SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ubora na bei ya simu ya Xiaomi Mi 11(na sifa zake)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

April 7, 2022

Simu ya xiaomi mi 11 ni simu nzuri ya android iliyotoka mwanzoni mwa mwaka 2021.

Umri wa simu umeshafikia zaidi ya mwaka lakini ni simu chache mpya zinazoizidi ubora Mi 11

Ni simu ngumu na yenye nguvu kwenye utendaji

Mfumo wa kamera ni wa kustaajabisha ukizingatia na bei ya simu.

Linganisha bei ya xiaomi mi 11 na sifa zake kwenye jedwari.

Na ulinganishe na simu zingine zenye bei sawa.

Kwa hakika mi 11 ni moja ya simu bora ya bei rahisi

Bei ya xiaomi Mi 11 Tanzania ikoje ?

Kwenye soko bei ya xiaomi mi 11 ya GB 128 na RAM GB 8 inaanzaia shilingi 1,553,321.26/=

Na xiaomi mi 11 ya GB 256 na RAM GB 8 inauzwa 1,646,172.26/=

Na Mi 11 kubwa zaidi ya GB 256 na RAM GB 12 bei yake inafika  1,808,702.14/=

Hizi ni bei za aliexpress unaweza kuagazia

Kwa maduka ya Tanzania maeneo ya kisutu wanauza Mi 11 ya GB 256 na RAM GB 8 kwa shilingi 2,200,000/=

Kwa nini mi 11 ni simu ya bei rahisi?

Ukitazama bei ya hii simu inazidi milioni.

Na bei zinatofautiana kulingana na ukubwa wa memori.

Simu ambazo zinatumia processor iliyomo kwenye Mi 11 huuzwa bei zaidi ya 1,600,000/=.

Mfano mzuri ni simu ya Vivo X70 Pro Plus, Sony Xperia I III na Oppo Find X3 Pro

Bei ya Vivo X70 Pro Plus ni shilingi 1,9652,76.72/=

Bei ya Sony Xperia 1 III ni shilingi 1,845,864.39/=

Bei ya Oppo Find X3 Pro ni shilingi 1,690,300.98/=

Lakini Mi 11 inachuana na hizo simu kwenye kila idara

Kulielewa hili fuatalia mtililiko wa sifa zote za simu ya xiaomi m1 11 uliopo

Sifa za Xiaomi Mi 11

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 888 5G
  • Core Zenye nguvu(1) – 1×2.84 GHz Kryo 680
  • Core yenye nguvu kiasi(3)-3×2.42 GHz Kryo 680
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.80 GHz Kryo 680
  • GPU-Adreno 660
Display(Kioo) AMOLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 11
  • MIUI 12.5
Memori UFS 3.1, 128GB,256GB na RAM 8GB,6GB,12GB
Kamera Kamera nne

  1. 108MP,PDAF(wide)
  2. 13MP(ultrawide)
  3. 5MP(macro)
  4. 20MP(wide, selfie camera)
Muundo Urefu-6.81inchi
Chaji na Betri
  • 4600mAh-Li-Po
  • Chaji-55W
Bei ya simu(TSH) /=

Upi ubora wa simu ya Xiaomi Mi 11?

Ukilinganisha simu ya xiaomi mi 11 na simu nyingi za bei utaona kuwa mi 11 ni simu ya gharama kubwa.

Simu zinauzwa bei ghari huwa na vitu vingi vyenye ubora

Xiaomi Mi 11 ni simu yenye uwezo wa juu kiutendaji.

Hiyo inachagizwa na aina ya processor ya simu iliyotumika

Hii ni aina ya smartphone inayojaza simu kwa dakika chache

Display yake inaweza kuonyesha rangi zinazofikia bilioni moja.

Simu inapokuwa na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi inapata uwezo wa kuonyesha kitu kama kinavyoonekana kwenye mazingira halisi

Ukitazama aina ya vioo, network na kamera yake utagundua upekee kwenye teknolojia zinazounda hivyo vitu

Tuzame kiundani zaidi kwenye kila nyanja

Nguvu ya Network

Xiaomi mi 11 inakubali aina zote za mitandao.

