Blackberry ni kampuni ya simu ambayo kwa sasa inajikongoja
Kwani tangu 2018 hawakutoa simu mpya
Bali palikuwa na tetesi za toleo la mwaka 2022 lililofahamika kama blackberry vienna 5g
Kwenye hii orodha kuna baadhi ya simu za blackberry na bei zake ambazo zimetoka kati 2017 – 2018
Hizi ni smartphone zenye batani pia
Baadhi ya Simu za Blackberry za Android
Blackberry Evolve
Simu ya Blackberry ilitoka mwaka 2018 ikiwa inatumia Android 8
Utendaji wake si mkubwa kwani inatumia processor yenye nguvu ndogo ya Snapdragon 450
Kioo cha Evolve ni aina ya IPS LCD chenye resolution ya 1080 x 2160 pixels
Ukubwa wake wa memori ni GB 64 na RAM ni GB 4
Ina kamera mbili ambazo zinatumia ulengaji wa PDAF ila ukusanyaji wa mwanga ni mdogo
Ukaaji wake wa chaji ni wa kuridhisha kutokana na kuwa na betri kubwa la wastani
Ukubwa wa betri ni 4000mAh
Simu hii inaweza kukaa na chaji muda mwingi kwa sababu processor inatumia haili umeme mwingi
Bei ya Blackberry Evolve
Wakati simu inatoka bei yake ilikuwa ni shilingi 737,232.00/=
Kiasi hiki cha pesa kinakupa picha kwa nini simu za blackberry hazikufanya vizuri tangu ujio wa Android na iPhone
Bei ni kubwa kuliko ubora wa simu
Blackberry Key2
Simu ya Blackberry key2 iliingia sokoni mwezi juni mwaka 2018
Ni simu ya android yenye batani pamoja na tachi
Utendaji wake ni wastani kutokana na simu kutumia memori za eMMC 5.1 na chip ya Snapdragon 660
Hii simu pia inalindwa na kioo cha Gorilla 3 upande wa screen
Gorilla 3 huwa ni vioo vigumu kuchunika
Kioo chake ni cha IPS LCD ambacho kina resolution kubwa ya 1080 x 1620 pixels
Kwenye memori kuna key2 ya GB 64 na GB 128
Hivyo kuna nafasi ya kutosha kuhifadhi mafaili ya kutosha
Ina betri lenye ujazo mdogo wa 3500mAh
Hivyo ukaaji wa chaji ni mdogo
Kamera zake ni nzuri kwani zinaweza kurekodi video za 4K kwa fremu za 30fps
Bei ya Blackberry key2
Wakati imetoka 2018 bei yake ilikuwa ni shilingi 1,228,720.00/=
Hii bei ni kubwa ambayo kwa wakati huo ungeweza kupata simu kali za samsung au redmi zinazoizidi key2 ubora kwa sehemu kubwa
Kwa sasa bei inaweza ikawa imepungua ila upatikanaji wake ni mgumu kwa Tanzania
Blackberry Motion
Blackberry motion ni simu ya Android 7.1 iliyotoka mwaka 2017
Blackberry hii sio simu ya batani kama zile za mwaka 2018
Chip iliyotumika na Blackberry motion ni Snapdragon 625
Snapdragon 625 ina utendaji wa chini kutokana na kila core kutumia Cortex A53
Blackberry motion ni simu isiyopitisha maji
Kama ikizama kwenye maji ya kina cha mita moja maji hayatoingia kwenye simu kwa muda wa nusu saa
Kioo chake ni cha ips lcd ambacho kina resolution ya 1080 x 1920 pixels
Ila memori yake ni ndogo ya GB 32
Betri yake ni la wastani lina ukubwa 4000mAh
Hivyo ukaaji wa chaji ni wa kuridhisha kwa chip yake haitumii umeme mwingi
Kamera yake ina ubora mdogo na resolution yake ni ndogo pia
Bei ya Blackberry Motion
Bei ya Blackberry motion ilikuwa ni shilingi 958,401.60/=
Bado ni kwamba hii bei ni kubwa hata kama ilikuwa ni miaka mitano iliyopita
Blackberry Aurora
Aurora ni blackberry nyingine ya mwaka 2017
Ni simu ndogo yenye kimo cha 5.5 hivyo haina batani
Inakuja na android toleo la 7 yaani Android Nougat
Ina kioo cha IPS LCD chenye resolution ya 720 x 1280 pixels
Betri yake ni ndogo lina ukubwa 3000mAh
Hivyo ukaaji wake ni wa kiwango cha chini
Utendaji wa simu kiujumla ni mdogo
Kwani simu inatumia processor yenye nguvu ndogo ya Snapdragon 425
Bei ya Blackberry Aurora
Wakati simu inatoka bei yake ilikuwa ni shilingi 500,000/= za Tanzania
Ubora wa simu unaonyesha ni simu ya kuuzwa 150,000/=
Hii ni moja ya sababu simu za blackberry zilikosa soko na zinashindwa kuinuka tena
Blackberry KeyOne
Blackberry KeyOne ni smartphone ya android yenye tachi na batani
Ilitoka mwaka 2017
Ni simu yenye inchi 4,5 hivyo ni simu ndogo inayojaa mkononi
Utendaji wake ni mdogo kutokana na simu kutumia chip ya Snapdragon 625
Snapdragon 625 ina nguvu ndogo
Kioo cha blackberry keyone ni aina ya IPS LCD na resolution ya 1080 x 1620 pixels
Ukaaji wa chaji pia si mkubwa
Kwa sababu betri ina ukubwa wa 3500mAh
Ina kamera moja yenye ukubwa wa 8MP
Na haitoi picha nzuri bali inaweza kurekodi video za full hd pekee
Bei ya Blackberry KeyOne
Hii simu bei yake wakati inatoka ilikuwa ni shilingi 712,657.60/=
Kiujumla katika list iliyopo hakuna simu inayoweza ikachuana na simu za miaka karibuni
Hasa ukizingatia kiasi cha pesa ambacho kinahitajika kupata blackberry zilizopo
Hii kampuni kwa sasa 2022 imebaki kuwa historia
Haiwezi kuingia hata kwenye 20 ya makampuni bora ya simu bora
Maoni 3 kuhusu “Simu Nzuri za Blackberry na Bei Zake (Android)”
Betrii inakaa na chaji kwa mida gani kama data ipo on 24 hrs
Betrii inakaa muda gani kama data ziko on muda wote
Brackberry ipi