Vifaa vyote vya kompyuta kuanzia kompyuta mpakato, simu janja, smartwatch nk huundwa na kitu kinaitwa mfumo endeshi
Mfumo endeshi ni mfumo unasimamia na kumeneji vitu vyote vilivyopo kwenye kompyuta au simu
Unapotumia simu kupiga picha, kuongea na mtu kazi ya kujua kifaa kipi kitumike kutoa huduma husika inafanywa na mfumo endeshi
Mifumo endeshi upande wa simu janja ipo ya aina nyingi ila inayotumiwa na watu wengi ni Android na iOS
Hivyo iOS ni mfumo endeshi uliotengenezwa na kampuni ya apple kwa ajili ya kutumika kwenye vifaa vya kampuni hiyo hasa simu janja za iPhones
Ufanyaji kazi wa iOS unatofautiana na Android kwani muundo wa ios ni tofauti
Hizi ni sifa za mfumo wa iOS
App za iOS
Mfumo endeshi wa iOS unatumia applikesheni ya apple app store kupata appliksheni kwa ajili ya kutumiwa kwenye iphones
Kwenye app store kuna app za kulipia na za bure kama ilivyo kwa simu za android
Lakini sio kila ya android inapatikana kwenye iOS
Kama ilvyoelezwa utendaji wa mifumo endeshi inatofautiana
Na pia haipo huru kama android ndio maana app store ina idadi ya app zipatazo milio maja na laki mbili mpaka kufikia mwaka 2021
Ambapo google play store mpaka kufikia mwaka 2017 ilikuwa na app milioni 3
Muundo wa faili upande wa app za iOS ni .ipa huku kwenye android ikiitwa .apk
iOS hutumiwa kwenye simu za apple tu
Mfumo endeshi wa iOS haukutengenezwa kutumika kwenye vifaa tofauti na vilivyoundwa na kampuni ya apple
Yaani huwezi kuikuta iphone orijino ikitumia mfumo endeshi wa android
Ama kukuta simu ya samsung ikitumia mfumo endeshi wa iOS
Hii ni tofauti na mifumo mingine kama windows ya microsoft na android ya google
Pamoja na kuwa Google ni wamiliki wa android na wenyewe wanatengeneza simu ila android utaikuta kwenye tecno, infinix, sony, samsung, nokia, oppo nk, ni mfumo huria
Ila iOS utaikuta kwenye iphones zote pekee yake kwa sababu ni mfumo uliofungwa kutumika kwenye kampuni moja tu.
iOS inaruhusu multitasking
Maana ya multitasking ni uwezo wa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja
Matoleo ya mwanzoni ya iOS yaliwekwa ukomo mkubwa sana wa kufungua app nyingi kwa wakati mmoja
Ni kuanzia toleo la iOS 4 ndiyo iliyokuja kuruhusu vitu vya aina saba kuweza kufanya kazi wakati simu ikifanya kazi nyingine
Vitu hivyo ni kusikiliza audio, kuchota taarifa za eneo, notification, kudownload vitu na mengineyo
Hii inamaanisha unaweza kufungua app ya kusikiliz miziki wakati huo kuna ujumbe wa notification umetokea na wakati huo huo kuna app inadownload mziki
Hii ndio maana ya multitasking, sio kitu kigeni hata android ipo
iOS inasapoti Face ID
Kwenye swala usalama iOS ina mfumo unaofungua ama kuiloki simu kwa kutumia sura ya mtu
Ufanisi wa face id ya ios ni mkubwa kuliko simu nyingi za matoleo ya kati
Kwa hiyo kwenye iphone kuna njia kama tatu za kulocki simu
Ambazo ni fingerprint, password na ya kutumia sura
Kuna hatua chache za kufuata kuiseti simu kutumia sura kama password
Ina mifumo saidizi kwa waremavu
iOS kama ilivyo kwa android, ios ina mifumo mbalimbali ya kumsaidia mremavu kutumia simu
Kwa mfano mfumo wa VoiceOver unasoma vitu vyote vya kwenye simu kwa sauti
Kusoma kwa sauti kunamuwezesha mremavu wa macho kujua wapi anatachi
Na inamuwezesha mtumiaji wa simu kutumia simu kwa kutikisa simu
Hitimisho
Kwa haya machache yanatosha kukufafanulia maana ya iOS kwenye vifaa vyote vya apple
Ila ni mambo mengi yameachwa yaliyomo kwenye mfumo huu wa simu za iphones
Kwa hiyo kama ukisikia android au ios basi jua kuwa hii ni mifumo endeshi kwa ajili ya simu janja tofaut tofauti
Maoni 3 kuhusu “Nini Maana ya iOS kwenye Simu za iPhone”
Hilo nalo somo asante bro
Dah Sawa Mm Nahitaji Sim
Unapatikana wapi