Hivyo kwa mpenzi wa magemu atafutrahia kuwa na hii simu
Infinix GT 10 Pro
Bei ya nfinix GT 10 Pro: 720,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM: 8GB
Katika hii orodha Infinix GT 10 Pro ni simu nyingine yenye uwezo mkubwa kiutendaji
Hii Simu imetoka mwezi agost ya mwaka 2023
Ni kipindi cha muda mrefu ila ni simu shindani kwa simu nyingi za mwaka 2024
Uwezo mkubwa wa kiutendaji unachagizwa na kutumia chip Mediatek dimensity 8050
Hivyo kiutendaji hii simu inaendana sana na Infinix Zero 30 5G
Maoni 7 kuhusu “Simu za Infinix zinazotamba na bei zake (2024)”
Utaitambuje kama simu hii ni feki au olijino make siku hizi simu nyingi unambiwa ni olijino kumbe hakuna ukija kutumia inaaza kuchemuka
Kabla hujanunua simu, soma kuhusu vitu ilivyonavyo(specifications) sehemu nzuri ya kupata taarifa nyingi za simu gsmarena. Halafu download app inaitwa CPU X, linganisha taarifa za simu za CPU X na spec ambazo ulizipata
Simu zenu ziko vizur nazipenda, naomba kuja bei ya NOT 40PTO
Nataka kujua bei za sasa
ndio hizi bei za sasa
Jamani mm naitaji kujua bei hot 10 kwa sasa
Naitaji smart 8 used niko kahama nyahanga