Simu ya xiaomi 12 pro ni simu ya android ambayo imetoka mwishoni mwa mwaka 2021
Xiaomi 12 Pro ina ubora ambao unachuana na simu ya samsung galaxy s22+ 5G
Kitu kinachofanya bei ya xiaomi 12 pro kuzidi shilingi milioni moja na laki tano
Ukifahamu sifa itakusaidia kutambua kama ni simu nzuri inayostahili kununuliwa kwa bei iliyopo hapo chini
Bei Xiaomi 12 Pro Tanzania
Bei ya xiaomi 12 pro ya ukubwa wa GB 256 na RAM ya GB 8 ni shilingi 2,000,000/=
Hii ni bei ya Aliexpress.
Kama unainunua aliexpress mpaka ifike Tanzania itakugharimu shilingi 2,020,000/=
Ukubwa wa memori si kitu kinachosababisha simu hii ya xiaomi kuwa na bei kubwa
Bali ni processor, kioo, software, kamera na aina ya bodi ya simu
Fuatalia uzielewe sifa zake zote kama zilivyoainishwa humu
Sifa za simu ya Xiaomi 12 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | LTPO AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 256GB,128GB na RAM 8GB,12GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.73 inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,208,447.23/= |
Upi ubora wa Xiaomi 12 Pro
Hii ni xiaomi ya daraja la kwanza hivyo tarajia ubora katika kila idara
Simu ina kioo ambacho kinaonyesha vitu bila kupoteza uhalisia wa rangi
Inatumia chip yenye utendaji mkubwa kitu kinachoifanya simu kuwa na nguvu
Ni simu ambayo ina mfumo reverse charging kwa maana inaweza kuchaji kifaa kingine
Chaji yake inawahi kujaza betri chini ya dakika 25
Uwezo wa Network
Simu ina network zote ikiwemo 4G na 5G
Network yake ya 5G haisapoti 5G ya mmWave ambayo huwa na kasi kubwa zaidi
Aina ya 4G simu inayotumia ni LTE Cat 24
Spidi ya juu kabisa ya kudownload ya LTE Cat 24 ni 2500Mbps
Hii ni kasi ambayo huwezi kuipata kwenye mitandao karibu yote Tanzania
Ila simu ina masafa mengi yakiwemo yanayotumika na mitandao ya simu nchini
Ubora wa kioo cha Xiaomi 12 Pro
Kioo cha xiaomi 12 pro ni cha aina ya LTPO AMOLED
Hiki ni kioo ambacho kina rangi bilioni moja tofauti na IPS LCD ambazo huwa na rangi milioni 16
Hii inamaanisha vitu vingi vitaonekana kwa rangi zake halisi
Kioo pia kinaongezewa ubora wa Dolby Vision na HDR10+
Uangavu wa kioo unaweza kuonyesha vitu vizuri simu ikiwa inatumika juani
Kwa sababu kiwango chake cha nits (vipimo vya uangavu) unafika 1000
Na uzuri mwingine wa kioo chake unachagizwa na simu kuwa na resolution na refresh rate kubwa
Ina refresh rate ya 120 na resolution ya 1440 x 3200 pixels
Nguvu ya processor ya Snapdragon 8 gen 1
Processor ambayo xiaomi 12 pro inatumia ni snapdragon 8 gen 1
Ni processor ya simu inayoshika nafasi ya pili kiuwezo nyuma ya apple a15 bionic
Kwenye app ya geekbench, snapdragon 8 gen 1 ina alama 1216
Wakati app ya antutu processor ina alama 1,037,000
Kiuhalisia hata exynos 2200 ya samsung galaxy s22+ inazidiwa na chip hii ya snapdragon
Hii inasababishwa na aina ya miundo ambayo chip imetumia
Kwenye core kubwa kuna Cortex X2
Na core zenye nguvu ndogo kumetumika muundo wa Cortex A710