Inaweza kutumia intaneti ya 4G na 5G ya masafa ya kati

Aina ya 4g iliyopo kwenye simu ni LTE Cat 22

Spidi ya juu kabiasa 4G aina ya LTE cat 22 inafikia 2500Mbps

Hii inamaanisha nini?

Kama simu inadownload file la ukubwa 1300MB, basi simu itamaliza kudownload kwa sekunde nne tu.

Ila hakuna mtandao unaotoa spidi ya ukubwa huu hapa Tanzania

Kikubwa simu inakubali network bands za mitandao ya simu hapa nchini.

Mi 11 ina network bands za 4G zipatazo 17 za kimataifa

Ubora wa kioo cha Xiaomi Mi 11

Amoled ndio kioo cha xiaomi mi 11.

Kiwango cha contrast kwenye vioo huwa ni kikubwa.

Ukubwa wa contrast unatengeza rangi za kutosha.

Hivyo display huonyesha vitu kwa rangi zake sahihi kwa asilimia kubwa

Kioo cha hii simu kinaweza kionyesha video za HDR10+

HDR10+ ni aina ya teknolojia ya video ambayo hujaribu kuonyesha vitu kama vinavyoonekana kwenye mazingira.

Kioo ni angavu sana na kina resolution inayofikia 1440 x 3200 pixels (kubwa sana)

Kwa sifa hizo inafanya kioo cha mi 11 kuwa na bei kubwa.

Hupaswi kuwaza kuhusu hilo.

Kioo kinalindwa na glassi ngumu kama utakavyoona ukiendelea kusoma sifa zote.

Nguvu ya processor ya Snapdragon 888 5G

Kwenye orodha ya processor za simu zenye uwezo basi snapdragon 888 5g ipo.

Kiutendaji snapdragon 888 5g inapitwa na processor chache kama MediaTek Dimensity 9000

Hii processor inaifanya Mi 11 ifungue app ya aina yoyote kwa kasi

Kwa mujibu wa alama geekbench, chip hii ina alama 1118.

Na alama za 3DMark zinafika 5304

Chipset za snapdragon 695 5g na Dimensity 900 hazioni ndani kabisa.

snapdragon 888 5g ina nguvu sana kwa sababu ya mgawanyo wake wa core nane

Uwezo wa Core kubwa sana

Core kubwa yenye nguvu sana kiutendaji ipo moja tu.

Spidi ya hii core inafikia 2.84GHz

Core imeundwa kwa kutumia muundo wa Kryo 680

Kryo 680 inatumia muundo wa Cortex X1

Cortex X1 huwa inapiga kazi kubwa bila kuzingatia matumizi ya chaji.

Kwa maana kwa ajili ya kufikia utendaji mkubwa pekee pale simu inapofanya kazi nzito

Uwezo wa Core kubwa kiasi

Core zenye nguvu kiasi zipo tatu.

Na zenyewe zimeundwa kwa Kryo 680 inayotumia Cortex A78

Utendaji wa Cortex A78 huwa ni mkubwa unaozingatia matumizi ya betri

Kwa hiyo core hizi huwa zinapiga kazi kwa matumizi madogo ya betri

Matumizi madogo ya umeme hupunguza nguvu ya utendaji wa processor

Uwezo wa Core Ndogo

Core ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kufanya kazi ndogo zipo nne

Na core zote zinatumia muundo wa Kryo 680.

Na spidi ya ila core inafikia 1.8GHz

Uwezo wa betri na chaji

Simu ya xiaomi mi 11 inatumia betri aina ya Li-Po yenye ujazo wa 4600mAh

Chaji yake inapeleka umeme wa kasi inayofikia wati 55W

Kwa mujibu wa majaribio ya gsmarena, chaji hii hujaza simu kwa dakika 50 tu.

Hivyo kama una safari ya haraka hustosubiria muda mrefu simu kujaa chaji

Tatizo,

Simu inakaa na chaji masaa machache kwa viwango vya kileo.

Ukiwa unatumia intaneti masaa yote mfululizo mi 11 itaisha chaji baada ya takribani masaa 11

Ni muda mchache kiujumla

Ukubwa na aina ya memori

Ukitaka kujua simu yenye uwezo mkubwa, angalia aina ya memori pia.

Kuna memori zenye kasi kubwa na kasi ndogo.

