Iwapo unatafuta simujanja ya 150,000 yenye sifa za kawaida Tecno Pop 2 F inaingia hapa
Haina sifa nyingi nzuri kama Samsung Galaxy NOTE 10 ambayo imetoka mwaka mmoja na pop 2 F
Kwa sababu hiyo bei ya Tecno Pop 2 F haiwezi kuzidi laki mbili popote pale hapa Tanzania
Hata hivyo, ukiimiliki usitarajie mambo makubwa mengi bali ni simu inayofaa kusukumizia siku mpaka utakapopata bajeti nzuri
Bei ya Tecno Pop 2 F ya GB 16
Simu hii ukubwa wake ni GB 16 na inauzwa kwa shilingi 150,000 dukani
Kama ukinunua kwa mtu unaweza kuipata hata kwa shilingi 75,000
Bei yake ndogo inasababishwa na vitu vingi ikiwemo memori ndogo, kamera, na utendaji wa chini kiujumla
Kama ukiangalia sifa zake utaona ufauti mkubwa ukilinganisha na toleo kama la Tecno Spark 10 au hata vivo y66 ya mwaka 2017
Sifa za Tecno Pop 2 F
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | 16GB na RAM 1GB |
Kamera | Kamera MOJA
|
Muundo | Urefu-5.4inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 150,000/= |
Upi ubora wa Tecno Pop 2 F
Ubora mkubwa wa hii simu ni kuwa na bei ndogo tu
Bei ambayo watu wengi wanaimudu kuinunua
Hivyo inawapa fursa kuweza kuwasiliana na kuingia mitandao ya kijamii na intaneti
Mambo mengine kama yanavyoonekana kwenye jedwari yanaweza yasiwavutie watu wengi
Ukizingatia matoleo ya miaka ya karibuni yanakuja na vitu vikubwa sana
Uwezo wa Network
Mtandao wa juu kabisa unaoweza kuutumia kwenye hii simu ni 3G
Wakati inatoka haikuwa inasapoti mtandao wa 4G
Hii inamaanisha hutoweza kupata kasi kubwa ya intaneti
Kwa sababu 4G na 5G ndizo zina kasi sana kwa sasa
Ila 3G inaweza kukupa kasi ya kulizisha kiasi japo kama unapoakuwa faili kubwa la GB 2 simu itachukua muda kumaliza kudownload.
Ubora wa kioo cha Tecno Pop 2 F
Kioo cha pop 2F ni aina ya IPS LCD
Ambacho hakina resolution kubwa, muonekano wa vitu si wa kuvutia sana
Hii inachangiwa na resolution ndogo ya 480 x 960 pixels
Kwa simu za siku hizi tena simu ya kawaida huwa zina 1080 x 1660 pixels
Kiwango kikubwa cha resolution kinafanya vitu vionekane vikiwa na rangi sahihi na zilizokolea kwa usahihi pia
Hata tecno pop 2 f ni simu ya bei ndogo na mambo yake mengi hayawezi kulingana na simu za bei ghali
Nguvu ya processor MediaTek MT6580m
Hii simu inapewa nguvu na processor ya Mediatek mt6580M
Utendaji wake ni wa chini sana kwani haina core zenye nguvu hata moja
Mfano wa core zenye nguvu hujulikana kama Cortex A75 na kuendelea
Inaundwa na core zenye kasi ndogo
Kwa muundo huu, hii sio simu nzuri anayependa kucheza magemu, kufungua app nyingi kwa wakati mmoja
Ila ni simu nzuri kwa mtumiaji anayetumia simu kupiga simu na kutuma sms na intaneti kiasi
Kwa sababu kazi hizo hazihitaji nguvu kubwa
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Tecno Pop 2 F ni ndogo na ina 2400mAh
Ukubwa wa 2400mAh unakaa muda mfupi kama ukiwa upo kwenye intaneti masaa mengi mfululizo
Pia simu haina mfumo wa chaji unaopeleka umeme mwingi
Pamoja na betri ndogo ila simu itachukua muda kujaa
Inafaa kama mara nyingi upo kwenye maeneo yenye uhakika wa umeme
Ukubwa na aina ya memori
Memori ya simu ni ndogo pia ina GB 16 tu na RAM ya GB 1
Kiwango hiki cha memori lazima kiwahi kujaa
Kikawaida kuna sehemu ya memori inachukuliwa na mfumo endeshi wa simu na appliksheni zinazokuja na simu
Mwisho wa siku simu inaweza ikabaki na memori ya GB 8 kwa kuweka mafaili yako wewe binafsi
Kiwango kinawahi kujaa baada ya muda mfumi
Kutokana na udogo wa memori unaweza kuongeza memori kadi kwa sababu simu inayo hiyo simu
Uimara wa bodi ya Tecno Pop 2 F
Bodi ya hii simu inaundwa kwa plastiki
Ni muhimu kuweka kava kuifanya simu isichunike rangi kirahisi
Kiujumla uimara wa bodi sio mkubwa
Na ni muhimu pia kuweka protekta kuilinda simu wakati ikidondoka bahati mbaya
Ubora wa kamera
Hii simu ina kamera moja tu yenye megapixel 5
Ukiwa unapenda kamera jua kua utahitaji simu yenye megapixel angalau 8 kabla ya kuangalia vitu vingine vinavyofanya kamera kuwa nzuri
Pitia: Simu zenye kamera nzuri za bei nafuu
Hata hviyo utaweza kurekodi video za full HD kwa kiwango cha 30fps
Ubora wa Software
Wakati inatoka ilikuwa inatumia Android 8.1
Ila leo huu matoleo ya android yamefika 13 yaani Android 13 na hivi karibuni Android 14 inakuja
Kwa bahati mbaya Tecno Pop 2 F haina uwezo wa kupokea toleo jipya
Kutokana na simu kuwa na utendaji mdogo na memori ndogo imeifanya simu kutumia Android aina ya Go Edition
Android Go Edition huwa inawekwa kwenye simu ambazo hazina nguvu kubwa, kwani ikiwekwa android ya kawaida simu inakuwa nzito zaidi
Washindani wa Tecno Pop 2 F
Kwa nyakati za miaka hii, simu hii ina washindani wengi wenye simu za bei nafuu
Japo nyingi zinauzwa kuanzia laki mbili na kuendelea
Simu hizo ni Samsung Galaxy a02, Redmi 9a, Redmi 10a na hata Tekno Spark 4
Hizo simu zinaiacha Tecno Pop 2 F kwa mbali japokuwa bei zake zinaongezeka kidogo
Neno la Mwisho
Kwa mwaka 2023, Tecno Pop 2 F sio simu ya kuwa nayo
Kwa sababu haina vitu vingi vinavyohitajika katika ulimwengu wa simu wa sasa
Ni simu ya kuwa nayo wakati ukijipanga kutafuta pesa ya kumiliki simu kali zaidi.
Maoni 3 kuhusu “Bei ya Tecno Pop 2 F na Sifa Zake (simu ya laki na nusu)”
Nina simu aina Tecno pop 2f inapata moto nikifungua data tatizo litakuwa nini nisaidieni
Kiukweli Tecno pop 2 ni simu yenye nguvu ndugu hiyo ndio sababu inapata Moto Sana, njia ni kupunguza background activities kama zipo
Nzuri san