Na pia core ambazo zinatumia nguvu ndogo zinatumia muundo wa Cortex A510
Uwezo wa betri na chaji
Ukubwa wa betri ya xiaomi 12 pro ni 4600 mAh aina ya Li-Po
Kiuwezo, simu inakaa na chaji masaa 74 kama ikiwa haitumiki mara kwa mara
Kwenye majaribio ya gsmarena, betri ya xiaomi inakaa na chaji masaa 10 na dakika 46 simu ikiwa inatumia intaneti muda wote
Kiujumla uwezo wa simu kukaa na chaji sio mkubwa
iPhone 13 Pro Max ambayo ina betri dogo inakaa na chaji masaa 18 simu ikiwa kwenye intaneti muda wote
Chaji ya xiaomi 12 pro inaijaza betri ya simu kwa dakika 21 tu
Hii inatokana na kasi ya chaji kupeleka umeme wa wati 120
Ukubwa na aina ya memori
Kwenye upande wa memori kuna xiaomi 12 pro ya GB 128 na RAM ya GB 8 na ya GB 256 na RAM ya GB 8 au 12
Hivyo kuna matoleo matatu
Aina ya memori simu inazotumia ni UFS 3.1 ambazo husafirisha data kwa kasi kubwa
Kitu kinachoifanya simu kuwaka kwa haraka
Na app kufunguka kwa sekunde chache
Uimara wa bodi ya Xiaomi 12 Pro
Kumbuka kuwa hii ni simu ya daraja la juu
Simu mpya za bei kubwa huwekewa bodi imara za kioo
Xiaomi 12 Pro ina kioo cha Gorilla Victus upande wa nyuma na mbele
Upande wa pembeni haijaainishwa aina ya bodi iliyopo
Simu ina urefu na upana wa inchi 6.73
Hivyo simu ni ndefu kiasi chake
Urefu ambao unaifanya simu kuwa na kauzito fulani wakati wa kuibeba
Kwani uzito wake ni gramu 204
Ubora wa kamera
Hii ni simu ya xiaomi macho matatu
Ina kamera ya Ultrawide inayopiga picha eneo pana sana kwa nyuzi 115
Pia ina kamera kwa ajili ya kupiga picha vitu ambavyo vipo mbali na kamera
Kamera ya aina hiyo huitwa Telephoto
Mfumo wake wa kamera una autofocus ya PDAF na dual pixel PDAF
Kitu kinachofanya picha kutokea kwa uzuri
Kwenye upande wa kurekodi video simu ipo vizuri zaidi
Inaweza kurekodi video kwa ubora mpaka wa 8K kwa kasi ya 24 fps na video za aina nyingine kwa kasi zaidi ya 60 fps
Ubora wa Software
Simu ya xiaomi 12 pro inakuja na mfumo endeshi wa android 12
Na inatumia pia software ya MIUI 13
Kwenye MIUI 13 kuna mfumo wa kuscreenshot unaoweza kupiga picha kwa urefu unaotaka wewe
Mfumo huo pia umeongezwa kwenye android 12
Kabla ya hapo mtu aliweza kupiga picha kipande cha screen pekee
Lakini pia toleo jipya la android lina kitu kinaitwa color extractor
Kwa maana rangi za vitu vingine vinanakili rangi ya theme (wallpaper)
Yapi Madhaifu ya Xiaomi 12 Pro
Udhaifu mkubwa wa simu hii ni uwezo mdogo wa kukaa na chaji
Mtumiaji wa simu atalazimika kuchaji zaidi ya mara moja kwa siku kama anatumia intaneti mara kwa mara
Kuchaji simu kwa chaji ya 120W mara kwa mara kunapunguza uwezo wa betri kukaa na chaji
Hivyo maisha ya betri yanakuwa mafupi
Kitu kingine ni simu kutokuwa na uwezo wa kuzuia maji kupenya
Fikiria simu ya daraja la kati ya samsung galaxy a73 haipistishi maji kwani ina IP67
Lakini simu hii haina
Neno la Mwisho
Bei ya xiaomi 12 pro ni ndogo ukilinganisha na ubora wa simu
Kwa muhitaji wa simu yenye uwezo mkubwa xiaomi hii itampa kila kitu kizuri kuhusu simu janja