Xiaomi mi 11 inatumia memori zenye kasi sana aina ya UFS 3.1

Spidi yake ya kusoma(read) na kuandika(write) inafika 2900MB/s

Kwa maana ukikopi file la GB 2.9, simu itakopi kwa sekunde moja tu

Na aina ya ram ambayo chip inatumia ni LPDDR5 yenye kasi zaidi kuliko ile iliyopo kwenye iPhone 13 pro max

Uimara wa bodi ya Xiaomi Mi 11

Japokuwa xiaomi mi 11 sio moja ya simu ambazo haziingii maji ila ina bodi ngumu kuvunjika

Simu imeundwa kwa kioo kigumu cha Gorilla Glass Victus

Screen yenye Gorilla Glass Victus inaweza isipasuke kama simu ikianguka kwa kimo cha mita mbili kutoka juu.

Fuatilia majaribio ya kampuni ya gorilla utaona ugumu wa vioo hivyo

Fremu zake ni za aluminium.

Hivyo swala la kuchunika pia ni gumu kwa kiasi kikubwa

Mi 11 ina urefu wa inchi 6.81 na uzito wa gramu 191(simu nyepesi)

Ubora wa kamera

Simu ina kamera nne ina kamera tatu

Kamera moja imewekewa teknolojia ya OIS inayotuliza video inayorokodiwa huku anayerokodi akiwa anatembea.

Kamera ya mi 11 inatoa picha nzuri nyakati za mchana na usiku.

Exposure na contrast yake inatofautisha rangi kwa uzuri

Zitazame picha zilizopigwa na smartphone ya Mi 11

Ubora wa video ni wa kuridhisha.

Hii simu inaweza kurekodi aina zote za video kwa spidi inayofikia 240fps

Kamera zake zinaweza kurekodi video zenye ubora wa HDR10+

Ubora wa Software

Xiaomi Mi 11 ni simu ya android 11 yenye software ya MIUI 12.5

Moja ya kitu kizuri cha MIUI ni aina ya screenshot.

screenshot inaweza kuchukua kurasa nzima kwa kuscroll

File Manager ya MIUI 12.5 ni nzuri ila haina sehemu ya kutachi mafaili.

MIUI 12.5 ya kimataifa huwa ina matangazo kwenye apps karibu zote za MIUI

Yapi Madhaifu ya Xiaomi Mi 11

Simu haina uwezo wa kuzuia maji kupenya kuokana na kukosa viwango vya IP68

Kamera zake hazina teknolojia nzuri ya autofocus aina dual pixel pdaf

Ina uwezo mdogo wa kukaa na chaji muda mrefu

Neno la Mwisho

Kama unahitaji simu yenye utendaji wa juu Mi 11 inakufaa na inauzwa kwa bei rahisi.

Simu haihitaji screen protector sababu ya ugumu wa kioo

Wazo moja kuhusu “Ubora na bei ya simu ya Xiaomi Mi 11(na sifa zake)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

xiaomi15ultra

Simu mpya za Xiaomi(Redmi) 2025 na bei zake

Hii ni orodha ya simu mpya za redmi na Xiaomi ambazo zimetoka mwanzoni mwa 2025 na mwishoni mwa 2024 Simu zilizoorodheshwa zipo za bei kubwa na bei ndogo Hivyo basi […]

iphone 16 pro

Kampuni bora za Simu duniani (2024/2025)

Pamoja na uwepo wa makampuni zaidi ya 100 ya kutengeneza simu bado kampuni zilezile zimeendelea kushika soko kwa sehemu kubwa duniani, kampuni hizo ni apple, samsung na xiaomi na nyinginezo. […]

huawei mate

Simu Bora 15 Duniani 2024 (na zitakazotamba 2025)

Kwa mwaka 2024, soko la simu janja yaani smartphone duniani lilitawaliwa na makampuni ya Apple, Samsung, Xiaomi, Vivo na Oppo Kwa hapa Afrika kampuni ya Samsung inaongoza kwa mauzo ikifuatiwa […]

Simu bora duniani na bei zake 2024

Leo tuzungumzie kuhusu simu bora duniani na bei zake kwa mwaka 2024 Kuna matoleo mapya ya simu kali yenye ubora wa kiutendaji na wenye nguvu madhubuti katika maeneo mengi Ubora […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company